TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, October 18, 2017

Prince Black kopa | Nadekezwa Remix Official Music Video

Sikiliza Nyimbo Tamu, Taarab safi kabisa kutoka kwa muimbaji Prince Black Kopa - Nadekezwa Remix. 
Prince Black Kopa ni mtoto wa Malkia wa Mipasho Tanzania na Africa Mashariki Bibi Khadija Kopa.

Monday, March 13, 2017

Adio mpya: SIMPI KIKI KUNGUNI WA MWENDO KASI - Mwamvita Shaibu.


Taarabuzetu.blogspot.com  imekuletea nyimbo mpya kabisa toka katika kundi la muziki wa Taarab Tanzania Ogopa Kopa chini ya Malkia wa Mipasho.
Nyimbo inakwenda kwa jina la - SIMPI KIKI KUNGUNI WA MWENDO KASI ikiwa imeimbwa na Mwamvita Shaibu.
Pata kuisikiliza usikie nini kasema.

Kuwa nasi.

Thursday, December 1, 2016

Download Audio Mpya: Omary Tego - Figisufigisu...


Pata kuisikiliza na kui-download nyimbo mpya ya Omary Tego - Figisufigisu akiwa ndani ya kundi la Yah TMK Modern Taarab chini ya Mkubwa Fellah... 
Sikiliza ladha tofauti.


Saturday, November 19, 2016

LIVE: CLOUDS TV NA PRINCE BLACK KOPA (MTOTO WA KHADIJA KOPA)...


Mtoto wa Malkia wa mipasho Prince Black Kopa atakuwa na Interview LIVE ndani ya Clouds TV siku ya Jumamosi tarehe 19 Novemba 2016 saa 3 mpaka 4 Usiku!.

Pia kutakuwa na utambulisho rasmi wa Video yake mpya ya "Nifagilieni Chocolate remix", kuna mambo mengi sana ataongelea kuhusu mziki wake na nyimbo hii mpya ikiwa ni remix.

Usikose kutizama ndani ya CLOUDS TV na SAKINA LYOKA.



Wednesday, October 26, 2016

YAH TMK TAARAB - YAIBOMOA JAHAZI MODERN TAARAB...



NI BENDI YAH TMK TAARAB -  YAIBOMOA JAHAZI MODERN TAARAB, YACHUKUWA SILAHA MUHIMU ZA KAZI.

Ule usemi unaosemwa na baadhi ya wadau wa taarab ya kuwa "Jahazi Modern Taarab bila ya Mzee Yussuf linasuasua" unaonekana kama unakubalika kwa asilimia fulani baada ya bendi hiyo kupoteza waimbaji muhimu pamoja na wapiga vinanda. 

Majina ya Fatma Nyoro, Chidi Boy, Moh'd Mauji, Mussa Mipango, Kichupa kwa sasa hayatosikika kwenye maonesho ya Jahazi. 

Pia kuna tetesi kuwa Khadija Yussuf ameenda Wakaliwao kwa Thabit Abdul.

Bendi ya TMK pia imeibomoa Coast Modern Taarab kwa kumpa shavu Omary Teggo na dada yake. 
Pia Bi Mwanahawa Ali (JEMBE GUMU) ametilishiwa saini katika bendi hiyo huku akipewa wimbo wa "SINA PUPA MUNGU ATANIPA".

#HAYA SASA - HAPA KAZI TU...


Thursday, October 20, 2016

Khadija Kopa Kuwasha Moto Krismas Morogoro. (Tizama Picha na Video)

Mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  akizungumza jambo na wanahari (hawapo pichani).

Kutoka kushoto ni mkuu wa matukio kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kurugira Maregesi,  Hamis Abdallah na Khadija Kopa.

Khadija Kopa akizungumza jambo.

Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat, akielezea namna atakavyopagawisha mashabiki wake.

 MALKIA wa muziki wa taarab ambaye ni Mkurugenzi wa Kundi la Ogopa Kopa, Khadija Kopa,  anatarajiwa kuwasha moto kwa kutoa burudani ya aina yake katika  Tamasha la Muziki wa Taarab  lililoandaliwa na mtandao wa habari wa Vijana, Tegemeo Arts Group ambalo linajulikana kwa jina la ‘Nani Zaidi’.


Tamasha hilo litakaofanyika siku ya X-Mass ya Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi usiku.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  amesema tamsha hilo linalenga kuhamasisha jamiii katika uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji hasa kina mama wanapopoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.
Amesema kwamba katika zoezi hilo pia kutakuwa na upimaji wa Ukimwi , saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake na kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mablimbali siku tano kabla ya tamasha hilo.

Alifafanua kuwa tamasha hilo litakuwa la aina yake kwani litakutanisha bendi za muziki wa dansi na wanamuziki wa taarab chini.
Miongoni mwa makundi ya taarab na bendi zitakazokuwepo ni Jahazi Modern Taarab, Ogopa Copa Clasic Band,  The East African Melody,  Five Stars Modern Taarab, FM Academia na Moro Jazz.
Mbali na hayo pia  kutakuwa na mechi katika ya Tanzania Veterans na Morogoro Veterans zote za mjini Morogoro zitakazokipiga Desemba 24 mwaka huu zikilenga kuhamasisha uchangiaji hiari wa damu.