TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Saturday, December 28, 2013

Aysher Vuvuzela vipi Ndoa au ni kimyakimya tu!?

Hy ni mapenzi tu hatutaki keroooooo
Wapenzi wa mwanamziki muimbaji wa Taarabu machachari wa kundi la Fivestar, Aysher Othman Vuvuzela wameulizia katika blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com kuwa, Aysher kafunga lini ndoa!?

Maswali haya yamekuja pale alipoanza kupost picha akiwa na mtu anayesema ni mpenzi wake huku wakiwa katika mapozi ya kimahaba.

Ameolewa au anazini tu!? ni dada mmoja aliuliza kwa shart la kutotaja jina lake, na Mr Hamad toka Gongola Mbota akasema "Akiachwa pia aje kutueleza hapa"

Baadhi ya post za Vuvuzela ni kama hizi:-

".unapokuwa upo kaatika mchana na usku waaangu uu' pungufu hayaajakamilika' yanakuwa maisha yangu' naona ndiyo ilivyoumbikaaa kuwa wewe ndio moyo wangu ' haakika imekwishalingika kuwa ww ndie roho yangu" my love ma happiness love u sana my saaaleh mkassy skassy byybbb"

I love him a lot and he lovs me much i knw that  tnks Allah kwa kunipa mpenz bora
Aaaaaaaaa mtuache jaman

Kwakweli blog hii bado haijapata habari kamili toka kwa Aysher mwenyewe baada ya kutafutwa kwenye simu yake na kutopatikana, ila tunamuomba Vuvuzela atueleze kama watu washakula ubwabwa ama bado tujiandae na michango...

Monday, December 16, 2013

Tamasha la Mitikisiko ndani ya Dar Live katika Matukio na Picha...

Ukumbi wa Burudani wa Dar Live usiku wa kuamkia jumapili ulitikisika kutokana na kufurika mashabiki ambao walijitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho la Mitikisiko ya Pwani lililoandaliwa na Redio TIMES FM kwa udhamini wa Vodacom.

Bendi tano za miondoko ya taarabu zilitoa burudani ya nguvu ambayo iliwafanya mashabiki wa miondoko hiyo washindwe kutulia katika viti vyao. Zifuatazo ni picha kadhaa katika matukio tofauti, Kundi la Supershine ndo lilikuwa la kwanza kutoa burudani na Stail ya Ngoma ya Kimwera.

Mwimbaji wa bendi ya Super Shine, Queen Salma akifungua pazia la burudani.
Nuru Moshi wa Super Shine akitoa burudani.…
Waimbaji wa Super Shine wakiimba.
Ally J wa kundi la Five Star akiimba jukwaani.
Maua Tego wa Five Star akitoa burudani...
Khadija Kopa (Kati) akicheza na waimbaji wake.
Fatma Machupa wa Jahazi akifanya vitu vyake.
Fatma Mahamud wa Jahazi akitoa burudani kwa mashabiki...
Mkurugenzi wa Mashauzi Isha Mashauzi na mdogo wake Saida wakifanya kazi iliyowapeleka ukumbini, yaani burudani tu.
Waimbaji wa Mashauzi Classic wakiimba...
Hashim Saidi Igwee akifanya vitu vyake jukwaani...

MC wa Shughuli nzima, Dida akiwakilisha kazi yake...
Mashabiki alijitokeza kwa wingi kupata burudani ya uhakika... Full Bata...!!


Hammer Q apata ajali...

Hammer Q.
Msani wa kutumainiwa katika band ya 5Stars Modern Taarabu Hammer Q, jana (Jumapili) alipata ajali mbaya ya pikipiki.

Hammer Q aliandika katika ukurasa wake wa facebook kutokana na ajali hiyo:-
Leo (Jumapili) kwenye saa kumi jioni nimepata ajali mbaya ya pikipiki maeneo ya kwenye geti la Vikindu pale pale kwa anae pajua, nashukuru sikuumia hata kidogo.

Japo nimetoka kwenye tairi, namaanisha kilichonipa msaada wa kunyanyuka wakati nimedondoka Ni tairi ya pik up kwamba nikaishika na kunyanyuka ila ilikua inakuja maeneo ya tumboni na mwenzangu aliekuwa dereva ameumia sana.

Asante asante Mungu ni mara nyingi sana unanitoa hizo sehemu asante asante.

Taarabu zetu inampa pole sana Hammer Q, Mungu yu pamoja nawe...

Je!, Nisahihi kwa msanii wa Taarabu kwenda kuimba katika Band nyingine isiyo ya kwake.

Hili hapa ni swali kutoka taarabuzetu.blogspot.com kwenda kwa wamiliki na wadau mbalimbali wa Taarabu hapa Tanzania, baadhi ya watu waliohojiwa na mwandishi walijibu kadri wajuavyo.

Swali na majibu yake ni hayo hapo chini:-

SWALI:-
Wasanii wengi wa Taarabu wamekuwa wakiwayumbisha sana mashabiki wao wasijue leo msanii huyu atakuwa wapi kutokana na tabia ya kwenda kuimba katika Show yoyote ya bendi za Taarabu na wakati yeye anatumikia bendi nyingine.

Hivi hii ni sawa au huwa ni makubaliano katika mkataba?
Kwanini wasanii wasitulie na kuhudhulia katika show za bendi yake tu!?

Naomba unifafanulie na unipe maoni yako ili nami niweze kuwajulisha wasomaji na wapenzi wa Blog ya Taarabu Zetu, Tafadhali...


Amin Salmin
Amin Salmin (Boss T Moto Modern Taarabu):-
Ok hapo kuna namna mbili:-
1. Na ndio kubwa zaidi ni kutokana na bendi anayoitumikia kutokua na maonesho kwa namana moja au nyingine na km unavyojua maisha magumu.

2. Hii ni zaidi kwa wale wasanii mastar au wenye uwezo wakati bendi ambazo hazina mastar hupenda kuwatumia kama mgeni mualikwa lkn kubwa ni kukosa kwa show ktk bende wanazo zitumikia na hali ya maisha.

Taarabu Zetu:-
Hivyo kwa upande wa wamiliki wanawaruhusu tu kwa vile hawawalipi vizuri kutokana na maelewano yao au?

Amin Salmin:-
Hapana unajua bendi zote hua hawalipi mshahara ikimaliza show kila msanii analipwa kutokana na viwango,so km itatokea atapata day work anakwenda nako analipwa vile vile akimaliza tu na hii ni kuhofia mivutano mwisho wa mwenzi.


Amani Mbilo
Amani Mbilo (Mtangazaji Bomba FM - Mbeya):-
Kwa mtazamo wangu kinachochangia:-
1. Ni kutoka na na wasanii wengi kuwepo kwenye kundi pasipo na mikataba ya uhakika usiyowabana

2. Masalahi ndio chanzo kikubwa wasaani wanaona ni bora wahaangaike wenyewe kwa kuwa mishahara midogo

3. Tamaa tu na kutokuwa na subira ya kuweza kukakaa katika band yake na kusubiri mshahara na posho wanazopata

4. Wasani wengi wanaamini show ndio zitakazo watambulisha na nyimbo zao kupendwa kupitia hizo shoow hivyo basi wanalazimika kufanya show nje ya band zao, Hawatutendei haki mashabikiiii.

Taarabu Zetu:-
Vizuri sana Amani, hivyo unashauri vp!? Wakae katika bendi bila kwenda kupiga show katika bendi zingine au waende tu kutokana na mishahara kuwa midogo kama ulivyosema?.

Amani Mbilo:-
Watengenezewe mikataba mizuri na ya haki, na walipwe vizuri ili watulie katika band zao.



Mgeni Kisoda
Mgeni Kisoda (Mpiga Kinanda 5Stars):-
Kaka maisha tu.

Taarabu Zetu:-
Kaka maisha yanafanya nini?

Mgeni Kisoda:-
Ndiyo yanayo mfanya mtu ahangaike...




Hamis Slim
Hamis Slim (Boss G5 Modern Taarabu):-
Huwa ni makubaliano kati ya mwenye bendi na msanii wake kwani wasanii wengine kwa siku asiposhika maiki huwa anahisi kama anaumwa.

Mwingne ni katika kuhitaji muonekano sizani kama kuna msanii ambaye ametoka kisanii utamkuta katika stage ovyoovyo zaidi akialikwa tu, sasa kwa hawa wengine huwa wanashindwa kutumia fursa wanazopewa na mabosi zao kuwa anaweza kuimbia bendi yoyote endapo amealikwa ili azidishe kukuwa kwake kisanii lakini sio kwenda kuimba na kukaa ktk stage ya bendi fulani wakati uko kwenye bendi nyingne ile unajizalilisha kama msanii na hata ile bendi yenyewe pia inaonekana haina uwezo wa kuibua vipaji vya wasanii wanategemea wasanii wa bendi zingine ni hivyo kaka hakuna zaidi ya hayo itakuwa uongo tu.

Taarabu Zetu:-
Kaka wengine wanadai masilahi ni kidogo mno ndo maana wanatoka nje kujitafutia, na kwavile maboss wanawalipa kidogo wanashindwa kuwazuia!! Vipi kuhusu hilo? Na kuhusu mashabiki wafanyeje katika ushabiki!?

Hamis Slim:-
Kwa maslahi kaka hilo cna uthibitisho nalo coz hakuna binadamu anayetosheka na pesa kaka mfano wasanii wa Jahazi ushawaona ktk majukwaa ya bendi nyingine? na wafanya vile ni kwa utaratibu wa boss wao lakini ckama wana maslahi makubwa la hasha.

Pili mbona wengine huwa hawafanyi hivyo na wapo ktk bendi wanazotoka hao wanaofanya hivyo au maslahi ni kwa hao wanaofanya hivyo tu ndio wanaojua maslahi?

Ndo maana nikakuambia kuhusu mengine uongo coz nilijua utakuja ktk swali hili 7bu wasanii nawajua anaweza kupewa pesa ya mkataba laki 5 na akatangaza kapewa milioni 5 baada ya muda anaanza visa mwishowe anakuambia maslahi!, je hili nalo unalichukuliaje!?

Taarabu Zetu:-
Dah!. Hiyo nayo ni kweli kabisa mkuu!! Jahazi wanautaratibu wao, maana hata kama una mapenzi ya kumuona msanii fulani ni lazima uende Jahazi na si kumsubiri katika bendi nyingine ili umuone. Msimamo unahitajika ili heshima ipatikane.

Hamis Slim:-
Yah! maboss wengine huwa hawataki kuwabana wafanyakazi wao co wanamuziki tu tatizo cc watanzania huwa hatujitambui nahatujui nn maana ya uhuru au nn haki za mfanyakazi kwa boss na nn haki za boss kwa mfanyakazi mara nyingi huwa zinaangaliwa haki za mfanyakazi kwa boss tu.


Hashim Said
Hashim Said IGwee (Kiongozi wa Wasanii Mashauzi):-
Kimtazamo wangu si mbaya kufanya hivyo ila haipendezi kwenda kuimba bendi nyingine cku ambayo bendi unayofanyia kaz iko ktk parfomance inatakiwa cku zile ambazo huna show si mbaya kwenda kusalimia jukwaa la bendi nyingine.

Mfano mimi hapa huwa kila jumatatu nakwenda lango la jiji magomen ambako hutumbuiza bendi ya EAST AFRICAN MELODY nakwenda kwa sababu cku hyo niko free lakini cku zingine huwez kunikuta bendi nyingine labda tusiwe na onyesho pahala.

Taarabu Zetu:-
Kwa upande wa mashabiki wako kaka wakufuate wewe au Mashauzi na East African Melody!? Na unaonaje mkitulia tu Bendi moja!?

Hashim Said IGwee:-
Mashabiki wangu nashukuru nnapokwenda Melody kutembea huwa wanakuwepo na hufurahia nnaposhirikiana na wasanii wenzangu ikumbukwe kwamba nilianzia Melody ndio nikaja Mashauzi wengi wa mashabiki wanalifahamu hilo huwa nakwenda pale kutembea siku ambazo niko off kikaz.


Warda Chande.
Warda Chande. (Mtangazaji - Passion FM):-
Kwakweli, it depends na mkataba ulivyo kama unamruhusu msanii kufanya kazi za nje kwa mda wa ziada baada ya kazi za Band (Siku ambazo band haipigi wala mazoezi hakuna) sio mbaya ni kutokana na hali halisi ya kimaisha mtu (Msanii) anaamua kufanya hivyo ili kuweza kuendesha maisha yake.

Lakini kwa upande mwingine kama mkataba wake haumruhusu kufanya hivyo na mwenyewe ameweza kusaini kwa mkono wake inabidi asifanye kazi nje ya band yake kwani atakuwa amekiuka mkataba (atakuwa kinyume na Mkataba).

Ushauri wangu kwa wamiliki wa band ni kuwapa uhuru wasanii wao kufanya kazi nje ya band kwa muda ambao band haifanyi kazi (Show) kwasababu hali halisi ya maisha inajulikana ni ngumu .
Kwa upande wa mashabiki inabidi tuelewe wasanii wapo katika kutafuta so kikubwa zaidi ni kupata burudani nzuri kutoka kwa msanii haijalishi katoka band gani au ni solo artist au leo yupo hapa na kesho unamuona pale, kikubwa ni kupata burudani (Kuburudika na Kuelimika.



Kais Mussa Kais
Kais Mussa Kais (Meneja - Supershine):-
Unajua kaka kuna ule urafiki kati ya bendi kwa bendi na msanii kwa msanii. Kwahiyo sio mbaya kwa msanii kwenda ktk bendi ingine na kuimba ni just urafiki kisanaa, lakini issue inakuja pale msanii anapoonekana ktk show zaidi ya tano au kumi za bendi nyingine tofauti na kule alipoajiliwa hili ni tatizo na limekuwa likifanywa sana na wasanii wa taarabu wenyewe wanaita "NDONDO" sio nzuri inawayumbisha wapenzi wasijue huyu msanii ni wa bendi gani haswa?.

Imefika wakati kwa viongozi wa taarabu kukemea jambo hili kwa ajili ya kuleta heshima kati ya bendi na msanii husika ni hayo tu!.




Kisolo Mwanamarui
Kisolo Mwanamarui (Mpiga Solo - Mashauzi):-
Kaka kuhusu swali lako ni zuli sana nikweli wasanii sasahivi wanaacha band zao nakwenda kufanya show kwingne tena hadi wamiliki waband wenyewe wenye majina hufanya hevyo kwaheyo kwakweri tunawayumbisha mashabiki ilakwa sisi wapigaji Vinanda ndio hatufanyi hivyo.

Mi nasema wasani tupunguze tamaa ya pesa tuendeleze muziki na bendi zetu kwani tuko juu kwasasa.




> > > > >    < < < < <

Hayo ndo maoni tuliyopata.
Mziki wa Taarabu sasa unazidi kukua na kukomaa, sisi kama wadau wakubwa wa mziki huu wa mwambao tunaomba wamiliki na wasanii wote kufikiri kwa makini jambo hili ili lisije kuwayumbisha, ni kama vile haijakaa vizuri kutokana na maoni hapo juu.

Sunday, December 15, 2013

RATIBA YA G5 MODERN TAARABU XMAS NA MWAKA MPYA.

Bendi ya G5 Modern Taarabu imetoa ratiba yake nzima katika msimu huu wa sikukuu za Xmas na Mwaka mpya.

Ratiba nzima ya maonyesho yake itakuwa kama ifuatavyo kama yalivyotumwa katika blog hii ya Taarabu Zetu:-

24/12/2013 MKESHA WA XMASS TUTAKUWA EQUATOR GRILL- MTONI PAMOJA NA MALKIA HADIJA KOPA NA BAIKOKO KIINGILIO 5000/= TU 

XMASS TUTAKUWA MATWA PUB - KIGAMBONI SAMBAMBA NA KHANGA MOJA KIINGILIO 5000/= 

BOXINGDAY TUTAKUWA MASHUJAA PUB -  VINGUNGUTI PAMOJA NA MAMA WA MAJANGA SNURA KIINGILIO 5000/= 
KARIBUNI KWA SAPOTI YENU MJE MUONJE NA NYIMBO MPYA KABISA KAMA (MUMEO KATAKA MWENYEWE).

MKESHA WA MWAKA MPYA 31/12/2013 TUTAKUWA KATIKA UFUNGUZI WA NELLY EXCUTIVE MOTEL - KINYEREZI NA MWAKA MPYA 1/1/2014 TUTAKUWA BALLDANCER PUB - CHAMAZI.

KATIKA KUWAFIKISHIA BURUDANI WAPENZI WA MAENEO YOTE SERA ZETU HATUBAGUI WAPENZI TUNAWAFIKIA POPOTE WALIPO.

Hiyo ndo Ratiba nzima, Kwa burudani zaidi wafuate G5 Modern Taarabu.

Friday, December 13, 2013

TWAHA WA DAR MODERN APIGWA MASHAUZI CLASSIC...

  Muimbaji wa kutegemewa wa bendi ya taarabu ya Dar Modern Taarabu, Twaha Mavoko jana katika onyesho la bendi ya Mashauzi Classic alipata kichapo toka kwa madada wa mjini kutokana na kupishana lugha kulikopelekea kadhia au dhahama hiyo. 


Twahaa alikwenda Mashauzi kutembea kama ilivyo utaratibu kwa wasanii kutembeleana katika show mbalimbali. lakini wakati show ikiendelea Twaha alionekana kurushiana maneno yaliyopelekea kushikana maungoni. na kwavile Twaha alikuwa peke yake na wale wanawake walikuwa wengi walimpiga na kumchana sikio. 
Mwandishi wa habari hizi hakuweza kufanikiwa kuongea na Twaha kutokana na fujo hiyo..


Wednesday, December 11, 2013

MATUSI YAMEZIDI KWENYE TAARABU...

Bendi ntingi za taarabu nchini zimedaiwa kuimba matusi katika nyimbo zao.
Blog ya taarabuzetu.blogspot.com imepokea malalamiko kadhaa toka kwa mashabiki wa mziki huu wengine wakitoa dukuduku zao katika page mbalimbali za facebook.

Wengi wamelalamikia nyimbo kuwa na mashairi makali sana na matusi yasiyofichika kwa mtu anayejua vyema kiswahili, na wengine kudai kuwa wengi wa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimbana wenyewe tu badala ya kuleta burudani ya mashairi mazuri na matamu kama zilivyo nyimbo za waimbaji wa zamani.

Hapa ni baadhi ya msg za wadau:-



AbbaMouk J kiukweli bila upendeleo wala chuki! Funga kazi nyimbo zao hazina mahudhui ya mziki wa taarab! kunanyimbo waliamba cjui nan machupa ndg yake rahma machupa! watu wengi waliokua wakiuona kwny tv waliuponda na kusema kama taarab zmeanza kua hv bas hata kwenyenyumba yng hazitoingia nakumbuka mara ya kwanza nmeuona nlikua npo singida sasa tulikuwa kwa mwenyeji wetu ndy ulirushwa ktk kipindi cha #Hawa_Hassan cha I T V,ukija kwa huo nzi wa kijani leo hii nlikua nachat na mtu alikua akiniuliza khs mambo hayo hayo ya mziki wa taarab akaniuliza hv umeusikia wimbo wa nzi wa kijani? nkamwambia bado kwahiyo hata huujui hata mashair yake? nkamwambia sijabahatika kuusikia akanambia sijapenda mashair wala uimbaj wao sikuweza kumuunga mkono cz sijawah kuusikia so wasanii wanatakiwa wanapoumiza vchwa vyao kutunga mashairi wajaribu kuweka chuki zao pembeni na kutumia mda wa ziada kujaribu kuchambua ni matukio yep yanaendana na jamii hata km unamjibu mpinzani wako lkn maudhui yasitoke nje ya kile ulichokikusudia.

Tende Mikidadi Sheshi Huo Wimbo Wa Inzi Wa Kijani Cjausikia Bado Lkn Kila Aliewahi Kuusikia Anasema Haufai,,Sasa Jiulize Kwanini Kila Mtu Anasema Haufai ?Unajua Vijembe Vipo Kwenye Taarab Lkn Visiwe Live Au Uijibu Nyimbo Ya Mtu Kiasi Hata Mtoto Akiusikia Anajua Umemjibu Fulani,,Binafsi Sipendi Nyimbo Za Aina Hiyo,,Halaf Zamani Ilikua Ushabiki Wa Band Lakini Siku Hizi Msanii Akishea Bwana Na Msani Mwenzie Kesho Kamtolea Nyimbo,,Ndomana Kuna Msemo Mtaani Kuwa Taarab Ni Mziki Wa Uswahilini,,Umejaa Umbea Na Vijembe Japo Si Kweli Hivyo Watunzi Mjiangalie ,Hatutaki Kuimbiwa Mambo Yenu Binafsi ,Tunataka Maudhui Yanayogusa Kila Mtu .

Amin Salmin Sheshi beshi ushairi wa tembe tumepishana sana wake ndio una matusi ya nguoni,ushairi wangu kwa nyimbo za mipasho huwa na pasha na kazi ya mipasho ni kupasha upashike ila hakuna matusi kwa mfano,Naona umepagawa,wenda mbio kila uchao,kiwewe kitakuuwa,sina wasi wasi mwenzio,hilo lako la rohoni daima lita kukerekata,kosa sio langu mm,mumeo ndotoni kunitaja,huna bizi we mzushi,is wa hamsini wala mia,hayo kwangu matapishi, ww unayojivuni,Ukiangalia kwa undani huo ni mpasho na sio nyimo ya tauhidi.

Sheshi Beshi Amin swadakta temba anatumia matusi na wewe mipasho yako iko live ndio nikasema mbinu ya tafsida kwenu ipo chini, huyu hajui ku2mia maneno mbadala ya visawe na wewe ku2mia mafumbo pia hujui, ila mm cna tatizo nasema tena hiyo ni feedback tu.

Tende Mikidadi Tatizo Baadhi Ya Watunzi Wanatunga Nyimbo Wakiwa Na Hasira Basi Hapo Hapo Anashika Kalam Na Kuaza Kuchamba Maana Si Kutunga Tena ,,Iko Cku Mtu Ataimba We Ms**ng Koma Na Mie,,Nadhani Hapo Serikali Itatangaza Kupiga Marufuku Muziki Wa Taarab Na Tabid Sasa Watu Wahamie Dansini Au Kuigiza Movie,,Ila Jamani Mi Nalia Na Mashairi Makali Yanini ?Halaf Kila Mtu Anajua Kabisa Kaimbwa Mtu Fulani,,Mbona Majanga ? 

Hizi ni baadhi ya Comment za watu wakiongelea mashairi ya Taarabu...

Wewe kama mdau unalizungumziaje hili suala la matusi na Vijembe vya waziwazi na kuwekeana mabifu!? 

T MOTO haina mpango wa kujibu wimbo wa Sitaki shari...

Jokha Kassim
Mkurugenzi wa T Moto Amin Salmin amesema T Moto haina mpango wa kuijibu nyimbo ya Sitaki Shari.

Salmin aliyasema haya kwa kusema:-
Kama nilivyo ahidi kutegua kitendawili, T MOTO kama T MOTO haina mpango wa kujibu wimbo wa Sitaki shari kwani kiwango chake kiko chini mno mbele ya Domo la Udaku,

Kwamaana hiyo JOKHA KASSIM ATATOKA NA NYIMBO YENYE KISA CHA KWELI YALIOMKUTA NA JINA LA NYIMBO HIYO NI "KUNA MUNGU NA SIO MIUNGU",
Yanini unaitaka roho yangu ,kikifa utapata faida gani, wewe hauna urithi kwangu kukeni wala kiumeni,

Hayo ni maneno ya Mkurugenzi Amin yakiwa na majigambo ya kujiamini.
Anawaomba mashabiki kusubiri nyimbo na wajribu kuringanisha kama kutakuwa na nyimbo zaidi ya hii...!!