TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 31, 2013

HASNA JUMA "MASAUTI"... KUTOKA MKUBWA NA WANAWE MPAKA G5 MODERN TAARABU.

Hasna Juma (Masauti).
Tasnia ya Taarabu imekuwa ikipanuka kila kukicha na ndio maana miaka ya hivi karibu tumekuwa tukishuhudia wasanii kadhaa wa bongo fleva wakihamia huko. 
Mfano halisi wa haya niyasemayo ni Hammer Q, Babu Ayubu, Mrisho Rajabu "B.S.S.", Abubakary Mzuri na wengineo. 

Hasna Juma "Masauti" ni jina lililozoeleka katika Bongo fleva hasa katika kambi ya mkubwa Fella pale TMK, lakini leo hii ukienda Ikweta Grill utamkuta akiwa na kundi zima la G5 Modern Taarab akifanya mazoezi na wenzake. 

Hasna ameshawahi kutoa wimbo katika Bongo fleva na kutamba sana tu!.Wimbo uliitwa "Smile akimshirikisha Young Fanny".

Thabit Abdul sasa hii njaa...!!!

Huyu ndio Thabit Abdul. Director, Mtunzi wa Mashairi, Producer, Mpiga Kinanda mahili, Mcharaza gitaa na na naa.....
Hapa akirekebisha shairi wakati akitengeneza nyimbo..
Thabit Abdul alikutwa na mwandishi wa mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com akitengeneza nyimbo huku akifanya kila kitu yeye mwenyewe kwa wakati mmoja!!. hapo anapiga Gitaa, Kinanda, Mashairi anarekebisha hapohapo pamoja na kumrekebisha msanii aliyekuwa akirekodi nyimbo yake. Kweli U-Director kazi... Hongera sana mkubwa...!!



DADA ZANGU WAIMBAJI WA TAARABU USWAZI KWETU CHOO CHA GHOROFA MTAWEZA KUPANDA NA HAYO MAGAUNI YENU...!!!? MAJANGA...!!!!


Tuesday, July 30, 2013

MATUKIO: KING'S WAKIREKODI NYIMBO ZAO TATU (3) LEO TAREHE 30/07/2013

Hanifa Maulid, Amina Mnyalu, Hanifa Juma wakiitikia wimbo wa Salha "No Discussion".
 Bendi ya King's Modern Taarabu, leo hii imefanikiwa kurekodi nyimbo zake tatu (3).
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwepo kwenye Studio wakati wa kurekodi, Mkurugenzi wa Bendi Mr Hamis Majaliwa alizitaja nyimbo hizo ni:- 
1. Nimechoka na kashfa zenu - Muimbaji Aisha Othmani Vuvuzela, Kinanda - Omary Kisila na Maneno Keyboard, Solo - Mfaume Masuku na Bass - Silva Mundele.
2. No Discussion - Muimbaji Salha Abdallah. Kinanda - Mzaka Nundu na Ibrahim Kamongo, Solo - Mfaume Masuku, Bass - Silva Mundele.
3. Sikuumbwa Mnisimange iliyoimbwa na chipukizi Sophia Yahya. Kinanda - Mzaka Nundu na Ibrahim Kamongo, Solo na Bass - Silva Mundele.
Nyimbo zote zimerekodiwa katika Studio ya Sound Crafters chini ya Producer Enrico.  
 
Salha wa Hammer Q.
Mr Hamis Majaliwa alisema huo ni ujio mpya wa King's, na akaomba wapenzi wa Taarabu wajiandae kupata vibao vizuri na murua kabisa. 

King's ni miongoni mwa bendi zilizoingia katika shindano la Kilimanjaro Music Awards na ilishindania bendi bora ya Taarabu lakini haikubahatika kushinda, ila wamejipanga vyema kuleta ushindani na ameahidi lazima mwakani wafanye vyema zaidi..

Picha mbalimbali King's wakiwa wanarekodi...

Hassan Ally na Aisha Vuvuzela akipiga pozz...!!
Maneno na Omary Kisila wakipapasa Vinanda.
Wapiga Gitaa wa ukweli Mfaume Masuku na Silva Mundele.
Mwa4 wa EATV akiwa na wasanii wa King's ndani ya studio ya Sound Clafters.
Omary Kisilaakisababisha...
Silva Mundele akiwa na Mrisho Rajabu.
Sophia Yahya akiimba nyimbo ya "Sikuumbwa Mnisimange"...
Aisha Vuvuzela akiimba nyimbo ya "Nimechoka na Kashfa zenu".
Mfaume Masuku akikung'uta Gitaa la Solo...
Omary Kisila akifanya yake...


Download Nyimbo mpya kabisa ya Five Stars Modern Taarabu - Habari ya Mjini. Mwimbaji Mwamvita Shaibu...

Mwamvita Shaibu - Habari ya Mjini.

Nyimbo:- Nipo kamili nimejipanga - Nyawana Matashtiti.


BENDI YA G5 MODERN IKIWA KAMBINI IKIFANYA MAZOEZI KWA AJILI YA SIKUKUU ZA IDD...

Wasanii wa G5 wakiwa Mazoezini.
Wanamuziki wa kundi la G5 Modern Taarabu wapo kwenye mazoezi makali wakijiandaa kwa Show mbalimbali watakazozifanya katika sikukuu ya Idd baada ya mfungo wa Ramadhani.

Mwandishi wa mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com alitembelea mazoezi hayo na kupata ratiba kamili ya Show...!!

Ratiba kamili ni hii:-

*** Idd Mosi - Watakuwa IKWETA GRILL - Mtoni kwa Azizi Ally.
*** Idd Pili - Watakuwa SIHA RESORT - Kitunda.
*** Idd Tatu - Watakuwa KALEMBO HALL - Buguruni.

Wapenzi wote wa Taarabu mnaombwa kuhudhulia ili kufurahia vitu tulivyoviandaa kwa ajili yenu. Alisema Mmoja wa wasanii Samira Rajabu.

Shaibu Bass akifanya mambo yake...
Ni katika Mazoezi.


AISHA KULELE ATHIBITISHA KUIHAMA NEW ZANZIBAR...

Aisha Kulele
 Muimbaji wakutegemewa wa New Zanzibar Stars, Aisha Kulele amesema kwamba yeye kwa sasa ni msanii halali kabisa wa G5 Modern Taarabu, na si msanii wa New Zanzibar Stars tena. 

Aisha aliyasema hayo baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari hizi kwamba inakuwaje anaonekana katika mazoezi ya G5 Modern wakati yeye ni msanii wa New Zanzibar? Akilithibitisha hilo Mkurugenzi mkuu wa G5 Modern, Hamisi Slim alisema kwamba ni kweli Aisha Kulele kwa sasa tupo nae na pia nina mipango ya kuchukuwa wasanii wengine wenye majina makubwa katika Taarabu nchini, uwezo huo ninao na hakuna shida, alimaliza.

HEEH!! AISHA MASANJA WA T MOTO, KULIKONI TENA, MBONA UPO G5?

Aisha Masanja wa T. Moto
 Muimbaji Aisha Masanja ambae kiuhalisia yupo T MOTTO Modern Taarabu ameonekana akifanya mazoezi na bendi nyingine ya G5 Modern Taarabu, mwandishi wa habari hizi alipotaka kujua imekuwaje tena mpaka anafanya mazoezi na G5? au tayari yeye ni msanii wa bendi hiyo au anakula kotekote? alikataa na kusema kwamba yeye mpaka sasa bado ni msanii wa T MOTTO ila hapa G5 yupo yupo tu na kama atapewa wimbo kuimba yupo tayari ataimba, alipoulizwa je Mkurugenzi wako Amin Salmin anajua kama upo hapa G5? alisema hajui juu ya hilo. Mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com unamuomba Aisha kuweka wazi!

MUSSA KIJOTI ASIMAMISHWA KAZI 5 STAR'S MODERN TAARABU!...

Mussa Kijoti
 Muimbaji Mussa Kijoti wa 5 Stars Modern Taarabu, amesimamishwa kuendelea kufanya kazi katika bendi hiyo kwa muda usiojulikana. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kiongozi mmoja wa bendi hiyo alisema "Mussa Kijoti amesimamishwa bendi na uongozi na ni mpaka tutakapo kaa kama uongozi kwa pamoja kujadili suala lake ila kwa sasa ataendelea kukaa pembeni". 

Alipotafutwa kwa njia ya simu msanii huyo alikanusha kusimamishwa kwake na kusema kwamba hana taarifa na hata uongozi haujampa barua ya kusimamishwa kwake, siku za hivi karibu msanii huyo ameonekana katika bendi ya G5 Modern Taarabu!

Monday, July 29, 2013

WASANII KUMI BORA CHIPUKIZI WALIOFANYA VIZURI 2008 MPAKA 2013!!!

Muziki wa Taarabu ni muziki unaopendwa na wengi hususani Ukanda huu wa Pwani. Kila kukicha Wasanii mbalimbali chipukizi wamekuwa wakijiingiza na kufanikiwa kufanya vizuri.

Yafuatayo ni majina ya Wasanii kumi bora wanaofanya vizuri kwa sasa kupitia vituo mbalimbali vya redio kama inavyoletwa kwenu na Mtandao Makini wa taarabuzetu.blogspot.com.

1. Mwanahawa Ally. "Chipolopolo”
Alipotoka Victoria na kwenda Dar Moern Taarabu walimdharau na kumbeza, lakini hakukata Tamaa alipitia Supershine na kudondokea King’s Modern Taarabu. Hapo ndipo Nyota yake ikaanza kung’aa na kufanikiwa kurekodi nyimbo 2 Matata sana “Mchumia Juani” na “Dunia Duara”
Huyo ndio Chipolopolo anashika namba moja!

2. Nyawana Fundikila.
Mwanzoni alikuwa Solo-Artist, akafanikiwa kutoa wimbo wake uitwa “Nipo kamili nimejipanga”. Wimbo ambao ulileta matatizo makubwa baina yake na Isha Mashauzi. Hkuishia hapo akatoa wimbo mwingine uitwa “Umesharoga wangapi”. Ndipo King’s walipogundua uwezo wake na kumjumuisha katika bendi, hata hivyo hakukaa sana akatimkia T. Motto Modern Taarab ambapo alitoa wimbo mmoja uitwa “Behind the Scene” Utunzi wake mwenyewe. Huyo ndio Nyawana anshika namba mbili!

3. Hanifa Maulidi.  "Jike la Chui"
Huyu ana safari ndefu ya muziki mpaka kufikia mafanikio. Kwa kifupi amepitia Super Shine, Melody, Coast, Mashauzi mpaka King’s alipofanikiwa kutoa wimbo mwingine nje ya Bendi uitwa “Makavu live” unaotamba sana katika vituo vya redio sasa hivi. Huyo ni Hanifa Maulidi ukipenda muite Jike la Chui anashika nafasi ya Tatu!

4. Aisha Othman. "Vuvuzela”
Mwanzoni wakati yupo Dar Modern na Director wake Mlidu Ally kumuita Aisha Vuvuzela alikuwa akichukia sana. Lakini sasa limekuwa ni jina maarufu ambalo linamtambulisha katika sanaa. Vuvuzela ana sauti nzuri sana kwenye kuimba. Alipotoka Dar Modern alijiunga na Mashauzi Classic ambapo hakukaa sana na sasa hivi ni msanii wa King’s Modern Taarabu. Hivi karibuni anatarajia kutoa wimbo mpya kabisa akiwa King’s Modern Taarabu. Huyo ndie Aisha Vuvuzela anashika nafasi ya nne!

5. Abdul Malick “Handsome wa Mashauzi”
Ukimuona hutaweza kuamini kwamba aweza kua na sauti nzuri kiasi kile. Mwanzoni alipokuwa King’s Director wake Kijoka hakuwa akimpa kipaumbele sana akaenda zake Coast kwa Omary Tego ambapo hakukaa sana akahamia Mashauzi Classic na kutoa wimbo “Sintosahau kwa yaliyonikuta”. Huyo ndio Abdul Malick ukipenda muite Handsome wa Mashauzi, yeye anashika nafasi ya tano!

6. Kibibi Yahaya.
Ukimuuliza nini siri ya mafanikio yako ataanza kwa kucheka halafu atakujibu ni mazoezi na nidhamu pindi ninapokuwa kazini. Kibibi alianzia Bendi ya Supershine, alipoona ameiva kidogo akaamua kwenda Coast Modern Taarabu kwa Omary Tego ambapo alifanikiwa kurekodi wimbo mmoja na kuhamia Bendi ya King’s ambapo napo amefanikiwa kurekodi wimbo mmoja pia. Kibibi ni msanii anaetegemewa sana na uongozi wa King’s kwa sasa. Huyo ndio Kibibi anashika nafasi ya sita!

7. Salha Abdallah wa Hammer Q
Wakati anaanza kuimba mashabiki walishindwa kumtofautisha kati yake na marehemu Mariam Hamisi kipindi hicho. Kiukweli wamefanana sana! Salha alianzia Dar Modern Taarab lakini mwezi uliopita amejiunga na King’s Modern Taarabu ambao chini ya Mkurugenzi wake Hamisi Majaliwa. Salha kwa sasa ana wimbo mpya ndani ya King’s Modern Taarabu ambao anasema ni mapema sana kuutambulisha. Huyo ndio Salha Abdallah mke halali wa Hammer Q. Yeye anashika nafasi ya 7!

8. Fatuma Mcharuko. Jahazi Modern Taarabu
Anapokuwa stejini anajituma sana ili kuhamasisha wapenzi na mashabiki. Katika albam iliyopita ya Jahazi, Fatuma alipewa wimbo mmoja kuimba ambao aliutendea haki sana! wimbo huo ambao mashabiki wameubadilisha
jina na sasa wanauita “Umenipandisha Mizuka Tawile! Tawile! Tawile! ni moto wa kuotea mbali na
kila unapopigwa ni lazima watu wanyanyuke na kucheza. Huyo ndio Fatuma Mcharuko Msanii toka Jahazi
Modern Taarab anashika nafasi ya nane!

9. Saida Mashauzi.
Hana muda mrefu katika muziki wa Taarabu hapa nchini. Ila ni mdogo wake Isha Mashauzi Mkurugenzi wa
Mashauzi Classic. Ana uwezo mkubwa wa kuimba kubadilisha sauti yake kulinga na wimbo husika anaoimba wakati huo. Huyo ndio Saida Mashauzi anashika nafasi ya tisa!

10. Kapteni Temba.
Kwa sasa ndio mkurugenzi wa Fungakazi Modern Taarabu, yenye mskani yake Kigamboni Dar. Alianza kama Solo-Artist kwa kutoa nyimbo zake kadhaa, mpaka pale alipofanikiwa kufungua bendi yake ya Funga kazi.
Kw muda huu yupo studio na kundi zima la Bendi yake wakirekodi Albamu nyingine tena. Huyo ndio Kapteni Temba Mchaga wa kwanza kuimba Taarabu hapa Tanzania.

Sunday, July 28, 2013

KING'S MODERN TAARABU WAKIWA MAZOEZINI, WAKIJIANDAA NA SHOW ZA IDD ZITAKAZOFANYIKA MKOANI MOROGORO......

King's Modern Taarabu wakiwa mazoezini...
 Katika harakati za shamrashamra za Idd, King's Modern Taarabu wanajifua vilivyo ili kuja kutoa burudani za nguvu na za uhakika kabisa.


Mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com alitembelea mazozini na kuzungumza na mkurugenzi wa King's na kutoa ratiba nzima ya IDD kama ifuatavyo:-

*** IDD MOSI - MIKUMI
*** IDD PILI - KILOMBERO
*** IDD TATU - KILOSA

Sophia Yahya.
Aisha Vuvuzela,
Amina Mnyalu.
Mzee mzima Doglas, kasimama imara...
Hadija Omary. Muimbaji machachari wa King's.
Hassan Ally, kama kawaida yake makamuzi yaleyale...
Kibibi Yahya.
Mzaka Nundu. Kinanda kinapapaswa kama kawa...

Salha wa Hammer Q ndani ya Nyumba...
Sophia Yahya (Kushoto) na Hanifa Maulid. Maandalizi ya ukweli...

5 STARS WAKIWA MAZOEZINI WAKIJIANDAA NA SHOW ZA IDD...

Fitina-Mpogo
Kundi la Taarabu la 5Stars Modern Taarabu lipo kambini likijifua vilivyo kwa ajili ya maandalizi ya Albam yao mpya ikiwa ni pamoja na maandalizi ya show za Idd.

Mtandao huu umeongea na mmoja wa viongozi na kueleza namna ya ratiba nzima ya show zao za Idd ilivyo:-

*** IDD MOSI - PUGU
*** IDD PILI - ROSH GARDEN - MWANDEGE PWANI
*** IDD TATU - KIBITI PWANI

"Show itakuwa kali sana, wakazi wa huko mkae tiyari kwa burudani nzuri na ya kupendeza, tunakuja kukonga nyoyo zenu".

Jasmin Akili (Kushoto) na Mariam BSS, Mazoezini....
Juma Mkina akipapasa Kinanda vilivyo.
Jumanne Ulaya kasimama kwenye Solo.
Maua Tego
Mwanvita Shaiba akiimba kwa hisia kali...
Thabit Abdul... Kinanda kinaongea hapo...
Zena Mohamed akishiriki katika kuimba, sauti tamutamu za 5Stars Modern Taarabu...