TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, October 30, 2013

FATMA YASINI NAE AIKIMBIA KING'S MODERN TAARABU...

Fatma Yasin
Wimbi la wasanii kuondoka ndani ya bendi ya Kings Modern Taarabu limeendelea baada ya msaani mwingine Fatma Yasini nae kuondoka na kujiunga katika bendi mpya iitwayo Rocky City Modern Taarabu. 

Fatma Yasini ndani ya bendi ya Kings Modern Taarabu ameimba wimbo uitwao "Sikuogopi nakupotezea" utunzi wake Director Kijoka.  

Akiongea na mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com Fatma alisema: "Unajua ndugu mwandishi, mimi ni msanii na mara nyingi huwa naangalia sehemu ninayothaminiwa na ndio maana nimekuja hapa Rocky City Modern Taarabu kwani Mkurugenzi wake ameonesha kunijari zaidi" alisema.

Tuesday, October 29, 2013

AISHA VUVUZELA AIACHA SOLEMBA KING'S MODERN TAARABU...


Msanii muimbaji anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki wa taarabu Aisha Othman "Vuvuzela" ameiacha solemba bendi ya King's na kutimkia 5Stars Modern Taarabu.

Taarabuzetu, tuliandika kwa mara ya kwanza juu ya taarifa juu ya Aisha Vuvuzela kwenda katika kambi ya 5 Stars kusaini mkataba na hadi muda ambao alikwenda tuliandika kwa ushahidi kabisa, lakini baadhi ya blog na media zilikanusha na kusema habari hizo sio za kweli. 

Leo hii mtandao wako makini wa taarabuzetu.blogspot.com unakuletea hitimisho la sakata zima lilivyo malizika. 

Mpaka sasa VUVUZELA ni msanii halali kabisa wa bendi ya 5 Stars na amesaini kuitumikia bendi hiyo kwa miaka miwili.

Taarabuzetu ilimtafuta mkurugenzi wa 5 Stars Mr Sharks ili kuthibitisha hili.
 Akiongea na mwandishi wetu, Mkurugenzi huyo alisema:- 
"Napenda kuchukua nafasi hii kuwathibitishia wananchi wote kwamba Aisha Othman "Vuvuzela" ni msanii wangu halali na nimemsainisha kwa muda wa miaka miwili, alipokuja aliniambia kwamba hana mkataba na bendi yake ya awali ya Kings ndipo nilipo msainisha kuitumikia bendi yangu, na muda huu tunavyo zungumza VUVUZELA yupo katika bendi yangu na ni msanii wangu kihalali". 

Alipopigiwa simu mkurugenzi wa bendi ya Kings Modern Taarabu kuulizwa juu ya kuondoka kwa msanii wake huyo, alijibu.. "Nina mkataba na VUVUZELA na nitachukua hatua kali dhidi yake ili kukomesha hili".

YUSUPH TEGO AITOSA 5 STARS NA KUTIMKIA MUSCAT..

Mpiga kinanda namba mbili wa bendi ya 5 Stars Modern Taarabu Yusuph Tego ametimkia Muscat kufanya muziki wa Hotel pasipo kupata ruhusa ya uongozi wake wa 5 Stars. 

Mwandishi wa habari hizi alimtafuta kwa simu mkurugenzi mkuu wa 5 Stars Mr Shark's ambae alisema Yusuph Tego ameomba ruhusa ya mwezi mmoja katika bendi hiyo na amesema kuwa anaenda kwao mara moja kusalimia, sisi kama uongozi hatuna taarifa za yeye kwenda Muscat ila nitafuatilia kwa karibu. 

Taarabu Zetu ilipopiga simu ya Yusuph haikupatikana kwa siku tatu mfululizo khali inayoonekana yupo mbali. 
Hawa ndio wasanii..

Saturday, October 26, 2013

KHADIJA KOPA KUANZA SHOW YA KWANZA MWANZA...

Malkia wa Mipasho TZ. Khadija O. Kopa.
Malkia wa mipasho Tanzania Bibie Khadija Omary Kopa! anatarajia kufanya show ya kwanza kabisa tokea atoke kwenye EDA ya kufiwa na mumewe. 

Taaribu tulizonazo Show hiyo ambayo imepangwa itafanyika tarehe 31 mwezi huu wa 10 ndani ya ukumbi wa VILLA PARK jijini Mwanza. 

Malkia huyo ameahidi kushusha burudani ya nguvu kwa mashabiki wake ambao walikuwa wamemkosa kwa muda mrefu sana. 

Baada ya kumaliza show hiyo, siku ya tarehe 3 mwezi wa 11 Khadija anatarajia kufanya show maalum kwa ajiri yake na wakazi wa Dar kwa ujumla ndani ya ukumbi wa DAR LIVE, hapo pia kutapita harambee kwa ajiri yake Khadija

Friday, October 25, 2013

HASSAN VOCHA NA HASNA MASAUTI, WAIBUKIA SUPERSHINE.

Hassan Vocha na Hasna Masauti
Waimbaji nyota wa bendi ya G5 Modern Taarabu ambao wapo katika mgomo wa kimaslahi kwa sasa, Hassan Vocha na Hasna Masauti wameibukia Supershine Modern Taarab. 

Waimbaji hawa nyota jana walionekana ndani ya Lango la jiji Magomeni katika show ya Supershine Modern Taarabu na kuimba nyimbo 2. Hasna Masauti akiimba "Huliwezi Bifu" na Hassan Vocha yeye akiimba "Mazoea Yanatabu" jambo lilillotafsiriwa na wapenzi kama ni dongo kwa Boss wao kwa kile wanachodai waimbaji hao. 

Alisikika kiongozi mmoja wa Supershine akisema atafanya mazungumzo haraka na vijana hao ili kujua kama wana mkataba pale G5 au hawana ili waweze kuwachukua kuongeza nguvu katika kikosi chao.

DOWNLOAD:- Nyimbo tatu (3) mpya kali kabisa za 5Star Modern Taarabu...!!!!!


MWIMBAJI - Hammer Q 
BENDI:- 5Star Modern Taarabu 






MWIMBAJI:- Maua Tego 
BENDI:- 5Star Modern Taarabu 






MWIMBAJI:- Zena Mohamedi 
BENDI:- 5Star Modern Taarabu

Tuesday, October 22, 2013

"BAD NEWS...":- Fundi mitambo wa Coast Modern Taarabu Afariki Dunia...

Wasanii wa Coast Modern Taarabu.
Kwa taarifa fupi tulizozipata ni kwamba, Fundi mitambo wa Coast Modern Taarabu anayeitwa kwa jina la Isiaka au maalufu Bamchawi afariki dunia jana jumatatu.

Kwa taarifa zaidi tutakuletea hapa tunazidi kufuatilia zaidi.

Sunday, October 20, 2013

NASSORO HUSSEIN CHOLLO NAE ATIMKIA MUSCAT..



Lile wimbi la wasanii wa taarabu kwenda Muscat kufanya shughuli za muziki limeendelea kushamili baada ya muimbaji wa Zanzibar One na T Motto Nassoro Hussein maarufu kama "Chollo" nae kuelekea huko. 

Chollo ambae alipokuwa Zanzibar One aliimba wimbo uitwao "Nastaleheshwa" na alipokuwa T Motto aliimba wimbo uitwao "Wewe sio daktari wa mapenzi". 

Kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na wimbi zito la wasanii wa taarabu kuondoka nchini na kwenda Oman kufanya shughuli za muziki wa Hotel, wiki mbili zilizopita Mgeni Kisoda na Amour Salehe "Zungu" nao walipanda ndege kuelekea huko pia.

Saturday, October 19, 2013

SHOW YA HADIJA KOPA NDANI YA DAR LIVE YASOGEZWA MBELE..

Hadija Kopa (Malkia wa Mipasho).
Hadija Omary Kopa, au malkia wa mipasho nchini Tanzania, ilibidi afanye show siku ya tarehe 19 mwezi huu ndani ya ukumbi wa DAR LIVE lakini kutokana na khali yake na maandalizi mengine makubwa imelazimika kusogezwa mbele mpaka tarehe 3 ya mwezi wa 11 na siku hiyo pamoja na burudani toka kwa malkia huyo lakini pia utapitishwa mchango kwa ajiri ya malkia huyo ili pesa itakayopatikana aweze kuanzia maisha yake mapya baada ya kutoka kufiwa na mumewe. 

Pia Kopa ana wimbo mpya kabisa uitwao "LADY WITH A COMFIDANCE" ambao atautoa hivi karibuni.

Thursday, October 17, 2013

AMOUR SALEHE ZUNGU AITOSA G5 MODERN TAARABU.

Amour Salehe a.k.a. Zungu.
Yule mpiga kinanda alietangazwa kwa mbwembwe na majigambo mengi na bendi ya G5 kwamba wamemsainisha mkataba akitokea Oman amewaacha solemba na kutimka zake tena Oman kuendelea na maisha yake ya kimuziki. 

Taarabu zetu ilipata nyeti hizo: "Mimi nilijua tu zungu lazima awalize G5, yule si mkaaji hapa nchini" alisikika shabiki mmoja wa bendi hiyo katika Bonanza la kila jumapili ambalo huwa linafanyika pale katika ukumbi wa ikweta mtoni kwa azizi ally. 

Siku kadhaa zilizopita mkurugenzi wa G5 Modern Taarabu Hamisi Slim alijinasibu kwamba amemchukua Zungu ili kuimalisha kikosi chake, lakini leo Zungu hayupo tena. 
Hao ndio wasanii wa Taarabu...!.

Tuesday, October 15, 2013

BI AFUA SULEIMAN:- SIWAJUI HAO KUMEKUCHA MODERN TAARABU.

Bi Afua Suleiman.
Kila kukicha katika tasnia ya taarabu kumekuwa kukiibuka bendi mpya mbalimbali na yote ni katika kujitafutia ridhiki na kutoa burudani kwa wapenzi, Lakini kumeibuka kamtindo kadogo kabaya sana! hizi bendi zinazoanzishwa zimekuwa zikitumia majina makubwa ya wasanii katika matangazo yao kwamba watakuwepo au huyo msaani ni mmiliki wa bendi hiyo jambo ambalo si kweli. 

Kuna hii bendi inaitwa Kumekucha Modern Taarabu "Masupastaa wa town" wameandika katika matangazo yao kuwa bendi hii ipo chini ya BI AFUA SULEIMAN jambo ambalo sikweli kwani Bibi huyu amekana hawafaham kabisa.

Monday, October 14, 2013

Kwenye Azimio la Arusha, Mwalimu Nyerere alisema haya kuhusu Wanawake:

"Ingefaa kuwauliza wakulima wetu, hasa wanaume, ni saa ngapi za juma na majuma mangapi kwa mwaka wanafanya kazi. Wengi hawafanyi kazi hata kwa nusu ya saa ambazo mpokea mshahara anafanya. Ukweli ni kuwa kwenye vijiji wanawake wanafanya kazi ngumu sana. Nyakati nyingine wanafanya kazi kwa saa 12 au 14 kwa siku. Wanafanya kazi hata siku za Jumapili na za sikukuu. Wanawake wanaoishi vijijini wanafanya kazi ngumu kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania. Lakini wanaume wanaoishi vijijini (na baadhi ya wanawake mijini) wako likizo kwa nusu ya maisha yao. Nguvu ya mamilioni ya wanaume kwenye vijiji na maelfu ya wanawake mijini ambazo kwa sasa zinapotezwa kwenye udaku, dansi na kunywa, ni hazina kubwa ya nchi ambayo inaweza kuchangia maendeleo ya nchi yetu zaidi ya ambavyo tunaweza kupata kutoka mataifa tajiri."

Takwimu za sasa zinaonyesha, wakulima wadogo wanawake wanazalisha takribani asilimia sitini (60%) ya chakula chote tunachotumia, lakini ni asilimia moja (1%) tu ndio wanaomiliki ardhi.

Unamuenzi vipi Baba wa Taifa..??

5 STAR'S MODERN TAARAB, YAIWEKA ALBAM YA UKURASA MPYA KIDEONI..

Ally J.
Bendi ya 5 Star's imefanikiwa kumaliza kufanya shooting nyimbo zote zilizopo katika Albam yae ya Ukurasa Mpya!. 

Akizungumza na blog hii Ally J alisema tunamshukuru mungu tumemaliza kufanya video na kazi iliyobaki ni kwa wapenzi wetu kununua video zetu original na sio feki ili kutusaidia sisi wasanii. 

Nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni:- 
Ukurasa Mpya - Ally J, 
Muomba mungu hatoki mtupu - Bi Mwanahawa Ally, 
Mwenye subira hubarikiwa - Sabaha Salum, 
Jipange Upya - Mariam Hamdani, 
Jibu ninalo nangoja mlopoke - Mariam B.S.S 

Albam hii ni miongoni mwa albam bora kabisa katika tasnia ya muziki wa Taarabu, wapenzi wote wa taarabu wataipenda...

BAADA YA KUITOSA JAHAZI, MGENI KISODA ATIMKIA MUSCAT!.

Mgeni Kisoda.
Yule mpiga kinanda maarufu ambae takribani mwezi mmoja umepita tokea aachane na bendi ya Jahazi Modern Taarabu Mgeni Kisoda ametimkia Muscat kwenda kupiga muziki wa Hotel. 

Akizungumza na mwandishi wa blog hii rafiki wa karibu wa Mgeni Kisoda na mmiliki wa bendi ya Taarabu iitwayo "Raha Original" yenye maskani yake Magomeni Dar es Salaam "Bwana Ostaadh" alisema Mgeni ameondoka na muimbaji wa kiume aliefahamika kwa jina moja tu la Eddy pamoja na mwanamke mmoja jina halikuweza kufahamika, huko wamekwenda kupiga muziki wa Hotel, kwani hata mimi pia huwa naenda mala moja moja!.

GUSAGUSA MINI BENDI YA KAMILISHA VIDEO YA "UNAJIDODO LINAKUCHUKUCHA"..

Baadhi ya wasanii wa Gusagusa Min Band wakiongozwa na Bi Afua Suleiman B52.
Bendi ya Taarabu ya Gusagusa Min Bendi ya jijini Dar es Salaam, imekamilisha video ya wimbo wa "Una jidodo linakuchukucha" wimbo ambao umeimbwa nae Bi Afua Suleiman "B-52". 

Akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com Mmiliki wa kampuni ya "Whatever Film Production" ambayo imefanya video hiyo "Mr Mwaila" amesema huo ni mwanzo tu wakuwaletea wapenzi wa taarabu video nzuri na zenye kiwango. 

Kwa upande wa Gusagusa Min Bend wenyewe wamesema hivi karibuni wataiachia video hiyo katika Televisheni mbalimbali hapa nchini na nchi za jirani ili wapenzi wapate burudani, na pia katika Blog hii ya Taarabu Zetu itakuwepo... Stay Tuned...!!!

Sunday, October 13, 2013

MOSI SULEIMAN:- MIMI SIO MSANII WA 5 STAR'S KWA SASA..

Mosi Suleiman.
Muimbaji mahiri wa Taarabu nchini Mosi Suleiman ambae juzi tu alitambulisha wimbo wake mpya wa bongo fleva, ameuambia mtandao huu kwamba yeye kwa sasa sio msanii wa 5 Stars na hana bendi yoyote ameamua kupumzika kwanza.

Mosi suleimani alikuwa akizungumza na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com kuelezea ni kwanini yupo kimya huku mashabiki zake wakipiga simu katika chumba chetu cha habari kutaka kujua ni wapi alipo kipenzi chao Mosi Suleiman.

"Unajua ndugu mwandishi, mimi nilikuwa pale 5 Stars ila kuna tofauti flani zilijitokeza kati yangu na uongozi nikaamua kuacha bendi basi".

HAMISI SLIM, TAFADHALI USITUMIE TENA MASHAIRI YANGU.

Hemedi Omary
Muimbaji wa bendi ya Bandari Modern Taarabu ambae pia ni msanii wa TOT Hemedy Omary amevunja ukimya na kumuonya Mkurugenzi wa bendi ya G5 Modern Taarabu, Hamisi Slim Kuacha mara moja kutumia mashairi yake.

Ni mashairi ambayo walikubaliana amuuzie lakini Mkurugenzi huyo akakiuka makubaliano hayo, mashairi ambayo Hamisi Slim anatakiwa kuacha kuyatumia ni:- 
** Muungwana hagombani, 
** Mwanamke kiwango, 
** Adivertise na 
** Kidole kimemponza ng'ombe. 

 Hemedy Omary alisema kwamba kuna pesa ndogo aliyopewa na bosi huyo, yupo tayari kumrejeshea bila wasiwasi ili wamalizane kabisa!.

TETESI: AISHA VUVUZELA ASAINI 5 STARS MODERN TAARABU..

Muimbaji wa Kings, Aisha Othman (Vuvuzela).
 "Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo linakuja". 

Yule muimbaji wakutegemewa wa bendi ya Kings Modern Taarabu, Aisha Othman Vuvuzela jana jumamosi mida ya saa 10 za jioni alionekana katika kambi ya bendi ya 5 Stars Mtoni kwa Azizi Ally Dar es Salaam akiwa na viongozi wakubwa wa bendi hiyo. 

Chanzo chetu cha habari toka ndani ya bendi hiyo kilisema kwamba Vuvuzela alikuja hapa, kwanza kabisa kuusoma mkataba then akiuafiki ndipo atasaini! lakini uwezekano wa yeye kujiunga na bendi yetu ni mkubwa sana sababu amesema hana mkataba na Kings analipwa mshahara tu.

Friday, October 11, 2013

HASSAN VOCHA NA HASNA MASAUTI WAGOMA G5 MODERN TAARABU...

Hassan Vocha.
Wasanii chipukizi wanaokuja kwa kasi ya ajabu katika tasnia ya taarabu Hassan Vocha na Hasna Masauti wamegoma kuendelea kuitumikia bendi ya G5 kwa kile kinachosemekana ahadi hewa ambazo wamekuwa wakiahidiwa na mkurugenzi wao Hamisi Slim. 
Hasna Masauti.
Chanzo chetu cha habari kilichopo ndani ya kundi hilo la G5 kilisema kwamba hawa watoto tokea waje hapa toka kwa mkubwa Fellah wamekuwa wakizungushwa kupewa pesa zao jambo lililopelekea Hassan Vocha kutaka kuikimbia bendi hii na kujiunga na Kings lakini juhudi za Adam Mlamali kumshawishi zilimrudisha tena kundini, lakini kilichofanyika baada ya kurudi tena katika bendi ni zile zile ahadi hewa zisizotimilika! "Unajua mkurugenzi wetu asipokuwa makini bendi haitofanikiwa itakuwa kila siku tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele, hawa watoto hawajaja katika show kibao mpaka sasa jambo linalopelekea mashabiki na wapenzi wao kuwaulizia kila tunapokwenda kupiga show!", 

Juhudi za kumtafuta kwa simu mkurugenzi wa G5 ziligonga mwamba kwani simu yake ilikuwa haipatikani hewani. Pia tulipo mtafuta Hassan Vocha ili kuthibitisha hili simu yake ilikuwa inaita bila majibu yoyote, tunawaahidi wasomaji wetu tutafuatilia zaidi.

RAMADHAN KISOLO NI STAR WETU WA MWEZI SEPTEMBER...!!

Ramadhani Kisolo mpiga Gitaa la Solo wa Mashauzi Classic...
Katika wapiga gitaa la solo ambao wanafanya vizuri sasa hivi katika tasnia ya Taarabu nchini Tanzania basi jina la "Ramadhan Kisolo Mwana Malui" litakuwa ni miongoni. 

Kisolo ambae kwa sasa ni mpiga Gitaa la solo namba moja wa bendi ya Mashauzi Classic ameongoza kwa kushirikishwa kupiga nyimbo nyingi sana mpya za Taarabu ikiwemo katika bendi tofauti mpaka kwa wasanii mmoja mmoja yaani zingzong". 

Katika mwezi wa tisa kisolo kapigia Mashauzi Classic Albam nzima, Funga Kazi Modern Taarabu albam nzima, kapiga wimbo mpya wa Nyawana Shetani kataja jina na nyinginezo nyingi.

NDAGE NDAGE:- SUPERSHINE MODERN TAARABU NI ZAIDI YA MASHAUZI.

Mpiga Kinanda wa Supershine Modern Taarabu, Ndage Ndage.
Aliyekuwa mpiga kinanda wa bendi ya Mashauzi Classic Said Ndage Au "Ndage Ndage" Ambae kwa sasa yupo katika bendi ya Supershine Modern Taarabu amesema anafurahia maisha katika bendi yake hiyo mpya kuliko mwanzoni alivyokuwa katika bendi ya Mashauzi. 

Ndage aliyasema hayo wakati anafanya mahojiano na mwandishi wa mtandao huu, "unajua ndugu mwandishi wakati nipo pale Mashauzi nilikuwa naonekana sina thamani yoyote, lakini tokea nimekuja hapa Supershine namshukuru mungu mambo yangu mazuri sana! Mkurugenzi na Meneja wangu wananitimizia kila ninachotaka.

Thursday, October 10, 2013

MAFIA MODERN TAARABU NA V.I.P. MODERN TAARABU, NI LIPI JINA SAHIHI KWA 5 STAR'S?.

 Wasomaji wetu leo bado tunaendelea kuwaletea mchakato wa kubadilishwa kwa jina la bendi ya 5 Stars, Siku ya jana kikao kiliendelea na wajumbe wa kamati waliendelea kujadiliana ni jina lipi haswa litakuwa mrithi sahihi wa 5 Star's?.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kuna mvutano mkubwa unaendelea, baadhi ya wajumbe wanapendekeza ni bora bendi iitwe Mafia Modern Taarabu na kuna wengine wanapendekeza nibora iitwe VIP Modern Taarabu. 

Bado mvutano mkali baina yao unaendelea muafaka bado, tuendelee kusubiri.

Wednesday, October 9, 2013

TETESI:- 5 STARS MODERN TAARABU KUITWA "V.I.P. MODERN TAARABU"...!!

Baadhi ya wasanii wa 5Stars Modern Taarabu wakiwa kazini.
Siku zote unapoona mtoto anakuwa mtundu, hasikii la kuambiwa, mkorofi n.k, wazee wa zamani watakwambia mtoto jina linamzuru mbadilishe jina atatulia! na kweli unapombadilisha mtoto anakaa sawa na kila kitu kwa upande wake kinakwenda vizuri. 

Bendi ya 5 Star's ni miongoni mwa bendi zilizokuwa zikifanya vizuri katika soko la taarabu mpaka kufikia kuogopwa na zile bendi zinazojiita kongwe hapa nchini. 

Bendi hii ambayo hapo mwanzoni ilikuwa na wasanii mahiri kama Ally J, Issa Kijoti, Shebe Juma, Tizo Mgunda, Husna Mapande na wengineo, ilipata ajari mbaya sana iliyopelekea wasanii 13 kufariki. 

Baada ya hapo bendi ilianzishwa upya chini ya mkurugenzi mpya Mwandame mkazi wa Mwanza na walifanikiwa kutoa albam mbili chini ya Director Ally J lakini bado bendi ilionekana kutokubalika kwa washabiki tena kama ilivyokuwa mwanzoni, jambo hili lilimfanya mkurugenzi Mwandame kuitosa bendi hii kwani aliona anapata hasara tu ukizingatia yeye aliwekeza ili apate faida na sivinginevyo. 

Baada ya hapo bendi ilinunuliwa na mkurugenzi Shark's ambae nae hakuona manufaa yoyote ndipo bodi ilipokaa na kuamua kubadilishwa kwa jina na kuitwa "VIP MODERN TAARABU", jina hili la Vip Modern Taarabu, Inasemekana limechomoza mapema mno tofauti na ilivyopangwa kwani inaonekana baadhi ya viongozi hawana siri, mtandao wetu ulimtuma kachero wetu katika kambi hiyo na kukutana na mmoja wa viongozi wa bendi hiyo ambae alisema kwamba kweli hilo jina lilipendekezwa lakini bado halijapitishwa rasmi tusubiri tuone kwani itakapokuwa sawa kila kitu kitawekwa bayana lakini mpaka sasa bado bendi inaitwa 5 Stars Modern Taarabu. 

Wasomaji wa blog yetu tunawaahidi kuendelea kufuatilia jambo hili na tutawaletea hapa hapa tusubiri, pia kwa uongozi wa 5Stars kama watapendekeza jina hili ni zuri kwakweli na linaonekana kuwa na Mvuto kabla ya kuanza kutumika, Taarabu Zetu imelipenda...!!!

MOSI SULEIMAN AGEUKIA BONGO FLEVA...!!

Mosi Suleiman.
Muimbaji wa Taarabu ambae kwa mara ya mwisho alikuwa katika bendi ya 5 Star's Modern Taarabu, Mosi Suleiman amegeukia upande wa pili kwa kutoa wimbo wa bongo fleva uitwao MAZOEA YANA TABU. 

Akizungumza na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com Mosi alisema nimeamua kuimba miondoko hii ya bongo fleva ili kuwadhihirishia wapenzi kwamba hata sisi wa Taarabu tunao uwezo mkubwa sana wa kuimba miondoko hii ya bongo fleva. 

Mosi amewaomba wapenzi wa muziki huo kumpokea na kumpa sapoti kubwa. 

Kabla ya kuwa na bendi ya 5 stars Mosi aliwahi kuimbia bendi kadhaa ikiwemo Victoria, T Motto na nyinginezo.

Tuesday, October 8, 2013

KINGEKE MODERN TAARABU YAMALIZA SHOOTING YA NYIMBO ZAKE MPYA!.

 Bendi ya Kingeke Morden Taarabu yenye makazi yake mkoani Morogoro, tayari imemalizia shooting ya nyimbo zake mpya kabisa ambazo editing yake itafanyiwa Zanzibar. 

Shooting hiyo ilitawaliwa zaidi na mazingira ya mji kasoro bahari yaani Morogoro. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msemaji wa bendi hiyo Hussein Iddy au "Baba Ubaya" alisema tumeamua kutumia location za mkoani kwetu Morogoro ili kuleta tofauti na video za wenzetu ambazo zimekuwa hazina mabadiliko mazingira yale yale tu! sisi tutakuwa mfano na sio mbaya kama wakiiga kutoka kwetu.

Monday, October 7, 2013

KHADIJA KOPA KUMALIZA EDA TAREHE 14/10/2013.

Khadija Kopa. "Malkia wa Mipasho".
Khadija Omary Kopa au malkia wa mipasho nchini Tanzania, anatarajia kumaliza EDA yake mwezi huu tarehe 14 na rasmi anaanza kazi tarehe 19 akiwa na kundi lake la TOT ndani ya ukumbi wa DAR LIVE Mbagala jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa simu akiwa kwake Bagamoyo, malkia huyo alisema nitaendelea kumkumbuka na kumuenzi marehemu mume wangu kwani ni pigo kubwa ameniachia na pengo lake halizibiki kwakweli, Jafary upendo wake kwangu ulikuwa hauna mfano, mwenyezimungu amlaze pema peponi mume wangu!. 

Wapenzi na wadau wa Adija Kopa mjiandae kumpokea!

HANIFA MAULIDI: MAKAVU LIVE KUWEKWA KIDEONI.

Hanifa Maulid aka Jike la Chui.
Wimbo wa "Makavu live" toka Kings Modern Taarabu ulioimbwa nae bibie Hanifa Maulidi jana tarehe 6/10/2013 umeanza kufanyiwa shooting na kampuni ya SOWETO PICTURE chini ya Thabit Abdul na Bobo Mautundu. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Hanifa alisema anamshukuru Mungu kwa kuanza vyema shooting ya wimbo wake na anategemea baada ya wiki moja itakuwa tayari, pia amesema kwamba anajiandaa kutoa wimbo mwingine wa audio ambao ameupa jina NAUFUNGA MTAA.

Katika wimbo huo kinanda atapiga Omary Kisila, 
Besi Gitaa atapiga Thabit Abdul na solo gitaa anaweza kuwa Chinyama Au Kisolo. 
Tusubiri.

ASHURA MACHUPA:- NZI WA KIJANI ILIFUTWA MAKUSUDI STUDIO..!

Ashura Machupa wa Fungakazi Modern Taarabu.
 Nzi wa kijani ni wimbo ambao kwa sasa ndio umekuwa habari ya mjini kulingana na vijembe vilivyomo katika wimbo huo, muimbaji wa wimbo huo ni Ashura Machupa kutoka katika bendi ya Fungakazi Modern Taarabu, ambae naweza kusema ameutendea haki wimbo huo, kwani amejua haswa kuichezea sauti yake katika Nzi wa kijani. 

Mapema Jana wakati anahojiwa na mtangazaji MWANAISHA SULEIMAN wa redio 5 Arusha katika kipindi cha taarabu, Ashura alisema wimbo huo wa Nzi Wa Kijani mara ya kwanza ulirekodiwa katika studio moja huko Sinza lakini kwa njama za wajanja wakafanikiwa kuufuta, lakini sisi tulihama na kurekodi kwingine.

TETESI: 5 STARS MODERN TAARABU, KUBADILISHWA JINA.

Baadhi ya wasanii wa 5Stars.
Bendi ya 5 stars Modern Taarabu inasemekana viongozi wake wapo mbioni kubadili jina la bendi hiyo ili kwenda na wakati. 

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake kiongozi mmoja wapo wa bendi hiyo alisema Jina hilo la 5 Stars limekuwa kama lina mikosi kwani bendi imekuwa haipandi ukizingatia mkurugenzi amewekeza pesa nyingi sana kwa kununua wasanii wenye majina makubwa katika tasnia ya taarabu lakini hakuna jipya. 

Jina jipya la bendi hiyo bado halijapatikana na hata kamati ya kuteua jina mbadala haijakaa, pia kuna wasanii watapunguzwa kazi, alisema.

Saturday, October 5, 2013

SUPERSHINE MODERN TAARABU, SIKU YA IDD-EL-HAJJI, KUTOA BURUDANI MAX BAR ILALA BUNGONI

Bendi ya Supershine Modern Taarabu yenye makazi yake Magomeni jijini Dar, siku ya idd el haji wanatarajia kufanya show ya nguvu katika ukumbi wao wa nyumbani wa MAX BAR ILALA. 

Akizungumza na mtandao huu meneja wa bendi hiyo Kais Mussa Kais alisema siku hiyo kutakuwa na burudani nyingi ndani ya ukumbi huo kwani wapo katika mazungumzo ya mwisho mwisho kuwaleta Baikoko na msaani mmoja mkubwa wa taarabu ambae atasindikiza show hiyo maalum ya Idd el haji. 

Supershine ndio habari ya mjini kwa sasa, kwani wanatamba na nyimbo zao mpya na siku hiyo wataimba nyimbo zote za zamani na watamalizia na nyimbo zao zote mpya walizoziachia hivi karibuni.

Wakazi wote wa Jijini mnakaribishwa kuja kupata burudani nzuri kabisa ndani MAX BAR ILALA BUNGONI.

MUSSA BESI WA JAHAZI, KUOA TAREHE 6 MWEZI HUU.

 Mpiga gitaa la besi katika bendi ya Jahazi Modern Taarabu Mussa Besi anatarajia kuuaga ukapera siku ya tareh 6 mwezi huu huko magomeni. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mussa alisema anawakaribisha wale wote wanaomfahamu na wasiomfahamu kwani kuna mambo mengi mazuri amewaandalia. 

Mussa Besi ni msanii mwenye historia ndefu kidogo katika tasnia hii ya taarabu na pia alishawahi kufukuzwa kazi pale Dar Modern kwa kosa la kwenda kurekodi nyimbo na Babu Ayubu wakati ana mkataba na mkurugenzi Feresh wa Dar Modern Taarabu. 

Sisi mtandao wa taarabuzetu tunampongeza na tunamtakia maisha mema katika ndoa yake.

Friday, October 4, 2013

MRIDU ALLY:- BAADA YA KUJIONDOA DAR MODERN TAARABU, AAMUA KUANZISHA BENDI YAKE...!!

Unapolitaja jina la Mridu Ally katika tasnia hii ya taarabu basi jua unamtaja mtu muhimu sana.

Mridu aliingoza vyema Dar Modern mpaka ikajizolea umaarufu mkubwa na mashabiki lukuki, lakini mwanzoni mwa mwaka huu aliamua kujiengua toka katika bendi hiyo na kufanya kazi zake zingine mpaka juzi alipotangaza kwamba ameamua kuanzisha bendi yake mwenyewe iitwayo Bombastic Modern Taarabu "WANA B KUBWA".

Mridu alisema kuwa tayari ameshaisajili bendi yake kisheria na hivi karibu ataingia kambini kujiandaa na ushindani uliopo kwa sasa.

MKURUGENZI WA DAR MODERN TAARABU, AENDA HIJJA...!

Baadhi ya wasanii wa Dar Moder Taarabu.
Bosi wa bendi ya Dar Modern Taarabu, Mr Abdallah Feresh ameenda Hijja kwenda kutimiza moja ya nguzo za dini ya kiislam.

Akizungumza na mtandao huu makini wa taarabuzetu.blogspot.com msanii kiongozi wa bendi hiyo ambae hakupenda kutajwa jina lake sababu yeye si msemaji wa familia, amesema kwamba hii ni ndoto ya siku nyingi ambayo alikuwa nayo bosi wao Abdallah Feresh, wakati huo huo wadau wa taarabu walimpongeza sana Feresh kwa maamuzi yake ya busara na kuwashauli wakurugenzi wengine wa bendi za taarabu kuiga mfano bora ulioonyeshwa na mkurugenzi wa Dar Modern Taarabu.

Thursday, October 3, 2013

T MOTTO YAPAGAWISHA BILA JOKHA KASIM...

Baadhi ya Waimbaji wa Bendi ya T MOTO.
 Bendi ya T MOTTO Modern Taarabu, siku ya J4 ilifanya show ya nguvu katika ukumbi wa Kapakabana Mwananyamala.

Bendi hiyo ambayo ilikaa muda mrefu bila kufanya show, ilikonga nyoyo za wapenzi wake kwa vibao vyao maridadi kama Domo la udaku, Behind the scene na Mwanamke hashuo, wadau walisikika wakisema kwamba wanaitaka bendi hiyo kufanya show kila J4 kama ilivyokuwa zamani.

Jokha Kassim, Muimbaji Nyota wa T MOTO.
Dosari iliyojitokeza katika show hiyo ni kutoonekana kwa Star wa bendi hiyo Jokha Kasim na pia kuonekana kwa sura ngeni nyingi za waimbaji wa bendi tofauti ambao walikuja kutoa msaada kwa bendi hiyo.

Kulikuwa na waimbaji watatu wa G5 na mpiga gitaa la solo mmoja wa bendi ya Kings Modern Taarabu anaitwa "silver mundele".

Mtandao huu uliweza kushuhudia Show hiyo iliyokuwa nzuri na ya kuvutia, T Moto mjipange vyema kwa kufanya show kama wapenzi wenu wanavyowaomba.

Wednesday, October 2, 2013

RATIBA YA G5 MODERN TAARABU KWA WIKI HII...

 JUMATANO NA KILA JUMATANO - CLUB KAKALA, KIGAMBONI,

KILA JUMAPILI - EQUATOR GRILL, MTONI.
 
African Stars, Twanga Pepeta.

Mkurugenzi wa G5 Modern Taarabu Mr Hamis Slim ameuambia mtandao huu kuwa, katika show yao ya Jumapili hii tarehe 6/10/2013 katika ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ally watakuwa na wakali wa miondoko ya Dance Tanzania TWANGA PEPETA, wataangusha bonge show.

Show hiyo imepewa jina la "USIKU WA TARADANCE" na Kiingilio kitakuwa ni Tshs. 5,000/=TU.

Ni burudani nzuri kabisa, maalumu kwa wakazi wa Mtoni na maeneo ya jirani, SI YA KUKOSA...

BENDI 3 ZAMNYEMELEA NYAWANA MALKIA WA KINYAMWEZI.

Nyawana Fundikira (Malkia wa Kinyamwezi).
 Ni baada ya kutoka na "Shetani kataja Jina" na kutamba sana katika vituo mbalimbali vya radio imewafanya mabosi wa bendi tatu tofauti hapa Nchini wamtafute Nyawana.

Anaitwa Malkia Wakinyamwezi kutokana na manjonjo yake pindi anapokuwa stejini, Huyu ni Nyawana Fundikira mtoto wa mzee Isale, Wimbo wake mpya wa Shetani Kataja Jina umemfanya awe gumzo mjini na kupelekea bendi 3 kubwa za taarabu hapa nchini kumuwania ili afanye kazi katika moja ya bendi hizo. 

Akizungumza na mtandao huu Nyawana alikili kuwepo na mipango hiyo ila amesema ni mapema mno kuzitaja bendi hizo kwani bado wapo katika mazungumzo na mambo yatakapokuwa mazuri basi mashabiki zake watajua ni bendi ipi mojawapo atakuwepo

MWANZILISHI WA TARADANCE, SAKATA LA THABIT ABDUL NA ALLY STAR LAENDELEA...

Ally Hemed "Star" a.k.a. Sharo Babu.
 Maelezo ya Ally star: 

Kuna mtu kamuingiza Abdallah Issa katika Malumbano yangu na Thabit Abdul
NATAKA KUMKUMBUSHA BIMA MODERN TAARAB Bend ambayo, Ally Star Sharobabu ni Mmoja kati ya Waasisi; Bend hiyo ilianzishwa 1985; BAADAE; 1987 Ikaanzishwa Bend ya MAMESH MODERN TAARAB; "KUFIKIA; 1988 Ikaja; ALL STAR MODERN TAARAB; "Baada ya miaka mi4 kufikia 1992 Ikaanzishwa; TANZANIA ONE THEATRE . BAADAE 1993 Ikazaliwa THE EAST AFRIKA MELODY; 94/95 Ikazaliwa DUMBAK MASTER'S chini ya Abdallah Issa Baada ya kuachana na Melody; Ingawa Abdallah Issa ameanza kuimba zamani, mwanangu Thabit Abdul "NAZI HAISHINDANI NA JIWE".

Kwa sasa mimi Sitafuti Umaarufu Mimi tayari maarufu kabla wewe hujaanza Chekechea, hakuna asiejua hilo, Nataka Utambue hivyo 2.

Mie siendi media kama unavyohaha wewe. Media wanataka kujua mambo toka kwangu
lakini kama unavyodai kua Media zote zinajua kama wewe ndio muasisi wa Taradance! hizo ni juhudi zako za kuhaha na Media lakini unatakiwa UNISHUKURU MIMI kwa kukuanzishia Taradance kama unabisha!
Nataka uweke wazi jambo hili:. "Nyimbo ya RUDI iliyo katika mtindo wa RHUMBA ambayo ni utunzi wa ALLY STAR SHAROBABU, na ukaimbwa na Ally Star; Na wewe Thabit Umeshiriki kupiga kinanda, wakati huo wewe Thabit Ukiwa na Bend ya TOT Taarabu ni kabla hamjaanzisha MASHAUZI. Je!, wimbo huo wa RUDI sio Taradance? 

Kosa langu kutokutangaza? HAYA NIMEKUBALI UMESHINDA WEWE KAMA KUANZISHA UMEANZISHA WEWE, SIONI FAIDA YA MABISHANO HAYA KILA LA KHERI. 

Huo ni walaka mzito ulioandikwa na ALLY STAR na kutumwa katika ofisi za taarabuzetu.blogspot.com, akijibu tuhuma toka kwa Thabit Abdul ambae alinukuliwa na mtandao huu akisema Ally Star si lolote si chochote na ameishiwa, sisi kama mtandao makini, sakata hili tunalirudisha kwenu wasomaji wetu mnaoujua ukweli mtoe maoni yenu ni nani yupo sahihi kati yao?.