TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, September 29, 2013

*SHINDANO LA KIGOLI * MZEE YUSUPH AIKACHA G5 MODERN TAARABU...

Mzee Yusuph.
Lile shindano la kigoli ambalo linaandaliwa na mwanadada maarufu hapa jijini Dar MAIMATHA limezua kasheshe baada ya mfalme Mzee Yusuph kukataa kupanda jukwaa moja na bendi ya G5 Modern Taarabu.

Akizungumza na mtandao huu chanzo chetu cha habari kilieleza kwamba muandaaji aliamua kuwashirikisha G5, Karunde Bend na msichana DYNA ili kunogesha zaidi shindano lake lakini alikutana na kipingamizi kikubwa toka kwa Mzee, inasemekana Mkurugenzi huyo wa Jahazi hakuhitaji kupanda jukwaa moja na bendi yoyote ya Taarabu, jambo lililopelekea kufutwa kwa matangazo yote yaliyokuwa yakitangaza kuwepo kwa G5 Modern Taarabu ili uwepo yeye pekee, mdau mmoja alisikika akilalamikia jambo hilo akisema si vizuri kubaguana wakati wote ni bendi zinazopiga mziki mmoja!.

MZEE YUSUPH AJA KIVINGINE...

Mzee Yusuph. Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarabu.
Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarabu Mzee Yusuph, amewaambia mashabiki na wapenzi wa bendi yake kwamba wajiandae kwa mambo mazuri toka katika bendi yake kwani albam atakayotoka nayo sasa hivi itakuwa tofauti na walivyo mzoea, 

Alikuwa akiyazungumza hayo wakati alipokuwa anafaya mahojiano na mtangazaji aitwae FROZA MHANDO wa redio free mwanza katika kipindi cha taarabu, amesema albamu yake sasa hivi itabebwa na wimbo usemao "CHOZI LA MAMA NI LAANA LINAPOTOKA KWA MWANA!", huu ni wimbo wenye mahadhi tofauti na walivyo nizoea! sitoimba mapenzi tena nimewaachia wengine waendelee kuimba.

Saturday, September 28, 2013

MPIGA KINANDA MASHUHURI, AMOUR SALEH NDANI YA G5 MODERN TAARABU...


Anaitwa Saleh Amour 'Zungu.' Amefunzwa ufundi huu na Band ya siku nyingi ya All Star, pia aliwahi kuwa na Twanga Pepeta, African Theater TOT na Band nyingi, na sasa atakuwa G5 Modern Taarabu...

G5 Modern Taarab yakamilisha mipango ya kumrudisha nchini mpiga kinanda mashughuli Amour Saleh Zungu toka nchini Muscut.

Akiongea na mtandao huu Mkurugenzi wa G5 alisema bend yake sasa anaiandaa kwa kuisuka zaidi ili iwe tishio zaidi na ameamua kumchukua Zungu kwa ajili ya kuimarisha zaidi upande wa upigaji vyombo.

Wiki ijayo kuanzia tarehe 30/9 Zungu ataanza mazoezi ya nyimbo tatu atakazozitengeneza yeye mwenyewe na tatu nyingine ataziteneza Omari Kisila ili kukamilsha albam ya Pili ya G5 Modern Taarabu.

Pia alisema mbali ya Zungu yupo msanii mwingine mkubwa, yeye atamtaja siku za hivi karibuni baada ya kukamilisha nyimbo yake kati ya hizo sita, yeye atakuwa ni "Surprise" kwa wapenzi wetu hivyo wasikae mbali.

Mkurugenzi Mr Slim alisema nyimba zitakuwa ni kali sana kutokana na jinsi walivyozipangilia na zitakuwa na radha tofauti tofauti kwasababu kila nyimbo itakuwa na muimbaji wake.

Show maalumu itafanyika kwa kuwatambulisha wasanii hao wapya baada ya kukamilisha nyimbo zao,

Mr Slim pia alisema wiki ijayo wataiachia Video ya nyimbo yao mpya "DONT BREAK MY HEART" ya  HASAN VOCHA.

Wapenzi wote wa G5 Modern Taarabu mambo mazuri ndo hayo...

Friday, September 27, 2013

DOWNLOAD NYIMBO MBILI MPYA ZA SUPERSHINE MODERN TAARABU "WANA RUSHA ROHO USITOE ROHO".

Nuru Moshi.

Nyimbo: Wafadhilaka 
Mwimbaji: Nuru Moshi 
Bendi: Supershine Modern Taarabu "Wana Rusha Roho Usitoe roho".

Queen Salma na Ally Mikidadi.

Nyimbo: Wosia wa Baba 
Waimbaji: Ally Mikidadi na Queen Salma 
Bendi: Supershine Modern Taarabu "Wana Rusha Roho Usitoe roho".

Thursday, September 26, 2013

SAIDA MASHAUZI AACHIKA NDOANI...

Saida Mashauzi.
Muimbaji wa Mashauzi Classic Saida Mashauzi ameachika ndoani baada ya kukaa na mumewe miezi minne tu. 

Akizungumza na mtangazaji wa times fm Dida leo hii alhamisi, dada wa msanii huyo Isha Mashauzi amethibitisha hilo kwamba mdogo wake huyo ameachika katika ndoa hiyo na sababu kubwa ya kuachana kwao ni kwamba mume hakuwa anataka mkewe aendelee kuimba tena taarabu jambo ambalo lilipata upinzani mkubwa toka kwa Saida mwenyewe na kukataa kuacha kuimba. 

Saida Mashauzi ni msanii anaekuja kwa kasi kwa sana kwa sasa, Isha Mashauzi amesema kwamba mdogo wake huyo bado hajapewa talaka.

USIKU MAALUM WA ISHA MASHAUZI - MANGO GARDEN LEO 26/9

 Mashauzi classic inakukaribisha Mango Garden Kinondoni:
Ni leo siku ya Alhamis ya tarehe 26/9/2013 ni "USIKU MAALUM WA ISHA MASHAUZ" ataimba nyimbo zote zake unazozijua na usizozifahamu. 

Mnakaribishwa sana USIKU MAALUM WA MASHAUZI, masapraiz kibao. 

Kama kawaida Kiingilio ni 5000 tu.

DAR MODERN TAARABU YAPOROMOKA KIWANGO...

Baadhi ya wasanii wa Dar Modern.
Bendi ya Dar Modern Taarabu ya jijini Dar es Salaam imekimbiwa na mashabiki katika maonesho yake, kwa sasa imebaki na show moja tu kwa wiki ambayo inafanyika katika ukumbi wa LANGO LA JIJI Magomeni Mikumi kila jumatano. 

Ukienda kuhudhulia tamasha hilo ajabu ni kwamba watu ambao wanaingia katika show zao ukiwahesabu kwa idadi hawafiki hata 15!.

Bendi hiyo ambayo hapo nyuma iliwahi kutamba na kibao chake maarufu PEMBE LA NG'OMBE imekosa mvuto baada ya kuondokewa na wasanii wake kadhaa wakiwemo Hammer Q, Salha, Mlidu Ally, Mape Kibwana, Hashim Said na wengineo wengi. 

Tunapenda kumshauri Mkurugenzi wake kuzinduka sasa na ajipange ili kuweza kuiinue Bendi na kuifufua, ajue anakoelekea sasa ni kugumu zaidi.

5 STAR'S WAELEKEA LINDI NA MTWARA BILA ALLY J WALA RAJABU KONDO!..

Baadhi ya wasanii wa 5Stars Modern Taarabu.
 Bendi ya 5 Stars Modern Taarabu imeanza ziara yake mikoa ya kusini pasipo na wasanii wake wawili mahiri ambao ni Ally J na Rajabu Kondo. 

Bendi hiyo ambayo imeondoka hapa jijini Dar kuelekea huko mikoani, jana wamefanya show ya nguvu Ruangwa, leo Nachingwea, kesho Masasi, Jumamosi watakuwa Mtwara, Jumapili watawapa raha wakazi wa Lindi mjini, na kumalizia siku ya Jumatatu pande za Mafia kwa mkurugenzi wao Shark's the Don!. 

Wanatarajia kurudi Dar wiki ijayo. Taarifa zinasema kwamba bendi inaendelea vizuri kutoa burudani kwa wakazi wa kusini.

Wednesday, September 25, 2013

BARUA YA WAZI:- KWA MAKAMPUNI YANAYODHAMINI VIPINDI VYA TAARABU REDIONI NA KATIKA TELEVISION MBALIMBALI NCHINI TANZANIA...

Taarabu ni muziki wenye asili ya mwambao na ukanda wa pwani kwa ujumla, muziki huu hapo zamani ulikuwa ni kiburudisho haswa mida ya jioni ambapo watu wanakuwa wametoka pwani au baharini kutafuta kitoweo kwa ajiri ya familia zao na wengine kuuza!, muziki huu umekuwa ukijizolea sifa na mashabiki lukuki kila kukicha jambo linalopelekea kupata udhamini wa makampuni makubwa wakiwekeza mamilioni ya pesa katika redio na television mbalimbali hapa nchini, hii yote ni kuonyesha ni kwa kiasi gani muziki huu unavyokubarika katika jamii. 

Lakini jambo la kushangaza na kustaajabisha ni kuona khali duni ya kimaisha anayoishi msaani husika ambae amesababisha hata hayo makampuni makubwa kuwekeza na kujinafasi kwa upana zaidi katika kujitangaza!, "waswahili wanasema, baniani mbaya kiatu chake dawa" wakati umefika sasa kwa haya makampuni kusaidia vikundi mbalimbali vya taarabu nchini bila ubaguzi wowote ili kuweza kujikimu na kumpa hamasa msanii kutengeneza nyimbo nzuri zaidi, nchi yetu bado haijafikia msanii au bendi kulipwa na vituo vya redio au television kulingana na kazi yao, basi ninyi makampuni mnawajibu wakudhamini pia bendi husika ili kujikimu na gharama za uendeshaji na sio kukimbilia katika vituo vya redio na television tu kudhamini. 

Khali inapoendea ipo siku viongozi wa bendi za taarabu watagoma kupigwa kwa nyimbo zao katika vipindi ambavyo ninyi makampuni mnadhamini humo mpaka mkae meza moja na kuona mnawajari kwa kiasi gani, "waungwana wanasema ukila na kipofu usimshike mkono", Taarabu inawatangazia bidhaa zenu, nanyi ni lazima muoneshe kuwajari, na sio kuwajari wamiliki wa vituo vya redio na television tu siku zote chanda chema huvikwa pete. 

KUWENI MAKINI NA MAKALA HII SIKU MOJA MTAKUMBUKA HAYA...

BREAKING NEWS:- THABIT ABDUL AACHA UKURUGENZI NDANI YA MASHAUZI CLASSIC...!!

Thabit Abdul "Jiko la Jela".
Mpiga kinanda maarufu Thabit Abdul au Jiko la Jela wa bendi ya 5 Stars leo tarehe 25/9/2013 ametamka rasmi kuachia ngazi ukurugenzi ndani ya bendi ya Mashauzi Classic.

Ufuatao ni ujumbe ambao ameutuma Thabit Abdul ndani ya ofisi zetu:- "Leo natangaza rasmi kuwa nimeacha Ukurugenzi ndani ya Mashauzi Classi, sababu sipati faida yakuwa mkurugenzi zaidi ya kupoteza muda wangu nakutengenezea watu tu maisha!". 

Thabit abdul pamoja na kwamba aliihama bendi ya Mashauzi, lakini aliendelea kuwa ni miongoni mwa wakurugenzi wa bendi hiyo.

RATIBA YA MAONYESHO YA G5 MODERN TAARABU...

Baadhi ya wasanii wa G5 Modern Taarabu.

BENDI YAKO UIPENDAYO YA G5 MODERN TAARAB INAKULETEA RATIBA YAKE YA MAONYESHO KAMA IFUATAVYO:- 

** KILA JUMAPILI EQUATOR GRILL MTONI, Watakonga nyoyo za wakaazi wa huko na vitongoji vyake, unakaribishwa sana.
** KILA JUMATANO CLUB KAKALA KIGAMBONI, Watu wa Kigamboni msikosi, Kila Jumatano ni mambo mazuri.

ALHAMISI 26/9/2013 TUTAKUWA EQUATOR GRILL MTONI KATIKA UZINDUZI WA CASH MONEY CAMP. TUTAKUWA PAMOJA NA OMARI TEGO NA FUNGAKAZI MODERN TAARAB wote mnakaribishwa G5 MODERN TAARABU ndio mpango wa mjini kwa sasa
KARIBUNI SANA...

Tuesday, September 24, 2013

JUMANNE ULAYA:- JAHAZI NIPENI MILIONI 15 TUVUNJE MKATABA 5 STARS...

Jumanne Ulaya.
Aliekuwa mpiga solo wa kutegemewa wa Jahazi Modern Taarabu lakini kwa sasa yupo 5 Stars Jumanne Ulaya imeripotiwa na tovuti moja kwamba bendi yake hiyo ya zamani ipo katika mipango ya kumrudisha tena kundini kwani safu ya wapigaji magita imepwaya sana. 

Akizungumza na mwandishi wa tovuti hii J4 alisema hata mimi taarifa hizo zimenifikia na kwakuwa muziki mimi ndio kazi yangu basi Jahazi wanipatie milioni 15 tu ili tuvunje mkataba hapa 5 Stars nilipo kwa sasa, mimi Jahazi bado naipenda na niliondoka sababu ya maisha tu kujaribu sehemu nyingine.

Sunday, September 22, 2013

BAKARI HANZURUNI AZIKWA...

 Bakari Hanzuruni amezikwa jana katika makaburi ya Kisutu.

Mpiga solo wa zamani wa bendi ya East African Melody Bakari Hanzuruni aliefariki ghafla juzi (Alhamisi) asubuhi kwa maradhi ya kichwa amezikwa jana saa 7 mchana katika makaburi ya kisutu jijini Dar es Salaam.

Hanzuruni ambae aliwahi kurekodi na bendi hiyo ya Melody mpaka jumatano alikuwa hana tatizo lolote na hata katika show ya Gusagusa Min Bend alionekana katika ukumbi wa Lango la jiji Magomeni. 

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.

Friday, September 20, 2013

MSIBA TENA, BAKARI HANZURUNI AFARIKI DUNIA...

Mpiga gitaa la solo wa zamani wa East African Melody BAKARY HANZURUNI amefariki dunia ghafla leo asubuhi hapa jijini dar. 

Akizungumza na mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com katibu wa East African Melody Mr Abuu amesema marehemu amekufa ghafla leo asubuhi kwa ugonjwa wa kichwa, homa ilipomzidia walimpeleka hospital pia alikuwa anafanyiwa dawa za suna ikiwemo kisomo yote katika kuokoa uhai wake lakini mwenyezimungu akamchukua. 

Marehemu katika uhai wake alipigia Melody wakati ndio anatoka Tanga kuja hapa Dar es Salaam, taratibu za mazishi zinafanywa maeneo ya kariakoo Dar es Salaam!.

WAIMBAJI WA TAARABU NCHINI PUNGUZENI KUJISIKIA...

 Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com tumepata malalamiko toka kwa watu mbalimbali wapenzi na wadau wa Taarabu Nchini kuwa, "Waimbaji wa Taarabu wanajisikia sana".

Imekuwa ni desturi kama sio tabia iliyoota mizizi kwa wasanii wa taarabu nchini Tanzania kuchelewa kufika katika show na wengine hudiriki hata kukataa kupiga picha na shabiki wake ambae amelipa pesa kuingia katika hiyo show yake. 

Leo nisingependa kuwataja wasanii husika ila wengi wao ni wale wenye majina makubwa katika tasnia hii ya taarabu nchini. 

Utakuta wameandika show inaanza saa 3 usiku lakini ajabu mpaka saa tano za usiku show haijaanza, kwanini mnakuwa mna malingo kiasi hicho? kumbukeni kuwa ninyi bila ya mashabiki hamuwezi kuthaminika! malingo sio uungwana tubadirike jamani na viongozi ni vyema mkizingatia hili ili kuwaridhisha mashabiki kupata walichokifuata.

VIONGOZI WA TAARABU, MNAWAENZI VIPI WASANII WANAOKUFA?

 Tokea kifo cha wasanii 13 wa 5 Star mpaka sasa ni wengi wametangulia mbele ya haki tukiamua kuwataja mmoja mmoja, lakini swali linakuja nini wamefanya hata tu kuwaenzi wasanii waliofariki hata kufanya kisomo cha pamoja kuwarehemu tu!. 

Mimi kama mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com na mdau mkubwa wa mziki huu wa mwambao, Katika kumbukumbu zangu 5 Star walifanya hitma ya pamoja iliyofanyika katika ukumbi wa PTA mtoni kwa azizi ally lakini baada hapo hakuna kilicho endelea tena, wakati mwingine huwa napatwa na maswali kwani katika tasnia ya taarabu hakuna chama kinachotetea masirahi na haki za wasanii? na kama kipo kinafanya kazi gani? ni aibu sana.

Viongozi wa Bendi za Taarabu ni vyema kama mngekaa pamoja mkajipanga kama timu moja mkaelewana namna ya kuweza kundeleza bendi pamoja na mambo mengine ya muhimu.

THABIT ABDUL:~ ALLY STAR HANA JIPYA, ALITISHA ZAMANI.

Thabit Abdul (Jiko la Jela).
 Director wa 5 Stars na mpiga kinanda mwenye njaa naweza kumuita hivyo Thabit Abdul jiko la jela ameyatupa maneno wakati alipokuwa akihojiwa na MWANAISHA SULEIMAN wa redio 5. 

Thabit alisema Ally Star kwanza sio muasisi wa mtindo wa taradance kama anavyojinadi katika vyombo vya habari ila anataka umaarufu tu. 

Ila kiukweli yeye ni zilipendwa hana jipya, aliendelea kusema kwamba yeye ndio muasisi wa mtindo huo wa taradance kila MEDIA inalitambua hilo. 

Kwa upande wake Ally Star alipopigiwa simu alisema yeye ndio kila kitu juu ya style hiyo na ameianzisha mwaka 1985!.

Thursday, September 19, 2013

JOKHA KASSIM AGEUKIA FILAM, AJA NA "MY FAULT".


"HII HAPA NI TRAILER TU YA FILAM YENYEWE":-

Mwimbaji mahili na wakutegemea katika tasnia ya Taarabu nchini Jokha Kassim wa T MOTO Modern Taarabu amegeukia katika uigizaji wa filam na anakuja na filamu inayoitwa "My Fault".

Akizungumza na mtandao huu Jokha alisema uigizaji ni kati ya vipaji vyake alivyojaaliwa na mwenyezi Mungu, na katika filamu hii wadau ndo watasema kama atakuwa anafaa kuimba Taarabu au Kucheza Filam.

Katika filamu hii kuna wasanii wengi wakongwe na wenye vipaji kama:-
Mzee Masinde
Muhogo Mchungu
M-2
Rakheem David
Mayugwa
Hassan Ally na mwenyewe Jokha Kassim.

Filam ipo mbioni kutoka wadau mkae mkao wa kula kumshuhudia Jokha akifanya vitu vyake katika muonekano mwingine.

AMIN SALMIN: OMARY KOPA NA AHMED MGENI NI HAZINA YA TAARABU ILIYOZIMIKA GHAFLA...

Amini Salmin akiuguza Mguu wake.
 Mkurugenzi Wa T MOTTO Amin Salmin amesema Omary Kopa na Ahmed Mgeni ndio waimbaji wakiume pekee ambao walikuwa ni kioo pekee king'aacho kwa waimbaji wa kiume wa taarabu hapa nchini kwetu. 

Kushoto Marehemu Ahmed Mgeni na Omary Kopa enzi za uhai wao.

 Amin aliyasema hayo wakati alipotembelewa nyumbani kwake mikocheni kwenda kumjulia khali kutokana na ajali ya gari iliyompata huko arusha wiki kadhaa zilizopita. 

Amini Salmin akitembelea Magongo.
Amini Salmin mkurugenzi wa T Moto akiwa kajipumzisha.
Amin alisema waimbaji wengi waliobakia kwa sasa wanaiga sauti za wasanii hao waliotangulia mbele ya haki hivyo kufanya kusiwe na jipya kwa waimbaji hao wakiume, wajipange kivyao sasa.

Wednesday, September 18, 2013

MSIBA WA AHMED MGENI WASABABISHA KUGHAIRISHWA KWA SHEREHE NA SHOW YA SUPERSHINE LEO JUMATANO. TIZAMA PICHA ZA MAZISHI YA AHMED MGENI.

 Msiba mzito ulioikuta familia ya wapenda taarabu nchini kwa kuondokewa na muimbaji maarufu Ahmed Mgeni, umesababisha ile paty ya birthday pamoja na show ya leo ya bendi ya Supershine kuahirishwa mpaka pale itakapotangazwa tena. 

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu meneja na mratibu wa shughuli hiyo Kais Mussa Kais alisema Ahmed Mgeni ni mtoto wetu Supershine na hata album yake hii mpya ya SITETEREKI ameitengeneza kwetu na alikuwa anaishi kwetu wakati yupo hapa Dar, tutafanya kisomo kwa ajili yake leo saa 10 jioni.

Sote njia yetu ni moja Ahmed Mgeni umetangulia sisituko nyuma yako mungu akuondoshee adhabu ya kaburi na akupe makazi mema peponi Amen.

Inna lillah waillah rajuun pumzika kwa amani PRICE AHMED MGENI

Tuesday, September 17, 2013

BREAKING NEWS - MSIBA: AHMED MGENI AFARIKI DUNIA LEO ZANZIBAR...

Marehemu, AHMED MGENI enzi za uhai wake.
Muimbaji Nyota na mashuhuli, mwenye uwezo mkubwa wa kuimba AHMED MGENI wa Zanzibar Njema amefariki dunia leo alfajiri huko visiwani unguja. 

Muimbaji huyo ambae amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. 

Akizungumza na mtandao huu dada wa marehemu aitwae LAISATY MGENI alithibitisha ni kweli Kaka yake amefariki dunia leo alfajiri visiwani humo.

Ahmed Mgeni enzi za uhai wake aliwahi kupitia bendi kadhaa za taarabu ila wimbo wake wa SITETEREKI ndio umempa sifa sana.

AHMED MGENI atazikwa leo Saa kumi jioni sehemu iitwayo Amani Fresh njia ya Ziwatue huko huko visiwani Zanzibar.

Taarabu Zetu tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na kipenzi chetu Ahmed Mgeni na mungu amlaze pema peponi, AMIN!!

DOWNLOAD NA SIKILIZA NYIMBO YA "SITETEREKI" YAKE AHMED MGENI..

SUPERSHINE KUADHIMISHA BIRTHDAY YA BENDI JUMATANO HII PALE MAX HALL ILALA BUNGONI

Baadhi ya wasanii wa Supershine Modern Taarabu.
 Bendi ya Supershine Modern Taarabu wana Rusha roho usitoe roho! kesho jumatano tarehe 18 wanatarajia kufanya sherehe ya birthday ya bendi katika ukumbi wa MAX HALL ilala Bungoni Dar!. 

Akizungumza na mtandao wa Taarabu Zetu meneja wa bendi hiyo Kais Mussa Kais alisema siku hiyo kutakuwa na keki 3 ambazo ni ya wasanii wa bendi, Wadau na Wapenzi wa Supershine na keki ya mwisho itakuwa maalum kwa wasanii ambao waliwahi kupitia Supershine kipindi cha nyuma.

Alikitaja kiingilio siku hiyo kuwa Wanaume Shilingi 4,000/= na Wanawake Shilingi 2,000/=, show itaanza saa 3 usiku.

Blog hii pia imepewa MWALIKO MAALUMU... Tutakuwepo na wote mnakaribishwa.

Monday, September 16, 2013

TIZAMA VIDEO NYIMBO MPYA YA: Ally Star "Mvuvi Kinda".

MANYANYASO, WIZI NA UZALILISHAJI KWA MASHAUZI CLASSIC...

Poster Feki iliyochongwa na tepeli huyo.
Siku yaIjumaa Tarehe 13/09/2013 waligundua Wizi, Unyanyasaji na Uzalilishaji wakati walipokuwa wameenda kufanya show maeneo ya Mbezi.

Blog Hii ilipata taalifakupitia kwa page ya Facebook ya "Mkurugenzi wa Mashauzi Classic" Isha Mashauzi, taarifa hiyo ilisomeka hivi:-
"Hii ndio Hali halisi ya manyanyaso niyapatayo ila namuachia mola yy ndo ano jua anisaidie hili duh kwel hii Haki".

Mwandishi wa Taarab Zetu baada ya kuisoma hiyo ikambidi aanze kudodosa na kufuatilia ni nini tatizo!?

Mkurugenzi wa Mashauzi C Mashauzilassic, Isha Mashauzi.
Tulichukuliwa na Promota .... (Jina tunalo) kwenda kupigashow siku ya Ijumaa tarehe 13/09/2013 katika Ukumbi wa La Villa Chika maeneo ya Mbezi, kilichonishangaza na kunisikitisha sana ni kitendocha kukuta Matangazo ya Mashauzi Classic (Posters) yakiwa na mchanganyiko wa wasanii tofauti, Waimbaji wa Jahazi na wacheza show wa iliyokuwa Victoria Sound, mtu huyo ambaye jina lake tunalo inasemekana ndo tabia yake ya kuandaa matamasha hewa, yeye hukutana na boss mwenye Ukumbi na kuongea naye habari za Tamasha akimweleza wasanii atakaowaleta namwisho wa siku huafikiananajamaa kuchua pesa za Show anaenda kutengeneza Posters feki kama hizi na kuzibandika kumridhisha Boss kisha yeye huingia mitini.

Siku ya tukia Mashauzi ilibidi wapige show tu kwakutokuwaangisha mashabiki wake lakini Tapeli huyo alikuwa tiyari kafanya mamboyake.

Mashauzi alipoulizwa atachukua hatua gani kwakitendo hicho alichofanyiwa alisema:- "Mimi kwakweli huwa sina matatizo na mtu ila kwa hili namuachia Mungu tu maana yeye ndo anajua yote, hata hivyo nitakutana na washauri wangu nione wanasemaji, kwasababu mtu mwenyewe tunamjua...".

taarabuzetu.blogspot.com imesikitishwa sana kwa kitendo hichi kilichofanywa kwa Mashauzi, si tunashauri huyo mtu afikishwe kwenye vyombo vinavyohusika ili aweze kuchukuliwa hatu, maana anavyobaki vile bila kuchukuliwa hatua yoyote anazoea na kuendelea na tabia yake hiyo chafu.

Mwisho tunatoa pole sana kwa kundi zima la Mashauzi Classic.

Sunday, September 15, 2013

SHETANI KATAJA JINA: YAWA GUMZO MOMBASA KENYA!

"Shetani kataja jina" ni Wimbo wa mapenzi lakini una asili ya mipasho ile ya kisasa zaidi. 

Muimbaji wa wimbo huu mpya ni Nyawana Malkia wa Kinyamwezi, 
Katika wimbo huu Kinanda kimepigwa nae Thabit Abdul, 
Besi gitaa limepigwa na Mussa Mipango, 
Solo Gitaa kapiga Ramadhan Kisolo. 

Akizungumza Na mwandishi wa habari hizi mtangazaji wa Redio 5 nchini Kenya Mwanaisha Suleiman alisema kwamba anastaajabu sana juu ya wimbo huu kwani hauna siku nyingi tokea umetambulishwa redioni lakini umekuwa ukipendwa na wasikilizaji hata katika vitongoji vya Mombasa umekuwa ukichezwa katika sherehe mbalimbali kwa sasa!.

DOWNLOAD NYIMBO YA ALLY STAR "BABU SHARO" - RUDI

Nyimbo: Rudi 
Mwimbaji: Allystar "Sharo Babu".

OMARY TEGO KUJA NA WIMBO MPYA...

Mkurugenzi wa Coast Modern Taarabu, Omary Tego.
 Mkurugenzi wa Coast Modern Taarabu Omary Tego the Special One au Mgodi unaotembea yupo katika maandalizi bab-kubwa! kufyatua kibao matata sana kiitwacho "UTABAKI KUWA WEWE". 

Mwandishi wa habari hizi ambae alijipenyeza mpaka katika kambi ya mazoezi yao iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam aliwakuta Tego na mwanadada Jamira Dolphin ambae kwa upande wake nae anatengeneza wimbo wake mzuri ambao una ujumbe wa mwanamke kumsifu mumewe!. 

Kambi hiyo ambayo wameifanya kuwa siri kubwa inaendeshwa na Director Thabit Abdul jiko la Jela. 

Haya wapenzi wa taarabu tusubiri!.

Saturday, September 14, 2013

BAADA YA KUTOKA NZI WA KIJANI *KAPTENI TEMBA ATUMIWA SMS ZA KUTISHIWA MAISHA YAKE *...

Kepteni Temba, Mkurugenzi wa Fungakazi Modern Taarabu.
 Kwa mara ya kwanza tulipo ripoti kwamba Kapteni Temba yupo studio kuurekodi wimbo wake uitwao "Nzi Wa Kijani" na ni DONGO kwa mtu mmoja maarufu sana hapa jijini Dar es Salaam, baadhi ya mitandao ilianza kubeza habari hiyo na kusema haina ukweli wowote, lakini baada ya kupita siku kadhaa tulilipoti kupotea kimaajabu wimbo huo studio wakati ulisharekodiwa tayari. 

Baada ya wimbo kupotelea kusikujulikana Temba hakuishia hapo alihama studio na kwenda kurekodi kwa mara ya pili katika Studio ya Soundcrafters Temeke.

Sasa sekeseke likaanza baada tu ya kutoka kwa wimbo huo studio na kuanza kusikika redioni. Mkurugenzi wa Funga Kazi Modern Taarabu bwana Kapteni Temba amekuwa akipata sms za vitisho na watu wasiojulikana wakimtumia sms katika simu yake jambo lililomlazimu kubadili line ya simu yake.

Watu hao waliendelea kuwatumia sms hata watangazaji ambao wamekuwa wakiupiga wimbo huo au wameonekana kama kushabikia kwa namna moja ama nyingine na wao wamekuwa wakitumiwa sms za vitisho wakiambiwa waache kucheza wimbo huo. 

Pia baadhi ya wadau wa taarabu nao wamekuwa wakitumiwa sms hizo za vitisho toka kwa mtu asiejulikana wakiaswa kuacha kushabikia mambo yasiyowahusu.

Kepteni Temba baada ya kuona hali inaendelea vile akaamua kwenda kuripoti polisi vitisho hivyo.

Thursday, September 12, 2013

DOWNLOAD NYIMBO MBILI KALI ZA ALLY STAR (SHARO BABU)...

Ally Star (Sharo Babu).
 Ni Ally Star au ukipenda muite "Sharo Babu", katoka na nyimbo zake takribani Tatu zikiwa kari kabisa katika miondoko ya Taarabu.

Sharo Babu aliuambia mtandao huu kuwa, nyimbo hizo amerekodi akiwa kama msanii wa kujitegemea yaani katoka nje ya kundi lake la TOT, ni nyimbo nzuri ambazo ni lazima atazipenda kila mtu.

Nyimbo zimetoka katika Audio na Vidio moja ya "Mvuvi Kinda". Nyimbo: Mvuvi Kinda 
Mwimbaji: Ally Star (Babu Sharo) 
Nyimbo: Bahati ya Paka 
Mwimbaji: Ally Star (Babu Sharo)

DOWNLOAD NYIMBO MPYA: INZI WA KIJANI - ASHURA MACHUPA (FUNGAKAZI MODERN TAARABU).

 Ile nyimbo iliyoripotiwa hapo awali kufutwa katika studio aliyokuwa katumia kuirekodi Kepteni Temba, sasa ipo hewani baada ya kubadirisha studio.

Siku moja iliyopita tuliitoa hapa hii nyimbo na baadhi ya watu waliichukua, tunapenda kuwaomba radhi ile haikuwa Inzi wa kijani, isipokuwa hii hapa ndo nyimbo yenyewe ni makosa ya kiufundi yalifanyika. Ile nyimbo iliitwa "Muungwana Haumbuki

Endelea kufurahia mtandao wako wa taarabuzetu.blogspot.com.
ASANTE.


Wimbo: Inzi wa Kijani 
Mwimbaji: Ashura Machupa 
Bendi: Fungakazi Modern Taarabu.

Wednesday, September 11, 2013

DEALERS MODERN TAARABU KUMTAMBULISHA RASMI "MUSSA KIJOTI"...

Mussa Kijoti.
Katika usiku wa "Chipolopolo" Tarehe 15 Jumapili, Bendi ya Dealers Modern Taarabu iliyo chini ya Mwanahawa Ally Chipolopolo inatarajia kumtambulisha rasmi muimbaji toka 5 Stars Mussa Kijoti katika tamasha lililopewa jina "Usiku wa Chipolopolo".

Akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com mkurugenzi wa bendi hiyo Chipolopolo amesema tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika siku ya jumapili tar 15 katika ukumbi wa Dealers Pub Keko, litasindikizwa na wasanii waalikwa ambao ni Omary Tego na Issa Kamongo.

Amewaomba wadau na wapenzi wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi sana siku hiyo.

DOWNLOAD NYIMBO MPYA: SHETANI KATAJA JINA - NYAWANA MALKIA WA KINYAMWEZI...

Nyawana (Malkia wa Kinyamwezi).



Mwimbaji: Nyawana Malkia wa Kinyamwezi
Nyimbo: Shetani Kataja Jina

BREAKING NEWS: MGENI KISODA AJIUNGA SUPERSHINE MODERN TAARABU...

Mgeni Kisoda.
Aliekuwa mpiga kinanda namba moja wa bendi ya Jahazi Modern Taarabu, Mgeni Kisoda jana saa moja usiku amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Bendi ya Supershine Modern Taarabu. 

Mgeni kisoda ni mpiga kinanda wa siku nyingi aliyewahi kupigie Victoria Modern Taarabu, Dar es Salaam Modern Taarabu na nyingine nyingi kabla ya kujiunga na Jahazi Modern Taarabu. Baada ya kujiunga na Jahazi kisoda alikuwa mpiga kinanda namba moja katika Bendi hiyo kabla hajaondoka wiki moja iliyopita.

Kisoda alipoulizwa anajisikiaje kujiunga na Supershine na kwanini kachukua uamuzi mapema hivi!? Mwenyewe alisema: Ünajua unapokuwa mtu muhimu lazima watu wakusumbue, ni kipindi kifupi kweli na nimefuatwa na bendi nyingi zikitaka nikafanye kazi nazo lakini hatukuweza kufikia makubaliano, lakini Supershine wamefikia kiwango ninachokitaka na kwakuwa ni kati ya bendi nizipendazo, nimesaini nitakuwa pale sasa, nawakaribisha wapenzi wangu wote Supershine Modern Taarabu".

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi meneja wa bendi hiyo Kais Mussa Kais alisema hiyo ni moja ya mikakati yake madhubuti zaidi katika kuiinua bendi yake, "unajua kama nilivyosema katika mahojiano ya awali, nimekuja Supershine kuleta mabadiliko ya muziki wenyewe, mpaka wasanii ndani ya bendi, nilianza na Ndage Ndage na sasa ni Mgeni Kisoda. Nawaahidi wadau kazi nzuri inaendelea., kikubwa mtuunge mkono.

Tuesday, September 10, 2013

HII NI SUPERSHINE MPYA MASHABIKI WATUPOKEE...

Kais Mussa Kais, Meneja wa Supershine Modern Taarabu.
Meneja wa bendi ya Supershine Taarabu Kais Mussa Kais, amewaomba wadau na wapenzi wa taarabu nchini kuwapokea na kuwapa sapoti kubwa ili waweze kufikia malengo. 

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na redio 5 ya Arusha katika kipindi cha taarabu na mtangazaji Mwanaisha Suleiman. 

Kais alisema amekuja kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia hii ya muziki wa mwambao haswa ndani ya bendi yake ya Supershine, Kais kabla ya kuwa meneja wa Supershine amewahi kuwa meneja wa T Motto zote za jijini Dar es Salaam. 

Kais Mussa ambaye kwa sasa ni Meneja wa Supershine pia ni mdau mkubwa wa muziki wa mwambao hapa Tanzania ambapo katika juhudi zake za kuinua mziki huu ameweza kujuana na watu wengi ikiwamo wamiliki wa bendi mbalimbali za taarabu, ameahidi kufanya makubwa hasa kwa bendi yake ya Supershine ila tu anaomba ushirikiano kwa wadau.

Taarabuzetu Blog tunamtakia mafanikio mema nasi tu pamoja naye "ku-promote" muziki wa Taarabu.

COAST MODERN TAARABU NA T MOTTO SHOW MNAFANYA KUMBI GANI....!?

Omary Tego wa Cost Modern Taarabu.
Wapenzi na mashabiki wa bendi za T MOTTO na COAST MODERN TAARABU kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipiga simu katika ofisi zetu kuulizia ni kumbi zipi za burudani ambapo zinapiga show bendi hizo mbili.
Baadhi ya wasanii wa Kundi la Muziki wa Taarabu la Tanzania Moto Modern Taarabu (T-Moto), wakiwa katika Studio.
Jamali masudi mkazi wa Yombo Buza alisema yeye ni shabiki mkubwa wa T MOTTO lakini amekuwa hajui ni kumbi gani wanapiga bendi hiyo hapa Dar ili akapate burudani live. 

Pia Leyla Kasim wa Tegeta Dar alipiga simu akiomba mtandao huu uulizie kwanini Omary Tego na bendi yake hawatangazi ratiba zao au hawana show yoyote?.

Mtandao wa taarabuzetu tunawaahidi wasomaji wetukuwa tutafuatilia na tutawapa majibu pindi tutakapowasiliana na mabos wa bendi husika.

KINGEKE MODERN TAARABU KUFANYA VIDEO YA NYIMBO ZAKE..

 Bendi ya taarabu iliyopo morogoro mji kasoro bahari KINGEKE MODERN TAARABU inatarajia kufanya shooting ya nyimbo zao mpya hivi karibuni. 

Akizungumza kwa njia simu toka mkoani morogoro mkurugenzi wa bendi hiyo MR KINGEKE alisema: "Nimepania kufanya video ya gharama na yenye mandhari mazuri ili kuleta utofauti zaidi katika video zetu maana tumekuwa tukiona kila bendi wanafanya video zao Hotelini, Baharini na sehemu za garden tu, ila sisi tutabadilika na wadau watakubali". 
Alimtaka mwandishi wa habari hizi kuhudhuria katika shooting hiyo morogoro wiki ijayo!

SHOGA MAARUFU JIJINI ASTAAFU USHOGA, AOKOKA...

Anti ASU (AMOS) Akiwa ndani ya kumbi za Starehe enzi zake.
Kama ni mpenzi wa taarabu na unatembea sana usiku katika kumbi mbalimbali hapa Dar es Salaam basi ni lazima utakuwa unamjua au unamfahamu shoga maarufu hapa jijini aitwae "Aunt Asu" mtoto wa magomeni mapipa.

Mtaalamu huyu wa kuwabandika kope akina dada ameuambia mtandao wa taarabuzetu kwamba ameacha kazi ya ushoga na kwa sasa ameokoka na amesha badili jina anaitwa "AMOS".

Anti Asu ambaye pia ameamua kuokoka na kukiri hadharani kwamba hataurejea kamwe ushoga, inaelezwa kwamba kwa sasa anatafuta mke wa kumzalia watoto na ambaye atampa mapenzi ya dhati.


Imedaiwa kwamba, hivi karibuni Othuman alijisalimisha katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), lililopo Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam ambako alitubu dhambi zake. 

Mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com aliamua kuingia mzigoni kufuatilia `ishu’ hiyo ambapo alifanikiwa kumnasa Othuman akiwa katika saluni moja ya kike iitwayo Emmy’s iliyopo Magomeni Mapipa jijini anakofanya kazi.

Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kuukana ushoga, kijana huyo alithibitisha ni kweli ameacha tabia hizo na kwa sasa ameokoka baada ya kubadili dini kutoka kwenye Uislamu na kwenda kwenye Ukristo akiitwa Amos. 

Anti Asu (AMOS) akicheza kwa Stail ya Pinda Mgongo.
``Nimeokoka kiukweli kabisa. Sitaki tena  kuusikia ushoga. Nimemkaribisha Yesu awe mwokozi wa maisha yangu. Najutia dhambi zangu na namuomba yeye (Mungu) anisimamie na kunilinda ili nisiweze kuanguka tena,’’ alisema Anti Asu ambaye anaonekana ni mwanaume halisi. Amesema kwamba, ameamua kuanza maisha mapya na kwamba anaishi katika kanisa la TAG Magomeni ambako amekuwa akikesha kwa maombi.

``Mimi nilikua shoga namba moja Tanzania baada ya marehemu Anti Kessy. Hakuna alieyekua ananifikia. Nimevunja ndoa zaidi ya 30 na nimetembea na wanaume hata zaidi ya 200. Nimeishi kinyumba na wanaume zaidi ya 10. 

Nimebakwa na kufanya kila aina ya ufilauni. Nani ambaye alikua ananifikia mimi?  Shoga gani ajitokeze hapa. Lakini sasa nimeachana na yote haya baada ya kubaini nilikua naitwa na Mungu. Nimeludi kwake na ninahisi amani moyoni mwangu,’’ amesema. 

Ameongeza kwamba kwa sasa anajiandaa kuoa kwani alipima kama ana maambukizi ya maradhi ya Ukimwi na majibu yameonyesha kwamba yupo salama.`` Nashukuru kwamba hata jogoo anawika.’’

Aliongeza kwamba sababu nyingine iliyosababisha  aokoke ni kutokana na kuugua sana tangu alipokumbwa na tukio la kubakwa na wanaume zaidi ya 10. 

Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Dunstan kanemba amethibitisha kuokoka kwa Anti Asu na kusema kwamba yeye ndiye aliyemuombea na kumkaribisha rasmi kanisani hapo. 

``NI kweli Amosi (Anti Asu) tunaye hapa. Ibada ya Jumapili iliyopita tulimuombea hadharani na alidondoka chini. Hii ni ishara kwamba alikua na mapepo yanayomsumbua. Kanisa limempa hifadhi ya kuishi hapawakati tunamjenga kiroho. 

Pia tunamhudumia kwa mavazi na mahitaji mengine,’’ alisema Kanemba. Aliongeza kwamba uamuzi aliofanya kijana huyo ni wa msingi na kuwataka watu wengine ndani ya jamii wenye matatizo kama hayo kufika kanisani hapo kupata msaada wa maombi. 

``kwa yoyote anayehitaji kumsaidia zaidi kimwili basi asisite kufika hapa kanisani. Tunaamini kuwa kuokoka kwake kutasaidia sana kuwafanya vijana wengine wenye tabia hiyo kuokoka pia au kuacha’’ alisema Kanemba.

Amewaasa wale mabwana zake wa zamani ambao wamekuwa wakiendelea kumsumbua kwa kumpigia simu kwamba waache mara moja kwani kwa sasa ameshaachana na shughuli ile. 
 
Mtandao wa taarabuzetu unampongeza Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni kwa kuokoa maisha na kuamua kumjenga Kiroho Amos (Anti Asu), pia tunampongeza Anti ASU kwa kuokoka.