TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, November 29, 2013

5Stars kuwasha moto wa burudani Jijini Arusha leo hii ya tarehe 29 Nov. 2013.

Baadhi ya wasanii wa 5Stars.
 Kikosi kizima cha 5Stars Modern Taarabu kipo jijini Arusha katika show iliyoandaliwa na Radio 5.

Taarabu zetu umetaarifiwa kuwa, show itafanyika kukiwa na wasaani wote Nyota wa 5Stars kama:-
Thabit Abdul a.k.a. Jiko la Jela a.k.a. The HERO.
Ally J
Jumanne Ulaya
Juma Mkima

Msanii aliyejiunga na 5Stars hivi karibuni Mgeni Kisoda naye yupo kutoa Burudani.
Mgeni Kisoda alitokea Jahazi kwa Mzee Yusuph kabla hajajiunga na 5Stars.

Wengine ni:
Hammer Q
Aysha Vuvuzela na wengine kibao watakuwepo.

5Stars wanategemea kufanya show yao leo na kesho kurudi Dar kuendelea na Ratiba zao.

Aysher Vuvuzela akiwa na Mgeni Kisoda.

"Poyoyo" ya Aisha Masanja kideoni.

Mwimbaji wa Taarabu Aisha Masanja yupo mbioni kufanya Video ya nyimbo yake "Poyoyo".

Aisha akizungumza na blog ya Taarabu zetu alisema siku ya jumapili tarehe 1 Desemba 2013 atafanya video ya nyimbo yake binafsi inayoitwa Poyoyo, ambayo ipo katika mahadhi ya Mduara.

Aisha alisema Video ataifanyia Gadaff Club iliyopo Yombo, katika wimbo huo kamshirikisha Omari Tego.
Audio imetengenezwa na Marlon Rinje na Video inatengenezwa na Said wa Dolphin.

Aisha ametoa wito kwa wadau wake wote kwa kusema:-
"Ma dada mpendeze munizidi mm hii kwaajili ya wauza sura wote na wanaume wauza sura mpo km kawaida ndani ya Gadafi Club Yombo, nitafanya video yangu live pale saa 11 jioni msikose wana".

Wote mnakaribishwa itakuwa free, yaani BUREE HAKUNA KIINGILIO.

Thursday, November 14, 2013

PICHA ZA MAZISHI YA MALKIA WA KINYAMWEZI, NYAWANA FUNDIKIRA HUKO TABORA...

Kadri muda uendavyo ndivyo watu walizidi kufika ulipo msiba wa Nyawana Fundikira, maeneo ya Gongoni, Tabora mjini hapo jana. Hata hivyo mwili wake ulichelewa kidogo kuwasili mjini lakini watu waliendelea kujazana wakikaa juani bila taabu yeyote. Hii ni ishara kuwa watu wa Tabora walimkubali sana Nyawana ambaye wao walipenda kumuita Mamaa Nyawana au Jembe!
Baada ya mwili kufika, japo ulichelewa ulifanyiwa maandalizi ikiwa pamoja na kuagwa kwa ndugu na jamaa walioko Tabora na baadae mida ya saa moja (1:00) usiku.
MAMAA NYAWANA AMEPUMZISHWA KATIKA MAKAZI YAKE YA MILELE KATIKA MAKABURI YA ITETEMYA  MKOANI TABORA NJE KIDOGO NA MJI.
MAZISHI YALICHELEWA KUTOKANA NA KUCHELEWA KUWASILI KWA MWILI WA MAREHEM.


 "MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU NYAWANA FUNDIKIRA".

Wednesday, November 13, 2013

HABARI NA PICHA: KATIKA MATUKIO YA MSIBA WA KUMUAGA NYAWANA...

 Marehemu Nyawana aliyefariki siku ya Jumatatu Tarehe 11 Novemba 2013 alitarajiwa kuzikwa leo Jumatano huko kwao Tabora, lakini kutokana na safari ya tokea jana kuwa ndefu sana, huenda asizikwe leo na akazikwa kesho.

Akizungumza na blog hii mume wa marehemu Kais Musa amesema mpaka mida ya saa sita wapo njiani na huenda wakafika saa kumi za jioni na ikawawia vigumu kuzika, ila kwa taarifa zaidi ni mpaka pale watakapofika.

Marehemu Nyawana amefariki akiacha watoto wawili wa Kiume na wa Kike:-
Said na Queen.
Mungu awape nguvu kwa wakati huu mgumu.

Zifuatazo ni picha mbalimbali ikiwa ni matukio ya msibani kwa baba wa marehemu Nyawani pale Magomeni akiwa anaagwa kwa safari ya Tabora.

Tunazidi kumuombea kwa Mungu apumzike kwa amani.

Tutakuwa tunawaletea taarifa kadri tutakavyokuwa tunazipata.


Thabit Abdul akishiriki katika kubeba Jeneza la marehemu Nyawana.

Said, mtoto wa kwanza wa marehemu Nyawana akifarijiwa.
Kais Mussa mume wa Marehemu Nyawana akihojiwa na Mtangazaji wa EATV.

Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa Passion Fm na Ecoprint waliokuwa wakifanya kazi pamoja na marehemu Nyawana.
Saida Mashauzi.
Anneth Nyoni, Anuary Sanga na Yunus Kanumba, ni watangazaji waliowafanya kazi pamoja na Marehemu Nyawana.
Dida Mtangazaji wa Times FM.
Hashimu Said, msanii wa Mashauzi Classic.
Isha Mashauzi.
Amin Salmin kulia na Kapteni Temba.
Wasanii mbalimbali wa Taarabu wakiwa msibani.
Wadada Mapacha wadau wakubwa wa mziki wa Taarabu wakiwa msibani kwa mpendwa wao, rafiki yao kipenzi Nyawana Fundikila.
Luiza Nyoni.
Ramadhani Kisolo, Warda Chande na Eunice Kanumba.
Omary Kisira kushoto na Kais Mussa.
Baadhi ya watangazaji wa Passion FM wakiwa na nyuso za hudhuni kwa kuondokewa na mtangazaji mwenzao Nyawana Fundikila.
Eunice Kanumba kushoto na Aisha Vuvuzela wakiwa katika maeneo ya msibani.
Picha:- Gosbert Njenga na Robert Kiatu.