TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, December 21, 2014

ISHA MASHAUZI KUIKOSA MIAKA 8 YA JAHAZI TRAVERTINE HOTEL LEO USIKU...


Isha Mashauzi.
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi ataikosa show ya Jahazi Modern Taarab kutimiza miaka minane tangu izaliwe.

Show hiyo inafanyika leo usiku katika ukumbi wa Travertine Hotel huku ikiaminika kuwa wasanii wote walioitumikia Jahazi watakuwepo.

Katika onyesho la Mashauzi Classic pale Mango Garden Alhamisi iliyopita, Isha alitumia kipaza sauti chake kuinadi show ya Jahazi na kuwataka wapenzi wa Mashauzi wasikose kwenda Travertine Jumapili.

Lakini mashabiki hao walipomuuliza kama na yeye atakuwepo, Isha akawajibu kwa kusema kuwa kwa bahati mbaya yeye hatakuwepo.

“Nina kazi nje ya mji, nasikitika kuwa sitakuwepo katika onyesho hilo, lakini nawatakia mafanikio mema na naomba mkawaunge mkono,” alisema Isha.

Tuesday, December 9, 2014

FIVE STARS: JIANDAE KUPATA NYIMBO TATU KALI...!! PATA PICHA ZA STUDIO NA MAJINA YA NYIMBO...

Baadhi ya wasanii wa kundi la 5Stars.

Kundi zima la Taarab 5Stars leo wameingia studio kurekodi nyimbo zao Tatu watakazoziachia hivi karibuni baada ya kumalizika kurokodiwa.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo kongwa ameongea na Taarabuzetu.blogspot.com na kuihakikishia kuwa nyimbo hizo zitakuwa nzuri na itakuwa ndo habari ya mjini zitakapotoka.

Amezitaja nyimbo hizo ni:-
UBAYA HAUNA SOKO - Mwanaidi Ramadhani.
KISHTOBE - Salha wa Hammer Q.
SINA GHUBU - Mape Kibwana.

Wapenzi wote wa Taarabu kaeni mkao wa burudani.
Je! Wajua maana ya "Kishtobe"?????

Zifuatazo ni picha mbalimbali wakiwa studio wakirekodi...

Waimbaji wa 5Stars.

Mape Kibwana, Anaimba "Sina Ghubu".
Mwanaidi Ramadhani akiimba "Ubaya hauna Soko".
Salha wa Hammer Q Akiimba "Kishtobe".
Salha akiwa na Ally J (Boss) ambaye amepiga vinanda ktk nyimbo hizo.

Wednesday, November 19, 2014

ISHA MASHAUZI AACHIA NGOMA YAKE MPYA KABISA “SURA SURAMBI”...


 
Isha Mashauzi.
Kuanzia mwishoni mwa wiki hii mashabiki wa taarab waatanza kuusikia rasmi radioni wimbo mpya kabisa wa Mashauzi Classic Modern Taraab unaokwenda kwa jina la “Sura Surambi”. 

Ni utunzi na uimbaji wake Isha Mashauzi na tayari ngoma hiyo imesharekodiwa wikiendi iliyopita kwenye studio za Sound Crafters Temeke jijini Dar es Salaam chini ya producer Enrico. 

“Sura Surambi” inategemewa kuendelea kumweka juu Isha Mashauzi kwa namna alivyoimba wimbo huo na hapana shaka itatosha kabisa kuthibitisha ni kwanini alistahili tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa taarab.

Monday, September 29, 2014

Download:- 'Wema Hauozi Ubaya Haulipizwi' - Asia Mzinga ndani ya Mashauzi Classic -


Pata kuisikiliza nyimbo mpya kutoka kwa Asia Mzinga Mwanamtama ikiwa ni nyimbo yake ya kwanza ndani ya Mashauzi Classic ikiwa ni maandalizi ya Albam Mpya ndani ya Mashauzi, "Sura Surambi" ndio Albamu mpya ijayo.

Isikilize kisha mpe point zake.

Thursday, September 25, 2014

Download na kusikiliza nyimbo mpya ya Isha Mashauzi - Nimlaumu Nani...!!!!


NI NYIMBO MPYA TOKA KWA ISHA MASHAUZI AKIWA KAIMBA KATIKA MIONDOKO YA RHUMBA.

ANASEMA NI KATIKA KUWAONESHA TU KUWA RHUMBA PIA ANAWEZA...!!!

##ISIKILIZE KISHA UMPE POINT ZAKE.

Saturday, September 20, 2014

Download: Nyimbo mpyaa... Sina Makuu - Ashura Machupa - G5 Modern Taarab...


Pata kusikiliza nyimbo mpya uimbaji wake Ashura Machupa ndani ya G5 Modern Taarab,
Huku kinanda kikisimamiwa na: Omar Kisila, Mipango na J Four. Mziki wote na Sauti ni Omar Kisila.

Tuesday, September 16, 2014

Download Nyimbo Mpya Mbili (2):- Hassan Voucher Ft Hasna - Sindano na Golkeeper

Saupi mbili tamu zikiungana wajua utapata nini!?
Ni Hassan Voucher na Hasna Mlamal "Masauti", katika nyimbo mbili "Sindano" na "Golkeeper".

Ni nyimbo nzuri zenye miondoko tofauti ili kukupa ladha tofauti wewe mpenzi wa kusikiliza miondoko tofauti tofauti.

Download hapa na uzisikilize kisha uwape shavu...!!!
 

Saturday, September 13, 2014

Misambano kuja na: Si mie ni Moyo...


Abdul Misambano akiwa mazoezini...!!!

Msanii mkongwe katika miondoko ya Taarabu Tanzania Abdul Misambano yupo mbioni kitoa nyimbo nyingine.

Akiongea na blog hii ya Taarabuzetu.blogspot.com mtu wa karibu na Misambano amesema Nyimbo itaitwa "Si mie ni moyo" na nyimbo ishaanza kufanyiwa mazoezi.

Kama unakumbuka ile nyimbo yake ya "ASU", basi tarajia kupata kitu kizuri na huenda zaidi ya Asu...
Kinanda kinasimamiwa na Mkali mwingine wa Vinanda Tanzania Omary Kisira.

Kaa mkao wa kusubiri...

DOWNLOAD: NGOMA MPYAAA!! MTU MZIMA HOVYO - WAKALIWAO MODERN TARADANCE...



 
Nyimbo imeimbwa na Hamuyawezi Kondo
Chini yake Thabit Abdul...!!!
Isikilize ngoma hii!!

Thursday, August 28, 2014

5STARS:- MPWAPWA MPOOO...!!!! JUMAPILI 31/08/2014...

ALLY J.
KWA MALA YA KWANZA KUNDI ZIMA LA 5STARS LIKIWA LIMEJAA WASANII WENYE VIPAJI, WEEK HII SIKU YA JUMAPILI 31/08/2014 WATAFANYA SHOW YA NGUVU MJINI MPWAPWA.

SHOW ITAKUWA KATIKA UKUMBI WA CCM MPWAPWA, WASANII KIBAO WATAKUWEPO.

MSAGA SUMU ATAKUWEPO KUNOGESHA ZAIDI SHOW HIYO.


JUMAPILI TAREHE 31/08/2014.

NJOO UPATE RAHA UPATE SHOW YA UKWELI KUTOKA KWA 5STARS CHINI YAKE ALLY J...!!

Thursday, August 7, 2014

G5 Modern ilivyopagawisha Flamingo Magomeni!! Pata picha za Wasanii...!!!

Anaitwa Bi. Mwanahawa Ally.
Ashura-Machupa
Ni kundi maalufu la miondoko ya taarab Tanzania, limesheheni waimbaji na wasanii kibao nyota katika miondoko hii ya mwambao!

Taarabuzetu.blogspot.com inaongea na Mkurugenzi wa kundi hili la G5 na kuongelea show yake ya Jumanne wiki hii pale Flamingo Bar Magomeni na kusema kuwa anashukuru sana kwa mashabiki kuwapokea vizuri maana bendi yake imekubalika kuliko karibu bendi zote zinazopiga pale.

G5 wanafanya show Flamingo Bar Magomeni Mwembechai kila siku ya Jamanne.

Pia Ratiba ya G5 iko hivi:-

-Siku ya Ijumaa sikukuu ya nanenane 8/8/2014 watakuwa Kalembo Bar Buguruni kwa kiingilio cha Tshs 5000/=tu
-Siku ya Jumamosi 9/8/2014 watakuwa Sisi Club maeneo ya Msasani kwa kiingilio cha Tshs 5000/=tu.

Wafuatao ni baadhi ya wasanii waliopagawisha pale Flamingo Bar Magomeni Mwembechai... Usikose kuwaone kila Jumanne...!!!

Dullah Kinanda.


Jumanne Ulaya.

Mwamvita-Shaibu

Omary Kisira

Sharifa Kimobitel

Zena

Wednesday, August 6, 2014

CHAMA CHA TAAARABU MBIONI KUFUFUKA...!!! Soma zaidi ndani ...

Mr Amin Salmin, Mkurugenzi wa T Motto
Ni Amin Salmin Mkurugenzi wa T Moto Modern Taarab alianzisha mada baada ya kuhudhulia Kongamano la wasanii katika television ya ITV.

Salmin alisema:- Nimepatwa na mshangao sana ktk kipindi cha malumbano ya hoja kilichorushwa live na ITV mada ilikua nini kifanyike kulinda hati miliki na kazi za wasanii kwa waharamia pamoja na midia kupiga nyimbo bila kumlipa msanii. Hakuna msanii wa taarab wala viongozi walijitokeza zaidi yangu mimi!!, kweli wahusika wa taarab tutafika? wasanii wa bongo movi walijitokeaza kwa wingi, kweli tunajitabua?

Baada ya Amin kutoa mada hii katika mtandao wa Facebook watu wengi walichangia wakisema wasanii wa taarab hawakuwa na taari ya tukio hilo hivyo kungekuwa na taarifa wangeweza kujitokeza na kutoa maoni yao.

Pia wengine walifunguka ki-vingine kwa kusema wasanii wa taarabu wamelala sana hawana habari ya kufuatilia haki zao na wala hawajua haki zao na pia hawana umoja wanajisikia sana...!!
Mr Hamis Slim, Mkurugenzi wa G5 Modern Taarab
Bi Siza Mazongela (Kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Sanaa na Masoko BASATA.
Amin aliendelea kwa kusema:- Inaeleweka wazi kipindi cha malumbano ya hoja hutangazwa wiki moja kabla ya kipindi husika,ila mada ilikua ina umuhimu sana kwani watu wa TRA,Basata,Kosota nk wote walikuwepo ila bado hatuja chelewa itv wao wamechokoza mada bali sisi tunaweza kujipanga tukafanya muendelezo kuna ya muhimu sana kwa faida ya wasani na sanaa kwa ujumla wake pia nadhani tungekua na umoja wetu nadhani ingekua kiunganishi kwetu kwani bongo movi Stive Nyerere ndie alietumika kuwapa taarifa wenzake bado nasisitiza umoja wa taarab unahitajika vyenginevyo tutakua tunatumia nguvu kubwa na maingizo kidogo.
Kuna kitu kinaitwa mrabaha maana yake ni mrejesho baada ya mauzo ya kazi za jasho la msanii kupitia TRA, tujiulize nani kati yetu kapata malipo hayo? kuna mengi ya msingi kwa wasanii na taifa.

Mr Ramadhani Said alisema :-
Amin niamini kwenu itakuwa ngumu mnajisikia sana umoja kwenu ngumu. Sisi tunaona wasanii wengine wanavyoshirikiana tofauti na nyinyi sisi wadau tunaomba sana kuweni na umoja wa kweli.

Mdau
Siza Mazongela akasema:-
Alisemalo Ramadhani Saidi namuunga mkono kwani chama cha taarabu kipo tangu enzi za kina marehem Abasi Mzee, kina Mzee Kibiriti, kina Mzee Mdigo, marehem Khamisi Joji, Bi Daima Abdallah, hao walikua na bend kama ifuatavyo:-
Egyptian, new Extra, Alwatan.
Hizo zote zilikuwa bend za taarabu chama kinaitwa TTA, (TANZANIA TAARABU ASSOCIATION), kimesajiliwa na kinatambulika, wasaanii wakiitwa kwenye vikao hawafiki, kwasasa Mwenyekiti alikua marehem Abrahmani Muchacho katibu nilikua mimi, naomba
Amin Salmin upange siku mimi na wewe twende BASATA tukatafute faili letu nikukabidhi ili tufanye utaratibu wa kuwaita kwenye kikao tufufue chama chetu, je upo tayari?

Sasa ilifikia kuwa Jumatatu ya tarehe 3/08/2014 wawe washafuatilia BASATA.

Mzee Yussuf naye alichangia:- Niko pamoja na nyote ishallah utasimama umoja wetu ila katiba ndio muhimu pia iwe ya kisawa sawa kanuni zisimame vizuri hiyo jtatu niambieni saa ngapi na mie ntakuwa basata.

Matumaini yaliendelea ya uwezekano wa kufanikiwa wa kupata umoja.

Hamis Slim naye kafunguka:- Mimi nawapongeza wote waliochangia na ktk kuongozea nipo tayari na shangazi yangu hapo Siza Mazongela kumsaidia hiyo jumatatu ili kuweza kufanikisha hilo pamoja na Mr Amin Salmin naomba kuwasilisha.
I know kaka mm binafsi nilikuwa napata tabu ktk hili coz hakuna kitu chcht kilicho na mafanikio paipokuwa na utaratibu unaoeleweka kiongozi dini zinaongozwa na misahafu na biblia basi hata inchi inaongozwa na katiba sambamba na chama chcht kile dunia vinaongozwa na katibu kwann sisi nina imani ya dhati inawezekana inshallah wakati sasa umefika na tumalize nguvu zetu ktk hili kwa faida ya wasanii wa vizazi vijavyo wasje wakaichukia tasnia hii tuliyoachia mm mkurugenzi na wasanii wangu wote wa G5 modern taarab tupo tayari kwa hali na mali naomba kuwasilisha.

Bi Siza Mazongela alikuwa serius zaidi kwa kuonesha machungu aliyokuwa nayo kwa kwenda BASATA siku hiyohiyo hakusubiri tena Jumatatu, alienda na kutuletea taarifa hizi:-
"Nimejaaliwa kwenda basata nimekutana na Mkurugenzi wa saana na masoko, jumatatu watakuwa na kikao cha kiofisi tumekubaliana twende Alhamisi, haya kazi kwako mjukuu wangu amini
Amin Salmin, nawale wote walio tayari kwa hili, na nimewaomba watutafutie fail la TTA, ndugu yangu Mzee Yusuf, kwenye faili katibaimo saana kuipitia na kuiboresha, naomba wadau mtuombee mungu atupe wepesi wa kufatilia hili swala".

Safari ya kufanikisha na juhudi zinaonekana, siku ya Alhamisi tarehe 7/08/2014 ndo siku tutakayopata jibu sahihi.

Taarabuzetu.blogspot.com inawatakieni mafanikio mema tupate viongozi wa kuweza kutupa muongozo tuweze kusonga mbele na kufuatilia haki za wasanii.

Monday, August 4, 2014

FIVE STAR KUFANYA SHOW YA NGUVU NANE NANE...!!

Taarabuzetu.blogspot.com imezungumza na kiongozi wa kundi la Fivestar Mr Ally J ambaye ni Muimbaji na mpiga kinanda mahili wa kundi hilo, amesema siku ya Nanenane watapiga show ya nguvu MSATA katika ukumbi wa Msukuma Pub.

Ally J amesema show hiyo itakuwa maalumu kwa wakazi wa maeneo hayo hivyo wasikose kwani hii itakuwa ni kwa ajili yao pamoja na surprise kibao zitakuwepo siku hiyo.

Kundi zima litakuwepo pale, kundi lililosheheni mastaa kibao...!!!
Ally J.
Zenna Mohamed, Mwamvita Shaib, Maryam BSS, Mussa Kijoti, Said Yusuf, Shaban Almas na wasanii wengine kibao watakuwepo kutoa burudani.


USIKOSE...!!!

Wednesday, July 30, 2014

Mashauzi Classic ilivyofanya makamuzi Mwanza...!!!

Kundi la Mashauzi wakiwa ndo wametua Mwanza kwa show za Eid!!!
Isha Mashauzi akiwa jukwaani pamoja na tajiri mtoto wa Mwanza Mr. Hamis Muya katika ukumbi wa Buzuruga Plaza.
Hashim Said akiimba Jukwaani...
Umati wa watu uliojaa Ukumbi wa Buzuruga Plaza wakipata burudani toka kwa MashauziClassic Eid Mosi!!!!
Kundi zima la Mashauzi Classic baada ya kukonga nyoyo za mashabiki wa Mwanza, sasa wataelekea jijini Bukoba kufanya makamuzi ndani ya ukumbi wa Liners Club Siku ya Eid Pili!!!

Baada ya Bukoba Eid Tatu watakuwa Jijini Musoma ndani ya ukumbi wa Magereza.

Mjiandae kupata burudani nzuri kabisa kutoka katika kundi bora kabisa - Mashauzi Classic...!!!!

Thursday, July 24, 2014

DOWNLOAD: "Full Kuenjoy", yake Black Kopa mtoto wa Malkia Khadija Kopa...

Black Kopa na Khadija Kopa (Mama).

Ujio wa Black Kopa mtoto wa Khadija Kopa, ni Sheedah...!!!!

Anakwenda kwa jina la Muhammed Kibwana au Black Kopa pia unaweza kumuita Prince Kopa, mtoto wa Malkia wa mipasha Tanzania Bi Khadija Kopa.

Ni msanii wa Muziki toka muda mrefu kama ilivyo kwa Mama yake, marehemu kaka yake (Omary Kopa) "Apumzike kwa amani", pamoja na ndugu zake wengine wamekuwa na kipaji cha kuimba karibu familia nzima.

Black Kopa yeye anasema ameanza kuimba siku nyingi akiwa amejikita sana katika mziki wa Bongo flaver na ameweza kutoa nyimbo kadhaa, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda, marafiki na familia yake pia wakawa wanamshauri ni kwanini asiimbe taarab wakati sauti nzuri ya kuimba anayo!?.

Hatimae kijana kaamua kujitoa mazima mwaka 2014 na kuachia nyimbo yake inayokwenda kwa jina la "Full kuenjoy".

Black Kopa akihojiwa na Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com
Anasema nyimbo hii inapatikana katika albam ya Ogopa Kopa's Classic Band" ambayo ni bendi changa na ni mpya kabisa inakuja hivi karibuni. Albam itaitwa "Lady with Confidence".

Katika nyimbo hii ameshirikiana na watu takribani wanane, wanne wapiga vyombo na wanne waitikiaji.

Waitikiaji ni:- 1). Warda Mlawa, 2). Shadya Shombeshombe 3). Rukia Manala na 4). Hemed Omary.

Wapiga vyombo ni:- 1). Omary Zungu au Omary Kinanda (Keyboard) 2). Harifa (Keyboard 2), 3). Miraji (Soro Gitaa), 4). Said James au Said Bass (Bass Gitaa).

Black Kopa anakuja kwa kasi anasema mashabiki wajiandae kupata radha mpya kabisa toka kwake na atafanyia remix pia nyimbo za kaka yake Omary Kopa kwa kuziimba.

Mashabiki anaomba saana sapoti yenu.

Tuesday, July 15, 2014

DOWNLOAD NYIMBO 4 MPYAA BADO ZA MOTO KABISA: DAR MODERN...


Kundi zima la Dar Modern Taarab limeachia Albam yake mpya kabisa inayokwenda kwa jina la "UBINAADAM KAZI", Pata kudownload na kusikiliza nyimbo tamu kabisa toka kwao.

Uzinduzi wa Albam hii "UBINAADAM KAZI" utafanyika siku ya Idd Mosi pale Travertine Magomeni.



Pakua hizo nyimbo usikiliza utamu uliopo kisha nakuletea tena nyimbo zingine mbili kali...!!!

DAR MODERN NDO HABARI YA MJINI...!!!

MASHAUZI CLASSIC YAPIGA HODI MWANZA SIKU YA IDD MOSI...!!!

Kundi la Taarab linalofanya vyema katika show zake mbalimbali "Mashauzi Classic" chini ya uongozi wake Isha Mashauzi, siku ya Idd Mosi watafanya show ya Uzinduzi wa Albam yao mpya ya "Asiyekujua hakuthamini!!!

Watakuwa katika ukumbi wa "BUZURUGA PLAZA" na kiingilio kitakuwa Tshs. 10,000/= tu kuanzia saa 3 Usiku mpaka baaaasi!!!

Kutakuwa na wasanii machachari wenye sauti za kuvutia kama Isha Mashauzi (Mkurugenzi), Hashim Said Thania Msomali, Saida Ramadhani, Zubeidah Andunje na wengine walio katika Mashauzi Classic.




SI YA KUKOSA MWANZA...!!!!!!