TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, May 4, 2014

Isha Mashauzi awatesa waimbaji wa kike Taarab katika tuzo za KTMA 2014...


Prezidaa wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhan Mashauzi.
Kwa mala nyingine tena katika tuzo za Kilimanjaro Music Award mwimbaji na Kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic Isha Ramadhan "Mashauzi" ameendelea kushikilia tuzo yake aliyoipata mwaka jana ya MWIMBAJI BORA WA KIKE WA TAARAB...

Katika tuzo hizo mwaka huu 2014 zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City siku ya Jumamosi 3/05/2014, Isha ameweza kuongeza bidii na kujinyakulia pia tuzo mbili zaidi za:-

Mwanamziki bora wa kike wa Taarab,
Mtumbuizaji bora wa kike wa Taarab.


Blog ya taarabuzetu.blogspot.com inakupa pongezi nyingi sana Isaha pamoja na kundi zima la Mashauzi Classic, ni juhudi zaidi.

Jahazi Modern Taarab yazidi kutamba Kilimanjaro Music Awards...

Kundi la Jahazi Modern Taarab linaloongozwa na Mfalme Mzee Yusuph limeendelea kung'ara katika tuzo za Kilimanjaro Music Awards baada ya kunyakua tuzo Nne katika sherehe zilizofanyika Mlimani City Dar es Salaam siku ya Jumamosi 3/05/2014.

Katika tuzo hizo Jahazi imezidikushikilia Tuzo yake ya KUNDI BORA LA TAARAB.


TUZO ZINGINE ZA JAHAZI NI:-

Wimbo bora wa taarabu Wasiwasi wako, - Mzee yusuph
Mwanamziki bora wa kiume wa taarab ni -  Mzee YusuphMtunzi Bora wa mwaka - Mzee Yusuph

Pongezi nyingi sana toka kwa blog ya taarabuzetu.blogspot.com kwako Mfalme Mzee Yusuph na Kundi zima la Jahazi Modern Taarab kwa kutwaa tuzo.