TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, June 22, 2014

Jahazi Modern Taarab yafunika uzinduzi wa albam ya "Chozi la Mama"...

Kundi la Jahazi Modern Taarab chini ya ukurugenzi wake Mfalme Mzee Yusuph usiku wa kuamkia leo Jumapili imewezi kufanikisha uzinduzi wa albam yake inayokwenda kwa jina la "Chozi la Mama", show ilikuwa nzuri na watu walifurika na kufurahia.
Mfalme Mzee Yusuph akisalimia mashabiki...

Mashabiki walicheza walivyoweza.

Meneja wa Jahazi Modern Taarab, Mohammed Rashid Mauji 'Father Mauji' pamoja na shabiki wa Jahazi wakizindua albamu mpya iitwayo "Chozi la Mama" ndani ya ukumbi wa Dar Live.

Mzee Yusuf (kulia) akiongea jambo kabla ya uzinduzi wa "Chozi la Mama". Katikati ni Aisha Abushily 'Mama wa madikodiko' kutoka Kenya.
Mzee Yusuf akiimba wimbo wa Chozi la Mama uliobeba jina la albamu iliyozinduliwa.

Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Mohammed Ally akiimba wimbo 'Kazi Unayo' kabla ya uzinduzi wa albamu mpya iitwayo Chozi la Mama.



Sunday, June 15, 2014

Download na kusikiliza nyimbo mpya ya Amidu:- Tiba ya Mapenzi - toka Jahazi Modern Taarab...


Khadija Yusuph anafaa kuwa mwimbaji bora wa Taarab Tanzania!??...

Anaitwa Khadija Yusuph Sauti ya Chiriku.
Aliyetokelezea wiki hii, mkumbuke enzi zile mdogo akiwa na East Africa Melody (watoto wa mjini), baadae Zanzibar Stars kisha JAHAZI (wana nakshi nakshi) akapita Five Stars (watoto wa bongo) akarudi Jahazi.

Ni sauti ya Chiriku ukisikia mwingine ni dublicate, huyo anafahamika kama Khadija Yussuf Mwinyi mwimbaji anaechapakazi sambamba na kaka yake ndani ya Jahazi Modern Taarab. Ni mwimbaji mzoefu mwenye sauti ya mvuto aimbapo kama ulivyosikia nyimbo akiwa na bendi tofauti.

Baadhi ya nyimbo alizoimba ni Mkodombwe, Zilipendwa, Uso wa guzo, Fisadi kiwembe (EAST AFRICA MELODY).
Langu jicho, Sitaki (ZANZIBAR STARS),
Riziki mwanzo wa chuki, Nimeokota kidude/title error (Five Stars).

Akiwa anapatikana Jahazi sasa hivi kabla ya kuondoka aliimba nyimbo za Mkuki kwa nguruwe, Hamchoki kusema, Kazi ya karima haingiliwi akarudi tena kwa spidi kubwa na kuachia vibao motomoto kama vile "Wagombanao ndio wapatanao" aliyoimba na kaka yake Mzee Yussuf, nyingine zilizobamba ni Nilijua mtasema, Zibeni njia, Mambo bado na hivi sasa ameachia wimbo mpya ambao unategemewa kushindaniwa Ktma 2015 kwa atakaejaaliwa.
Wimbo huo ni Hasidi hana sababu.

Zisikilize kwa makini nyimbo zake kihususani
1 Zilipendwa EAMELODY
2 Langu jicho ZNZSTARS
3 Mkuki kwa nguruwe JAHAZI
4 Riziki mwanzo wa chuki FIVE STARS
5 Hasidi hana sababu/Mpya JAHAZI

Kuna nyimbo zingine kama:
** Mdudu wa Sikio
** Mambo bado.

Ukisha kuzisikiliza kwa makini jiulize anafaa kuwa mwimbaji bora wa Taarabu kule KTMA kwa msimu ujao?

Kihistoria tukimtoa Khadija Kopa mwanzilishi pekee wakike anaetamba kwa sasa basi Khadija Yussuf anafuata, kwa kuthibitisha hili angalia uhusika wake KTMA 2011-2014.

Zibeni njia sio riziki yake, mwacheni mtoto wa watu na yeye ni kiumbe anaemuamini Mungu ni maneno ya wimbo wa Zibeni njia:

"Na moyo sultani na ibada nafanya sana sikupata kwa ubwete
kama sina mwangu ndani, Mola namuomba sana, nafanya kazi nipate".

Pata kusikiliza na kudownload Nyimbo hii ya Jahazi Modern Taarab iliyoimbwa na Rahma Machupa...