TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, November 19, 2014

ISHA MASHAUZI AACHIA NGOMA YAKE MPYA KABISA “SURA SURAMBI”...


 
Isha Mashauzi.
Kuanzia mwishoni mwa wiki hii mashabiki wa taarab waatanza kuusikia rasmi radioni wimbo mpya kabisa wa Mashauzi Classic Modern Taraab unaokwenda kwa jina la “Sura Surambi”. 

Ni utunzi na uimbaji wake Isha Mashauzi na tayari ngoma hiyo imesharekodiwa wikiendi iliyopita kwenye studio za Sound Crafters Temeke jijini Dar es Salaam chini ya producer Enrico. 

“Sura Surambi” inategemewa kuendelea kumweka juu Isha Mashauzi kwa namna alivyoimba wimbo huo na hapana shaka itatosha kabisa kuthibitisha ni kwanini alistahili tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa taarab.