TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, September 20, 2015

Aysher Othman (Vuvuzela) ajifungua mtoto wa kike (Baby Girl), wadau wampongeza, angalia hapa...!!

Ajifungua kwa Operation.

Aysher Othman akiwa bado na Mimba, wakati huo hajui atajifungua mtoto wa aina gani, Hongera zake kwa uvumilivu wote akiwa mja mzito.
Pongezi toka facebook kwake Monte Hakunaga...
Pongezi toka facebook kwake Maureen Mnyele...

Baby Girl, karibu katika Ulimwengu wa "mateso" lakini tutakulinda mpaka hapo utakapokuja kujua mema na mabaya.
Timu nzima ya blog hii www.taarabuzetu.blogspot.com inatoka pongezi nyingi sana kwa mama ...., bibie Aysher kwa kupata mtoto, pia pole sana kwa kujifungua kwa Operation.

Tuesday, August 25, 2015

Download Nyimbo Mpya ya Professor - "I love u mara millioni". Kuna watu wanaimba bwana...!!!!


Anaitwa Professor MK katoa kibao chake murua cha Taarab.
Katika kuonesha umahiri wake, nyimbo inaitwa "I love u mara millioni" ni msanii kutoka Wajela jela Zanzibar.

Download na kusikiliza hii nyimbo safi kabisa, kuna watu kumbe wapo wanaimba...!!!

TAMASHA LA COST NITE KUAHIRISHWA...!!!


Mratibu wa tamasha la Coast Nite Bw Emmauel ameeleza sababu zilizo pelekea kuailishwa kwa tamasha hilo lililo kua lifanyike ijumaa tar 28/8 escape One. 


Mratibu huyo kwanza amesema gharama ya kibali cha kufanya tamasha iko juu sana.
Pili kibali cha kuingiza wasanii toka nje ya nchi pia kiko juu sana na
Tatu kodi wanayo takiwa kulipa wasanii toka nje ya nchi ni kubwa ambayo them mashurooms wameilalamikia.

Mwisho Bw Emmanuel ametumia nafasi hii kuyashukuru makampuni yaliyo jitokeza kudhamini tamasha hilo ya precision air, clouds, push, ic, dasami, kapari, eventlites na mwananchi na kuahidi udhamini huo utatumika hapo mbeleni.

Kiongozi wa Them Mashurooms Band Bw John Katana amesema hawakuwa tayari kulipa kodi ya asilimia 15 kutoka kwenye mapato yao kwa kuwa kwanza iko juu sana ukilinganisha na kwao pili awakupewa taarifa mapema juu ya kodi hiyo hivyo anatalajia waandaaji kampuni ya On Point Solutions Ltd watazingatia hayo watakapokuwa tayali hapo baadae.

Friday, August 7, 2015

Download AUDIO MPYA: Mr & Mrs Hammer Q - Vijumba Jumba - Wamekuja ki - Vingine...

Mr & Mrs Hammer Q
Ni Mr & Mrs Hammer Q katika nyimbo Mpya waliyoipa jina la "Vijumba Jumba".

Ni nyimbo Tamu, Nyimbo nzuri iliyo tofauti kabisa na Miondoko ya Taarabu za hivi sasa, ni Taarabu asilia iliyoimbwa na watu wawili Mr & Mrs, wakiimba kwa kupokezana, utaipenda.

Hammer Q ameongea na blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com na kusema yupo katika mkakati kabambe wa kurudisha Taarabu asilia ile Taarabu ya kipindi kileee...!!

Ni nyimbo nzuri kusikiliza na Familia yako, Sherehe na Popote pale unaisikiliza kwa raha zako.


Download hapa uisikilize:-

Saturday, August 1, 2015

ANGALIZO: Viwanja vya wasanii wilayani Mkuranga...

Mkurugenzi wa Global One Group Bw Adam Emmanuel amewataka wasanii kua makini katika swala zima la umiliki wa ardhi.

Bw Adam ametoa angalizo hilo kufatia kupewa taarifa ya uwepo wa viwanja kwa ajili ya wasanii wilayani mkuranga mkoa wa pwani jambo lililo mfanya kufika ofisi ya aridhi wilayani humo na kupewa taratibu za kupata kiwanja katika maeneo yaliopimwa kwanza unanunua fomu tsh 15,000 pili ombi lako likipita kwa kiwanja cha makazi sq mita 1 ni tsh 3,250/ na ujazo wa chini ni sq 400 na baada ya hapo unasubili hati inapokua tayari unalipia tsh 20,000/ na kukabiziwa hati yako.

Hivyo swala la viwanja vya wasanii kwa garama ya tsh 50,000/ linaleta mashaka makubwa sana utalatibu wa kupata kiwanja halali cha serikali unalipia 15,000/ ya fomu ya maombi, ukipata unapewa ofa na unatakiwa kulipia tsh 3,250/ kwa sq mita 1 na unapoitwa kuchukua hati unalipia tsh 20,000/ unakabiziwa hati yako, malipo yote yanafanyika kupitia benk ya NMB.

Hofu hii inakuja kwa kuwepo taarifa ya viwanja vya wasanii kwa garama ya tsh 50,000/.


Onyesho la COAST NITE lasogezwa mbele kidogo...


Onyesho la COAST NITE na THEM MASHUROOMS BAND toka kenya lililo kua lifanyike leo Jumamosi tar 1/8/2015 sasa kufanyika Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu pale pale ESCAPE ONE mikocheni.

Karibuni sana na Poleni kwa usumbufu / Mabadiriko haya.

UNAWEZI KUAMINI KUWA TANZANIA HAKUNA TAARAB SIKU HIZI...!? Muziki wa Taarab unautata ...! HEBU SOMA HAPA...

-->
Muziki wa Taarab unautata wa vyanzo viwili.

1. Kuna wanaosema taarab iliingia nchini mwetu kupitia ikitokea Mombasa.

2. Kuna tafiti nyingine ambazo zinaonyesha Sultan Barghash wa Zanzibar aliwapeleka wanamuzikiwawili Misri kujifunza upigaji wa Taarab,na hao waliporudi ndo walipanda mbegu ya Taarab nchini mwetu.

Taarab imekuwa nahistoria ambayo ya kuwa na aina nyingi za taarab, na mpaka leo mabadiliko ya taarab yanaendelea. Imefikia sasa kuna hata vikundi vya taarab vina wacheza show. Taarab imekuwa pia ni ya kucheza na si kusikiliza ujumbe tu kama ilivyokuwa zamani.

-->


Tunaweza kukubaliana mabadiliko katika kila kitu kwamba hata binadamu ana mabadiliko ya marika yaani utoto, ujana, umakamo, uzee hatimaye ukongwe.

Mabadiliko haya ya kimaumbile hayamfanyi mtu/binadam abadilike kuwa ngedere. Lakini si vyema kumfananisha au kughafilisha wasifu wa mtu/mwanadamu na ngedere. Kwa sababu mtu/mwanadamu asilani atabaki kuwa mtu/mwanadamu hali kadhalika ngedere asilani atabaki kuwa ngedere.

Taarab ni taarab na huu muziki mpya ambao bado haujapata jina kamili iwe ni mipasho au rusha roho utabakia kuwa rusha roho au mipasho na asilani huwezi kuwa taarab.

Kuhusu maswali ya hapo juu yanaweza kujibiwa na tafiti nyingi kuhusu muziki wa Taarab zilizoandikwa na kurekodiwa na taasisi na watafiti mahiri wa muziki (Outstanding Musicologists) kama vile kina Said A.M. Khamis, Werner Graebner, Mohamed El-Mohammady Rizk, K.M. Askew, Global Music Centre na vyuo vikuu mbali mbali hususani vya Ulaya na Marekani.

ZAIDI: Said A.M. Khamis anapagawishwa na mabadiliko katika nidhamu ya muziki wa Taarab - Wondering About Change: The Taarab Lyric and Global Openness. Nordic journal of African Studies 11(2): 198-205 (2002). Said A.M. Khamis* University of Bayreuth, Germany. (http://www.njas.helsinki.fi/pdf-files/vol11num2/khamis2.pdf). Nadhani Bwana Said A.M. Khamis tupo kwenye upande mmoja wa mtazamo kwamba hii iliyokuja sasa ni mipasho au rusha roho ni aina nyingine ya muziki na siyo taarab.





-->
Wengi wanapagawishwa na mabadiliko yanayoendelea ambayo yanatokana na sababu nyingi, lakini pia ni vizuri kujiuliza kama taarab "halisi" ni ipi ambayo ndicho kipimo cha taarab.

Kipimo changu cha taarab halisi kinaanzia kwenye tungo (Ushairi wenye vina na maudhui au hata kama ni bashrafu ni bashrafu iliyopigika katika mtindo na ala za okestra ya taarab).

Tofauti nyingine imelalia kwenye muziki wa Taarabu: kimuziki (ala zitumikazo, mtindo wa muziki unaopigwa kimapigo (Rhythm), ghani (melody), na mwafaka (harmony). Halafu linakuja suala la nidhamu ya muziki wa taarab: Mtindo wa utumbuizaji wa muziki wa taarab (presentation style) kuanzia wajihi wa wanamuziki (performers personalities), muundo ukaaji jukwaani (stage arrangement), mtindo wa jukwaani na majukwaa (stage setting and arrangement), mazingira ya utumbuizaji (performance aura), wahudhuriaji na aina wahudhuriaji onyesho (audience and audience target/ audience demography). vigezo hivyo nilivyovitaja na vinginevyo ndivyo vinavyoitofautisha taarab na chakacha au na mipasho au rusha roho.

Kabla ya mipasho na rusha roho palikuwepo chakacha lakini haikuwahi kutokea kuchanganya taarab na chakacha. Au siyo?

Haya mambo ndiyo ya kutaka serikali ya sultani iteue Sultani mwanamke. Ikishateuliwa Sultani mwanamke huo si usultani tena. Au Vatikani wamchagua Papa mwanamke, ikitokea kuchaguliwa papa mwanamke huo si Ukatoliki tena.

Vivyo hivyo ikiwa kama taarabu itapigwa kwa ala za muziki wa dansi, na wacheza shoo tena shoo hizi za kiwana mipasho, na tungo zisizo za kishairi na maneno yasiyo na staha, na kupigwa kwenye kumbi za vilevi basi hiyo si taarab ni mipasho au rushaa roho na si taarab.

Hebu niambie leo ukute watu wanapiga muziki wao kwa kutumia accordian, gitaa baridi na manyanga halafu wakuambie hii ni heavy metal, utaafikiana nao au utafikiri wamepatwa na ugonjwa wazimu.

Sunday, July 19, 2015

TIZAMA PICHA MZEE YUSUF ALIVYOFUNIKA SIKUKUU YA EID MOSI, DAR LIVE

Mzee Yusuf akizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya Ukumbi wa Dar Live katika Sikukuu ya Eid Mosi.
Fatma Kassim akiwapa raha mashabiki wa Dar Live.
Mfalme Mzee Yusuf akipelekeshana puta na wanenguaji wake wakati wa shoo hiyo ndani ya Dar Live.
Mfalme Mzee Yusuf na malikia wake, Leila Rashid wakinogeshana jukwaani.
Mfalme Mzee Yusuf akifanya yake kwenye kinanda.

Thursday, July 16, 2015

Mr. Hamis Slim achukua Fomu rasmi kwa ajili ya kugombea... Mcheki hapa...

Mr. Hamis Slim akichukua Fomu ya kuwania U - Diwani katika kata ya Mtoni akiwa pamoja na Prince Muumini Mwinjuma.
Hamis Slim aliongea na Blog hii ya Taarabuzetu.blogspot.com na kusema "Leo hii nimechukua fomu ya kuwania udiwani kata ya Mtoni nikisindikizwa na wana ccm wa kata yangu pamoja na swahiba yangu Muumin Mwinjuma.

Bwana Slim ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya G5 Modern Taarab aliongeza "Imani yangu kubwa ni Ushindi ili niweze kuwatumikia wananchi wenzangu wa kata ya Mtoni, ni mengi nimepanga kuyafanya iwapo nitachaguliwa".

Mtandao huu unamtakia kila la kheri katika mbio zake hizi za Uongozi...

Omary Teggo amumwagia sifa kemkem Asya Maryam Utamu...

Asya Maryam "Asya Utamu".
Mkombozi jiandae kupokea mtiti wa watu coz show umeileta mahala sahihi kbs kwn Dar live ni ukumbi unaofanya vzr kwa ss kwa DAR na kikubwa zaidi Album ya "Sioni thamani ya pendo" ni Album ilosheheni nyimbo nzuri sana sana na mwanangu Asya Maryaam ameitendea haki hii nyimbo ameimba vizuri mno.

Kama kawaida yake huyu bint kwani ni mmoja kati ya wanafunzi wangu nnaojivunia walotoka katika mkono wangu leo hii kufika kubeba Album ambayo inafanya vizuri!, ama kwa hakika ni jambo la kujivunia kwangu na kwa Thabit. Maneno ya Omary Tego hayo...!!!
Omary Teggo!!

Saturday, July 11, 2015

Five Star kuvamia mkoani Pwani Idd...


Katika kusherehekea sikukuu ya idd, Five Star kuvamia mkoani pwani.

Akiongea na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Bw Ally Juma (Ally j) amesema EID Mosi watakua MSATA Msukuma Pup- na EID pili watakua LUGOBA SHELL.

Bw Ally J amewataka wakazi wa maeneo husika kujitokeza kwa wingi kusherekea sikukuu kwa burudani toka kwa mwana Five Star.

Endelea pia kutembelea blog hii ya www.taarabuzetu.blogspot.com

Sunday, July 5, 2015

Ratiba hii hapa ya Idd Mosi... Mashauzi, Dar Modern...

ISHA RAMADHANI, MKURUGENZI WA MASHAUZI CLASSIC.

Mashauzi classic modern taarab baada ya kukomba tuzo za kili 2015 wanatalajia kuwaonyesha kazi iliowafanya watwae tuzo hizo wakazi wa Bagamoyo na vitongoji vyake siku ya Idd Mosi.
Show hiyo kali itafanyika katika ukumbi wa Mageti mia.

Akiongea na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com meneja wa bendi hiyo Bw Suma Raga amesema Mashauzi hawajaribu wanafanya.

******************************************


Kushoto Hassan Vocha Msanii wa Dar Modern.

Katika kusherekea sikukuu ya idd On Point Solutions Limited wakishilikiana na Dar modern taarab watafanya onyesho maalum siku hiyo katika ukumbi wa LEKAM PUB Buguruni.
Si ya kukosa.

Friday, July 3, 2015

Hamis Slim wa G5 Modern Taarab atangaza nia...!!!

Mkurugenzi wa G5 Modern Taarab Mr. Hamis Slim
Mkurugenzi wa bendi ya Taarab ya G5 Modern Taarab Mr. Hamis Slim, ametangaza rasmi nia yake ya kuwatumikia wananchi wa Mtoni kwa Azizi Ally.

Hamis alijieleza mwenyewe katika maelezo haya hapa:-

Assalaam aleyko watanzania wenzangu hususani wanamtoni wenzangu, tumshukuru mungu kwa kutufikisha tena salama ktk mwezi huu mtukufu wa ramadhani mwezi ambao unatufanya tumrudie mola wetu kwa kutimiza zile nguzo tano za kiislam.

Pamoja na hayo pia mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi basi itakuwa si vibaya mimi km kijana imara niliyelelewa madhubuti na Chama Cha Mapinduzi kutangaza nia yangu ya kutaka kugombea nafasi ya Udiwani ktk kata yangu ya Mtoni.

Mimi kijana mwenzenu Hamis Slim wakati ukifika nitachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya udiwani wa kata ya Mtoni kwa minajali ya kuleta maendeleo muonekano na si maendeleo simulizi, shime vijana wenzangu tuamke sasa tuungane mkono kulikomboa taifa letu kwa mawazo chanya kwa pamoja tunaweza.

Nitaomba nafasi baada ya kutafakari takribani miaka mitano na kuona fursa nyingi tulizonazo ktk kata ya Mtoni kushindwa kutumiwa kwa maslahi na manufaa ya wananchi wa mtoni
Badala yake kutumiwa na watu wengine wa nje ya mtoni.

Changamoto hizi ndizo zilizonilpelekea kuwa na maamuzi ya kugombea kwa ajili ya kuleta Mabadiliko mapya, Fikra mpya, Ubunifu mpya, Uongozi mpya na kuondoa uongozi ulio na mawazo mgando.

Kwakuwa uwezo ninao sababu ninazo nia ya kugombea ninayo kwa pamoja na wanamtoni wenzangu tutashinda na kuibadili na kuivusha kata ya mtoni pale ilipofikishwa hakika SLIM ndio chaguo lako (HAMIS SLIM HAKIKA ATATUFIKISHA)
Bwana Hamis alipoulizwa kuhusu kugombea Ubunge alisema:-

Naamini kila mtu anatamani kugombea nafasi hiyo ya Ubunge, ni nafsi kubwa sana ambayo nitafanya hivyo baada ya kuwatumikia kwanza wananchi wenzangu na kuona uwezo wangu katika utendaji kazi, nataka wananchi wenyewe waje kusema kama nafaa. Najiamini ipo siku nitakuwa pale Bungeni kutetea na kuleta maendeleo ya wananchi wangu, watanzania wenzangu.

Taarabuzetu.blogspot.com inakutakia kila la kheri Bwan Hamis Slim.


Thursday, July 2, 2015

Onyesho maalum la Coast Nite (Kosa Uchekwe)

Mkurugenzi wa On Point Solution Bw. Bahati.
Mkurugenzi wa On Point Solutions Limited Bw Bahati Singh amewataka wapenzi na mashabiki wa mziki wa enzi hizo kukaa tayari kwa onyesho maalum la COAST NITE (kosa uchekwe).

Bwana Bahati amesema onyesho hilo linatalajiwa kufanyika mwezi ujao Jumamosi ya tar 1 katika ufukwe wa Escape one mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akiongea na mtandao huu Bw Bahati amesema usiku huo maalum utasindikizwa na THEM MUSHROOMS BEND toka jijini nairobi nchini kenya na THE EAST AFRICAN MELODY na DAR MODERN TAARA Za hapa nyumbani tanzania.

Bw Bahati ameongeza kwa kusema hii si ya kukosa "KOSA UCHEKWE"

Dar Modern kutoa nyimbo Sita...

Baadhi ya wasanii wa Dar Modern
Dar Modern Taarab wako katika maandalizi ya nyimbo mpya.

Akiongea na mtandao huu mkurugenzi wa mziki wa bendi hiyo Bw Mlamal Adam amesema kwa sasa wanajianda na nyimbo mpya sita. "Tupo kwenye maandalizi ya kutoa nyimbo sita ambapo zitakuwa tiyari mtazipata hapa www.taarabuzetu.blogspot.com

Majazi Modern Taarab inakuja kuwashika...

Mwimbaji wa Majaz Modern Taarab Mrisho Rajab
Mkurugenzi wa Majazi Modern Taarab Bw Majaliwa amewataka wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo kukaa mkao wa kula kwa ujio mpya wa bendi hiyo.

Akiongea na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com kwa njia ya simu Bw Majaliwa amesema pamoja na ukimya wa muda mrefu lakini bendi yao ipo hai na wanatalajia kurejea jukwaani muda si murefu.
"Baada ya kukaa kwa muda mrefu tukiwa kimya, sasa tupo katika maandalizi makubwa ya ushindani katika tasnia hii ya muziki, tunakuja kuonesha kuwa sisi ni nani katika burudani, hii yote itakuwa baada ya mfungo wa Ramadhani".

Saturday, June 27, 2015

Bendi ya Them Mushrooms kutua Dar es Salaam!!!!

Wasanii wa Them Mushrooms
Kuna tetesi zinazodai kuwa bendi ya Them Mushrooms ya jijini Nairobi inatalajiwa kutua jijini Dar kushiliki kwenye tamasha la COAST NITE linalotalajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza hapa Tanzania mwezi wa nane.

Tamasha hilo ufanyika mara mbili kila mwaka jijini Nairobi kwa kuzishilikisha bendi za taarab toka hapa nchini Tanzani.

Bendi zilizo wahi kushiriki kwenye tamasha hilo ni New Zanzibar star, The East African Melody, TOT taarab, Mashauzi na Dar Modern.
Kwa mwaka huu jijini Nairobi tamasha hilo litafanyika ijumaa ya tar 6 mwezi wa kumi (06/10/2015) na moja na bendi itakayo kwenda itajulikana mwezi ujao wa saba.


Coast Nite ni tamasha lililo sajiliwa Nairobi na sasa tunalisajili Tanzania hivyo litakua linafanyika Nairobi na Dar kila mwaka Lengo letu ni ifikapo 2017 iwepo Afika Mashariki nzima Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda kwani kote huko mazungumzo yanaendelea vizuri. Mmoja wa waandaaji wa Tamasha hilo aliimegea Blog hii ya Taarabuzetu.blogspot.com 

Thursday, June 25, 2015

Je!, Waijua Bendi ya Them Mushrooms ya Nchini Kenya....?????



Them Mashurooms,
Bend ya nchini Kenya ni moja ya bend maalufu afrika mashariki iliyo dumu kwa zaidi ya miaka 40 na imejipatia umaalufu mkubwa barani ulaya kwa ushiliki wao katika maonyesho mbali mbali barani humo.



Pamoja na kua na umri mkubwa lakini bendi hiyo bado ipo imara kama chuma cha reli.
Bendi zilizo wahi kushiliki tamasha la "Coast nite" mjini nairobi toka Tanzania ni New Zanzibar star, Melody, TOT Taarab, Mashauzi na Dar modern.

Baadhi ya picha wakiwa kwenye matamasha hizi hapa:-







Kwa habari zaidi juu ya Them Mushrooms Band utaendelea kuzipata hapa...

Karibu sana.

Saturday, June 13, 2015

Mfalme Mzee Yusuph kutangaza nia kuwania ...

Mfalme wa Taarab Mzee Yusuph, Mkurugenzi wa Jahazi
Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Mfalme wa Taarab Mzee Yusuph siku ya Jumamosi ya tarehe 13/06/ 2015 katika onesho lake pale Travertine Magomeni atatangaza nia.

Mzee yusuph ambaye ni Muimbaji na Mpiga kinanda mahili ameidokezi blog hii ya Taarabuzetu.blogspot.com kuwa, siku hiyo atatangaza nia yake ya kugombea ..... katika kinyang'anyilo kinachokuja. Mmeamua kujitosa kwa kuona kuwa anafaa ila kaahidi kuzungumza mengi zaidi mbele ya mashabiki.

Usikose siku hiyo kumsapoti Mfalme Mzee Yusuph...

Saturday, June 6, 2015

UZINDUZI WA #OGOPA KOPA'Z WASOGEZWA MBELE"...

Malkia Khadija omary kopa
ULE uzinduzi wa kundi jipya la mipasho Tanzania, #Ogopa kopa'z uliyokuwa ufanyike Juni 13 mwaka huu 2015, ndani ya #Escape One, jijini Dar es salaam, umesogezwa mbele ili kuupisha mwezi mtukufu wa #Ramadhan.

Mkurugenzi wa kundi hilo, Malkia Khadija omary kopa alisema jijini Dar es salaam jana akiueleza mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com kuwa, Uongozi wa juu ndani ya kundi lake ulifikiria makubaliano ya kuusogeza mbele uzinduzi huo:-
"Tunaomba radhi mashabiki wetu na tunaahidi kutangaza tarehe nyingine ya uzinduzi hata kabla ya kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan, tumeona ni busara kutoa fursa kwa mashabiki wetu ambao ni Waislam ili kujiandaa na swaumu," alisema malkia au '#Mama #mukubwa'.

"Tarehe rasmi itatangazwa ili wapenzi na mashabiki wote washuhudie Uzinduzi huu wa aina yake ambao naamini haujawahi tokea katika ulimwengu huu wa mipasho". Aliongeza Malkia wa Mipasho.

Huyo ndo Malkia mwenyewe kasema, sisi yetu macho na Masikio...!!!


Baadhi ya Wasanii Nyota wa Ogopa Kopa's

Friday, May 29, 2015

MSIBA:- Mama mlezi wa Dar Modern Taarab afiwa...!!!

Mama mlezi wa Dar Modern Taarab Mrs Nahiy.A Fereshi amefiwa na baba yake mzazi al maarufu mzee kidole jana katika hosipitali ya Hindu mandal.
Marehemu anatalajiwa kuzikwa Matombo Morogoro kesho jumamosi.

Wednesday, May 27, 2015

King's Modern Taarab yakamilisha nyimbo Tatu kali...!!!!




King's modern taarab baada ya kusimama kwa muda mrefu hivi sasa imekamilisha nyimbo tatu kali na inatalajia kuanza kuzifanyia video wiki hii ambayo inaelekea mwishoni mwa mwezi wa tano.

Akiongea na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com mkurugenzi wa bendi hiyo Bw. Nassoro a.k.a Kijoka amesema kwa hivi sasa wako kwenye mazoezi ya nguvu wakijipanga kuwapa wapenzi na mashabiki wao radha ile ile ya King's muda si mrefu.

Kaa mkao wa kiburudani zaidi kusubiria Nyimbo pamoja na Video nzuri kabisa kutoka bendi yako ya King,s, baada ya nyimbo kutoka ni mfurulizo tu wa burudani…!!!