TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, March 30, 2015

Video: Full Ku-enjoy, Soma kilichomo. Coming Soon...

Kaa katika mkao kwa kufaidi!.

Ni Video mpya kabisa inakujia hivi karibuni toka kwa Prince Black Kopa, mtoto wa Malkia wamipasho Tanzani Bi. Khadija Kopa.
Wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka ndivyo ilivyo katika uimbaji wa huyu Prince Black Kopa.

Audio ya hii Video ilitoka miezi kadhaa iliyopita na kutikisa katika anga la musiki huu wa Taarabu, sasa katika kukamilisha hii nyimbo ni zawadi ya Video nzuri kwa mashabiki, video iliyochukuliwa picha na kutengenezwa na kampuni ya Digital Vibe. Video Nzuri, Nyimbo nzuri nakundi zuri Ogopa Kopas Classic.

Katika video hii utapata radha tamu na mchanganyo wa picha toka pande mbalimbali zenye mandhari nzuri Jijini Dar es Salaam na Morogoro.

Video iko full mzuka, kundi zima la Ogopa Kopas Classic utawaona ndani, pamoja na Bi. Zayana (Picha kwenye kava) utamuona akiwa amejiachia mwanzo mwisho.

Baada ya siku chache Video utaiona hapa hapa taarabuzetu.blogspot.com, kaa mkao wa subra...!!!

Monday, March 9, 2015

MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI WATHIBITISHA RASMI MTANANGE WA JAHAZI NA MASHAUZI CLASSIC...



Hatimaye wakurugenzi wa Mashauzi Classic na Jahazi Modern Taarab, wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwepo kwa onyesho la pamoja la makundi hayo yenye nguvu katika muziki wa taarab.

Onyesho hilo litafanyika mwezi huu Jumapili tarehe 22 ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni.

Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi, wamesema siku hiyo hatumwi mtoto dukani.

Wakiongea katika mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu jioni katika hotel ya Travertine Hotel, wakurugenzi hao ambao wote ni waimbaji nyota, wakasema onyesho hilo si mpambano lakini pia sio la masihara kwani kila bendi imejipanga kuhakikisha inaangusha burudani iliyokwenda shule.

Pichani juu kutoka kushoto ni: Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Rashid, Isha Mashauzi, Mzee Yussuf na Seif Magwaru meneja wa Jahazi Modern Taarab.

Tuesday, March 3, 2015

Wimbo maalumu wa Msiba wa Capt John Komba uko hapa...

Ni wimbo ulioimbwa na kikundi cha TOT kwa ushiriki wao Khadija Kopa na Abdul Misambano.