TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, April 1, 2015

Ogopa Kopas Classic kuachia nyimbo 3.! Hodi Nairobi...

Bendi inayokuja kwa kasi hapa Bongo katika tasnia ya musiki wa Taarab Ogopa Kopas Classic inayoongozwa na Malkia wa Mipasho Tanzania Bi Khadija Kopa, inatarajia kuachia nyimbo kali 3.

Akiongea na mtandao huu wa Taarabuzetu.blogspot.com mmoja wa wasanii wa kundi hilo amesema nyimbo zimeweza kurecodiwa na zipo tiyari na kinachosubiriwa ni kuachiwa tu kwa vyombo vya habari, Radio pamoja na blog hii.

Ogopa Kopas bendi inayopendwa Tanzania na nje ya Tanzania inatarajia kufanya shoo ya nguvu siku ya Pasaka katika jiji la Nairobi Kenya, baada ya hiyo show wataelekea Mombasa tena wanakohitajika kufanya shoo nyingine. Nyimbo zote kali zitaimbwa ikiwa na nyimbo mpya tatu...!!!

Baada ya show hizo kali nje ya Tanzania Ogopa Kopas Classic watarudi nyumbani Bongo kuachia nyimbo zao mpya kabisa zikiwa zimeimbwa na wasanii nyota waliojikuta wapo pamoja katika bendi pendwa.

Hivyo baada ya Pasaka ni nyimbo mpya utazisikia toka kwa wasanii pendwa, majina na waimbaji katika hizo nyimbo ni kama unavyozisoma katika picha hii hapa chini!!.


Usikose kabisa kuzisikiliza nyimbo hizi.



Baadhi ya wasanii wa Ogopa Kopas Classic katika picha wakiwa studio.