TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, May 29, 2015

MSIBA:- Mama mlezi wa Dar Modern Taarab afiwa...!!!

Mama mlezi wa Dar Modern Taarab Mrs Nahiy.A Fereshi amefiwa na baba yake mzazi al maarufu mzee kidole jana katika hosipitali ya Hindu mandal.
Marehemu anatalajiwa kuzikwa Matombo Morogoro kesho jumamosi.

Wednesday, May 27, 2015

King's Modern Taarab yakamilisha nyimbo Tatu kali...!!!!




King's modern taarab baada ya kusimama kwa muda mrefu hivi sasa imekamilisha nyimbo tatu kali na inatalajia kuanza kuzifanyia video wiki hii ambayo inaelekea mwishoni mwa mwezi wa tano.

Akiongea na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com mkurugenzi wa bendi hiyo Bw. Nassoro a.k.a Kijoka amesema kwa hivi sasa wako kwenye mazoezi ya nguvu wakijipanga kuwapa wapenzi na mashabiki wao radha ile ile ya King's muda si mrefu.

Kaa mkao wa kiburudani zaidi kusubiria Nyimbo pamoja na Video nzuri kabisa kutoka bendi yako ya King,s, baada ya nyimbo kutoka ni mfurulizo tu wa burudani…!!!

Monday, May 18, 2015

Modern Taarab nani zaidi 2015 yaja...!!!

Aliebuni mpambano wa Modern Taarab nani zaidi 2007 Bw Emmanuel Kalugira aeleza nia yake ya kuurejesha tena mwaka huu baada ya mpambano huo kupolwa na times fm mwaka 2009 baada ya kuupeleka times fm mwaka 2008.

Bw Emmanuel ameuambia mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com kuwa, baada ya kituo alichofanya nacho mwaka 2007 cha C2C tv kubadilisha uongozi wake na ungozi ulioingia kutokua na upenzi na jambo hilo ilio mpelekea kuwasiliana na kituo cha time fm kuwaomba washilikiane kulifanya mwaka 2008.

Baada ya hapo uongozi wa times fm ukatoa kauli zinazosema uongozi haukotayali kushilikiana na mtu katika jambo hilo ndio likazaliwa tamasha la “Mitikisiko ya Pwani”.

Saturday, May 16, 2015

Jitokezeni kwenye maonyesho ya 5stars - Ally J...

Mkurugenzi wa 5Stars Ally J akiwa anawajibika jukwaani.
Mkurugnzi wa five star modern taarab Bw Ally Juma maarufu Ally J amewataka wapenzi, mashabiki na wadau wa taarab kujitokeza kuiunga mkono bendi hiyo. 

Akiongea na Taarabuzetu.blogspot.com Bw Ally J amesema pamoja na misukosuko ilioikuta bendi hiyo  lakini ameamua kusimama kidete kuhakikisha bendi hiyo inasimama imara ili kulinda ajira za wasanii wake wanaojipatia vipato vyao kutokana na vipaji vyao. 

Ally J amewataka wapenzi wa taarab kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho yao na kuyaomba makampuni, mashirika na taasisi kujitokeza kudhamini maonyesho yao pamoja na bendi ili kunusulu ajira za wasanii wa bendi hiyo.

Wednesday, May 13, 2015

HAWA NDIO WASANII WALIOTEULIWA KUWANIA TUZO ZA KTMA 2015. TENDA HAKI KATIKA KUWACHAGUA...!!





Baada ya mchakato wa muda mrefu kupokea maoni ya wapenzi na wadau wa muziki ili kutengeneza vipengele vya tuzo za mwaka huu, hatimae listi imetoka. Hawa hapa ndio wasanii watakao wania tuzo za mwaka huu.

Orodha ya wasanii waliongia katika kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Music Awards 2015:

MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA- KIUME
1. Mzee Yusuf
2. Christian Bella
3. Diamond Platnumz
4. Ally Kiba
MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA- KIKE
1. Vanessa Mdee
2. Khadija Kopa
3. Isha Mashauzi

4. Shaa
5. Dayna Nyange

3.MWIMBAJI BORA WA KIUME - TAARAB
1. Mzee Yussuf

MWIMBAJI BORA WA KIUME - BONGO FLEVA
1. Ali Kiba
2. Ben Pol
3. Jux
4. Diamond
5. Belle 9
MWIMBAJI BORA WA KIUME - BENDI
1. Jose Mara
2. Kalala Junior
3. Khalidi Chokoraa
4. Chaz Baba
5. Nyoshi El Sadat

MWIMBAJI BORA WA KIKE - TAARAB
1. Khadija Kopa

MWIMBAJI BORA WA KIKE - BONGO FLEVA
1. Lady Jaydee
2. Vanessa Mdee
3. Linnah
4. Grace Matata
5. Malaika
MWIMBAJI BORA WA KIKE - BENDI
(Hakukuwa na washindani)


WIMBO BORA WA MWAKA
1. Mwana – Ali Kiba
2. Nani kama Mama – Christian Bella
3. Gere – Weusi
4. Nitasubiri – Jux
5. Bongo Hip Hop – Fid
WIMBO BORA WA KISWAHILI (BENDI)
1. Otilia – FM Academia
2. Kiu Ya Haki – Mashujaa Band
3. Sauti ya Marehemu – Mapacha Watatu
4. Ganda la Muwa – Twanga Pepeta
5. Wale Wale – Vijana Ngwasuma
WIMBO BORA WA R&B
1. Nitasubiri – Jux
2. Unanichora – Ben Pol
3. Vitamin Music – Belle 9
4. Sisikii – Jux
5. Ni Penzi – Damian Soul
WIMBO BORA WA HIP HOP
1. Bongo Hip Hop – Fid Q
2. Mfalme – Mwana FA
3. Kipi Sijasikia – Proffesor Jay
4. Gere – Weusi
5. I See Me – Joh Makini
6. XO – Joh Makini
WIMBO BORA WA REGGA/DANCE HALL
1. Let Them Know – Maua
2. Mama Afrika – Warriors From The East
3. Maisha Magumu – Warriors From The East
4. Greeting For You – Ras Six
5. Tujimwage – Deddy
RAPA BORA WA MWAKA (BENDI)
1. Ferguson
2. Msafiri Diouf
3. Sauti ya Radi
4. J4
5. Kabatano

MTUNZI BORA WA MWAKA- TAARABU
1. Mzee Yusuf 

MTUNZI BORA WA MWAKA- BONGO FLEVA
1. Ally Kiba
2. Diamond
3. Ben Pol
4. Barnaba
5. Jux
MTUNZI BORA WA MWAKA- BENDI
1. Jose Mara
2. Nyoshi El Saadat
3. Rogart Hegga Katapila
4. Hussein Jumbe
5. Richard Mangustino
MTUNZI BORA WA MWAKA- HIP HOP
1. Fid Q
2. Mwana FA
3. Joh Makini
4. Nikki wa Pili
5. Kala Jeremiah
MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA- BONGO FLEVA
1. Nahreel
2. Man Water
3. Mesen Selekta
4. Tudd Thomas
5. Marco Chali

MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA- TAARAB
1. Enrico

MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA- BENDI
1. Allan Mapigo
2. Enrico
3. Said Comorien
4. Amoroso
5. Ababuu Mwana Zanzibar
VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA
1. Mdogo Mdogo – Diamond
2. Nitampata Wapi – Diamond
3. Mwana – Ally Kiba
4. Olethemba – Linah
5. Asante – AY
WIMBO BORA WA AFRO POP
1. Mwana – Ali Kiba
2. Mdogo Mdogo – Diamond
3. Niseme – Yamoto Band
4. Nitakupwelepweta – Yamoto Band
5. Kanyaboya – Mesen Selekta
6. Hawajui – Vanessa Mdee
WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA
1. Nani Kama Mama – Christian Bella
2. Basi Nenda – Mo Music
3. Nitampata Wapi – Diamond
4. Nasimama – Lady Jaydee
5. Historia – Lady Jaydee
.WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA
1. Waite – Mrisho Mpoto
2. Vuma – Vitalis Maembe
3. Tumetoka Mbali – Jagguar Music
4. Mama Shabani – Ifa Band
5. Omwana – B.K Sande
MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKIA
1. Baraka Da Prince
2. Beka Tittle
3. Afromaniac
4. Alice
5. Billnas
.WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA
1. Forever – Lady Jaydee ft Dabo
2. Mfalme – Mwana FA fr G-Nako
3. Kipi Sijasikia – Prof Jay ft Diamond
4. Kiboko Yangu – Mwana FA ft Ali Kiba
5. Kerewa – Shetta ft Diamond
BENDI BORA YA MWAKA
1. FM Academia
2. The African Stars
3. Mapacha Watatu
4. Mashujaa Band
5. Msondo Ngoma


KIKUNDI BORA CHA MWAKA- BONGO FLEVA
1. Yamoto Band
2. Weusi
3. Navikenzo
4. Makomando
5. B.O.B

Monday, May 4, 2015

Bw Bahati Singh akanusha kuwa yeye ni Mkurugenzi wa wa Dar Modern Taarab - Isome hapa usikie alichosema...


Mr Bahati Sigh


Mkurugenzi mkuu wa on point solutions limited Bw bahati singh akanusha uvumi ulioenea ukidai yeye ndie mkurugenzi wa dar modern kwa sasa. 

Akitoa ufafanuzi juu ya swala hilo Bw singh ameuambia mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com kuwa, kampuni yake imefanya makubaliano na bendi hiyo ya Dar Modern wa kuratibu maonyesho sita na baada ya hapo itatazama kama ipo haja ya kuendelea na uratibu huo. 

Bw singh amesisitiza yeye sio mkurugenzi wa Dar modern ila kampuni yake ndio inayoratibu ujio mpya wa Modenika na Dar Modern Taarab.

Sunday, May 3, 2015

Friday, May 1, 2015

Mzee Yusuf: Ni wakati mzuri wa kupunguza marafiki wanafiki...


Sikua na fikra kua ntafika hapa nilipo wakati naanza ilikua mbinde we ukiimbe nini we katika waimbaji utaingia wapi nikasema nathubutu, kipendacho roho ikanitambulisha kwa wananchi na mashabiki wa mziki huu wa morden taarab ambao leo umevamiwa mpk na masela na ma sister duu. Ilikua hivi hadi leo miaka kumi na moja.

Nafafanua kuimba niliimba miaka ya 90 nikiwa na kikundi chetu flani nikaimba G Cleef nikaenda E A Melody kote huko niliimba na siku record lkn mana nikiongeza yote ntakua na miaka mingi.

Kwa leo naitambua hii walonijua watu kisawa sawa ahsanteni niliitwa Professor mpk leo Mfalme Mzee wa starehe.

Ahsanteni sana kwa saport yenu nyote.
Pia ni wakati mzuri wa kupunguza marafiki wanafiki. Ambao wapo humu kwa maslahi yao.

Jahazi Modern Taarab kuzindua Albam mpya...

Waimbaji wa Jahazi Modern Taarab.
 


Kuna tetesi jahazi modern taarab wanampango wa kuzindua albam yao mpya mwanzo wa mwezi huu wa tano, jina la ukumbi, tarehe na siku bado havijajulikana.

Mtandao huu umejaribu kuutafuta uongozi wa Jahazi kuthibitisha hili lakini haukufanikiwa, zaidi tutawajuisha wapenzi wa Jahazi Modern Taarab.