TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 19, 2015

TIZAMA PICHA MZEE YUSUF ALIVYOFUNIKA SIKUKUU YA EID MOSI, DAR LIVE

Mzee Yusuf akizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya Ukumbi wa Dar Live katika Sikukuu ya Eid Mosi.
Fatma Kassim akiwapa raha mashabiki wa Dar Live.
Mfalme Mzee Yusuf akipelekeshana puta na wanenguaji wake wakati wa shoo hiyo ndani ya Dar Live.
Mfalme Mzee Yusuf na malikia wake, Leila Rashid wakinogeshana jukwaani.
Mfalme Mzee Yusuf akifanya yake kwenye kinanda.

Thursday, July 16, 2015

Mr. Hamis Slim achukua Fomu rasmi kwa ajili ya kugombea... Mcheki hapa...

Mr. Hamis Slim akichukua Fomu ya kuwania U - Diwani katika kata ya Mtoni akiwa pamoja na Prince Muumini Mwinjuma.
Hamis Slim aliongea na Blog hii ya Taarabuzetu.blogspot.com na kusema "Leo hii nimechukua fomu ya kuwania udiwani kata ya Mtoni nikisindikizwa na wana ccm wa kata yangu pamoja na swahiba yangu Muumin Mwinjuma.

Bwana Slim ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya G5 Modern Taarab aliongeza "Imani yangu kubwa ni Ushindi ili niweze kuwatumikia wananchi wenzangu wa kata ya Mtoni, ni mengi nimepanga kuyafanya iwapo nitachaguliwa".

Mtandao huu unamtakia kila la kheri katika mbio zake hizi za Uongozi...

Omary Teggo amumwagia sifa kemkem Asya Maryam Utamu...

Asya Maryam "Asya Utamu".
Mkombozi jiandae kupokea mtiti wa watu coz show umeileta mahala sahihi kbs kwn Dar live ni ukumbi unaofanya vzr kwa ss kwa DAR na kikubwa zaidi Album ya "Sioni thamani ya pendo" ni Album ilosheheni nyimbo nzuri sana sana na mwanangu Asya Maryaam ameitendea haki hii nyimbo ameimba vizuri mno.

Kama kawaida yake huyu bint kwani ni mmoja kati ya wanafunzi wangu nnaojivunia walotoka katika mkono wangu leo hii kufika kubeba Album ambayo inafanya vizuri!, ama kwa hakika ni jambo la kujivunia kwangu na kwa Thabit. Maneno ya Omary Tego hayo...!!!
Omary Teggo!!

Saturday, July 11, 2015

Five Star kuvamia mkoani Pwani Idd...


Katika kusherehekea sikukuu ya idd, Five Star kuvamia mkoani pwani.

Akiongea na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Bw Ally Juma (Ally j) amesema EID Mosi watakua MSATA Msukuma Pup- na EID pili watakua LUGOBA SHELL.

Bw Ally J amewataka wakazi wa maeneo husika kujitokeza kwa wingi kusherekea sikukuu kwa burudani toka kwa mwana Five Star.

Endelea pia kutembelea blog hii ya www.taarabuzetu.blogspot.com

Sunday, July 5, 2015

Ratiba hii hapa ya Idd Mosi... Mashauzi, Dar Modern...

ISHA RAMADHANI, MKURUGENZI WA MASHAUZI CLASSIC.

Mashauzi classic modern taarab baada ya kukomba tuzo za kili 2015 wanatalajia kuwaonyesha kazi iliowafanya watwae tuzo hizo wakazi wa Bagamoyo na vitongoji vyake siku ya Idd Mosi.
Show hiyo kali itafanyika katika ukumbi wa Mageti mia.

Akiongea na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com meneja wa bendi hiyo Bw Suma Raga amesema Mashauzi hawajaribu wanafanya.

******************************************


Kushoto Hassan Vocha Msanii wa Dar Modern.

Katika kusherekea sikukuu ya idd On Point Solutions Limited wakishilikiana na Dar modern taarab watafanya onyesho maalum siku hiyo katika ukumbi wa LEKAM PUB Buguruni.
Si ya kukosa.

Friday, July 3, 2015

Hamis Slim wa G5 Modern Taarab atangaza nia...!!!

Mkurugenzi wa G5 Modern Taarab Mr. Hamis Slim
Mkurugenzi wa bendi ya Taarab ya G5 Modern Taarab Mr. Hamis Slim, ametangaza rasmi nia yake ya kuwatumikia wananchi wa Mtoni kwa Azizi Ally.

Hamis alijieleza mwenyewe katika maelezo haya hapa:-

Assalaam aleyko watanzania wenzangu hususani wanamtoni wenzangu, tumshukuru mungu kwa kutufikisha tena salama ktk mwezi huu mtukufu wa ramadhani mwezi ambao unatufanya tumrudie mola wetu kwa kutimiza zile nguzo tano za kiislam.

Pamoja na hayo pia mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi basi itakuwa si vibaya mimi km kijana imara niliyelelewa madhubuti na Chama Cha Mapinduzi kutangaza nia yangu ya kutaka kugombea nafasi ya Udiwani ktk kata yangu ya Mtoni.

Mimi kijana mwenzenu Hamis Slim wakati ukifika nitachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya udiwani wa kata ya Mtoni kwa minajali ya kuleta maendeleo muonekano na si maendeleo simulizi, shime vijana wenzangu tuamke sasa tuungane mkono kulikomboa taifa letu kwa mawazo chanya kwa pamoja tunaweza.

Nitaomba nafasi baada ya kutafakari takribani miaka mitano na kuona fursa nyingi tulizonazo ktk kata ya Mtoni kushindwa kutumiwa kwa maslahi na manufaa ya wananchi wa mtoni
Badala yake kutumiwa na watu wengine wa nje ya mtoni.

Changamoto hizi ndizo zilizonilpelekea kuwa na maamuzi ya kugombea kwa ajili ya kuleta Mabadiliko mapya, Fikra mpya, Ubunifu mpya, Uongozi mpya na kuondoa uongozi ulio na mawazo mgando.

Kwakuwa uwezo ninao sababu ninazo nia ya kugombea ninayo kwa pamoja na wanamtoni wenzangu tutashinda na kuibadili na kuivusha kata ya mtoni pale ilipofikishwa hakika SLIM ndio chaguo lako (HAMIS SLIM HAKIKA ATATUFIKISHA)
Bwana Hamis alipoulizwa kuhusu kugombea Ubunge alisema:-

Naamini kila mtu anatamani kugombea nafasi hiyo ya Ubunge, ni nafsi kubwa sana ambayo nitafanya hivyo baada ya kuwatumikia kwanza wananchi wenzangu na kuona uwezo wangu katika utendaji kazi, nataka wananchi wenyewe waje kusema kama nafaa. Najiamini ipo siku nitakuwa pale Bungeni kutetea na kuleta maendeleo ya wananchi wangu, watanzania wenzangu.

Taarabuzetu.blogspot.com inakutakia kila la kheri Bwan Hamis Slim.


Thursday, July 2, 2015

Onyesho maalum la Coast Nite (Kosa Uchekwe)

Mkurugenzi wa On Point Solution Bw. Bahati.
Mkurugenzi wa On Point Solutions Limited Bw Bahati Singh amewataka wapenzi na mashabiki wa mziki wa enzi hizo kukaa tayari kwa onyesho maalum la COAST NITE (kosa uchekwe).

Bwana Bahati amesema onyesho hilo linatalajiwa kufanyika mwezi ujao Jumamosi ya tar 1 katika ufukwe wa Escape one mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akiongea na mtandao huu Bw Bahati amesema usiku huo maalum utasindikizwa na THEM MUSHROOMS BEND toka jijini nairobi nchini kenya na THE EAST AFRICAN MELODY na DAR MODERN TAARA Za hapa nyumbani tanzania.

Bw Bahati ameongeza kwa kusema hii si ya kukosa "KOSA UCHEKWE"

Dar Modern kutoa nyimbo Sita...

Baadhi ya wasanii wa Dar Modern
Dar Modern Taarab wako katika maandalizi ya nyimbo mpya.

Akiongea na mtandao huu mkurugenzi wa mziki wa bendi hiyo Bw Mlamal Adam amesema kwa sasa wanajianda na nyimbo mpya sita. "Tupo kwenye maandalizi ya kutoa nyimbo sita ambapo zitakuwa tiyari mtazipata hapa www.taarabuzetu.blogspot.com

Majazi Modern Taarab inakuja kuwashika...

Mwimbaji wa Majaz Modern Taarab Mrisho Rajab
Mkurugenzi wa Majazi Modern Taarab Bw Majaliwa amewataka wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo kukaa mkao wa kula kwa ujio mpya wa bendi hiyo.

Akiongea na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com kwa njia ya simu Bw Majaliwa amesema pamoja na ukimya wa muda mrefu lakini bendi yao ipo hai na wanatalajia kurejea jukwaani muda si murefu.
"Baada ya kukaa kwa muda mrefu tukiwa kimya, sasa tupo katika maandalizi makubwa ya ushindani katika tasnia hii ya muziki, tunakuja kuonesha kuwa sisi ni nani katika burudani, hii yote itakuwa baada ya mfungo wa Ramadhani".