TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, January 27, 2015

Audio: Hivi ndivyo nilivyo - Thania Msomali...


Ni zamu ya Thania Msomali katika Safari ya mziki huu wa Taarab, hapa ana single yake mpya kabisa na ndo mwanzo wake katika maandalizi ya kuweza kutoa Albam yake.

Anaomba sapoti kwa mashabiki wooote.

Download na kuisikiliza hapa.

Friday, January 23, 2015

HIVI NDIVYO NILIVYO...!!! NI Thania Msomali huyo baada ya kutoka Mashauzi!!!!.


Ni Thania Msomali huyo anakuja na kitu "Hivi ndivyo nilivyo", ni msanii machachali sana asiyependa masihara awapo mbele ya MIC, anapenda kazi, anapenda kujituma ili kuwaridhisha mashabiki wake.

Thania Msomali ametokea mbali katika sanaa hii ya Taarab, kwani ameanza safari yake ya muziki akiwa 5Stars akaja T-Moto kisha akajiunga na kundi la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi, pamoaja na juhudi zake zote katika mziki anasema Mwalimu wake aliyemfanya afike hapo alipo ni mtaalamu wa kupapasa Vinanda anayekwenda kwa jina la Omary Kisira, aliyempika na akapikikika haswa.
Thania amejiengua mwenyewe katika kundi la Mashauzi baada ya kuona kuwa sasa anaweza kufanya kitu yeye kama yeye.

Thania aliiambia blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com kuwa, maandalizi yake ya kutoa hii nyimbo yameanza muda mrefu ili kuhakikisha anatoa kitu kilicho bora maana ndo nyimbo yake ya kwanza anayotarajia kumuinua katika gemu hili!, hajakurupuka bali amejiandaa na amefanya mazoezi ya kutosha.

Hapa katuonjesha baadhi ya mistari iliyomo katika hiyo nyimbo:-
"Namshukuru mola manani kunipa wazazi bora duniani wamenilea kwa dira wakanifunza Ihsani.
Ooh mimi nipo simple jamani tenamodel wa ukweli mwenye heshima mm naogopa sana kujivunjia heshima uwongo kwangu ni ghali napenda twabia njema.
Tangu mdogo nimekuwa naridhika na changu kutwa kucha zangu dua nisigombane na watu".


Baada ya siku mbili nyimbo utaipata hapa...!!!

Thania kama msanii mchanga, amekubaliana na changamoto zote atakazokumbana nazo, pia anawasihi wasanii wote kupendana na kusaidiana pale unapoona mwenzako amekwama au anakwenda sivyo, hata mawazo tu.

"Napenda kuwashukuru wale wote waliofanikisha kwa mimi kuwepo hapa nilipo:- Walimu wangu Fikirini Urembo na Kibibi Yahaya, vilevile nitakuwa mwizi wa fadhila kukosa kutoa shukrani zangu kwa walimu wangu waliopita ambao ni Ally Jay, Shaibu wa Mwamvita pamoja na Kali Kiti Moto Mafya.
Namalizia na pongezi kubwa ziwaendee Amin Salmin mkurugenzi wa T-Moto pamoja nae Ismail Suma Ragger meneja wa mashauzi classic".

Anaomba wapenzi wote wa Taarab kumpokea na wausikilize kwa makini wimbo wake huo ili wajue ni nini kaimba, na zaidi ya yooote! huu ni mwanzo tu yaani mvua za rasharasha masika inakuja, ni mvua ya mawe kama si Elinino.