TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, February 16, 2015

Unajua kilichompata Msanii Hammer Q siku ya Wapendanao (Valentine's Day)!!?, Kisome hapa...

Hammer Q.
Kwa maelezo yake mwenyewe Hammer Q alichofanyiwa huko Mbagala alikiandika katika ukurasa wake wa facebook nami nakuletea hapa kama alivyoandika mwenyenye, hii inaitwa "Copy and Paste".



Ndugu zangu napenda kuwataarifu mtu yeyote atakaekupigia cm au kukusms kwa jambo lolote lile kupitia namba yangu ya cm huyo mtu sio mimi kuanzia usiku wa jana,,, maana watu kadhaa tayari wameshataka kutapeliwa kupitia hiyo namba

Jambo jengine siku ya jana niliwekwa ktk kituo kidogo cha polisi kilichopo maji matitu mbagala kwakosa la mimi kuibiwa cm na dj mmoja anaejulikana km dj shushu ambae anafanya kazi ktk bar moja iliyopo mbagala mzambarauni inaitwa GEMA ambapo mimi niliitwa kwa ajili ya kwenda kuchukua advance kwa ajili ya show ya jumamos ijayo nilipofika pale nilikuta kuna show ambapo alikuwepo joha kassim,, bwana misosi na dogo Amiri lkn bwana misosi hakutokea alikua na msiba ndipo menej wa bar /ukumbi ule akaja kuniomba kabla ya jumamosi ya show nakave ile nafasi ya bwana misosi kwa makubaliano mengine sikukataa lkn nikamwambia meneja siwezi kufanya show na cd hasa sehem km nafanya show na band akaniomba nipande hata kwa nyimbo moja tu nikamkubalia ila wanasema hawakuwa na nyimbo zangu kwenye mashine yao na nikaonane na dj nilipofika kwa dj akaniuliza nyimbo zako zipo kwrnye cm nikamwabia zipo akaomba nimuachie cm yangu kwa ajili ya kuchukua nyimbo nikamkabidhi kwa mashart ya kwamba cm yangu iwe salama akakubali nikarudi kwenye meza yangu kusubiri mda wa jukwaani lkn km dakika kumi akaniita kupitia mic nilipofika ananiambia kwanini nimechukua cm bila kumwambia nikamshangaa sababu sikurudi kufata cm nayy muda wote aliku ktk lile eneo lake la kazi akajikubalisha ku imepotea mikononi mwake.

Tukakubaliana niondoke na mashine moja inaitwa numack lkn wakati nimechukua nikiwa naondoka lilitokea kundi la watu akiwemo huyo dj na mwenye ukumbi wakanikaba nikiwa kwenye pikipiki nikadindoka wakaichukua ile mashine na wakanitukana na baunsa wao kutishia kunipiga ila hawakunipiga baada ya hapo nilienda kituoni lkn wakati nataka kuchukua pikpik kwa ajili ya kwenda kituoni yule mkurugenz aliwakoromea madereva bodaboda kuwa atakaenipakia yoyote asirudi tena pale hakuna alietaka kunipakia ikanibidi kutaka kutembea na miguu kwenda kituoni ila kabla sijafika mbali boda boda mmoja alikuja speed nakuniambia dandia pkpk tuondoke hao maana wakimkamata watampiga alikua bwamdogo flan akanipeleka kituoni nikafungua kesi nikapewa barua ya kumpelekea dj ili aende kituoni.

Wakati nishapewa barua ya polisi nataka kuondoka kituoni ikatoke defender nikamskia askari mmoja akisema huyu **ma huyu hapa wakasimamisha gari na kunifata.

Tukiwa palepale nnje kituoni kuna askari mmoja alionekana kunijua vyema akawa anawafahamisha wenzake hapo kila askari aliongea lake kuna alienitukana kuna alienikashifu mpk mmoja akaniambia huyu mzanzibari tu hatwambii kitu DAH HIYO ILINIUMA SANA SANA nikakutwa nakunjwa na askari huyo nikabebwa nakuingizwa kituoni nikanyang'anywa zile barua zao walizonipa nakuniambia kuwa nimeharibu vyombo vya mziki (sio kweli) sababu sikugusa chombo zaidi ya nilichopewa na dj pia ikaja kauli nimeiba ile numCk (sio kweli) sababu ndio ilokua inatumika kwenye show.

Nikawekwa kituoni mpk Asubuh ya leo nikatoka kwa dhamana lkn nikaangalie kilichoharibika nilipe nikakakuta kila kitu chao kizima na mashine yao walosema imeibiwa ipo lkn kuna waya ulikakatika thamani yake elfu kumi na tano na leo pale polis nilipoulizia khs cm yangu nikajibiwa na mkurugenz wa ule ukumbi kuwa dj hapatikani na hajulikani anakaa wapi sikupata ushirikiano wwt mpk ss na kwa kauli ya watu pale sio mimi wa kwanz kufanyiwa vile ktk huo ukumbi na hata itokee msanii anafanyiwa vurugu uongozi wa hapo hawakai upande wa msanii hayo ni kwa kifupi tu yaliyonikuta usiku wa wapendanao. by HAMMER Q.

Hiyo ndo skendo iliyomkuta Hammer Q.

Tunarudi katika suala la Umoja wa wasanii upo wapi!???
Kama kungekuwa na umoja huo naamini suala hili la kunyanyaswa kwa wasanii lingefanyiwa ufumbuzi na wangeweza kufuatilia hii ishu ili kujulikana nani mwenye makosa na anastahili adhabu gani ki-sheria.

Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com imeongea na Hammer Q akasema yupo tiyari kwa ajili ya kulipa huo waya wao wenye dhamani ya Tshs. 15,000/= japo anaamini hahusiani na uharibifu huo na pia anahofia kufanya muendelezo wa kesi kufuatilia simu yake kwasababu ashaona kuna ushirikiano kati ya Polisi na Mwenye Bar.

Sisi tunatoa pole sana kwa Hammer Q pia tunasisitiza kufanya liwezekanalo kwa wasanii wa Taarabu kufanya mpango wa UMOJA!!!.


Wednesday, February 4, 2015

Audio:- Abdallah Maajabu - Nipe Imani... Sikiliza na Download nyimbo tamu...


Anaitwa Abdallah Maajabu au waweza kumuita Maajabu Classic!!
Ni msanii mchanga katika muziki huu wa Taarab na amejitokeza kwa kujitangaza na nyimbo yake ya kwanza kabisa.

Maajabu ameamua kufanya kweli Maajabu baada ya kutoa nyimbo yake hii tamu kabisa inayokwenda kwa jina la "Nipe Imani".

Nipe Imani ni nyimbo iliyotulia ukiisikiliza hutoamini kama Abdallah kweli ni nyimbo yake ya kwanza ni kama msanii mkongwe na ameshirikisha pia wasanii wenzake ambao ni wachanga pia.

Walioitikia katika huu wimbo ni Swaumu Ally na Producer Kaju.

Maajabu Classic anasema ndoto zake ni kufanya mapinduzi makubwa ya kuurudisha mziki wa Taarabu katika hadhi yake ya mwanzo maana sasa ushaanza kupoteza maana.

Maajabu hajawahi kuimbia bendi yoyote na yupo tayari kufanya kazi na mtu au bendi yoyote itakayomhitaji.

Nyimbo ipo hapa isikilize na U-download, usisite kutoa ushauri wako au Pongezi...!!!