Bendi ntingi za taarabu nchini zimedaiwa kuimba matusi katika nyimbo zao.
Blog ya taarabuzetu.blogspot.com imepokea malalamiko kadhaa toka kwa mashabiki wa mziki huu wengine wakitoa dukuduku zao katika page mbalimbali za facebook.
Wengi wamelalamikia nyimbo kuwa na mashairi makali sana na matusi yasiyofichika kwa mtu anayejua vyema kiswahili, na wengine kudai kuwa wengi wa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimbana wenyewe tu badala ya kuleta burudani ya mashairi mazuri na matamu kama zilivyo nyimbo za waimbaji wa zamani.
Hapa ni baadhi ya msg za wadau:-
AbbaMouk J
kiukweli
bila upendeleo wala chuki! Funga kazi nyimbo zao hazina mahudhui ya mziki wa
taarab! kunanyimbo waliamba cjui nan machupa ndg yake rahma machupa! watu wengi
waliokua wakiuona kwny tv waliuponda na kusema kama taarab zmeanza kua hv bas
hata kwenyenyumba yng hazitoingia nakumbuka mara ya kwanza nmeuona nlikua npo
singida sasa tulikuwa kwa mwenyeji wetu ndy ulirushwa ktk kipindi cha #Hawa_Hassan
cha I T V,ukija kwa huo nzi wa kijani leo hii nlikua nachat na mtu alikua
akiniuliza khs mambo hayo hayo ya mziki wa taarab akaniuliza hv umeusikia wimbo
wa nzi wa kijani? nkamwambia bado kwahiyo hata huujui hata mashair yake?
nkamwambia sijabahatika kuusikia akanambia sijapenda mashair wala uimbaj wao
sikuweza kumuunga mkono cz sijawah kuusikia so wasanii wanatakiwa wanapoumiza
vchwa vyao kutunga mashairi wajaribu kuweka chuki zao pembeni na kutumia mda wa
ziada kujaribu kuchambua ni matukio yep yanaendana na jamii hata km unamjibu
mpinzani wako lkn maudhui yasitoke nje ya kile ulichokikusudia.
Tende Mikidadi Sheshi
Huo Wimbo Wa Inzi Wa Kijani Cjausikia Bado Lkn Kila Aliewahi Kuusikia
Anasema Haufai,,Sasa Jiulize Kwanini Kila Mtu Anasema Haufai ?Unajua
Vijembe Vipo Kwenye Taarab Lkn Visiwe Live Au Uijibu Nyimbo Ya Mtu Kiasi
Hata Mtoto Akiusikia Anajua Umemjibu Fulani,,Binafsi Sipendi Nyimbo Za
Aina Hiyo,,Halaf Zamani Ilikua Ushabiki Wa Band Lakini Siku Hizi Msanii
Akishea Bwana Na Msani Mwenzie Kesho Kamtolea Nyimbo,,Ndomana Kuna Msemo
Mtaani Kuwa Taarab Ni Mziki Wa Uswahilini,,Umejaa Umbea Na Vijembe Japo
Si Kweli Hivyo Watunzi Mjiangalie ,Hatutaki Kuimbiwa Mambo Yenu Binafsi
,Tunataka Maudhui Yanayogusa Kila Mtu .
Amin Salmin Sheshi
beshi ushairi wa tembe tumepishana sana wake ndio una matusi ya
nguoni,ushairi wangu kwa nyimbo za mipasho huwa na pasha na kazi ya
mipasho ni kupasha upashike ila hakuna matusi kwa mfano,Naona
umepagawa,wenda mbio kila uchao,kiwewe kitakuuwa,sina wasi wasi
mwenzio,hilo lako la rohoni daima lita kukerekata,kosa sio langu
mm,mumeo ndotoni kunitaja,huna bizi we mzushi,is wa hamsini wala
mia,hayo kwangu matapishi, ww unayojivuni,Ukiangalia kwa undani huo ni
mpasho na sio nyimo ya tauhidi.
Sheshi Beshi Amin
swadakta temba anatumia matusi na wewe mipasho yako iko live ndio
nikasema mbinu ya tafsida kwenu ipo chini, huyu hajui ku2mia maneno
mbadala ya visawe na wewe ku2mia mafumbo pia hujui, ila mm cna tatizo
nasema tena hiyo ni feedback tu.
Tatizo
Baadhi Ya Watunzi Wanatunga Nyimbo Wakiwa Na Hasira Basi Hapo Hapo
Anashika Kalam Na Kuaza Kuchamba Maana Si Kutunga Tena ,,Iko Cku Mtu
Ataimba We Ms**ng Koma Na Mie,,Nadhani Hapo Serikali Itatangaza Kupiga
Marufuku Muziki Wa Taarab Na Tabid Sasa Watu Wahamie Dansini Au Kuigiza
Movie,,Ila Jamani Mi Nalia Na Mashairi Makali Yanini ?Halaf Kila Mtu
Anajua Kabisa Kaimbwa Mtu Fulani,,Mbona Majanga ?
Hizi ni baadhi ya Comment za watu wakiongelea mashairi ya Taarabu...
Wewe kama mdau unalizungumziaje hili suala la matusi na Vijembe vya waziwazi na kuwekeana mabifu!?