Nyimbo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa Taarabu nchini “BONGE LA BWANA” sasa ipo hewani.
BONGE LA
BWANA imerekodiwa katika Studio za Soundcrafters kwa Enrico.
Kinanda
kimepigwa na Kally akishirikiana na Thabit Abdul.
Solo
limepigwa na Ramadhan Kisolo.
Bass
amepiga Jumanne Boya, Johncena Bass.
Akizungumza
na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com mwimbaji wa wimbo huo Hasheem Saidy(Mzee wa Majanga) alisema:- “Mzigo wenyewe ndo huo hapo nimeuachia watu
wausikilize, naamini wataupenda tu na asiyeupenda aseme...”, alisema na
kuongeza “Maana mashairi yametulia na yanamvuto wa hali ya juu, vyombo
vimepigwa na wataaramu tupu, mi nasema mwaka huu ni wetu hakuna atakayetukamata
na katika show zetu tunataka kuwaonesha kuwa Mashauzi Classic ipo juu!!”.
Mashauzi Classic Modern wakiwa mzigoni... |
BONGE LA BWANA
Inakamilisha Albam ya Tau “3” ya Mashauzi Classic, Albam imebeba jumla ya nyimbo
Sita “6”.
Nyimbo
zilizomo katika Albam hiyo pamoja na waimbaji ni kama ifuatavyo:-
1. “Asiekujua
hakuthamini”, umeimbwa na Isha Mashauzi na Saida, “Wimbo huu ndo umebeba jina
la Albam”.
2. “Ni mapenzi tu”, umeimbwa na Zubeda Malik,
3 . “Ropokeni yanayowahusu”, umeimbwa na
Saida Ramadhan.
4. “Mapenzi hayana dhamana”, huu umeimbwa tena
na Isha Mashauzi,
5. “Tupendane”, umeimbwa na Saida Ramadhan.
6. “Bonge la Bwana”, Umeimbwa na Hasheem
Saidy
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi...!!! |
Mtandao huu ulipoulizia siku ya Uzinduzi
alisema muda bado haujapangwa hivyo tutawataarifu, tunajipanga kwa kuja kutoa
burudani kali zaidi siku ya Ufunguzi…!!
2 comments:
GOOD WORK MDADA....
Post a Comment