Muziki wa taarabu umekuwa ukipata mafanikio kila
kukicha na kufanya hata makampuni makubwa hapa Tanzania kuanza kutangaza
bidhaa zao kupitia vipindi vya muziki huo katika Redio na televisheni
mbalimbali, Lakini asilimia kubwa ya wasanii wa muziki huu
wamekuwa hawajui haki zao au wao pia kukiuka mikataba ambayo wamekuwa
wakiwekeana kiholela na wamiliki mbalimbali wa mabendi husika.
Mfano
Msaani kama Bi mwanahawa ally! amekuwa akizitumikia bendi zaidi ya mbili
ama tatu kwa kurekodi nyimbo mpya au kufanya Show katika bendi zote hizo.
Sasa balaa ni pale bendi hizo zote zinapoingiza
albamu zake sokoni, utakuta katika kila albamu moja kuna nyimbo mpya kaimba
Bi Mwanahawa Ally, sasa hapa kwanza mashabiki wanashindwa kujua huyu
mama yupo bendi ipi moja wapo kati ya hizo?.
Ukirudi upande wa pili
wakulaumiwa ni viongozi wa bendi hizo, ni kwanini wanamuimbisha Bi mkubwa
huyo wakati hawana mkataba nae?.
Imefika wakati sasa kwa viongozi wa Taarabu na wasanii kwa ujumla kuzijua haki zao kisheria ili kila mmoja
afanye kazi kulingana na mkataba unavyosema.
Hii tabia ya kuandikishiana
mkataba kama mnapeana maji ya kunywa imepitwa na wakati sasa. TUBADILIKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment