SUPERSHINE MODERN TAARABU KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA MAX BAR ILALA.
Baadhi ya wasanii wa Supershine
Bendi ya Supershine Modern Taarabu baada ya kutoka katika
Shangwe za sikukuu ya IDD, leo siku ya Jumatano wanatarajia kuporomosha
burudani ya nguvu katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala.
Akizungumza na
mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Msanii wa bendi hiyo ambae
pia ni MC Hassan Zumo aliwaomba wapenzi wa bendi hiyo kujitokeza kwa
wingi kuja kushuhudia mambo mazuri ambayo wameyaandaa kwa muda wote wa
kipindi cha Ramadhani.
Supershine Modern Taarabu huwa wanatoa burudani zao katika kumbi za Max Bar Ilala kila
Jumatano na Lango la jiji kila Alhamisi, wapenzi wote mnakaribishwa.
0 comments:
Post a Comment