Mtoto wa Malkia wa mipasho Prince Black Kopa atakuwa na Interview LIVE ndani ya Clouds TV siku ya Jumamosi tarehe 19 Novemba 2016 saa 3 mpaka 4 Usiku!.
Pia kutakuwa na utambulisho rasmi wa Video yake mpya ya "Nifagilieni Chocolate remix", kuna mambo mengi sana ataongelea kuhusu mziki wake na nyimbo hii mpya ikiwa ni remix.
Usikose kutizama ndani ya CLOUDS TV na SAKINA LYOKA.
NI BENDI YAH TMK TAARAB -
YAIBOMOA JAHAZI MODERN TAARAB, YACHUKUWA SILAHA MUHIMU ZA KAZI.
Ule usemi unaosemwa na baadhi ya wadau wa taarab
ya kuwa "Jahazi Modern Taarab bila ya Mzee Yussuf linasuasua"
unaonekana kama unakubalika kwa asilimia fulani baada ya bendi hiyo kupoteza
waimbaji muhimu pamoja na wapiga vinanda.
Majina
ya Fatma Nyoro, Chidi Boy, Moh'd Mauji, Mussa Mipango, Kichupa kwa sasa
hayatosikika kwenye maonesho ya Jahazi.
Pia
kuna tetesi kuwa Khadija Yussuf ameenda Wakaliwao kwa Thabit Abdul.
Bendi ya TMK pia imeibomoa Coast Modern Taarab
kwa kumpa shavu Omary Teggo na dada yake.
Pia
Bi Mwanahawa Ali (JEMBE GUMU) ametilishiwa saini katika bendi hiyo huku akipewa
wimbo wa "SINA PUPA MUNGU ATANIPA".
Mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah, akizungumza jambo na wanahari (hawapo pichani).
Kutoka kushoto ni mkuu wa matukio kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kurugira Maregesi, Hamis Abdallah na Khadija Kopa.
Khadija Kopa akizungumza jambo.
Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat, akielezea namna atakavyopagawisha mashabiki wake.
MALKIA wa muziki wa taarab ambaye ni Mkurugenzi wa Kundi la Ogopa Kopa, Khadija Kopa, anatarajiwa kuwasha moto kwa kutoa burudani ya aina yake katika Tamasha la Muziki wa Taarab lililoandaliwa na mtandao wa habari wa Vijana, Tegemeo Arts Group ambalo linajulikana kwa jina la ‘Nani Zaidi’.
Tamasha hilo litakaofanyika siku ya X-Mass ya Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi usiku.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah, amesema tamsha hilo linalenga kuhamasisha jamiii katika uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji hasa kina mama wanapopoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.
Amesema kwamba katika zoezi hilo pia kutakuwa na upimaji wa Ukimwi , saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake na kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mablimbali siku tano kabla ya tamasha hilo.
Alifafanua kuwa tamasha hilo litakuwa la aina yake kwani litakutanisha bendi za muziki wa dansi na wanamuziki wa taarab chini.
Miongoni mwa makundi ya taarab na bendi zitakazokuwepo ni Jahazi Modern Taarab, Ogopa Copa Clasic Band, The East African Melody, Five Stars Modern Taarab, FM Academia na Moro Jazz.
Mbali na hayo pia kutakuwa na mechi katika ya Tanzania Veterans na Morogoro Veterans zote za mjini Morogoro zitakazokipiga Desemba 24 mwaka huu zikilenga kuhamasisha uchangiaji hiari wa damu.
Leo Mpenzi wa Taarab - Nyimbo tabu za mwambao nakuletea nyimbo nzuri, tamu kabisa kutoka kwa mwanadada anayekwenda kwa jina la Shadya Shombeshombe kutoka ndani ya Ogopa Kopa Classic. Nyimbo iko poa sana unaweza kuisikiliza na kuipakua ukawa nayo.
Nimekuletea Single mpya kabisa kutoka kwa mtoto wa Malkia wa Mipasho Tanzania, Africa Mashariki, Africa na Dunia nzima (Kama unabisha ulizia utaambiwa).
Single inakwenda kwa jina la "NIMEMPATA MWENYE MASLAHI"
Isikilize na kudownload hapa kusikia zaidi amempata mwenye Maslahi gani??? Kumbuka ni nyimbo kalikali tu kutoka OGOPA KOPA CLASSIC BAND.