Saturday, January 3, 2015
Sunday, December 21, 2014
ISHA MASHAUZI KUIKOSA MIAKA 8 YA JAHAZI TRAVERTINE HOTEL LEO USIKU...
![]() |
| Isha Mashauzi. |
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi ataikosa show ya Jahazi Modern
Taarab kutimiza miaka minane tangu izaliwe.
Show hiyo inafanyika leo usiku katika ukumbi wa Travertine Hotel huku ikiaminika kuwa wasanii wote walioitumikia Jahazi watakuwepo.
Katika onyesho la Mashauzi Classic pale Mango Garden Alhamisi iliyopita, Isha alitumia kipaza sauti chake kuinadi show ya Jahazi na kuwataka wapenzi wa Mashauzi wasikose kwenda Travertine Jumapili.
Lakini mashabiki hao walipomuuliza kama na yeye atakuwepo, Isha akawajibu kwa kusema kuwa kwa bahati mbaya yeye hatakuwepo.
“Nina kazi nje ya mji, nasikitika kuwa sitakuwepo katika onyesho hilo, lakini nawatakia mafanikio mema na naomba mkawaunge mkono,” alisema Isha.
Tuesday, December 9, 2014
FIVE STARS: JIANDAE KUPATA NYIMBO TATU KALI...!! PATA PICHA ZA STUDIO NA MAJINA YA NYIMBO...
![]() |
| Baadhi ya wasanii wa kundi la 5Stars. |
Kundi zima la Taarab 5Stars leo wameingia studio kurekodi nyimbo zao Tatu watakazoziachia hivi karibuni baada ya kumalizika kurokodiwa.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo kongwa ameongea na Taarabuzetu.blogspot.com na kuihakikishia kuwa nyimbo hizo zitakuwa nzuri na itakuwa ndo habari ya mjini zitakapotoka.
Amezitaja nyimbo hizo ni:-
UBAYA HAUNA SOKO - Mwanaidi Ramadhani.
KISHTOBE - Salha wa Hammer Q.
SINA GHUBU - Mape Kibwana.
Wapenzi wote wa Taarabu kaeni mkao wa burudani.
Je! Wajua maana ya "Kishtobe"?????
Zifuatazo ni picha mbalimbali wakiwa studio wakirekodi...
![]() |
| Waimbaji wa 5Stars. |
![]() |
| Mape Kibwana, Anaimba "Sina Ghubu". |
![]() |
| Mwanaidi Ramadhani akiimba "Ubaya hauna Soko". |
![]() |
| Salha wa Hammer Q Akiimba "Kishtobe". |
![]() |
| Salha akiwa na Ally J (Boss) ambaye amepiga vinanda ktk nyimbo hizo. |
Monday, November 24, 2014
Wednesday, November 19, 2014
ISHA MASHAUZI AACHIA NGOMA YAKE MPYA KABISA “SURA SURAMBI”...
Kuanzia mwishoni mwa wiki hii mashabiki
wa taarab waatanza kuusikia rasmi radioni wimbo mpya kabisa wa Mashauzi Classic
Modern Taraab unaokwenda kwa jina la “Sura Surambi”.
Ni utunzi na uimbaji wake
Isha Mashauzi na tayari ngoma hiyo imesharekodiwa wikiendi iliyopita kwenye
studio za Sound Crafters Temeke jijini Dar es Salaam chini ya producer Enrico.
“Sura Surambi” inategemewa kuendelea kumweka juu Isha Mashauzi kwa namna
alivyoimba wimbo huo na hapana shaka itatosha kabisa kuthibitisha ni kwanini
alistahili tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa taarab.
-2.jpg)
-2.jpg)













