TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, April 29, 2014

DOWNLOAD:- NYIMBO MPYA NNE (4) TOKA KWA WAKALI WAO MODERN TAARADENCE...

Thabit Abdul, Mkurugenzi wa Wakali Wao.
Hii nyimbo ya "Kalieni Viti" imefanyiwa marekebisho kwa wale waliokuwa nao mnaombwa kutumia hii mpya, imeboreshwa!!

Friday, April 18, 2014

HAMMER Q ANA SIRI NZITO...!!!

Katika picha hii hapo juu kuna Hammer Q na AT, halafu kuna maneno hapo kati yameandikwa "Loading..." bila shaka kila kitu anacho Hammer Q mwenyewe, maana taarabuzetu.blogspot.com ilipomuuliza hii picha inamaana gani!! Aliishia kusema "Kuna siri nzito...!"

Hammer Q wapenzi wako wa burudani wanasubiri hiyo siri yako waweze kuijua na mtu wa kuitoa ni wewe mwenyewe.

Usiweke watu roho juu bana, kama kuna kitu kinatoa hapo achia tu watu waburudike.

Sisi "Still waiting...!"

Wednesday, April 9, 2014

5STAR NDANI YA GREEN PARK, TABATA JUMAMOSI HII YA TAREHE 12 APRIL 2014.

Ally J.
Five Star Modern Taarab' kuwasha moto ndani ya GREEN PARK TABATA MAWENZI' J'mosi ya Tar 12.

Akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com kiongozi wa kundi hilo Ally J ambaye ni mpiga kinanda machachari hapa nchini, alisema ni ujio wao wa kasi ya ajabu akiwa na wasanii wakali na wenye sauti za kuvutia, mashairi mapya yenye nyimbo za aina tofauti, wataimba nyimbo za zamani na mpya zitakuwepo.

Karibu uje ukutane na waimbaji kama ZENNA MOHAMED, MARYAM BSS, ASHURA MACHUPA na MACHIPUKIZI WENYE UWEZO WA HALI YA JUU. 

Hanifa Maulid (Jike la Chui)
Katika show hiyo kutakuwa na mgeni mualikwa HANIFAH MAULID "Jike la Chui" halafu kuna ALLY J, MUSSA KIJOTI, SAID YUSSUF na wengneo. 

Ally J anasema anaendelea kutafuta chipukizi zaidi kwa nia ya kuwainua kimziki na 5Star inachukua chipukizi kwa nia ya kuwafua zaidi.

USIKOSE...!!!!

Tuesday, March 25, 2014

Pongezi:- Aisha Masanja kwa kupata mtoto...

Aisha Masanja (Mama ... )
Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com inatoa pongezi nyingi sana kwa msanii wa Taarabu Aisha Masanja kwa kujifungua mtoto wa kike leo hii mida ya saa sita mchana, 6:00PM.

Sunday, March 23, 2014

MSIBA:- SHAMIRA HAMISI WA KINGEKE MORDEN TAARAB YA MOROGORO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI...

Muimbaji wa bendi ya kingeke modern taarab yenye makazi yake mkoani morogoro aitwae Shamila Hamisi amefiwa na baba yake mzazi ktk ajari ya gari iliyotokea mkoani mbeya juzi. Msanii huyo ambae kwa sasa anatamba na wimbo wake "SITOLIPIZA UBAYA". ndani ya bendi hiyo amekuja mkoani dar kwa mazishi ya baba yake na leo wametoa tatu ya msiba wa mzee wake huyo. Akizungumza na mtandao huu afisa habari wa bendi hiyo ametoa pole kwa niaba ya wasanii wote wa kingeke na uongozi kwa ujumla. Sisi taarabuzetu pia tukiwa kama wadau tunatoa pole kwa msanii huyo kuondokewa na baba yake kipenzi mzee Hamisi bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihidimiwe. Wakati huo huo bendi hiyo ya kingeke ipo ktk mchakato wa kurekodi nyimbo zao mpya kabisa hivi karibuni kwahiyo wadau na wapenzi wa taarabu wa morogoro na tanzania kwa ujumla wakae mkao wa kupata vitu vizuri toka kwao.

Saturday, March 22, 2014

DOWNLOAD: Nyimbo mpya ya Khadija Kopa - Lady With Confidence...

Malkia wa Mipasho Tanzania Bi. Khadija Kopa.

DOWNLOAD NA KUSIKILIZA: Nyimbo Nne (4) mpya za Dar Modern...

Kundi la Dar Modern ndo habari ya mjini kwa sasa...

Hapa wanakupa fulsa ya kusikiliza na Kudownload nyimbo zao mpya kabisa ambazo ni gumzo katika vituo mbalimbali vya Radio nchini.

Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com inakupa nyimbo hizo na zingine zinafuata siku nyingine, usikae mbali...!!

Friday, March 21, 2014

Ajali ya kukumbukwa: Five Star Modern Taarab...

Kila inapofika tarehe kama ya leo ya mwezi huu (21/3/20011), huleta kumbukumbu mbaya ya wanamziki wa 5Stars Modern Taarab, ajali iliyotokea maeneo ya Morogoro.


Baadhi ya wasamalia wema waliokuwa kwenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajili ya Basi ndogo la Wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama miili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni mbao lililokuwa limeharibika njiani, katika barabara kuu ya Iringa- Morogoro , eneo la Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Mikumi, karibu na Kijiji cha Doma, Wilaya ya Mvomero usiku


Ni ajali iliyopoteza watu 13 kati ya hao 12 walifariki papo hapo na mmoja
alifariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini.
Kazi Yake mola Haina makosa mbele yao nyma yetu Mungu awalaze mahala pema peponi Aamin.

MPAMBANO: Hadija Yusuph amgalagaza Isha Mashauzi...

Jana Alhamisi ya Tarehe 20 Machi kulikuwa na mpambano mkali wa nani muimbaji mzuri wa Taarab kati ya Hadija Yusuph wa Jahazi na Isha Mashauzi wa Mashauzi Classic.

Mpambano huo ulifanyika katika kipindi cha Ambaa na Mwambao ndani ya Passion FM kikiongozwa na mtangazaji machachari Warda Chande aka "Mwana Dar es Salaam".

Mpambano huo umetokana na mabishano makali baina ya wapenzi wengi wa Taarabu na kupelekea kuandaliwa kwa mpambano huo.

Mpaka mpambano unamalizika ukiwa na wapiga kula kumi na sita (16) katika simu na Msg, Kura 12 zikisema Hadija ni bora zaidi na 4 zikisema Isha ni bora zaidi.

Mpambano huu nauleta kwako mdau utoe maoni yako ni nani zaidi!?
Hadija au Isha!?

Thursday, March 20, 2014

DOWNLOAD: Nyimbo mpya Tatu za G5 Modern...

Samira na Aisha.
Kundi la G5 Modern Taarab limefwatua nyimbo 4 mfululizo na kuomba mashabiki wazisikilize.

Nyimbo zilizotolewa ni pamoja ni ulioimbwa kwa ushirikiano na Muumini Mwinjuma.

Nyimbo aliyoimba Muumini inakwenda kwa jina la Kigodoro Kimeloa ambayo tuliwawekea mashabiki na tunaamini mmeisikiliza na kuifurahia.

Leo tumekuwekea nyimbo Tatu ambazo zimeimbwa na:-
*** Aisha Kulele - Ametaka mwenyewe
*** Samira - Nitanyamaza nikifa
*** Sharifa Mnoga - Mambo Hadharani


Tuesday, March 18, 2014

DOWNLOAD: Nyimbo mpya kabisa ya Taarab toka kwa Mwinjuma Muumini...

Prince Mwinjuma Muumini.

Hatimae Muumini Mwinjua atoa nyimbo yake ambayo ameiimba kwa miondoko ya Taarab.

Kwa kawaida Muumini ni mwibaji wa muziki wa dance na ameimbia katika Bendi mbalimbali hapa Nchini zikiwemo Twanga Pepeta, Mchinga Sound, Victoria Sound, Tamtam na zingine.

Msikilize hapa na nyimbo yake "Kigodoro Kimeloa" akiwa na kundi la G5 Modern Taarab. Wimbo: Kigodoro Kimeloa 
Mwimbaji: Mwinjuma Muumini & G5 Modern Taarab

Saturday, March 1, 2014

BREAKING NEWS: Salha wa Hammer Q apata mtoto...!

Salha na Mwanae hapo pembeni!!
Msanii, mwimbaji mahili katika miondoko ya Taarab Tanzania Salha wa Hammer Q leo ameleta furaha ya ndoa katika nyumba kwa kujifungua mtoto wa kike.

Baba wa mtoto Hammer Q ambaye ni msanii wa kundi la mduara la Offside Trick aliiambia taarabuzetu.blogspot.com kuwa, mkewe amejifungua mtoto huyo wa kike leo tarehe 1/3/2014 mida ya saa nane (8:22) Mchana katika Hospitali ya Zakhem Mbagala.
"Mtoto kazaliwa akiwa na afya njema kabisa na tunamuomba Mungu amlinde na amkuze vyema mwanangu". Alisema Hammer Q

Blog hii inampa pongezi sana Mr & Mrs Hammer Q kwa kupata mtoto, Mungu awajalie kuwa na maisha mazuri mje kupata watoto wengine tena.

Friday, February 28, 2014

Hashim Said:- Sitoshiriki tena tuzo za Kilimanjaro Music Awards...

Hashim Said "Mzee wa Majanga".
Sitoshiriki tena tuzo za Kilimanjaro Music Awards zimejaa ubabaifu kila mwaka nilishiriki mwaka jana nimegundua mapungufu kibao. Hayo ni maneno ya Msanii mwimbaji mwenye kipaji ndani ya Mashauzi Classic anayeitwa Hashim Said Igwee "Mzee wa Majanga" ameyasema haya akiongea na mwandishi wa blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com

Hashim alipoulizwa ni Mapungufu gani ameyaona!?

Mapungufu ni mengi sana hasa kwa washindi wa tuzo kujijua kuwa wanakwenda kuchukua hizo tuzo, yaani huwa wanapewa taarifa kabisa kuwa leo unapata tuzo! Sasa haya ni mashindano kweli au kupeana??? iko wapi nafasi ya watanzania wanaopiga kura?

Kiukweli Tanzania bado sana katika suala hili, tujifunze kupitia wenzetu mfano tuzo za KORA tuzo za KISIMA kule kenya mpaka tuzo za muziki kule Marekani, lakini sasa kwa mtindo huu wa kupeana kila siku badala ya kuwapa chachu wasanii hasa wanaochipukia watakuwa wanawapa chuki.

Nitakuja kushiriki iwapo baraza la Sanaa Tanzania likifanya marekebisho au kuanzisha Tuzo za Baraza na si hizi za watu binafsi zinazotoa tuzo kwa kujuana na kupeana. 
 
Mimi ni mwanamuziki wa siku nyingi hasa katika tasnia hii ya taarab, niliingia kwa mara ya kwanza mwaka jana nimejionea mwenyewe kiukweli sihitaji kushiriki tena nawaomba wasije wakaweka jina langu tena anavyonitunza mke wangu inatosha sanaaaa.