TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, February 28, 2014

Hashim Said:- Sitoshiriki tena tuzo za Kilimanjaro Music Awards...

Hashim Said "Mzee wa Majanga".
Sitoshiriki tena tuzo za Kilimanjaro Music Awards zimejaa ubabaifu kila mwaka nilishiriki mwaka jana nimegundua mapungufu kibao. Hayo ni maneno ya Msanii mwimbaji mwenye kipaji ndani ya Mashauzi Classic anayeitwa Hashim Said Igwee "Mzee wa Majanga" ameyasema haya akiongea na mwandishi wa blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com

Hashim alipoulizwa ni Mapungufu gani ameyaona!?

Mapungufu ni mengi sana hasa kwa washindi wa tuzo kujijua kuwa wanakwenda kuchukua hizo tuzo, yaani huwa wanapewa taarifa kabisa kuwa leo unapata tuzo! Sasa haya ni mashindano kweli au kupeana??? iko wapi nafasi ya watanzania wanaopiga kura?

Kiukweli Tanzania bado sana katika suala hili, tujifunze kupitia wenzetu mfano tuzo za KORA tuzo za KISIMA kule kenya mpaka tuzo za muziki kule Marekani, lakini sasa kwa mtindo huu wa kupeana kila siku badala ya kuwapa chachu wasanii hasa wanaochipukia watakuwa wanawapa chuki.

Nitakuja kushiriki iwapo baraza la Sanaa Tanzania likifanya marekebisho au kuanzisha Tuzo za Baraza na si hizi za watu binafsi zinazotoa tuzo kwa kujuana na kupeana. 
 
Mimi ni mwanamuziki wa siku nyingi hasa katika tasnia hii ya taarab, niliingia kwa mara ya kwanza mwaka jana nimejionea mwenyewe kiukweli sihitaji kushiriki tena nawaomba wasije wakaweka jina langu tena anavyonitunza mke wangu inatosha sanaaaa.

Wednesday, February 26, 2014

DOWNLOAD NYIMBO MPYA - "NAUFUNGA MTAA - ANIFA MAULID" ...


NYIMBO:- NAUFUNGA MTAA 
MWIMBAJI:- ANIFA MAULID "JIKE LA CHUI".

SINA BAND, ANAYENIHITAJI NIKO TIYARI "ANIFA MAULID"...

Anifa Maulid "Jike la Chui".
Anaitwa Anifa Mohamed "Jike la Chui" mwimbaji machachari katika tasnia ya muziki wa Taarabu Tanzania, amefunguka kuhusiana na yeye yupo wapi kwa sasa.

Akizungumza na mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com Anifa amesema kwasasa hana bendi yoyote anayoifanyia kazi yaani yupo "Free" kwenda kuimba popote na yupo tayari kuingia mkataba na bendi yoyote itakayomuhitaji.

Amesema mala nyingi amekuwa akiimba katika jukwaa la TOT kama msanii mualikwa tu na si muimbaji wa TOT. Anakula "Ndondo".

Katika ujio wake mpya Anifa baada ya "Makavu Live" amekuja na nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la "Naufunga Mtaa". Ni nyimbo ambayo ameimba kutokana na kisa cha ukweli mtaani kwao.

Nyimbo hii ametunga mwenyewe na kupata ushauri kidogo toka kwa Thabit Abdul, Kaptani Temba na Hemed Omary.

Nyimbo hiyo ameimba kwa kuitikiwa na wasanii wa Wakali wao Modern Taradance, Asia Bin Mariam na Muya walio chini ya Mkurugenzi Thabit Abdul Jiko la Jela.
Anifa kushoto akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Taarabu "Ambaa na mwambao" Passion FM.
Anifa anamshukuru sana Khadija Kopa kwa kumpa ushirikiano mkubwa sana katika uandaaji mzima wa nyimbo yake kwani alikuwa naye kuanzia mazoezi mpaka kwenye kurekodi, ametoa ushauri mkubwa sana!!.

Ni nyimbo nzuri na ya ukweli, Isikilize utaipenda!.

Friday, February 21, 2014

Mgeni Kisoda: Hakuna mpiga kinanda anayemkubali kama...

Mgeni Kisoda akipapasa kinanda katika mahojiano.
Anaitwa Mgeni Kisoda mtaalamu wa kupapasa Kinanda toka Jahazi hadi Dar Modern.

Ni mpiga kinanda mzuri ambaye hana historia ndefu ya kufanyia katika bendi mbalimbali, ila kwa hivi sasa yupo Dar Modern na anamiliki Bendi yake inayokwenda kwa jina la Maisha Band na yeye kama Mkurugenzi.

Katika mahojiano na taarabuzetu.blogspot.com Kisoda amesema hakuna mpiga kinanda mkali na anayetamani kufikia kama yeye, ambapo alisema ni Mzee Yusuph na anayemfutia ni Ally J, Hakuna mwingine na kama wa tatu basi ni yeye mwenyewe Mgeni Kisoda.

Hassan Vocha awashauri watangazaji wa vipindi vya Taarab...

Hassan Vocha.
Anaitwa Hassan kwa jina maalufu anajulikana kama Hassan Vocha, ni msanii muimbaji wa muziki wa taarab katika kundi la Dar Modern Taarab.

Akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com Vocha alisema muziki ameanza kuimba takribani miaka mitatu sasa ambapo alianza kuimba katika miondoko ya Bongo Flavor akiwa kwa Mkubwa Fella TMK, baada ya kuachana na muziki huo alijaribu na mduara kidogo akashirikiana na Shilole katika nyimbo ya "Paka la Bar" na kisha kujidumbukiza katika muziki huu wa mwambao katika kundi la Dar Modern.

Hassan Vocha ametoa malalamiko kwa watangazaji naomna baadhi wanavyoendesha vipindi kwa upendeleo, anasema unakuta mtangazaji anapiga zaidi ya nyimbo mbili za bendi moja wakati nyimbo anazo nyingi tu za bendi tofauti tofauti, hilo ni tatizo.

Ameshauri wanapopiga nyimbo kuwe na uwiano wa nyimbo, anapopiga nyimbo ya bendi moja basi asirudie tena kupiga nyimbo za bendi hiyo na badala yake apige bendi nyingine ili nazo zisikike, ni hayo tu.

Hassan Vocha alipoulizwa ni muimbaji gani wa Taarab anavutiwa naye kwa sasa!? Akasema kwa kipindi hiki hakuna msanii anayeimba na kuvutiwa naye kwani wanapiga kelele tu, waimbaji wazuri walishatangulia mbele za haki (Wapumzike kwa amani), "Nilikuwa navutiwa sana na uimbaji wa Omary Kopa".

Vocha anashukuru sana kwa mashabiki wake kwa kumsapoti na kuwa pamoja naye katika show mbalimbali.

Monday, February 17, 2014

TWAHA MALOVEE ATANGAZA KUIACHA RASMI DAR MODERN....

Muimbaji machachali na wa kutumainiwa ndani ya Dar Moder Twaha Malovee.
Muimbaji tegemezi na wa siku nyingi ndani ya bendi ya Dar Modern Taarab Twaha Malovee, amejitangaza rasmi kwamba yeye kwa sasa si msanii tena wa bendi hiyo na ameamua mwenyewe kuacha wala hajafukuzwa na kiongozi yeyote yule.

"Ndugu mwandishi nimeacha kazi Dar Modern na sina kinyongo na mkurugenzi wangu, FERESH namshukuru sana amenisaidia sana tena sana nampongeza kwa huruma yake kwa wasanii!. Unajua pale kuna ubaguzi unafanywa na kiongozi mmoja alieletwa kubagua wasanii aliowakuta na kuwapa kipaumbele zaidi wale aliowaleta yeye.
Mimi ni bonge la muimbaji najitambua siwezi kuburuzwa nimeamua kuacha bendi ili waendelee na nawatakia maendeleo wafike mbali. Kwa sasa nipo katika mazungumzo na bendi moja kubwa ya taarabu na wakati ukifika kila kitu kitakaa sawa na wapenzi na wadau wangu nitawafahamisha" alimaliza kwa kusema.

Wiki iliyopita Twaha aliibukia katika jukwaa la Supershine na kuimba nyimbo moja, baada ya hapo alipomaliza kuimba alijitangaza rasmi kuacha kazi Dar modern nakuwaambia wapenzi na mashabiki zake kwamba wasijisumbue kumfuata katika uzinduzi wa albam mbili za bendi hiyo uliofanyika Travetine Magomeni kwani hatokuwepo jambo lililotafsiriwa na wapenzi kwamba labda Twaha ana mpango au yupo njiani kujiunga na kundi hilo la Supershine Modern Taarab.

Tusubiri tuone Twaha atajiunga na bendi gani!!.

Aysher Othman a.k.a. Vuvuzela ametoa pongezi kwa wale wote waliofanikisha na kuhudhuria Harusi yake.

Aysher Vuvuzela au Mrs Saaleh Mkassy akiwa na mumewe mpendwa.
Ilikuwa ni mchana wa saa 7 Ijumaa 14 Feb, siku ya wapendanao Aysher Othman alifunga ndoa na bwana Saaleh Zakaria Mkassy baada ya mshuko wa swala ya ijumaa.

Usiku wa saa tatu siku ya jumamosi kulikuwa na party iliyofanyika katika ukumbi wa Kibo Garden Kimara Rombo.
Kings Morden Taarab ilisindikiza party hiyo kwa burudani nzuri kabisa na wadau wa ukweli walifurahia!.

Mamaa Zeka na Mamaa Dabo S nawashukuru sana...! ilikuwa raha kuolewa ni stara na wasaani wa Kings walinipa zawadi nawashukuru wote. Alisema Bi Harusi huyo.

"Ilikuwa ni siku ya furaha kwangu, kwa sasa naitwa Mrs Saaleh Mkassy mamaa Vuvuzela" Alisema Aysher.

"Natoa shukurani nyingi sana kwa wote waliofanikisha kufanyika kwa harusi yangu, wote waliohudhuria na waliochangia kwa namna moja ama nyingine nasema
ASANTENI SANA...!!!"

MASHAUZI CLASSIC KUMIMINA UHONDO MANGO GARDEN MWISHO WA MWEZI HUU, MASHABIKI KUWA MAJAJI WA VIDEO YA ASIYEKUJUA HAKUTHAMINI

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi.

ALHAMISI ya tarehe 27 Feb, mwezi huu kutakuwa na tukio la aina yake katika ukumbi wa Mango Garden katika onyesho maalum la Mashauzi Classic. 

Mashabiki wa kundi hilo linaloongozwa na Isha Mashauzi, watapata fursa ya kuwa majaji wa video ya wimbo mkali “Asiyekujua Hakuthamini”. 

Ni kwamba siku hiyo video ya “Asiyekujua Hakuthamini” itatambulishwa rasmi huku mashabiki wakipewa nafasi ya kutoa kasoro kazi hiyo na kisha itakwenda kufanyiwa marekebisho ya mwisho (final editing). 

Meneja wa Mashauzi Classic, Suma Raga ameiambia Taarabu Zetu kazi hiyo imefanyika katika kiwango cha hali ya juu, lakini bado mwamuzi wa mwisho ni mshabiki wa Mashauzi Classic. “Kazi hizi tunazifanya kwaajili yao, bila wao sisi hatupo, kwahiyo tunaileta kazi mikononi mwao ili tupate maoni yao. Tutakuwa tukiendelea na mfumo huu hadi mwisho wa nyimbo zote za albam ya “Asiyekujua Hakuthamini” ambayo itabeba jumla ya nyimbo sita,” alifafanua Suma Raga.

Pia sku hiyo ya tarehe 27 Feb,
watatambulisha nyimbo tatu mpya zitakazokuwa katika albam ijayo ya nne ambayo itaitwa "Wasafi wa mavazi wachafu wa nafsi" mbili katika hizo ni utunzi wake Hashim Said (Mzee wa Majanga)

Saturday, February 15, 2014

AYSHER VUVUZELA AFUNGA NDOA...

Aysher Othman "Vuvuzela".
Mwimbaji machachari na mwenye uwezo mkubwa wa kuimba ndani ya Kings Modern Taarab Othman Aysher Vuvuzela jana mchana amefanikiwa kufunga ndoa yake kwa amani.

Ndoa hiyo imefungwa jana huko Kiluvya nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kufana sana.

Baada ya ndoa Aysher aliwashukuru sana ndugu, jamaa na marafiki wote walioweza kufanikisha ndoa yake kufungwa, shukurani pia kwa wale wote waliohudhulia.
http://taarabuzetu.blogspot.com/

http://taarabuzetu.blogspot.com/
Taarabu Zetu inakupa pongezi sana Aysher na mumeo kwa kuweza kufanikisha na kufikisha ndoto uliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

Mungu awabariki sana, Mdumu, Mpate watoto na muishi kwa amani.

UZINDUZI WA ALBAM MBILI DAR MODERN WAFANA...

Waimbaji wa Dar Modern Taarab wakiwajibika jukwaani.
 Bendi ya Dar Modern Taarab yenye makazi yake jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo walifanya uzinduzi wa albam zao mbili kwa mpigo katika ukumbi wa Travertine Magomeni.
Albam zilizozinduliwa ni: "KITWITWI" NA "NGOMA IMEPASUKA".

Ilikuwa ni kama picha ya Kihindi watu wakitegemea siku ya mwisho sterling anakufa lakini sivyo ilivyokuwa.

Pamoja na kuwepo na burudani katika ukumbi wa jirani wa LANGO LA JIJI toka kwao East African Melody lakini Wana wa pembe la Ng'ombe walijaza watu isivyo kawaida.

Shukrani ziende kwa uongozi mzima wa Dar Modern kwa kufanya maandalizi mazuri.
Mnenguaji wa Baikoko akifanya yake.
Show ilianza saa 3 kama ilivyo ada na walioanza kuleta raha ni BAIKOKO ambao walichengua mashabiki vilivyo na kuwafanya washindwe kukaa vitini!

Baada ya hapo waliingia wenyewe wenye shughuli nikimaanisha Dar Modern ambao walipiga nyimbo tatu mfululizo zilizowafanya watu kumwagika jasho kwa kucheza.
Wasanii wa kundi la Kibao Kata wakiburudisha mashabiki.
Ilipofika saa sita usiku walipanda wana Kibao Kata ngoma yenye asili ya mkoani Tanga nao walipiga nyimbo zao 3 mfululizo na kuwafanya mashabiki wao kupiga mayowe wakiomba kuongezwa kwa wimbo mwingine toka kwao.
Waimbaji wa Dar Modern - Mwanvita Shaibu, Zubeda Mlamali na Mosi Suleiman.
Katika raundi ya mwisho walipanda tena Dar Modern Taarab wakiongozwa na Bi Mwanahawa ally ambae aliwapa wapenzi wake burudani ya nguvu, baadae walipanda wasanii wengine kama Zubeda Mlamali, Mosi Suleiman, Hasna Mlamali, Mwamvita Shaibu na wengineo.
Waandishi wakikabidhiwa CD za Nyimba.
Ukumbi ulikuwa umefurika mbayaa...!!
Mashabiki hawakukaa kadri burudani ilivyokuwa ikiendelea ukumbini hapo...!
Show ilimalizika saa kumi kasoro za alfajiri na kuwafanya wapenzi na mashabiki wa Dar Modern kulidhika na kushusha pongezi za nguvu kwa wasanii na viongozi kwa ujumla.

Bendi hiyo itakuwa ikitumbuiza katika ukumbi huo wa Travetine Magomeni kila ijumaa ilikuwapa burudani wakazi wa Magomeni na vitongoji vyake mfano kama Sinza, Mwananyamala, Manzese na sehemu zingine za karibu.

Tunawaahidi kuwawekea nyimbo zao mpya ili muweze kuzisikiliza na kuzi-download!.
Hongereni sana Dar Modern kwa kazi nzuri mliyoifanya.
BIG UP SANA!.

Friday, February 14, 2014

LEO NI LEO DAR MODERN TAARAB PALE TRAVERTINE...

Leo siku ya Wapendanao inayofanyika Duniani kote, tarehe 14 Februali katika ukumbi wa Travertine Magomeni patakuwa hapatoshi.

Kundi zima la Dar Modern Taarab litakuwa pale katika kuwapa raha WAPENDANAO, Albam mbili kwa pamoja zitazinduliwa pamoja na Show kali kutoka kwa wanamziki wapya kabisa waliojiunga kwa utambulisho wa hii leo.

Wapenzi wote wa Dar Modern mnakaribishwa kwa kiingilio cha Tshs. 7,000/= tu

AMIN SALMIN KUPIMA DAMU LEO 14 FEB SIKU YA WAPENDANAO....

Mkurugenzi wa T Motto, Mr. Amin Salmin.
Mkurugenzi wa bendi ya T MOTTO Amin Salmin leo Feb 14 atapima damu mbele ya waandishi wa habari. 

Amin Ameamua kuwa kinyume kidogo na walio wengi katika siku ya wapendanao. Siku hii yeye atakwenda AMREF mbele ya waandishi wa habari na atapima damu na atachangia kwa jamii kwaajili ya watu wasiojiweza na si vinginevyo. 

Akizungumza na mwandishi matata wa blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com Amin amesema jamii imekuwa ikipotoshwa na tamaduni za kimagharibi kwa kufuatisha mambo yasiyo wahusu wala kujua faida au hasara ya hicho wanachofuatisha. 

Siku hizi imekuwa ndio mtindo kwa jamii kujiandaa kwa ajiri ya ngono kwa kisingizio cha siku ya wapendanao!, huu ni upuuzi na ujinga upendo upo kila siku na sio tarehe 14 kama wanavyodanganywa!. 

 Ifike wakati tufanye mambo mazuri kwa ajiri ya taifa letu na sio kufuatisha mkumbo tu. 

Mtandao huu unatoa pongezi kwa mkurugenzi huyu wa T MOTTO kwa uamuzi wake wa busara ambao unapaswa kuigwa katika jamii yoyote ya wapenda maendeleo! 
Hongera sana AMIN SALMIN!.

MASHAUZI KUFANYA BONGE LA SHOO MORO, DODOMA NA KILOSA...

Mashauzi Classic ikiongozwa na Super Woman Mkurugenzi mwenyewe Isha Mashauzi leo siku ya Valentine watadondosha bonge la show kwa wapendanao mji kasoro Bahari Morogoro.

Tarehe 14 Februali ni siku ya wapendanao, siku inayoadhimishwa Duniani kote.

Mmoja wa wasemaji wa Mashauzi alisema, siku hii ya Valentine watakuwa Morogoro katika maeneo ya Nanenane ndani ya BZhotel, Mashauzi wataimba nyimbo zao zote na wataimba pia nyimbo zao mpya zilizo katika Albam yao ya Tatu "Asiyekujua Hakuthamini", pia kutakuwa na Nyimbo za Albam ya Nne, ni full shangwe.

Baada ya Show ya nguvu Morogoro, kundi hili machachari la Mashauzi litaelekea Dodoma siku ya Jumamosi na kushusha show moja ndani ya Royal Village, show zitakuwa zilezile kali tu.

Katika ziara hiyo Mashauzi Classic siku ya Jumapili watakuwa ndani ya Kilosa katika ukumbi wa Babylon Hall.

Wakazi wa maeneo hayo mnaomba kuwa na maandalizi ya kutosha kuipokea mashauzi maana kutakuwa na burudani tu mwanzo mwisho, ndo kitu kinachowaleta huko.

Sunday, February 9, 2014

BIFU LA ISHA MASHAUZI, THABIT ABDUL LAFIKIA PABAYA...!!

Mkurugenzi wa Wakaliwao Modern Taradance Thabit Abdul
Gazeti moja la Udaku la Jumamosi ya tarehe Feb, 8 limeandika Bifu baina ya Boss wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi na Boss wa Wakaliwao Thabit Abdul kuwa limefikia pabaya na ni vita nzito baina yao.

Gazeti hilo limeandika chanzo ni kudhulumiana wakati Thabit yupo Mashauzi na ndio chanzo cha yeye kuanzisha Wakaliwao Modern Taradance na Thabit kuiba kipande cha Nyimbo ya Isha ambacho kinabeba Albam yake kiitwacho "Wasafi wa Mavazi, Wachafu wa Nafsi"

Katika kuendelea mwandishi wa gazeti hilo alisema aliweza kuongea na wahusika kwa nyakati tofauti ambapo Thabit alipoulizwa alisema:- (NUKUU)
"Hataki malumbano na Mwanamke, yeye sio kiwanda cha Maneno, maneno kila mtu anatamka hivyo kama anajiona ni muasisi wa neno "Wasafi wa mavazi, wachafu wa nafsi" basi imekula kwake. Isitoshe yeye ni mdogo sana kwangu kisanii hivyo nimempuuzia, tokea aliponidhulumu nahisi kama ananifuatafuata sana, naamua kunyamaza kulinda heshima yangu tu". (Mwisho wa kunukuu)
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi

Pia mwandishi huyo aliongea na Isha kwanjia ya simu na kusema:- (NUKUU)
"Mimi sina malalamiko, kwani kila kibaya changu lazima muandike? Muulizeni huyo Thabit na bendi yake na msiandike lolote kuhusu bendi yangu. Muulizeni kama huko aliko kaoa au kaolewa? Karibu sana na kwaheri". (Mwisho wa Nukuu)

Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com baada ya kuisoma taarifa hiyo ya bifu ilifanya mpango wa kuongea na Thabit kuweza kujua ni kwanini watupiane maneno makali kiasi hicho!?

Thabit alisema:- "Ni kweli nimeongea na mwandishi wa gazeti hilo la ( Jina la Gazeti) akiniulizia kuhusiana na hicho kionjo cha Nyimbo yangu kiitwacho "Wasafi wa mavazi, wachafu wa nafsi", ni kweli kipo katika nyimbo lakini nilichomjibu huyo mwandi ni tofauti ni jinsi alivyoandika, mi sina maneno makali kiasi hicho yeye mwenye kaongea yake na sijapenda kwakweli, ila nilichomwambia ni kuwa, "kila mtu anatamka maneno kama yeye ametamka pia kalikuta". Nimesikitishwa na kwa Isha kunitusi namna hiyo kwakweli kanivunjia heshima... Sipendi malumbano naye na pia sina wazo la kumjibu kwa kunitukana kwake.

Blog hii baada ya kuongea na Thabit mwandishi alimpigia simu Isha naye aweze kuthibitisha usemi wake dhidi ya Thabit, simu ya Isha ilikuwa haipatikani kwa kipindi cha muda mrefu, hata hivyo mwandishi alipata stori za chinichini kuwa, Boss huyo wa Mashauzi Classic pia analalamikia mwandishi wa gazeti hilo kuwa hakusema maneno makali vile kwa Boss mwenzio huyo wa Wakaliwao mr. Thabit bali mwandishi alikuwa anakolezea mwenyewe.

Sisi kama blog, na wadau wakubwa wa Taarab hapanchini tumefuatilia ishu nzimaya malumbano yenu Wakurugenzi na kuamini kuwa kilamtu anakuwa anasimamia kwenye ukweli wake, lakini sasa ifikie wakati Mabifu katika muziki wa Taarab tuyaache na tuendeleze mziki wetu kwani namna hii inaleta picha mbaya sana kwa jamii na inawaondolea mshikamano baina ya ninyi wasanii, mabifu yanawapotezea ushirikiano! Hakuna kitu kizuri kama Ushirikiano...!!

Tunawasihi na kuwaomba kilammoja wenu atoe chuki kwa mwenzie, Malumbano na chuki ziishe asitokee mtu kati yenu akaanzisha malumbano haya tena, fanyeni kazi kwa pamoja, Mshikano ili kuboresha maisha yenu pamoja na wasanii wanaowazunguka.

UPENDO, USHIRIKIANO,/MSHIKAMANO Daima ndio nguzo imara...!!!

Thursday, February 6, 2014

AISHA VUVUZELA NA DUME MARIOO...

Aysher na AT wakiwa Studio wakianda "Dume Marioo".
Anaitwa Aysher Othman (Vuvuzela) msanii mwimbaji machachali wa Taarabu hapa Tanzania amegeukia kwenye Miduara.

Akizungumza na blog hii ya Taarabuzetu.blogspot.com Vuvuzela alisema tiyari ameshaingia Studio kurecord nyimbo yake ya mduara inayokwenda kwa jina la "DUME MARIOO" akiwa ameshirikiana na A.T.

Aysher pia amesema katika upande wa mduara Meneja wake ni AT na nyimbo hiyo imerekodiwa katika studio za AT pia.

Kuhusu Taarabu Aysher anasema yupo kama kawaida ila anachotaka kufanya ni kuwaonesha watu kuwa fani anaiweza kotekote maana anavipaji vingi na akiamua kuimba Dance anaweza pia.

Aysher yupo kundi gani kwasasa!?
"Nimerudi kings kwa majaliwa @ kabla Five Stars haijavunjwa rasmi@ na nyimbo itatoka mwezi wa 3 si sasa ila mkao wa kula kaeni hii ni sauti ya mtoto wa Uswahilini mwenye kipaji cha kuzaliwa si kuiga wala kubabaisha, ni sauti ya Vuvuzela".
Aysher Othman (Vuvuzela).
Wapenzi wote wa mduara na wapenzi wa Aysher Othman (Vuvuzela) wakae mkao wa kula kuweza kupokea radha mpya toka kwake

TWAHA WA DAR MODERN TAARAB, AKANA KUMKIMBIA HASSAN VOCHA!....


Muimbaji wa bendi ya Dar-es-Salaam Modern Taarabu Twaha malovee amekanusha habari zilizoandikwa na baadhi ya mitandao kwamba amemkimbia Hassan vocha msanii mpya aliejiunga na bendi hiyo akitokea G5 Modern taarab!.

Akizungumza na blog hii makini Twaha alisema, mimi ni muimbaji ninae jiamini na najua kuimba ndio maana nimefanya kazi mpaka mapacha watatu katika dansi, kamwe siwezi kumkimbia Vocha!, kilichotokea ni kuwa mimi nilikuwa nasumbuliwa na maralia ndio maana hata katika mazoezi ya Dar Modern nilikuwa sionekani, pia sijajiunga na gusagusa, sikweli ni uzushi tu mtu anapokuona umehudhuria show ya bendi yoyote basi huzusha kuwa umejiunga nayo.

Nawaahidi na kuwahakikishia wapenzi wa Dar Modern Taarabu kuwa, nipo na nitaendelea kuwa nao, wasikose tamasha kubwa la Valentine tutakalolifanya pale Travertine Magomeni siku hiyo Wapendanao tarehe 14 February 2014, siku hiyo nitapanda jukwaani na kuimba.