TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, February 9, 2014

BIFU LA ISHA MASHAUZI, THABIT ABDUL LAFIKIA PABAYA...!!

Mkurugenzi wa Wakaliwao Modern Taradance Thabit Abdul
Gazeti moja la Udaku la Jumamosi ya tarehe Feb, 8 limeandika Bifu baina ya Boss wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi na Boss wa Wakaliwao Thabit Abdul kuwa limefikia pabaya na ni vita nzito baina yao.

Gazeti hilo limeandika chanzo ni kudhulumiana wakati Thabit yupo Mashauzi na ndio chanzo cha yeye kuanzisha Wakaliwao Modern Taradance na Thabit kuiba kipande cha Nyimbo ya Isha ambacho kinabeba Albam yake kiitwacho "Wasafi wa Mavazi, Wachafu wa Nafsi"

Katika kuendelea mwandishi wa gazeti hilo alisema aliweza kuongea na wahusika kwa nyakati tofauti ambapo Thabit alipoulizwa alisema:- (NUKUU)
"Hataki malumbano na Mwanamke, yeye sio kiwanda cha Maneno, maneno kila mtu anatamka hivyo kama anajiona ni muasisi wa neno "Wasafi wa mavazi, wachafu wa nafsi" basi imekula kwake. Isitoshe yeye ni mdogo sana kwangu kisanii hivyo nimempuuzia, tokea aliponidhulumu nahisi kama ananifuatafuata sana, naamua kunyamaza kulinda heshima yangu tu". (Mwisho wa kunukuu)
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi

Pia mwandishi huyo aliongea na Isha kwanjia ya simu na kusema:- (NUKUU)
"Mimi sina malalamiko, kwani kila kibaya changu lazima muandike? Muulizeni huyo Thabit na bendi yake na msiandike lolote kuhusu bendi yangu. Muulizeni kama huko aliko kaoa au kaolewa? Karibu sana na kwaheri". (Mwisho wa Nukuu)

Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com baada ya kuisoma taarifa hiyo ya bifu ilifanya mpango wa kuongea na Thabit kuweza kujua ni kwanini watupiane maneno makali kiasi hicho!?

Thabit alisema:- "Ni kweli nimeongea na mwandishi wa gazeti hilo la ( Jina la Gazeti) akiniulizia kuhusiana na hicho kionjo cha Nyimbo yangu kiitwacho "Wasafi wa mavazi, wachafu wa nafsi", ni kweli kipo katika nyimbo lakini nilichomjibu huyo mwandi ni tofauti ni jinsi alivyoandika, mi sina maneno makali kiasi hicho yeye mwenye kaongea yake na sijapenda kwakweli, ila nilichomwambia ni kuwa, "kila mtu anatamka maneno kama yeye ametamka pia kalikuta". Nimesikitishwa na kwa Isha kunitusi namna hiyo kwakweli kanivunjia heshima... Sipendi malumbano naye na pia sina wazo la kumjibu kwa kunitukana kwake.

Blog hii baada ya kuongea na Thabit mwandishi alimpigia simu Isha naye aweze kuthibitisha usemi wake dhidi ya Thabit, simu ya Isha ilikuwa haipatikani kwa kipindi cha muda mrefu, hata hivyo mwandishi alipata stori za chinichini kuwa, Boss huyo wa Mashauzi Classic pia analalamikia mwandishi wa gazeti hilo kuwa hakusema maneno makali vile kwa Boss mwenzio huyo wa Wakaliwao mr. Thabit bali mwandishi alikuwa anakolezea mwenyewe.

Sisi kama blog, na wadau wakubwa wa Taarab hapanchini tumefuatilia ishu nzimaya malumbano yenu Wakurugenzi na kuamini kuwa kilamtu anakuwa anasimamia kwenye ukweli wake, lakini sasa ifikie wakati Mabifu katika muziki wa Taarab tuyaache na tuendeleze mziki wetu kwani namna hii inaleta picha mbaya sana kwa jamii na inawaondolea mshikamano baina ya ninyi wasanii, mabifu yanawapotezea ushirikiano! Hakuna kitu kizuri kama Ushirikiano...!!

Tunawasihi na kuwaomba kilammoja wenu atoe chuki kwa mwenzie, Malumbano na chuki ziishe asitokee mtu kati yenu akaanzisha malumbano haya tena, fanyeni kazi kwa pamoja, Mshikano ili kuboresha maisha yenu pamoja na wasanii wanaowazunguka.

UPENDO, USHIRIKIANO,/MSHIKAMANO Daima ndio nguzo imara...!!!

0 comments:

Post a Comment