TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 30, 2014

Mashauzi Classic ilivyofanya makamuzi Mwanza...!!!

Kundi la Mashauzi wakiwa ndo wametua Mwanza kwa show za Eid!!!
Isha Mashauzi akiwa jukwaani pamoja na tajiri mtoto wa Mwanza Mr. Hamis Muya katika ukumbi wa Buzuruga Plaza.
Hashim Said akiimba Jukwaani...
Umati wa watu uliojaa Ukumbi wa Buzuruga Plaza wakipata burudani toka kwa MashauziClassic Eid Mosi!!!!
Kundi zima la Mashauzi Classic baada ya kukonga nyoyo za mashabiki wa Mwanza, sasa wataelekea jijini Bukoba kufanya makamuzi ndani ya ukumbi wa Liners Club Siku ya Eid Pili!!!

Baada ya Bukoba Eid Tatu watakuwa Jijini Musoma ndani ya ukumbi wa Magereza.

Mjiandae kupata burudani nzuri kabisa kutoka katika kundi bora kabisa - Mashauzi Classic...!!!!

Thursday, July 24, 2014

DOWNLOAD: "Full Kuenjoy", yake Black Kopa mtoto wa Malkia Khadija Kopa...

Black Kopa na Khadija Kopa (Mama).

Ujio wa Black Kopa mtoto wa Khadija Kopa, ni Sheedah...!!!!

Anakwenda kwa jina la Muhammed Kibwana au Black Kopa pia unaweza kumuita Prince Kopa, mtoto wa Malkia wa mipasha Tanzania Bi Khadija Kopa.

Ni msanii wa Muziki toka muda mrefu kama ilivyo kwa Mama yake, marehemu kaka yake (Omary Kopa) "Apumzike kwa amani", pamoja na ndugu zake wengine wamekuwa na kipaji cha kuimba karibu familia nzima.

Black Kopa yeye anasema ameanza kuimba siku nyingi akiwa amejikita sana katika mziki wa Bongo flaver na ameweza kutoa nyimbo kadhaa, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda, marafiki na familia yake pia wakawa wanamshauri ni kwanini asiimbe taarab wakati sauti nzuri ya kuimba anayo!?.

Hatimae kijana kaamua kujitoa mazima mwaka 2014 na kuachia nyimbo yake inayokwenda kwa jina la "Full kuenjoy".

Black Kopa akihojiwa na Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com
Anasema nyimbo hii inapatikana katika albam ya Ogopa Kopa's Classic Band" ambayo ni bendi changa na ni mpya kabisa inakuja hivi karibuni. Albam itaitwa "Lady with Confidence".

Katika nyimbo hii ameshirikiana na watu takribani wanane, wanne wapiga vyombo na wanne waitikiaji.

Waitikiaji ni:- 1). Warda Mlawa, 2). Shadya Shombeshombe 3). Rukia Manala na 4). Hemed Omary.

Wapiga vyombo ni:- 1). Omary Zungu au Omary Kinanda (Keyboard) 2). Harifa (Keyboard 2), 3). Miraji (Soro Gitaa), 4). Said James au Said Bass (Bass Gitaa).

Black Kopa anakuja kwa kasi anasema mashabiki wajiandae kupata radha mpya kabisa toka kwake na atafanyia remix pia nyimbo za kaka yake Omary Kopa kwa kuziimba.

Mashabiki anaomba saana sapoti yenu.

Tuesday, July 15, 2014

DOWNLOAD NYIMBO 4 MPYAA BADO ZA MOTO KABISA: DAR MODERN...


Kundi zima la Dar Modern Taarab limeachia Albam yake mpya kabisa inayokwenda kwa jina la "UBINAADAM KAZI", Pata kudownload na kusikiliza nyimbo tamu kabisa toka kwao.

Uzinduzi wa Albam hii "UBINAADAM KAZI" utafanyika siku ya Idd Mosi pale Travertine Magomeni.



Pakua hizo nyimbo usikiliza utamu uliopo kisha nakuletea tena nyimbo zingine mbili kali...!!!

DAR MODERN NDO HABARI YA MJINI...!!!

MASHAUZI CLASSIC YAPIGA HODI MWANZA SIKU YA IDD MOSI...!!!

Kundi la Taarab linalofanya vyema katika show zake mbalimbali "Mashauzi Classic" chini ya uongozi wake Isha Mashauzi, siku ya Idd Mosi watafanya show ya Uzinduzi wa Albam yao mpya ya "Asiyekujua hakuthamini!!!

Watakuwa katika ukumbi wa "BUZURUGA PLAZA" na kiingilio kitakuwa Tshs. 10,000/= tu kuanzia saa 3 Usiku mpaka baaaasi!!!

Kutakuwa na wasanii machachari wenye sauti za kuvutia kama Isha Mashauzi (Mkurugenzi), Hashim Said Thania Msomali, Saida Ramadhani, Zubeidah Andunje na wengine walio katika Mashauzi Classic.




SI YA KUKOSA MWANZA...!!!!!!

USIKOSE!:- NI UZINDUZI WA ALBUM MPYA YA DAR MODERN TAARAB...

Kundi zima la Dar Modern Taarab lenye maskani yake pale Magomen lililosheheni wasanii wakali na wenye vipaji vya hali ya juu, watashusha burudani ya uhakika pale Travertine Magomeni siku ya Idd Mosi ikiwa ni UZINDUZI wa Albamu yao mpya kabisa iliyopewa jina la "UBINAADAM KAZI".

Kutakuwa na wasanii waalikwa kama kawaida na Surprise kibao...!!

USIKOSE!!!


Wednesday, July 9, 2014

Mashauzi Classic: Mmoja aachishwa kazi na mwingine asimamishwa...


Mkurugenzi wa Mashauzi Classic - Isha Mashauzi.
Kundi la Taarab Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi linalofanya shughuli zako jijini Dar es Salaam, Tanzani na Show zake kila Alhamisi hufanyika Mango Garden imewasimamisha kazi wasanii wake wawili.

Taarifa zilizofika katika meza yetu ya Taarabuzetu.blogspot.com zinasema wasanii hao wamesimamishwa toka Ijumaa ya tarehe 13/06/2014, waliosimamishwa ni Thania Msomali na Fatma Seif.
Fatma Seif katika kundi hilo la Mashauzi amewahi kuimba nyimbo iitwayo “Mdomo wako utakuponza” katika albam ya “Si bure unamapunngufu”.
Habari zilizotufikia kwa upande wa Fatma kisa cha kusimamishwa ni kutohudhuria show ya Mashauzi siku hiyo na kudaiwa kuonekana katika bendi ya Gusagusa Min iliyokuwa na Show pia siku hiyo.
Mwandishi wa habari hii baada ya kupata habari hizi alimpigia simu Fatma mwenyewe aweze kueleza kisa hasa cha yeye kusimamishwa kazi.
Fatma:- “Mimi siku hiyo sikwenda kazini kwasababu nilikuwa naumwa, kiongozi wangu alinipigia simu kuniambia nihudhulie kwenye show nikamwambia siwezi kwasababu naumwa, akaniacha siku ya pili yake akanipigia simu tena kuniulizia hali yangu nikamwambia bado nipo nyimbani tu, lakini cha kushangaza akanitumia ujumbe kuwa kunisimamishwa kazi miezi mitatu (3), kesho yake akanitumia ujumbe tena wa kuwa Nimeachishwa kabisa kazi hivyo niko huru kutafuta bendi yoyote, kwakweli imeniuma sana maana sijui kama ndo hili tatizo la mimi kuugua.
Alipoulizwa Fatma amechukua uamuzi gani?
"Sijachukua uamuzi wowote na hivi sasa nipo tu nyumbani bado akili yangu haijatulia hivyo sijajua kitu cha kufanya, acha kwanza nitulie".

KWA UPANDE WA THANIA MSOMALI:
Baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari hii alisema:
Thania:- “Mimi nilikuwa naumwa na nilitoa taarifa kwa uongozi, nimeenda Hospitali kufanyiwa uchunguzi nikaonekana (Akataja ugonjwa) hivyo nikaandikiwa dawa ambazo niliendelea kuzitumia, baada ya kama week mbili nikawa najisikia vizuri na nikaamua kwenda kuripoti kazini lakini cha kushangaza kidogo nikaambiwa niendelee kupumzika kwanza mpaka nipone ndo niende, nimekaa nyumbani tena baada ya siku kadhaa Mashauzi walikuwa wanapiga Mango nikaomba tena nihudhulie kazini ila nikaambia nisubiri tu ila nikaomba basi niende kuangalia show nikaruhusiwa ila sikuimba.
Sasa kinachoniweka njia panda ni kuwa, hali yangu ni nzuri nimeimarika ki-afya na ninahamu ya kuimba ila nikiuelezea uongozi wangu kuwa nataka kuripoti kazini wanasema nisubiri tu sasa nitasubiri hadi lini!? Kwa kweli sijajua muafaka upo wapi na hatma yangu sijajua maana naendelea kusubiri tu na wala sijaelezwa kitu”.
Thania Msomali.
 Blog hii iliongea pia na Kiongozi wa wasanii katika kundi la Mashauzi Mr Hashim Said na kusema:-

"Fatma tulimuondoa ktk bend kwa utovu wa nidhamu, alitega kuja kazini kwa kisingizio cha kuumwa.

Yote hayo yametokana na siku hiyo ilikuwa ni alhamisi na bendi tuliigawa mara mbili baadhi walikwenda Mwanza kikazi na baadhi wakabaki Dsm kikazi waliokwenda mwanza waliambatana na Mkurugenzi waliobaki Dsm walibaki na mimi pale Mango Garden kikazi akiwemo Fatma! 

Lakini cha kushangaza Fatma alinitumia ujumbe muda wa saa moja usiku akidai anaumwa! Nikamuuliza huu ugonjwa umeanza saa hizi kwa kuwa ni muda wa kuja kazini? nikamwambia lazima aje kazini sababu waimbaji waliokuwapo ni wachache. 

Kinachoonekana ni kuwa Fatma alimaindi suala la yeye kubakishwa Dsm! La kushangaza zaidi kazini hakuja na akaonekana huko Mbagala akiwa na bendi hizi za mitaan akiimba hapo ndipo nilipomsimamisha kazi, kibaya zaid alishindwa kuomba msamaha Uongozi ukaamua kumuondoa katika bendi sababu hatuwezi kuwa na msanii asiekuwa na uzalendo na bendi yke! 

Thania nae tumemsimamisha kutokana na kiwango chake kila kukicha kinashuka na tumempa nafasi ya kufanya mazoezi zaidi ili akiwa vizuri basi atarudi kazini ".

Hiyo ndo habari kamili, kilichotokea hapo kimeongelewa ni Utoro/Utegaji na nidhamu ya kazi, wasanii kutokuwa na uzalendo na Bend zao.

Friday, July 4, 2014

UJUMBE MZITO WA HAMMER Q KWENDA KWA #LIL GETTO WA AKHENATON RECORD...

Hammer Q
 Nimepata data zako bob

Lakini Na amini kuwa MUNGU pekee ndie ana mamlaka ya kuamua lolote juu yangu na sio wewe Nitakupenda km binaadam mwenzangu hata km nimestuka kuna mabaya unayonitendea naamini hujui ulitendalo...!

Nitaendelea kuishi kwa uhalisia wa maisha yangu na ilivyoumbwa roho yangu sitakulipiza baya lako kwa baya langu sababu Mimi kwa sasa nimekua sio mtu wa visasi na roho yangu ni nyeupe kabisa sitakutendea baya bali nitakuombea kwa mungu akubadilishe kutoka roho mbaya uliyonayo na akuongoze ktk njia sahihi

Jifundishe kuTii haja za moyo wako si maneno ya watu...! Kawaida Yangu huridhika na nilichonacho kwa kuamini ndicho MUNGU alichonipa na kuna siku nitapata zaidi...! Na unavyonidharau nitazid kukuheshim na kujituma maana unanipa uchungu wa kutafuta mafanikio...!

Huwa na Amini na mimi ni muhimu ktk jamii ndio mana nimeumbwa...! nakushangaa sana unavokua mtu wa kujaribu kuniharibia rizki zangu kana kwamba umeziumba ww Nasijui ingekuaje kama ungepewa funguo ya rizki

We Fanya unavofanya niharibie unavoniharibia mimi namuachia Mungu kisha Nikutakie ramadhan NJEMA Na mungu akutilie wepes ktk kubadilika .ningekusema pembeni ningemkosea mungu lkn nimekuchana kweupe kuridhisha roho yang.

Bob (Lil Ghetto).
Blog hii ilimpigia simu Hammer Q ili kujua ni nini kilichopelekea yeye kuandika ujumbe mzito namna hii kwenda kwa Bob (Lil Ghetto)

"Unajua huyu jamaa ni mbinafsi sana, mimi baada ya kujiunga nae sikujua kitu lakini nimekuja kuona mambo yake sio kabisa ndo nikaona bora nijitoe tu nifanye mambo yangu mimi kama mimi, lakini hata baada ya kutoka amekuwa akinifuatilia sana, hapa juzi tu tena kanifanyia fitna katika jitahada zangu za kujitafutia ndo nikaamua kuandika ujumbe huu na ninaamini utakuwa umemfikia. Sijaandika kwa siri nimeandika kweupe nikiwa na uhakika wa ujumbe kumfikia mlengwa!". 


Katika kundi la Offsidetrike liliokuwa likiongozwa naye Lil Ghetto na Hammer Q kwasasa yupo Lil Ghetto mwenyewe (Pekee).