Mkurugenzi wa Mashauzi Classic - Isha Mashauzi. |
Kundi la Taarab Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi linalofanya shughuli
zako jijini Dar es Salaam, Tanzani na Show zake kila Alhamisi hufanyika Mango
Garden imewasimamisha kazi wasanii wake wawili.
Taarifa zilizofika katika meza yetu ya
Taarabuzetu.blogspot.com zinasema wasanii hao wamesimamishwa toka Ijumaa ya
tarehe 13/06/2014, waliosimamishwa ni Thania Msomali na Fatma Seif.
Fatma Seif katika kundi hilo la Mashauzi amewahi
kuimba nyimbo iitwayo “Mdomo wako utakuponza” katika albam ya “Si bure
unamapunngufu”.
Habari zilizotufikia kwa upande wa Fatma
kisa cha kusimamishwa ni kutohudhuria show ya Mashauzi siku hiyo na kudaiwa
kuonekana katika bendi ya Gusagusa Min iliyokuwa na Show pia siku hiyo.
Mwandishi wa habari hii baada ya kupata
habari hizi alimpigia simu Fatma mwenyewe aweze kueleza kisa hasa cha yeye
kusimamishwa kazi.
Fatma:- “Mimi siku hiyo sikwenda kazini kwasababu nilikuwa naumwa, kiongozi
wangu alinipigia simu kuniambia nihudhulie kwenye show nikamwambia siwezi
kwasababu naumwa, akaniacha siku ya pili yake akanipigia simu tena kuniulizia
hali yangu nikamwambia bado nipo nyimbani tu, lakini cha kushangaza akanitumia
ujumbe kuwa kunisimamishwa kazi miezi mitatu (3), kesho yake akanitumia ujumbe
tena wa kuwa Nimeachishwa kabisa kazi hivyo niko huru kutafuta bendi yoyote,
kwakweli imeniuma sana maana sijui kama ndo hili tatizo la mimi kuugua.
Alipoulizwa Fatma amechukua uamuzi gani?
"Sijachukua uamuzi wowote na hivi sasa nipo
tu nyumbani bado akili yangu haijatulia hivyo sijajua kitu cha kufanya, acha
kwanza nitulie".
KWA UPANDE WA THANIA MSOMALI:
Baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari
hii alisema:
Thania:- “Mimi nilikuwa naumwa na nilitoa taarifa kwa uongozi, nimeenda
Hospitali kufanyiwa uchunguzi nikaonekana (Akataja ugonjwa) hivyo nikaandikiwa
dawa ambazo niliendelea kuzitumia, baada ya kama week mbili nikawa najisikia
vizuri na nikaamua kwenda kuripoti kazini lakini cha kushangaza kidogo
nikaambiwa niendelee kupumzika kwanza mpaka nipone ndo niende, nimekaa nyumbani
tena baada ya siku kadhaa Mashauzi walikuwa wanapiga Mango nikaomba tena
nihudhulie kazini ila nikaambia nisubiri tu ila nikaomba basi niende kuangalia
show nikaruhusiwa ila sikuimba.
Sasa kinachoniweka njia panda
ni kuwa, hali yangu ni nzuri nimeimarika ki-afya na ninahamu ya kuimba ila
nikiuelezea uongozi wangu kuwa nataka kuripoti kazini wanasema nisubiri tu sasa
nitasubiri hadi lini!? Kwa kweli sijajua muafaka upo wapi na hatma yangu
sijajua maana naendelea kusubiri tu na wala sijaelezwa kitu”.
Thania Msomali. |
"Fatma tulimuondoa ktk bend kwa utovu wa nidhamu, alitega kuja kazini kwa kisingizio cha kuumwa.
Yote hayo yametokana na siku hiyo ilikuwa ni alhamisi na bendi tuliigawa mara mbili baadhi walikwenda Mwanza kikazi na baadhi wakabaki Dsm kikazi waliokwenda mwanza waliambatana na Mkurugenzi waliobaki Dsm walibaki na mimi pale Mango Garden kikazi akiwemo Fatma!
Lakini cha kushangaza Fatma alinitumia ujumbe muda wa saa moja usiku akidai anaumwa! Nikamuuliza huu ugonjwa umeanza saa hizi kwa kuwa ni muda wa kuja kazini? nikamwambia lazima aje kazini sababu waimbaji waliokuwapo ni wachache.
Kinachoonekana ni kuwa Fatma alimaindi suala la yeye kubakishwa Dsm! La kushangaza zaidi kazini hakuja na akaonekana huko Mbagala akiwa na bendi hizi za mitaan akiimba hapo ndipo nilipomsimamisha kazi, kibaya zaid alishindwa kuomba msamaha Uongozi ukaamua kumuondoa katika bendi sababu hatuwezi kuwa na msanii asiekuwa na uzalendo na bendi yke!
Thania nae tumemsimamisha kutokana na kiwango chake kila kukicha kinashuka na tumempa nafasi ya kufanya mazoezi zaidi ili akiwa vizuri basi atarudi kazini ".
Hiyo ndo habari kamili, kilichotokea hapo kimeongelewa ni Utoro/Utegaji na nidhamu ya kazi, wasanii kutokuwa na uzalendo na Bend zao.
0 comments:
Post a Comment