|
Mr Amin Salmin, Mkurugenzi wa T Motto |
Ni Amin Salmin Mkurugenzi wa T Moto Modern Taarab alianzisha mada baada ya kuhudhulia Kongamano la wasanii katika television ya ITV.
Salmin alisema:- Nimepatwa na mshangao sana ktk kipindi cha malumbano ya hoja
kilichorushwa live na ITV mada ilikua nini kifanyike kulinda hati miliki
na kazi za wasanii kwa waharamia pamoja na midia kupiga nyimbo bila
kumlipa msanii. Hakuna msanii wa taarab wala viongozi walijitokeza zaidi
yangu mimi!!, kweli wahusika wa taarab tutafika? wasanii wa bongo movi
walijitokeaza kwa wingi, kweli tunajitabua?
Baada ya Amin kutoa mada hii katika mtandao wa Facebook watu wengi walichangia wakisema wasanii wa taarab hawakuwa na taari ya tukio hilo hivyo kungekuwa na taarifa wangeweza kujitokeza na kutoa maoni yao.
Pia wengine walifunguka ki-vingine kwa kusema wasanii wa taarabu wamelala sana hawana habari ya kufuatilia haki zao na wala hawajua haki zao na pia hawana umoja wanajisikia sana...!!
|
Mr Hamis Slim, Mkurugenzi wa G5 Modern Taarab |
|
Bi Siza Mazongela (Kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Sanaa na Masoko BASATA. |
Amin aliendelea kwa kusema:-
Inaeleweka
wazi kipindi cha malumbano ya hoja hutangazwa wiki moja kabla ya
kipindi husika,ila mada ilikua ina umuhimu sana kwani watu wa
TRA,Basata,Kosota nk wote walikuwepo ila bado hatuja chelewa itv wao
wamechokoza mada bali sisi tunaweza kujipanga tukafanya muendelezo kuna
ya muhimu sana kwa faida ya wasani na sanaa kwa ujumla wake pia nadhani
tungekua na umoja wetu nadhani ingekua kiunganishi kwetu kwani bongo
movi Stive Nyerere ndie alietumika kuwapa taarifa wenzake bado
nasisitiza umoja wa taarab unahitajika vyenginevyo tutakua tunatumia
nguvu kubwa na maingizo kidogo.
Kuna
kitu kinaitwa mrabaha maana yake ni mrejesho baada ya mauzo ya kazi za
jasho la msanii kupitia TRA, tujiulize nani kati yetu kapata malipo hayo?
kuna mengi ya msingi kwa wasanii na taifa.
Mr
alisema :-
Amin
niamini kwenu itakuwa ngumu mnajisikia sana umoja kwenu ngumu. Sisi
tunaona wasanii wengine wanavyoshirikiana tofauti na nyinyi sisi wadau
tunaomba sana kuweni na umoja wa kweli.
Mdau akasema:-
Alisemalo
Ramadhani Saidi namuunga mkono kwani chama cha taarabu kipo tangu enzi
za kina marehem Abasi Mzee, kina Mzee Kibiriti, kina Mzee Mdigo, marehem
Khamisi Joji, Bi Daima Abdallah, hao walikua na bend kama ifuatavyo:-
Egyptian, new Extra, Alwatan.
Hizo zote zilikuwa bend za taarabu chama
kinaitwa TTA, (TANZANIA TAARABU ASSOCIATION), kimesajiliwa na
kinatambulika, wasaanii wakiitwa kwenye vikao hawafiki, kwasasa
Mwenyekiti alikua marehem Abrahmani Muchacho katibu nilikua mimi,
naomba Amin Salmin
upange siku mimi na wewe twende BASATA tukatafute faili letu
nikukabidhi ili tufanye utaratibu wa kuwaita kwenye kikao tufufue chama
chetu, je upo tayari?Sasa ilifikia kuwa Jumatatu ya tarehe 3/08/2014 wawe washafuatilia BASATA.
naye alichangia:- Niko
pamoja na nyote ishallah utasimama umoja wetu ila katiba ndio muhimu
pia iwe ya kisawa sawa kanuni zisimame vizuri hiyo jtatu niambieni saa
ngapi na mie ntakuwa basata.Matumaini yaliendelea ya uwezekano wa kufanikiwa wa kupata umoja.
naye kafunguka:- Mimi nawapongeza wote waliochangia na ktk kuongozea nipo tayari na shangazi yangu hapo Siza Mazongela kumsaidia hiyo jumatatu ili kuweza kufanikisha hilo pamoja na Mr Amin Salmin naomba kuwasilisha.
I
know kaka mm binafsi nilikuwa napata tabu ktk hili coz hakuna kitu
chcht kilicho na mafanikio paipokuwa na utaratibu unaoeleweka kiongozi
dini zinaongozwa na misahafu na biblia basi hata inchi inaongozwa na
katiba sambamba na chama chcht kile dunia vinaongozwa na katibu kwann
sisi nina imani ya dhati inawezekana inshallah wakati sasa umefika na
tumalize nguvu zetu ktk hili kwa faida ya wasanii wa vizazi vijavyo
wasje wakaichukia tasnia hii tuliyoachia mm mkurugenzi na wasanii wangu
wote wa G5 modern taarab tupo tayari kwa hali na mali naomba kuwasilisha.
Bi
alikuwa serius zaidi kwa kuonesha machungu aliyokuwa nayo kwa kwenda BASATA siku hiyohiyo hakusubiri tena Jumatatu, alienda na kutuletea taarifa hizi:-
"Nimejaaliwa
kwenda basata nimekutana na Mkurugenzi wa saana na masoko, jumatatu
watakuwa na kikao cha kiofisi tumekubaliana twende Alhamisi, haya kazi
kwako mjukuu wangu amini Amin Salmin,
nawale wote walio tayari kwa hili, na nimewaomba watutafutie fail la
TTA, ndugu yangu Mzee Yusuf, kwenye faili katibaimo saana kuipitia na
kuiboresha, naomba wadau mtuombee mungu atupe wepesi wa kufatilia hili
swala".Safari ya kufanikisha na juhudi zinaonekana, siku ya Alhamisi tarehe 7/08/2014 ndo siku tutakayopata jibu sahihi.
Taarabuzetu.blogspot.com inawatakieni mafanikio mema tupate viongozi wa kuweza kutupa muongozo tuweze kusonga mbele na kufuatilia haki za wasanii.