Mr Amin Salmin, Mkurugenzi wa T Motto |
Salmin alisema:- Nimepatwa na mshangao sana ktk kipindi cha malumbano ya hoja kilichorushwa live na ITV mada ilikua nini kifanyike kulinda hati miliki na kazi za wasanii kwa waharamia pamoja na midia kupiga nyimbo bila kumlipa msanii. Hakuna msanii wa taarab wala viongozi walijitokeza zaidi yangu mimi!!, kweli wahusika wa taarab tutafika? wasanii wa bongo movi walijitokeaza kwa wingi, kweli tunajitabua?
Baada ya Amin kutoa mada hii katika mtandao wa Facebook watu wengi walichangia wakisema wasanii wa taarab hawakuwa na taari ya tukio hilo hivyo kungekuwa na taarifa wangeweza kujitokeza na kutoa maoni yao.
Pia wengine walifunguka ki-vingine kwa kusema wasanii wa taarabu wamelala sana hawana habari ya kufuatilia haki zao na wala hawajua haki zao na pia hawana umoja wanajisikia sana...!!
Mr Hamis Slim, Mkurugenzi wa G5 Modern Taarab |
Bi Siza Mazongela (Kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Sanaa na Masoko BASATA. |
Kuna kitu kinaitwa mrabaha maana yake ni mrejesho baada ya mauzo ya kazi za jasho la msanii kupitia TRA, tujiulize nani kati yetu kapata malipo hayo? kuna mengi ya msingi kwa wasanii na taifa.
Mr Ramadhani Said alisema :-
Amin niamini kwenu itakuwa ngumu mnajisikia sana umoja kwenu ngumu. Sisi tunaona wasanii wengine wanavyoshirikiana tofauti na nyinyi sisi wadau tunaomba sana kuweni na umoja wa kweli.
Mdau Siza Mazongela akasema:-
Alisemalo Ramadhani Saidi namuunga mkono kwani chama cha taarabu kipo tangu enzi za kina marehem Abasi Mzee, kina Mzee Kibiriti, kina Mzee Mdigo, marehem Khamisi Joji, Bi Daima Abdallah, hao walikua na bend kama ifuatavyo:-
Egyptian, new Extra, Alwatan.
Hizo zote zilikuwa bend za taarabu chama kinaitwa TTA, (TANZANIA TAARABU ASSOCIATION), kimesajiliwa na kinatambulika, wasaanii wakiitwa kwenye vikao hawafiki, kwasasa Mwenyekiti alikua marehem Abrahmani Muchacho katibu nilikua mimi, naomba Amin Salmin upange siku mimi na wewe twende BASATA tukatafute faili letu nikukabidhi ili tufanye utaratibu wa kuwaita kwenye kikao tufufue chama chetu, je upo tayari?
Sasa ilifikia kuwa Jumatatu ya tarehe 3/08/2014 wawe washafuatilia BASATA.
Mzee Yussuf naye alichangia:- Niko pamoja na nyote ishallah utasimama umoja wetu ila katiba ndio muhimu pia iwe ya kisawa sawa kanuni zisimame vizuri hiyo jtatu niambieni saa ngapi na mie ntakuwa basata.
Matumaini yaliendelea ya uwezekano wa kufanikiwa wa kupata umoja.
Hamis Slim naye kafunguka:- Mimi nawapongeza wote waliochangia na ktk kuongozea nipo tayari na shangazi yangu hapo Siza Mazongela kumsaidia hiyo jumatatu ili kuweza kufanikisha hilo pamoja na Mr Amin Salmin naomba kuwasilisha.
I know kaka mm binafsi nilikuwa napata tabu ktk hili coz hakuna kitu chcht kilicho na mafanikio paipokuwa na utaratibu unaoeleweka kiongozi dini zinaongozwa na misahafu na biblia basi hata inchi inaongozwa na katiba sambamba na chama chcht kile dunia vinaongozwa na katibu kwann sisi nina imani ya dhati inawezekana inshallah wakati sasa umefika na tumalize nguvu zetu ktk hili kwa faida ya wasanii wa vizazi vijavyo wasje wakaichukia tasnia hii tuliyoachia mm mkurugenzi na wasanii wangu wote wa G5 modern taarab tupo tayari kwa hali na mali naomba kuwasilisha.
Bi Siza Mazongela alikuwa serius zaidi kwa kuonesha machungu aliyokuwa nayo kwa kwenda BASATA siku hiyohiyo hakusubiri tena Jumatatu, alienda na kutuletea taarifa hizi:-
"Nimejaaliwa kwenda basata nimekutana na Mkurugenzi wa saana na masoko, jumatatu watakuwa na kikao cha kiofisi tumekubaliana twende Alhamisi, haya kazi kwako mjukuu wangu amini Amin Salmin, nawale wote walio tayari kwa hili, na nimewaomba watutafutie fail la TTA, ndugu yangu Mzee Yusuf, kwenye faili katibaimo saana kuipitia na kuiboresha, naomba wadau mtuombee mungu atupe wepesi wa kufatilia hili swala".
Safari ya kufanikisha na juhudi zinaonekana, siku ya Alhamisi tarehe 7/08/2014 ndo siku tutakayopata jibu sahihi.
Taarabuzetu.blogspot.com inawatakieni mafanikio mema tupate viongozi wa kuweza kutupa muongozo tuweze kusonga mbele na kufuatilia haki za wasanii.
0 comments:
Post a Comment