Hatimaye wakurugenzi wa Mashauzi Classic na
Jahazi Modern Taarab, wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kuthibitisha
kuwepo kwa onyesho la pamoja la makundi hayo yenye nguvu katika muziki wa
taarab.
Onyesho hilo litafanyika mwezi huu Jumapili tarehe
22 ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni.
Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf na mkurugenzi
wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi, wamesema siku
hiyo hatumwi mtoto dukani.
Wakiongea katika mkutano huo wa waandishi wa
habari uliofanyika Jumatatu jioni katika hotel ya Travertine Hotel, wakurugenzi
hao ambao wote ni waimbaji nyota, wakasema onyesho hilo si mpambano lakini pia
sio la masihara kwani kila bendi imejipanga kuhakikisha inaangusha burudani
iliyokwenda shule.
Pichani juu kutoka kushoto ni: Meneja wa Mashauzi Classic
Ismail Rashid, Isha Mashauzi, Mzee Yussuf na Seif Magwaru meneja wa Jahazi
Modern Taarab.
0 comments:
Post a Comment