Mkurugenzi wa bendi ya Taarab ya G5 Modern Taarab Mr. Hamis Slim, ametangaza rasmi nia yake ya kuwatumikia wananchi wa Mtoni kwa Azizi Ally.
Hamis alijieleza mwenyewe katika maelezo haya hapa:-
Assalaam
aleyko watanzania wenzangu hususani wanamtoni wenzangu, tumshukuru
mungu kwa kutufikisha tena salama ktk mwezi huu mtukufu wa ramadhani
mwezi ambao unatufanya tumrudie mola wetu kwa kutimiza zile nguzo tano
za kiislam.
Pamoja na hayo pia mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi basi
itakuwa si vibaya mimi km kijana imara niliyelelewa madhubuti na Chama
Cha Mapinduzi kutangaza nia yangu ya kutaka kug
ombea
nafasi ya Udiwani ktk kata yangu ya Mtoni.
Mimi kijana mwenzenu Hamis
Slim wakati ukifika nitachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya udiwani wa
kata ya Mtoni kwa minajali ya kuleta maendeleo muonekano na si
maendeleo simulizi, shime vijana wenzangu tuamke sasa tuungane mkono
kulikomboa taifa letu kwa mawazo chanya kwa pamoja tunaweza.
Nitaomba nafasi baada ya kutafakari takribani miaka mitano na kuona
fursa nyingi tulizonazo ktk kata ya Mtoni kushindwa kutumiwa kwa maslahi
na manufaa ya wananchi wa mtoni
Badala yake kutumiwa na watu wengine wa nje ya mtoni.
Changamoto hizi ndizo zilizonilpelekea kuwa na maamuzi ya kugombea kwa
ajili ya kuleta Mabadiliko mapya, Fikra mpya, Ubunifu mpya, Uongozi mpya
na kuondoa uongozi ulio na mawazo mgando.
Kwakuwa uwezo ninao sababu
ninazo nia ya kugombea ninayo kwa pamoja na wanamtoni wenzangu
tutashinda na kuibadili na kuivusha kata ya mtoni pale ilipofikishwa
hakika SLIM ndio chaguo lako (HAMIS SLIM HAKIKA ATATUFIKISHA)
Bwana Hamis alipoulizwa kuhusu kugombea Ubunge alisema:-
Naamini kila mtu anatamani kugombea nafasi hiyo ya Ubunge, ni nafsi kubwa sana ambayo nitafanya hivyo baada ya kuwatumikia kwanza wananchi wenzangu na kuona uwezo wangu katika utendaji kazi, nataka wananchi wenyewe waje kusema kama nafaa. Najiamini ipo siku nitakuwa pale Bungeni kutetea na kuleta maendeleo ya wananchi wangu, watanzania wenzangu.
Taarabuzetu.blogspot.com inakutakia kila la kheri Bwan Hamis Slim.