TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, November 12, 2013

NYAWANA KUZIKWA KESHO TAREHE 13 NOV. TABORA.

Nyawana Fundikira.
Msanii na mtangazaji wa Passion FM Nyawama Fundikira kuzikwa kesho Jumatano nyumbani kwao Itetemwa mkoani Tabora.

Kwa siku ya leo kutakuwa na maandalizi na kisomo kitakachofanyika maeneo ya Makanya maalufu kwa bibi Nyau Magomeni, kisomo kitakuwa kati ya saa 7 na safari inatarajiwa kuwa saa kumi na moja 11 jioni.

Wote mnaombwa kuhudhuria kwa wingi kumsindikiza ndugu yetu mpendwa.

Mungu amlaze mahali pema peponi, sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.

Monday, November 11, 2013

BAD NEWS: NYAWANA KAIS FUNDIKIRA KAFARIKI...!!!


Nyawana enzi za uhai wake.
Ni habari za kusikitisha na kuhudhunisha tumezipata muda huu kuwa Nyawana Fundikira (Malkia wa Kinyamwezi) amefariki.

Taarabu Zetu imeongea na mume wa Nyawana ambaye ni Kais Musa na kuthibitisha kutokea kwa kifo cha mkewe.

Nyawana amefariki leo mida ya saa 8 akiwa Mwananyama Hospitali na msiba utakuwa Mwananyamala Nyumbani kwake.

Mungu amlaze mahali pema peponi... Amina.

Kumbukia Nyimbo yake kwa kuisikiliza hapa:-

Nyimbo inaitwa:- Shetani Kataja Jina

DEALER'S MODERN TAARABU, WAIBIWA VIFAA VYA MUZIKI...

Bendi mpya ya Dealer's Modern Taarabu inayoongozwa na Mwanahawa Ally Chipolopolo imeibiwa vifaa vya muziki. 

Bendi hiyo iliibiwa vifaa vyake vya muziki vikiwa stoo baada ya kumaliza show yake, vifaa vilivyoibiwa vimetajwa zikiwemo Mic 5, Wire za Mic 5, wire za Vinanda 2 pamoja na vifaa vingine ambavyo thamani yake ni zaidi ya laki nane. 

Akizungumza na mwandishi wa blog hii ya Taarabu Zetu Mkurugenzi wa bendi hiyo Mwanahawa Ally "Chipolopolo" alisema wizi huo ulitokea Tar 3 wakati yeye yupo Travetine katika show ya DIDA wa times.

Mpaka sasa mwizi hajapatikana ila mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo ndo anashikiliwa.

Sunday, November 10, 2013

WASANII WATATU WASIMAMISHWA 5 STARS KWA UTOVU WA NIDHAMU..

Zena Mohamed
Bendi ya 5 Stars ambayo ilifanya ziara hivi karibuni katika mikoa ya Mbeya, Sumbawanga na Mpanda, imewasimamisha wasanii watatu kwa utovu wa nidhamu waliouonyesha kipindi wapo katika ziara hiyo. 
 

Mpelelezi wetu aliyejichomeka ndani ya bendi hiyo aliwataja wasanii hao kuwa ni Zena Mohamedy, Mariam B.S.S na Mariam Hamdani. 
Mariam B.S.S.
Sababu kubwa ya kusimamishwa kwao taarifa zinasema ni kukiuka masharti ya kambi na baadhi yao kwenda kulala nje na wanaume zao!, 

Taarabuzetu ilimtafuta Thabit Abdul ambae alikili kusimamishwa kwa wasanii hao akisema ni kwa utovu wa nidhamu tu!.

Friday, November 8, 2013

MRIDU ALLY KUITAMBULISHA LEO BOMBASTIC MODERN TAARABU...

Mridu Ally "TX".
Baada ya kuyatumikia makundi ya wenzake kwa muda mrefu, hatimaye mtunzi na mcharaza gitaa maarufu wa muziki wa Taarabu nchini, Mridu Ally 'Tx' mwezi uliopita "October 2013" alianzisha kundi lake la miondoko ya Taarabu liitwalo Bombastic Modern Taarabu "Wana B Kubwa".

Akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com Mridu alisema kundi lake linaundwa na wasanii wanane baadhi wakiwa ni chipukizi na kutamba kama alivyoweza kuwainua chipukizi wengine waliokuja kutamba nchini ndivyo atakavyofanya kwa wasanii hao wapya.

Alisema kundi hilo linatarajia kuanza rasmi leo kwa kujitambulisha maeneo ya Tabata kabla ya kuendelea katika maonyesho yao ya mwishoni mwa wiki.

"Katika kuhangaika kwangu, nimejianzishia kundi langu binafsi linaliofahamika kwa jina la 'Bombastic Modern Taarab na linaundwa na wasanii kama nane hivyo wengi wao wakiwa ni chipukizi hasa kwa waimbaji, lengo nao kuwainua kama nilivyofanya kwa akina Tizo Mgunda, Salha Abdallah, Sikudhani Ally, Mauji na wengineo," alisema Mridu.

Mridu aliyewahi kulipigia kundi la Mlimani Park 'Sikinde' na kupitia makundi kama Babloom Modern na Dar Modern, alitaja kikosi kizima cha Bombatic kuwa ni yeye (Mridu) kama mpiga solo, Gitaa la besi linaungurumishwa na Mudi Dirima, na mpapasa kinanda ni Ally Juma 'Za Mkwezi'.

Safu ya uimbaji ina wasanii Mwafatu Mohammed, Nuru Njama, Mwajabu Mtinginya, Fatuma Jafari na Cheka Dadi.

"Tayari tumeshakamilisha baadhi ya nyimbo ambazo tutazitambulisha katika maonyesho yetu ya Jumatano na Ijumaa maeneo ya Tabata kabla ya Jumamosi na Jumapili kuwepo Mwananyamala na Buguruni," alisema Mridu.

Mridu ndiye mtunzi wa nyimbo zilizowahi kutamba nchini kama:
'Acha Shobo' wa Babloom,
Pembe la Ng'ombe,
Kitu Mapenzi na Malavidavi.

HATIMAE BI MWANAHAWA ALLY NA BI AFUA SULEIMAN WAPATANISHWA...!!

Bi Afua Suleiman na Bi Mwanahawa Ally.
Wakongwe wa taarabu nchini Tanzania Bi Afua Suleiman na Bi Mwanahawa Ally ambao walikuwa na uhasama mkubwa, wamepatanishwa na kwa sasa sio mahasimu tena!. 

Akizungumza na mwandishi wa blog hii Bi Mwanahawa alisema watu ndio waliokuwa wanatugombanisha, lakini kwa sasa tumewabaini na haitotokea tena kufarakana. 

Kwa upande wa Bi Afua yeye nae alimshukuru Mungu kwa kupatana na mwenzake na kuahidi kutosikia maneno yoyote kwani waja wamezoea kuyazua maneno. 

Ugomvi wa Bi Afua na Bi Mwanahawa ulikuwa ukiwagawa wapenzi..lakini kwa sasa yamekwisha.

Saturday, November 2, 2013

Leo Jumamosi Novemba 2: MASHAUZI CLASSIC WAKIWA NA MALKIA WA MIPASHO WATAKUWA MOROGORO.


Kama kawaida yake Presdaa/Mkurugenzi wa Mashauzi Classic ISHA MASHAUZI ameahidi burudani ya nguvu leo Jumamosi tarehe 2 Novemba 2013 katika ukumbi wa Tanzanite Complex akiwa na Malkia wa Mipasho KHADIJA KOPA, Pamoja na MSAGA SUMU atatoa burudani pia.

Wote mnakaribishwa kujionea Burudani ya nguvu.

AYSHER VUVUZELA - "SIJAOLEWA ILA NIKITAKA BWANA NITASEMA"...

Aysher Vuvuzela
Muimbaji machachari wa 5Stars Modern Taarabu Aysher Othman (Vuvuzela) amekerwa na baadhi ya tabia ya wanaume katika ukurasa wa Facebook, taarabuzetu.blogspot.com katika pitapita yake imekutana na status aliyoitoa mwenyewe.

"Kiukweli wanaume wa humu facebook ni hatari urafk ni mzuri lkn mnaingia sana inbox na cjaana msemacho wengi wenu hamna ni kila akuombae urafki akikuadd ukimuacept anakutongoza na wengine ukikataa sio wastaarabu na maneno machafu juu hebu punguxeni sipo humu kwa ajili ya kutafuta bwana kweli sijaolewa ila nikitaka bwana kupitia humu ntasema huu mda wa kutengeneza pesa sio mapenzi ugonjwa wa moyo tuheshimiane ukiona huna la kusema usinisumbue mi unipende leo umeniona humu na mkeo nyumban achen umalaya mnaboaaaaaaa wenye twabia hzo acheni"


Pia leo Jumamosi Aysher atakuwa Rufita Tabata kutoa Burudani kwa mwaliko wa bendi ya Fungakazi Modern Taarabu, ameahidi kucheza na mashabiki watakaofika kushuhudia.

Friday, November 1, 2013

ASHURA MACHUPA ASHINDWA KUFIKIA MUAFAKA WA KUJIUNGA NA KING'S MODERN TAARABU..

Ashura Machupa
Ashura Machupa ni muimbaji wa kutumainiwa katika bendi ya Fungakazi Modern Taarabu na ameimba wimbo mpya unaotamba kwa sasa wa "Inzi wa Kijani" 

Siku za hivi karibuni zilizagaa habari kwamba muimbaji huyo anatakiwa na uongozi wa King's na taratibu za makubaliano zilikuwa zinaendelea kimyakimya!. 

Taarabuzetu ilipopata habari ilimtafuta mkurugenzi wa kings MR MAJALIWA ambae nae alikili kuwa na mazungumzo na binti huyo lakini mpaka hatua za mwisho muafaka haukupatikana hivyo kumuachia aendelee kuitumikia bendi yake ya Fungakazi.

TETESI:- MLIDU ALLY KURUDI DAR MODERN TAARABU..

Baada ya kuonekana wazi kwamba bendi ya Dar Modern Taarabu imekosa mwelekeo tokea Mlidu Ally kutoka kundini, uongozi wa bendi hiyo upo mbioni kumrudisha tena ili kuleta chachu na ushindani mkubwa uliopotea. 

Taarifa za ndani zilizopatikana toka katika uongozi huo zinasema kiongozi mmoja wa juu alishauri kurudishwa mara moja kwa mpiga gitaa huyo ambae pia alikuwa kiongozi wakati yupo Dar Modern. 

Bendi hiyo kwa sasa imepoteza wapenzi na imekuwa haina mvuto hata inapofanya show katika ukumbi wake wa nyumbani wa lango la jiji magomeni mikumi wamekuwa hawapati wapenzi.

MAZOEZI YA BENDI MPYA ROCKY CITY MODERN TAARABU YASUASUA.

Bendi mpya iliyoanzishwa wiki moja iliyopita ya ROCKY CITY MODERN TAARAB imeanza kupata ugumu wa tasnia hii kutokana na miundombinu mibovu waliyonayo haswa kifedha kuwayumbisha. 

Akizungumza na Mwandishi wa blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com kwa sharti la kutotajwa jina lake mpiga gitaa wa bendi hiyo alisema kwamba wanafikiria kusimamisha mazoezi ya kuandaa nyimbo mpya mpaka pale watakapojipanga upya kuhusu fedha, kwani mpaka sasa uongozi huwa una nunua chakula kwa baadhi ya wasanii na jioni unatoa elfu 3 kama nauli kwa baadhi ya wasanii jambo linalofanya wengine kulalamika.

WASANII G5 MODERN TAARABU, WAANZA KULALAMIKIA UONGOZI..

Bendi ya G5 Modern Taarabu imeanza kukumbwa na mtikisiko baada ya baadhi ya wasanii kufikisha malalamiko yao katika ofisi zetu kwamba wamekuwa wakipigwa danadana kila kukicha na uongozi wao haswa mkurugenzi wao. 
"Unajua wakati tunaanza hapa G5 kila msanii alikuwa na matumaini kwamba mambo yatakuwa mazuri kimaslahi kutoka na maongezi ya ahadi nono, lakini kadri siku zinavyosonga mambo yamekuwa yakibadilika tu, hakuna tunachokielewa. sisi wengine tuna familia, tuna watoto ambao hawana baba, sasa unaponidanganya unakuwa hunitendei haki". alisema msanii mmoja ambae alikataa kutajwa jina lake!.

Wednesday, October 30, 2013

FATMA YASINI NAE AIKIMBIA KING'S MODERN TAARABU...

Fatma Yasin
Wimbi la wasanii kuondoka ndani ya bendi ya Kings Modern Taarabu limeendelea baada ya msaani mwingine Fatma Yasini nae kuondoka na kujiunga katika bendi mpya iitwayo Rocky City Modern Taarabu. 

Fatma Yasini ndani ya bendi ya Kings Modern Taarabu ameimba wimbo uitwao "Sikuogopi nakupotezea" utunzi wake Director Kijoka.  

Akiongea na mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com Fatma alisema: "Unajua ndugu mwandishi, mimi ni msanii na mara nyingi huwa naangalia sehemu ninayothaminiwa na ndio maana nimekuja hapa Rocky City Modern Taarabu kwani Mkurugenzi wake ameonesha kunijari zaidi" alisema.