TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, November 8, 2013

MRIDU ALLY KUITAMBULISHA LEO BOMBASTIC MODERN TAARABU...

Mridu Ally "TX".
Baada ya kuyatumikia makundi ya wenzake kwa muda mrefu, hatimaye mtunzi na mcharaza gitaa maarufu wa muziki wa Taarabu nchini, Mridu Ally 'Tx' mwezi uliopita "October 2013" alianzisha kundi lake la miondoko ya Taarabu liitwalo Bombastic Modern Taarabu "Wana B Kubwa".

Akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com Mridu alisema kundi lake linaundwa na wasanii wanane baadhi wakiwa ni chipukizi na kutamba kama alivyoweza kuwainua chipukizi wengine waliokuja kutamba nchini ndivyo atakavyofanya kwa wasanii hao wapya.

Alisema kundi hilo linatarajia kuanza rasmi leo kwa kujitambulisha maeneo ya Tabata kabla ya kuendelea katika maonyesho yao ya mwishoni mwa wiki.

"Katika kuhangaika kwangu, nimejianzishia kundi langu binafsi linaliofahamika kwa jina la 'Bombastic Modern Taarab na linaundwa na wasanii kama nane hivyo wengi wao wakiwa ni chipukizi hasa kwa waimbaji, lengo nao kuwainua kama nilivyofanya kwa akina Tizo Mgunda, Salha Abdallah, Sikudhani Ally, Mauji na wengineo," alisema Mridu.

Mridu aliyewahi kulipigia kundi la Mlimani Park 'Sikinde' na kupitia makundi kama Babloom Modern na Dar Modern, alitaja kikosi kizima cha Bombatic kuwa ni yeye (Mridu) kama mpiga solo, Gitaa la besi linaungurumishwa na Mudi Dirima, na mpapasa kinanda ni Ally Juma 'Za Mkwezi'.

Safu ya uimbaji ina wasanii Mwafatu Mohammed, Nuru Njama, Mwajabu Mtinginya, Fatuma Jafari na Cheka Dadi.

"Tayari tumeshakamilisha baadhi ya nyimbo ambazo tutazitambulisha katika maonyesho yetu ya Jumatano na Ijumaa maeneo ya Tabata kabla ya Jumamosi na Jumapili kuwepo Mwananyamala na Buguruni," alisema Mridu.

Mridu ndiye mtunzi wa nyimbo zilizowahi kutamba nchini kama:
'Acha Shobo' wa Babloom,
Pembe la Ng'ombe,
Kitu Mapenzi na Malavidavi.

0 comments:

Post a Comment