Mwimbaji wa Taarabu Aisha Masanja yupo mbioni kufanya Video ya nyimbo yake "Poyoyo".
Aisha akizungumza na blog ya Taarabu zetu alisema siku ya jumapili tarehe 1 Desemba 2013 atafanya video ya nyimbo yake binafsi inayoitwa Poyoyo, ambayo ipo katika mahadhi ya Mduara.
Aisha alisema Video ataifanyia Gadaff Club iliyopo Yombo, katika wimbo huo kamshirikisha Omari Tego.
Audio imetengenezwa na Marlon Rinje na Video inatengenezwa na Said wa Dolphin.
Aisha ametoa wito kwa wadau wake wote kwa kusema:-
"Ma
dada mpendeze munizidi mm hii kwaajili ya wauza sura wote na wanaume wauza
sura mpo km kawaida ndani ya Gadafi Club Yombo, nitafanya video yangu
live pale saa 11 jioni msikose wana".
Wote mnakaribishwa itakuwa free, yaani BUREE HAKUNA KIINGILIO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment