"Ingefaa kuwauliza wakulima wetu, hasa wanaume, ni saa ngapi za juma na
majuma mangapi kwa mwaka wanafanya kazi. Wengi hawafanyi kazi hata kwa
nusu ya saa ambazo mpokea mshahara anafanya. Ukweli ni kuwa kwenye
vijiji wanawake wanafanya kazi ngumu sana. Nyakati nyingine wanafanya
kazi kwa saa 12 au 14 kwa siku. Wanafanya kazi hata siku za Jumapili na
za sikukuu. Wanawake wanaoishi vijijini wanafanya kazi ngumu kuliko mtu
mwingine yeyote Tanzania. Lakini wanaume wanaoishi vijijini (na baadhi
ya wanawake mijini) wako likizo kwa nusu ya maisha yao. Nguvu ya
mamilioni ya wanaume kwenye vijiji na maelfu ya wanawake mijini ambazo
kwa sasa zinapotezwa kwenye udaku, dansi na kunywa, ni hazina kubwa ya
nchi ambayo inaweza kuchangia maendeleo ya nchi yetu zaidi ya ambavyo
tunaweza kupata kutoka mataifa tajiri."
Takwimu za sasa
zinaonyesha, wakulima wadogo wanawake wanazalisha takribani asilimia
sitini (60%) ya chakula chote tunachotumia, lakini ni asilimia moja (1%)
tu ndio wanaomiliki ardhi.
Unamuenzi vipi Baba wa Taifa..??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment