Marehemu Nyawana aliyefariki siku ya Jumatatu Tarehe 11 Novemba 2013 alitarajiwa kuzikwa leo Jumatano huko kwao Tabora, lakini kutokana na safari ya tokea jana kuwa ndefu sana, huenda asizikwe leo na akazikwa kesho.
Akizungumza na blog hii mume wa marehemu Kais Musa amesema mpaka mida ya saa sita wapo njiani na huenda wakafika saa kumi za jioni na ikawawia vigumu kuzika, ila kwa taarifa zaidi ni mpaka pale watakapofika.
Marehemu Nyawana amefariki akiacha watoto wawili wa Kiume na wa Kike:-
Said na Queen.
Mungu awape nguvu kwa wakati huu mgumu.
Zifuatazo ni picha mbalimbali ikiwa ni matukio ya msibani kwa baba wa marehemu Nyawani pale Magomeni akiwa anaagwa kwa safari ya Tabora.
Tunazidi kumuombea kwa Mungu apumzike kwa amani.
Tutakuwa tunawaletea taarifa kadri tutakavyokuwa tunazipata.
|
Thabit Abdul akishiriki katika kubeba Jeneza la marehemu Nyawana. |
|
Said, mtoto wa kwanza wa marehemu Nyawana akifarijiwa. |
|
Kais Mussa mume wa Marehemu Nyawana akihojiwa na Mtangazaji wa EATV. |
|
Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa Passion Fm na Ecoprint waliokuwa wakifanya kazi pamoja na marehemu Nyawana. |
|
Saida Mashauzi. |
|
Anneth Nyoni, Anuary Sanga na Yunus Kanumba, ni watangazaji waliowafanya kazi pamoja na Marehemu Nyawana. |
|
Dida Mtangazaji wa Times FM. |
|
Hashimu Said, msanii wa Mashauzi Classic. |
|
Isha Mashauzi. |
|
Amin Salmin kulia na Kapteni Temba. |
|
Wasanii mbalimbali wa Taarabu wakiwa msibani. |
|
Wadada Mapacha wadau wakubwa wa mziki wa Taarabu wakiwa msibani kwa mpendwa wao, rafiki yao kipenzi Nyawana Fundikila. |
|
Luiza Nyoni. |
|
Ramadhani Kisolo, Warda Chande na Eunice Kanumba. |
|
Omary Kisira kushoto na Kais Mussa. |
|
Baadhi ya watangazaji wa Passion FM wakiwa na nyuso za hudhuni kwa kuondokewa na mtangazaji mwenzao Nyawana Fundikila. |
|
Eunice Kanumba kushoto na Aisha Vuvuzela wakiwa katika maeneo ya msibani. |
Picha:-
Gosbert Njenga na Robert Kiatu.