TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, January 31, 2014

DAR MODERN TAARABU YATAMBULISHA WASANII WAPYA NA ALBUM MBILI...

Baadhi ya wasanii wa Dar Modern Taarabu.
Kundi maarufu la miondoko ya Taarabu nchini Dar Modern Taarabu jana Alhamisi limetambulisha wasanii wapya watakaoungana na wasanii wengine kuunda kundi na kuboresha zaidi.

Akizungumza na blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com katika kikao walichokiandaa makamu wa Rais wa Bendi hiyo Bakari Hassani amesema wamechukua wasanii wengi kutoka bendi tofauti tofauti ili kuboresha bendi na kukabiriana na ushindani uliopo.
Baadhi ya Viongozi wa Dar Modern katika Mkutano wa jana wakiwa na baadhi ya wasanii.
Makamu huyo wa Rais aliwataja wasanii waliowachukua ni:-
- WAIMBAJI WAPYA NI HASSAN VOCHA ALIYEKUWA KWA SAID FELLA (G5 MODERN)
- ZUBEDA MLAMALI KUTOKA NEW ZNZ STAR,
- MWAMVITA SHAIBU, MOSSY SULEIMAN NA BI MWANAHAWA ALLY WOTE WAMETOKEA 5 STAR MODERN TAARAB,
- AMOUR MAGULU,
- RAMADHAN KISOLO KATOKEA MASHAUZI NA 

- MGENI KISODA WA JAHAZI (5STARS)

Pia katika mkutano huo uliokuwa umehudhuliwa na waandishi mbalimbali wa habari nchini, Dar Modern waliweza kutambulisha Album zao mbili kwa pamoja ambazo watazizindua tarehe 14 Feb siku ya wapendanao katika ukumbi wa Travertine Magomeni.

Album alizitaja kuwa ni:
1. KITWITWI - IMEIMBWA NA SIKUDHANI ALLY NA 
2. OH! MY HONEY IMEIMBWA NA HASSAN VOCHA.

Katika album hizo kutakuwa na nyimbo kama:-
1. Kitwitwi

2. Oh my honey
3. Sikuamini macho yangu
4. Siwanyimi uzuri

NYINGINE NI:-
1. Malipo Duniani
2. Naenda kwa Mume wangu
3. Ngoma imepasuka

Nyimbo zote zimetoka na baadhi zimeshaanza kusikika radioni, Mr. Bakari amesema pia baadhi ya nyimbo zingine zipo katika maandalizi zitaingizwa katika album hizo.

WADAU WOTE WANAKARIBISHWA SIKU YA VARENTINE 14 FEB PALE TRAVERTINE MAGOMENI KUJA KUPATA BURUDANI YENYE RADHA MPYA KUTOKA DAR MODERN TAARABU MPYA YA 2014.

Thursday, January 30, 2014

DAR MODERN TAARABU KUTAMBULISHA WASANII WAPYA LEO...!!

Kundi la muziki wa mwambao Tanzania, Dar Modern Taarabu leo linatarajiwa kukutana na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es salaam ili kuzungumuzia ujio mpya wa kundi hilo .

Kwa mujimbu wa taarifa ya kundi hilo kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu rais wake Mr. Bakari Hassan mkutano huo utafanyika leo tarehe 30/01/2014 kwenye makao makuu ya kundi yaliyopo magomeni kuanzia saa 4:00 Asubuhi.

“Mada itakayozungumzwa  ni ujio mpya wa bendi ya Dar modern Taarabu ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha wasanii wapya waliojiunga na kundi hili na pia kutambulisha albamu zetu mbili” alisema Hassan katika taarifa yake. 

Kaimu rais huyo alisema kuwa albamu ambazo majina yake yatawekwa wazi leo zinatarajia kuzinduliwa February 14 ambayo itakuwa ni siku ya wapendanao maarufu kama valentine day katika ukumbi wa Tranertine Magomeni.

“Naomba ieleweke kwamba siku zote tumeendelea kufanya kama kawaida lakini sasa tunataka kuanza mwaka mpya kwa kishindo ili kuhakikisha Dar Modern Taarabu inarudi kwenye chati kama ilivyokuwa enzi za albamu zetu za mwanzo” alisema.

Alisema kuwa kundi hilo limewahi kutamba na albamu kadhaa ikiwamo ya Pembe la ng'ombe ambayo ilichangia kuifanya liwe juu na kujulikana kwa mashabiki wengi wa mziki wa mwambao  wa ndani na nje ya Tanzania.

Albamu nyingine ni Vijimambo tu vishanshida, Sote twapata riziki na Kitu Mapenzi na sasa liko mbioni kuzindua albamu mbili kwa mpigo wakati wa Valentine day.

Wednesday, January 29, 2014

DOWNLOAD NYIMBO MPYA TATU (3) ZA WAKALIWAO MODERN TAARADANCE...!!!!

Download hapa Nyimbompya kabisa zilizoimbwa na kundi linalokuja kutishia amani bendi kongwe hapa nchini kundi la Wakaliwao Modern Taaradance chini yake Mkurugenzi Thabit Abdul.


Subira haina Kikomo - Wakaliwao Modern Taaradance
Muimbaji - Asia Mariam



Kalieni Viti sio Umbea - Wakaliwao Modern Taaradance
Muimbaji - Hamuyawezi Kondo


Sema na Mume wako - Wakaliwao Modern Taaradance
Muimbaji - Farida Kindamba

WAKALIWAO MODERN TAARADANCE YAKAMILISHA TATU KALI...! SALHA WA HAMMER NDANI...!!!

Mkurugenzi wa Wakaliwao Thabit Abdul "Jiko la Jela".
Wakaliwao Modern Taaradance ni kundi la Taarabu lililoanzishwa hivi karibuni na mkongwe wa muziki hapa nchini anayejulikana kwa jina la Thabit Abdul a.k.a Jiko la Jela.

Kundi hili baada ya harakati za hapa na pale hivi sasa limefanikiwa kuipua nyimbo zake mpya tatu (3) chini ya Producer/Director Thabit Abdul

Mkurugenzi huyo (Thabit) alizungumza na Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com na kuzitaja nyimbo hizo ambazo ni za kuanzia tu katika ujio wa Albam, alizitaja ni:-
1. Kalieni Viti sio Umbe - Imeimbwa na Hamuyawezi Kondo
2. Subira haina Kikomo - Imeimbwa na Asia Mariam
3. Sema na Mume wako - Imeimbwa na Farida Kindamba

Pia katika kukamilisha Albam nzima itakayokuwa na jumla ya nyimbo Sita (6).
Nyimbo zitakazokamilisha Albam alizitaja kuwa ni:-
4. Naishi Naisha - Ataimba Mwalim
5. Watu na Bahati zao - Ataimba Aisha
6. You and Me - Ataimba Thabit

Warda Chande "Mwana Dar esSalaam" Mtangazaji wa Passion FM katika Kipindi cha Taarabu - Ambaa na Mwambao akipozz na Thabit Abdul baada ya Mahojiani.

Akihojiwa na mtangazaji Warda Chande wa Passion FM katika kipindi cha Ambaa na Mwambao Thabit alisema Nyimbo zote hizo ni Utunzi wake, Kinanda, Solo na Vingine vyote Sijui Director vyote kafanya mwenyewe... Ni Hatareeee...!!!!

Amesema Albam itakuwa tiyari kabla ya Sikukuu ya Pasaka ambapo ndo itakuwa uzinduzi rasmi ila kwasasa wanafanya show zao siku mbili kwa wiki:-
** Kila Jumatano CHITOZ Kijitonyama (Miti mirefu) na
** Kila Ijumaa Y Bar - Kinondoni Moscow (Nyumbani)

Mkurugenzi huyo wa Wakaliwao alisema bendi yake amesheheni vichwa vikali na vyenye vipaji na amechukua wasanii wasio na majina maalufu isipokuwa wawili tu ambao ni wakongwe katika gemu:-
* Abdul Misambano ambaye atakuwa kama mlezi wa Bendi
* Salha wa Hammer - ambaye atatikisa bendi zote za taarabu kwa umahili wake katika kuimba.

Pia wanahitajika wataalamu wa kupiga Solo na Base! Thabit amesema ni lazima wawe wakali kama au kumzidi yeye katika kucharaza vyombo hivyo. (Nafasi ya kazi hiyo).

Thabit Abdul amewaomba wadau wa mziki wa Taarabu hapa nchini na nchi za nje kumsapoti na kujiandaa vyema katika uzinduzi wake siku hiyo ya Passaka

Friday, January 24, 2014

DOWNLOAD HAPA NYIMBO YA SNURA - UKO NYUMA SANA...

Tunamkaribisha sana Snura katika uringo huu wa mziki wa Mwambao.

Download hapa Nyimbo yake ya:- 
Uko nyuma sana

5Stars ipo mikononi mwangu kwa sasa - Ally J

Mtangazaji wa Passion FM Warda Chande akiwa na mcharaza kinanda wa 5Stars Ally J.
Baada ya aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa 5Stars Mr. Shark's kuivunja Bendi yake na vyombo kuvifungia ndani na kisha kuwapa wasanii wote uhuru wa kwenda wanakotaka, Ally J ameamua kuichukua bendi ili aiendeleze.

Ally J ameyazungumza hayo akiwa anahojiwa na Blog hii pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na mtangazaji wa kipindi cha Taarabu "Ambaa na Mwambao" Passion FM Warda Chande.

Amesema kuanzia sasa Bendi ipo mikononi mwake baada ya kukaa na aliyekuwa Mkurugenzi Mr. Shaks na kuyamaliza.
Ally J akionesha manjonjo yake katika kusakata muziki wa Mwambao.
Kinachofuata kwa sasa ni kuvumiliana tu, Bendi ipo itakuwa imara kama mwanzo, kama kawaida na wasanii wote wapo imara kuendeleza Bendi hivyo hakuna kitakachoharibika wala kupungua.

Ally J ambaye ni mpiga kinanda mkongwe aliyewahi kupigia bendi mbalimbali hapa nchini amechukua uamuzi wa kuiendeleza bendi kwa mapenzi yake makubwa huku akiomba wito kwa wadau wa Taarabu na wenye nia ya dhati kuiendeleza 5Stars kuwa wajitokeze ktk mazungumzo ya Udhamini kama ilivyokuwa kwa Shak's.

Wapenzi wote wa 5Stars wasiteteleke bali wasubiri tu ujio mpya kwa sura na sauti zilezile.

AMIN SALMIN:- T Moto haijafa na wala haitakufa...

Mkurugenzi wa Bendi ya T Moto Amin Salmin amefunguka kwa kusema kuwa, T Moto ipo ngangari haijafa wala haitakufa na hivi karibuni itaanza harakati zake kwa nguvu mpya.

Amin alisema hayo baada ya tetesi kutoka kwa wadau mbalimbali wa taarabu kuulizia katika blog hii siku chache zilizopita.

Amin Salmin alisema:- Mimi ndio mmiliki wa T Moto, kweli bendi imekua kimya kwa muda sasa hii kutokana na sababu kuu mbili:- Moja T Moto nilivunja uongozi wa kuisimamia bendi ukinitoa mm wakati nafanya hayo kwa bahati mbaya nami nikapata ajali na bendi kubaki chini ya wasaanii wenyewe nao baada ya muda wakashindwa kuiendesha ndipo nikazuwia maoshesho kwa muda ili kujipa muda wa kijiuguza kwa muda wa miezi sita, nilikua mgonjwa ila kwa ss nashukuru nimerudi ktk hali yangu ya kawaida, "T Moto haijafa na wala haitakufa" karibuni tu itaanza harakati zake na kutoa upinzani km kawaida tunawaomba mashabiki na wapenzi wategemee uhondo kutoka kwetu kwani tunajua nini wanapenda na nn tuwafanyie.

Wale wapenzi wote wa burudani na wadau wa T Moto habari ndo hiyo, Bendi ipo karibu kuingia kambini.


Picha zikionesha Mkurugenzi wa T Moto Mr. Amin akiuguza mguu wake.

Amin hapa akiwa na hali nzuri kiasi karibu kuingia mzigoni.




Wednesday, January 22, 2014

TETESI:- BAADA YA 5STARS KUVUNJWA BENDI MBILI ZINGINE KUFUATA

Mkurugenzi wa T Moto Amin Salmin akiwa na Jokha Kassim.
Baada ya Bendi maalufu na iliyokuwa juu kimziki 5Stars Modern Taarabu kuvunjwa kuna bendi zingine mbili (2) zipo mahututi au zimekufa kimyakimya.

Baadhi ya wapenzi wa Taarabu hapa nchini na sehemu mbalimbali Duniani wanaopitia katika blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com wamekuwa wakituma msg, Email na simu kuulizia hatma ya baadhi ya makundi ambayo hawayasikii kwa sasa.
Mwandishi wa blog hii pia amekuwa na mashaka kidogo kitu ambacho kilimfanya aanze kufanya uchunguzi wa suala hilo.

Tumeongea na baadhi ya wasanii wa bendi ya T Moto Modern Taarabu na kusema kuwa hawana Show bendi yao kwa muda mrefu sasa na wamekuwa wakihaha sehemu ya kujipatia riziki na kuhudumia familia zao. "Bendi ipo haijafa kwasababu hatujatangaziwa hivyo ila ndo hivyo hatuna show hata moja kitu kinachotufanya tuishi maisha ya kukosa ajira. Mmoja wa wasanii alifunguka.
Mwandishi wa blog hii anafanya mawasiliano na Mkurugenzi wa T Moto ili aweze kufunguka naye kuhusu hatma ya wasanii wake.

Wasanii wa Bendi ya Fungakazi Modern Taarabu.
Bendi nyingine inayoonekana kuzama ni Fungakazi Modern Taarabu iliyo chini ya Mkurugenzi Kaptain Temba.
Inadaiwa bendi hii haina wasanii kwa sasa kwasababu hawakutani kwa show wala kwa maongezi yoyote, inaonesha bendi imekufa au inaelekea pabaya.

Wasanii wa Fungakazi Modern Taarabu kwa sasa hawasikiki na hawafanyi show yoyote hapa mjini, kwahiyo inaonesha hawana ajira.

Wakurugenzi wa T Moto na Fungakazi mnaombwa na wapenzi wa Taarabu pamoja na wasanii wenu kufanya mpango wa kuendeleza Bendi na kupanga Show kama ilivyokuwa mwanzo.

NDAGE NDAGE SI MSANII WA SUPERSHINE TENA - "KAIS MUSA"

Ndage Ndage.
Kais Mussa Kais Manager wa Supershine.
Msanii na mpiga kinanda maarufu Ndage Ndage ameondoka katika bendi ya Supershine bila kuuaga uongozi.

Taarifa za kutoweka kwake zimezungumzwa na Meneja wa Supershine Modern Taarab Mr. Kais Musa kwa kuiambia blog hii kuwa:-
Ndage Ndage alikuwa msanii wetu, tumempangishia Chumba kwa miezi sita lakini ameka kwa kipindi kidogo tu akadai salio kwa mwenye Nyumba akarudishiwa, akauza vitu tulivyomnunulia kama Godor na Feni (Pangaboy) kisha akatoweka. Kais alisema.



Aliongeza kwa kusema, kutokana na kuonesha utovu wa nidhamu wa hali yajuu hatumtaki tena na hatuhitaji kuwa naye kwenye bendi maana tunawapiga kinanda wakutosha na Bendi iko poa imesimama vya kutosha.

Katika pekua pekua na juhudi ya mwandishi wa blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com ili kupata habari zaidi, ilimpigia simu Ndage na simu yake ikawa haipatikani kwa muda mrefu, baada ya kuwa hapatikani, zikapatikana taarifa kuwa: Ndage aliuza vitu pamoja na kurudisha Chumba ili apewe salio lililopo kutokana na kuugua hivyo kutokuwa na pesa ya kujitibia na yeye mwenyewe kurudi nyumbani kwao.

Taarabuzetu tunawasihi wasanii wote wa Taarabu kuwa na nidhamu kwa viongozi kuwashirikisha matatizo yenu ili kujua ni kitu gani kinaweza kufanyika, mtu wa kuendeleza muziki huu wa Taarab ni wasanii wenyewe.

Monday, January 20, 2014

BENDI YA 5STARS IMEVUNJWA, ANAYETAKA VYOMBO AKANUNUE, ANAYEMTAKA MSANII AMCHUKUE...!!

Baadhi ya wasanii waliokuwa wakiunda kundi la 5Stars
 Kundi maarufu la mziki wa mwambao Tanzani 5Stars limevunjwa na wasani wapo huru kwenda popote.

Akizungumza na Blog hii aliyekuwa mmiliki wa Bendi hiyo Mr. Shaks amesema Bendi amevunjwa hataki tena kusikia mambo ya Bendi, amechoka na anataka kufanya mambo mengine sasa.

Mr. Shanks aliendelea kwa kusema sababu zilizomfanya aivunje Bendi ni kutoona faidi yake toka aanzishe na imekuwa kero kwake kwa kerere za wasanii kila siku, ameamua kuvunja mikataba ya wasanii wote pamoja na kwamba wengine alikuwa nao kwa mikataba ya muda mrefu kama miaka miwili (2) "Bora nipate hasara hii kuliko kuendelea kupata hasara" Alisema.

Aysher (Vuvuzela) na Mgeni Kisoda.

"Kwasasa sitaki mtu aniambie kitu chochote kuhusu Bendi, wasanii nimewapa uhuru mapema waweze kwenda kokote wanakotaka na mimi nifanye mambo yangu mengine
Mwenye Kuhitaji vyombo vya mziki anitafute tufanye biashara na kama atahitaji jina la 5Stars nitampa ila mimi basi". Shaks alisema.

Hammer Q Na Salha
Kwa habari zadi kuhusiana na kuvunjwa kwa 5Star tutasikia wasanii wanasemaje.
Tuvumilie kidogo.




Thursday, January 16, 2014

OFFSIDE TRICK WAACHIA NGOMA MPYA:- TALAKA ...

Kundi machachari la miondoko ya miduara Tanzania Offside Trick linaloongozwa na wakali wawili Hammer Q na Lil Gheto Jana January 15, 2014 limetambulisha single yake mpya inayokwenda kwa jina la TALAKA.

Akizungumza na blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com msanii wa kundi hilo Hammer Q alisema single hii ni kati ya nyimbo zinazokamilisha album yao mpya itakayotoka hivi karibuni, "nyimbo zote za album nzima zimekamilika na hii ndio ilikuwa nyimbo ya mwisho".

Alipoulizwa ni kwa nini single hii wameipa TALAKA!? Hammer Q alisema, siku hizi Talaka imekuwa ni kitu cha kuwaida tu kutokana na kudanganyana katika Mapenzi, watu wanafunga ndoa leo week moja wanaachana "Ni kama umeenda kununua Vocha" yaani hawaoni taabu, mtu anatoa Talaka kama anagawa Vipeperushi...!!

Wapenzi wa Mduara kaeni tiyari kuipokea Album ambayo itakuwa na ladha kibao za mduara halisi toka kundi bora kabisa la Mduara Tanzani Offside Trick "Watoto wa Kizanzibari".

SIKILIZA NA DOWNLOAD HAPA "TALAKA".


Friday, January 10, 2014

FATMA ALLY (MAMA SHUGHULI) AWAPASHA WATANGAZAJI WA VIPINDI VYA TAARABU.

Fatma Ally (Mama Shughuli) kushoto akiwa na Warda Chande wa Passion FM.
Anaitwa Fatma Ally au ukipenda muite Mama Shughuli, ni muimbaji wakutumainiwa katika bendi ya Jahazi Modern Taarabu.

Jana akizungumza na Warda Chande wa Passion FM katika kipindi cha Ambaa na Mwambao kinachosikika mida ya saa Saba mpka saa Kumi za jioni aliongelea mambo mengi sana yahusuyo muziki na maisha yake kidoogo.


Katika maongezi yake Fatma aliongea kuhusu kukerwa kwake na baadhi ya watangazaji wa vipindi vya Taarabu kwa tabia yao ya kuacha kuzungumzia nyimbo pamoja na waimbaji wake na badala yake wanatumia nyimbo hizo kutengenezeana vijembe kwa watu walio na chuki nao halafu nyimbo inakuja kuonekana na ujumbe tofauti.

"Watangazaji wa vipindi vya Taarabu wamekuwa wakitumia muda mwingi kujisifia, kujisema wao na kuwazungumzia watu wengine kwa kuwapa vijembe vya taarabu katika nyimbo tunazoimba badala ya kuzichambua na kuzizungumzia, tabia hiyo kwakweli huwa siipendi naomba wabadirike!" Alisema Fatma.

Fatma ni msanii wa siku nyingi na amejaribu kulinganisha muziki ule wa zamani na wa sasa akasema muziki wa sasa umekosa maadili, umezidi Matusi na Vijembe vya waziwazi kati ya wasanii kwa wasanii, unatunga nyimbo na kuiimba lakini anatokea mtu mwingine anakujibu kwa kukukejeli... Mambo kama hayo hayakuwepo zamani.

Fatma Ally a.k.a. Mama Shughuli kabla ya kujiunga na Jahazi alikuwa katika Bendi ya Babloom.
Akiwa Jahazi ameweza kuimba Nyimbo kama:-
Ng'ombe wa Maskini,

Shukurani ya Punda na
Hata bado hujanuna.

Thursday, January 9, 2014

NANI MKALI WA MDUARA? AT au OFFSIDE TRICK... Ni Ijumaa hii 10/01/2014 Zanzibar.

Ni AT au OFFSIDE TRICK!? Ni show kali na ya aina yake kutokea nchini Tanzania.

Ni kundi maarufu la miondoko ya miduara Tanzania na msanii maarufu wa miondoko hiyo pia ambao ni mahasimu wakubwa pia, siku ya Ijumaa wataoneshana nani mkali, nani mbabe wa miondoko hiyo ndani ya Ukumbi wa Polisi Mess mjini Zanzibar.

Show hiyo pia itasindikizwa na mwanadada Shilole pamoja na kundi lake machachali katika kunogesho show.

Kiingilio kimepangwa kuwa Tsh. 5,000/= tu kuanzia saa mbili usiku mpaka Majogoo...!!

Unakaribishwa kushuhudia mpambano huo mkali...!!

JAHAZI MODERN TAARAB YAFAFANUA NI KWANINI WAMEAMUA KUPELEKA UTAMBULISHO WA NYIMBO MPYA MOROGORO

KUNDI la Jahazi Modern Taarab limefafanua ni kwanini limeamua kuuchagua mji wa Morogoro kama kituo chao cha kwanza cha kutambulishia nyimbo zao mpya zitakazounda albam yao mpya ijayo. 

Jahazi wanatagemewa kufanya onyesho maalum Morogoro kwaajili ya kuwaonyesha nyimbo mpya mashabiki wao Ijumaa ya tarehe 31 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex. 

Jana kiongozi wa Jahazi Modern Taraab Mohamed Mauji alifanya mahojiano na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV kinachoongozwa na mtangazaji Hawa Hassan (Kama wanavyoonekana pichani) ambapo msanii huyo alitoa sababu kadhaa ni kwanini wameichagua Morogoro. Kipindi hicho kitaruka hewani Jumamosi hii saa 11 jioni. 

Mauji ambaye ni mcharazaji gitaa la solo miongoni mwa sababu nyingi alizozitoa ni pamoja na kusema kuwa mji wa Morogoro ni ngome yao kubwa (ukiondoa Dar es Salaam) na hivyo safari hii wameupa heshima ya kipekee. 

Mara zote Jahazi imekuwa ikianza kutambulisha nyimbo mpya jijini Dar es Salaam na baadae kufuatiwa na uzinduzi na baada ya hapo ndio wanazipeleka nyimbo mpya mikoani. 

Mauji pia katika mahojiano yake hayo alifichua mikakati yao mikubwa ya kukukabiliana na ushindani kwa mwaka huu wa 2014.

Sunday, January 5, 2014

JAHAZI KUPELEKA NYIMBO MPYA MORO MWISHO WA MWEZI HUU.

KUNDI bingwa la miondoko ya mwambao, Jahazi Modern Taarab litaanza kutambulisha nyimbo zake mpya mwishoni mwa mwezi huu ambapo mji wa Morogoro utakuwa wa kwanza kupata uhondo huo. 

Jahazi watafanya onyesho maalum mjini humo Ijumaa ya Januari 31 ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex. 

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Jahazi kupiga ndani ya ukumbi huo uliofunguliwa kiasi cha mwaka mmoja uliopita. 

Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo Warda Makongwa wa Planet FM ya mjini humo, wameamua kuandaa onyesho hilo kufuatia maombi ya mashabiki wengi waliotaka Jahazi nayo ibishe hodi ndani ya Tanzanite Complex. 

Warda amesema Jahazi halitaenda hivi hivi bali litaandamana na nyimbo mpya kabisa ambazo hazijawahi kusikika hapo kabla. 

Amefafanua kuwa nyimbo hizo ni sehemu ya maandalizi ya albam mpya ijayo ya Jahazi Modern Taarab inayoongozwa na Mfalme Mzee Yussuf.

Thursday, January 2, 2014

5STARS WAFUNIKA DAR LIVE...

Kundi la 5Stara likionesha umahili wake katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwenye ukumbi wa Dar like siku ya tarehe 1/1/2014.