KUNDI la Jahazi Modern Taarab limefafanua ni kwanini limeamua kuuchagua
mji wa Morogoro kama kituo chao cha kwanza cha kutambulishia nyimbo zao
mpya zitakazounda albam yao mpya ijayo.
Jahazi wanatagemewa kufanya onyesho maalum Morogoro kwaajili ya
kuwaonyesha nyimbo mpya mashabiki wao Ijumaa ya tarehe 31 mwezi huu
ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.
Jana kiongozi wa Jahazi Modern Taraab Mohamed Mauji alifanya mahojiano
na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV kinachoongozwa na mtangazaji
Hawa Hassan (Kama wanavyoonekana pichani) ambapo msanii huyo alitoa
sababu kadhaa ni kwanini wameichagua Morogoro. Kipindi hicho kitaruka
hewani Jumamosi hii saa 11 jioni.
Mauji ambaye ni mcharazaji gitaa la solo miongoni mwa sababu nyingi
alizozitoa ni pamoja na kusema kuwa mji wa Morogoro ni ngome yao kubwa
(ukiondoa Dar es Salaam) na hivyo safari hii wameupa heshima ya kipekee.
Mara zote Jahazi imekuwa ikianza kutambulisha nyimbo mpya jijini Dar es
Salaam na baadae kufuatiwa na uzinduzi na baada ya hapo ndio
wanazipeleka nyimbo mpya mikoani.
Mauji pia katika mahojiano yake hayo alifichua mikakati yao mikubwa ya
kukukabiliana na ushindani kwa mwaka huu wa 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment