Kundi la muziki wa mwambao Tanzania, Dar Modern Taarabu leo linatarajiwa kukutana na
waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es salaam ili
kuzungumuzia ujio mpya wa kundi hilo .
Kwa mujimbu wa taarifa ya kundi hilo kwa vyombo vya habari
iliyosainiwa na kaimu rais wake Mr. Bakari Hassan mkutano huo utafanyika leo tarehe 30/01/2014
kwenye makao makuu ya kundi yaliyopo magomeni kuanzia saa 4:00 Asubuhi.
“Mada itakayozungumzwa
ni ujio mpya wa bendi ya Dar modern Taarabu ikiwa ni pamoja na
kuwatambulisha wasanii wapya waliojiunga na kundi hili na pia kutambulisha
albamu zetu mbili” alisema Hassan katika taarifa yake.
Kaimu rais huyo alisema
kuwa albamu ambazo majina yake yatawekwa wazi leo zinatarajia kuzinduliwa February 14 ambayo itakuwa ni siku ya wapendanao maarufu kama valentine day katika ukumbi wa Tranertine Magomeni.
“Naomba ieleweke kwamba siku zote tumeendelea kufanya kama
kawaida lakini sasa tunataka kuanza mwaka mpya kwa kishindo ili kuhakikisha Dar Modern Taarabu inarudi kwenye chati kama ilivyokuwa enzi za albamu zetu za
mwanzo” alisema.
Alisema kuwa kundi hilo limewahi kutamba na albamu kadhaa
ikiwamo ya Pembe la ng'ombe ambayo ilichangia kuifanya liwe juu na kujulikana
kwa mashabiki wengi wa mziki wa mwambao
wa ndani na nje ya Tanzania.
Albamu nyingine ni Vijimambo tu vishanshida, Sote twapata riziki
na Kitu Mapenzi na sasa liko mbioni kuzindua albamu mbili kwa mpigo wakati wa Valentine day.
0 comments:
Post a Comment