Hassan Vocha. |
Akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com Vocha alisema muziki ameanza kuimba takribani miaka mitatu sasa ambapo alianza kuimba katika miondoko ya Bongo Flavor akiwa kwa Mkubwa Fella TMK, baada ya kuachana na muziki huo alijaribu na mduara kidogo akashirikiana na Shilole katika nyimbo ya "Paka la Bar" na kisha kujidumbukiza katika muziki huu wa mwambao katika kundi la Dar Modern.
Hassan Vocha ametoa malalamiko kwa watangazaji naomna baadhi wanavyoendesha vipindi kwa upendeleo, anasema unakuta mtangazaji anapiga zaidi ya nyimbo mbili za bendi moja wakati nyimbo anazo nyingi tu za bendi tofauti tofauti, hilo ni tatizo.
Ameshauri wanapopiga nyimbo kuwe na uwiano wa nyimbo, anapopiga nyimbo ya bendi moja basi asirudie tena kupiga nyimbo za bendi hiyo na badala yake apige bendi nyingine ili nazo zisikike, ni hayo tu.
Hassan Vocha alipoulizwa ni muimbaji gani wa Taarab anavutiwa naye kwa sasa!? Akasema kwa kipindi hiki hakuna msanii anayeimba na kuvutiwa naye kwani wanapiga kelele tu, waimbaji wazuri walishatangulia mbele za haki (Wapumzike kwa amani), "Nilikuwa navutiwa sana na uimbaji wa Omary Kopa".
Vocha anashukuru sana kwa mashabiki wake kwa kumsapoti na kuwa pamoja naye katika show mbalimbali.
5 comments:
Hassan vocha angewataja tu hao watangazaji wenye upendeleo.
Kwa upande wangu mimi naona Dida anampendelea zaidi shoga'ake Isha Mashauzi, hakuna siku ambayo hajapiga nyimbo ya Isha, ktk kipindi chake LAZIMA narudia tena LAZIMA apige nyimbo za Isha, akisingizia eti hapigi nyimbo zakupooza! Mimi sikuhizi nikisikia kaweka wimbo wa Isha nabadili channel, kwani sioni jipya kwake.
mie mwenyewe cpendi dida anavofanya anapendelea xana asichague wala kubagua atakae mzika hamjui km Isha mashauz radio ile km y kwake vile jirekebishe dida mbk kusoma sms yan ataushia kununua magari n kukarabat nyumba z wenzio ajenge yake
mie mwenyewe cpendi dida anavofanya anapendelea xana asichague wala kubagua atakae mzika hamjui km Isha mashauz radio ile km y kwake vile jirekebishe dida mbk kusoma sms yan ataushia kununua magari n kukarabat nyumba z wenzio ajenge yake
blog hii no kubania coment ukweli usemww dida acha hyo tabia ww mdau toka bagamoyo
blog hii no kubania coment ukweli usemww dida acha hyo tabia ww mdau toka bagamoyo
Post a Comment