-->
Muziki wa Taarab unautata wa vyanzo viwili.
1. Kuna wanaosema taarab iliingia
nchini mwetu kupitia ikitokea Mombasa.
2. Kuna tafiti nyingine ambazo zinaonyesha
Sultan Barghash wa Zanzibar aliwapeleka wanamuzikiwawili Misri kujifunza
upigaji wa Taarab,na hao waliporudi ndo walipanda mbegu ya Taarab nchini mwetu.
Taarab imekuwa nahistoria ambayo ya kuwa na aina nyingi za taarab, na mpaka leo
mabadiliko ya taarab yanaendelea. Imefikia sasa kuna hata vikundi vya taarab
vina wacheza show. Taarab imekuwa pia ni ya kucheza na si kusikiliza ujumbe tu
kama ilivyokuwa zamani.
-->
Tunaweza kukubaliana mabadiliko katika kila kitu kwamba hata binadamu ana
mabadiliko ya marika yaani utoto, ujana, umakamo, uzee hatimaye ukongwe.
Mabadiliko haya ya kimaumbile hayamfanyi mtu/binadam abadilike kuwa ngedere.
Lakini si vyema kumfananisha au kughafilisha wasifu wa mtu/mwanadamu na
ngedere. Kwa sababu mtu/mwanadamu asilani atabaki kuwa mtu/mwanadamu hali
kadhalika ngedere asilani atabaki kuwa ngedere.
Taarab ni taarab na huu muziki
mpya ambao bado haujapata jina kamili iwe ni mipasho au rusha roho utabakia
kuwa rusha roho au mipasho na asilani huwezi kuwa taarab.
Kuhusu maswali ya hapo juu yanaweza kujibiwa na tafiti nyingi kuhusu muziki wa Taarab
zilizoandikwa na kurekodiwa na taasisi na watafiti mahiri wa muziki (Outstanding
Musicologists) kama vile kina Said A.M. Khamis, Werner Graebner, Mohamed
El-Mohammady Rizk, K.M. Askew, Global Music Centre na vyuo vikuu mbali mbali
hususani vya Ulaya na Marekani.
ZAIDI: Said A.M. Khamis anapagawishwa na
mabadiliko katika nidhamu ya muziki wa Taarab - Wondering About Change: The
Taarab Lyric and Global Openness. Nordic journal of African Studies 11(2):
198-205 (2002). Said A.M. Khamis* University of Bayreuth, Germany.
(http://www.njas.helsinki.fi/pdf-files/vol11num2/khamis2.pdf). Nadhani Bwana
Said A.M. Khamis tupo kwenye upande mmoja wa mtazamo kwamba hii iliyokuja sasa
ni mipasho au rusha roho ni aina nyingine ya muziki na siyo taarab.

-->
Wengi wanapagawishwa na mabadiliko yanayoendelea ambayo yanatokana
na sababu nyingi, lakini pia ni vizuri kujiuliza kama taarab "halisi"
ni ipi ambayo ndicho kipimo cha taarab.
Kipimo changu cha taarab halisi kinaanzia kwenye tungo (Ushairi wenye vina na
maudhui au hata kama ni bashrafu ni bashrafu iliyopigika katika mtindo na ala
za okestra ya taarab).
Tofauti nyingine imelalia kwenye muziki wa Taarabu:
kimuziki (ala zitumikazo, mtindo wa muziki unaopigwa kimapigo (Rhythm), ghani
(melody), na mwafaka (harmony). Halafu linakuja suala la nidhamu ya muziki wa
taarab: Mtindo wa utumbuizaji wa muziki wa taarab (presentation style) kuanzia
wajihi wa wanamuziki (performers personalities), muundo ukaaji jukwaani (stage
arrangement), mtindo wa jukwaani na majukwaa (stage setting and arrangement),
mazingira ya utumbuizaji (performance aura), wahudhuriaji na aina wahudhuriaji
onyesho (audience and audience target/ audience demography). vigezo hivyo
nilivyovitaja na vinginevyo ndivyo vinavyoitofautisha taarab na chakacha au na
mipasho au rusha roho.
Kabla ya mipasho na rusha roho palikuwepo chakacha
lakini haikuwahi kutokea kuchanganya taarab na chakacha. Au siyo?
Haya mambo
ndiyo ya kutaka serikali ya sultani iteue Sultani mwanamke. Ikishateuliwa
Sultani mwanamke huo si usultani tena. Au Vatikani wamchagua Papa mwanamke,
ikitokea kuchaguliwa papa mwanamke huo si Ukatoliki tena.
Vivyo hivyo ikiwa
kama taarabu itapigwa kwa ala za muziki wa dansi, na wacheza shoo tena shoo
hizi za kiwana mipasho, na tungo zisizo za kishairi na maneno yasiyo na staha,
na kupigwa kwenye kumbi za vilevi basi hiyo si taarab ni mipasho au rushaa roho
na si taarab.
Hebu niambie leo ukute watu wanapiga muziki wao kwa kutumia
accordian, gitaa baridi na manyanga halafu wakuambie hii ni heavy metal,
utaafikiana nao au utafikiri wamepatwa na ugonjwa wazimu.