TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Saturday, August 31, 2013

TETESI:- MWINJUMA MUUMIN AJIUNGA NA G5 MODERN TAARABU...

 Kuna tetesi kuwa Kiongozi wa Victoria Sounds - Mwinjuma Muumini amejiunga na G5 Modern.
 
Mwanamuziki nguli na mkongwe katika ulimwengu wa dansi nchini Mwinjuma Muumin au Kocha wa Dunia inasemekana amejiunga na bendi ya taarabu ya G5 Modern Taarabu inayomilikiwa na Hamisi Slim.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa taarabu wa eneo la Mtoni kwa Azizi Ally ambapo bendi ya G5 hufanya maonesho yake, wamesema kwamba wamekuwa wakimshuhudia Muumin akihudhuria katika maonyesho ya bendi hiyo usiku wa manane jambo walilo tafsiri kwamba Muumin amejiunga na bendi hiyo.

Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Hamisi Slim aliweka wazi kuwa, hakuna kitu kama hicho, isipokuwa Muumin ni rafiki yake wa muda mrefu hivyo huwa anamtembelea tu!.

Thursday, August 29, 2013

MARIAM HAMDANI:- QUEEN SALMA NI MWALIMU WANGU

Queen Salma.
 Msanii Nyota wa 5 Star's Modern Taarabu, Mariam Hamdani amekili na kusema kwamba Queen Salma ambae ndie muimbaji nyota wa Supershine Modern Taarabu ndio mwalimu wake katika uimbaji wa taarabu. 

Ameyasema hayo wakati alipokutwa katika mazoezi ya Supershine na mwandishi wa habari hizi. 

Unajua nina safari ndefu sana katika muziki huu wa taarabu nchini, na mwanzilishi wa safari yangu ni Queen Salma, mimi namthamini na kumheshimu kama mama yangu mzazi!. 

Kwa upande wake Queen Salma alimshukuru Mariam Hamdani kwa kukumbuka wapi alipotoka na mungu amjaalie.

JUMANNE ULAYA:- SIBISHANI NA WATOTO WADOGO KWENYE MUZIKI...

Jumanne Ulaya J4.
 Mpiga gitaa la solo wa siku nyingi na msanii wa 5 Stars Modern Taarabu kwa sasa Jumanne Ulaya au J4 amevunja ukimya na kuwaambia wale wote wanaojidanganya kumfuata kwa karibu katika upigaji wa chombo hicho wanajidanga na kamwe wasitegemee kama ipo siku moja watamfunika. 

Aliyasema hayo baada ya mpiga solo wa Jahazi Modern Taarabu Mohamedy Mauji kuonekana kama amejibu habari iliyoandikwa na blog hii kwamba Jumanne Ulaya ni mpiga solo bora wa taarabu kwa sasa hapa nchini. 

Mauji alisema yeye ni bora kwa sasa na hana mpinzani...! Mmh! tutaandaa pambano maana...!

Wednesday, August 28, 2013

DOWNLOAD: Nyimbo mpya ya Hassan Zumo - Niacheni Nipagawe...

Mwimbaji: Hassan Zumo
Nyimbo: Niacheni Nipagawe

*Kinanda kimepigwa nae Omary Kisila 
*Solo gitaa limepigwa na Ramadhan Kisolo
*Besi gitaa kapiga Side James.

G5 MODERN TAARABU IMEKUJA KUWASHIKA WAKAZI WA ILALA NA VITONGOJI VYAKE.

Wasanii wa G5 Modern Taarabu


Bendi ya G5 Modern Taarabu kuwasha moto Mx Bar Ilala kila siku ya Alhamisi.

Katika kile kinachoonekana kama kuwaendea zaidi wananchi wa kipato cha kati Bendi ya G5 Modern Taarabu kwa mara ya kwanza toka ianzishwe inatarajia kufanya show katika ukumbi wa MAX HALL ilala siku ya Alhamisi hii na kila Alhamisi itakuwa ipo pale. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mpiga besi wa bendi hiyo ambae pia ni kiongozi Shaibu Besi alisema kwamba watahakikisha burudani inakuwa ya nguvu sana ambapo wamejiandaa kupiga show ya kila Alhamisi.

Wapenzi wote wa Taarabu na G5 Modern Taarabu wanambwa kuhudhulia kwa wingi kuja kupata burudani na G5 Modern Taarabu.

SUPERSHINE MODERN TAARABU, KUMTAMBULISHA MPIGA KINANDA WAO MPYA LEO JUMATANO...

Baadhi ya wasanii wa Supershine Modern Taarabu.


Supershine Modern Taarabu leo Jumatano katika Ukumbi wa Max Bar Ilala watamtambulisha rasmi mpiga kinanda wao mpya Ndage Ndage.

Bendi ya Supershine ambayo kwa sasa imekuwa ndio gumzo la jiji zima la Dar, leo jumatano wanatarajia kufanya utambulisho wa nyimbo zao mpya na pia watamtambulisha rasmi mpiga kinanda wao mpya "Ndage Ndage" aliejiunga nao akitokea Mashauzi Classic. 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Mkurugenzi wa bendi hiyo Dk Noh! alisema kwamba wakazi wa Buguruni, Vingunguti, Tabata, Ilala, Kariakoo na maeneo ya jirani wafike kwa wingi kupata burudani nzuri toka Supershine Taarabu, "Tunawaahidi kutakuwa na burudani nzuri na ya kupendeza, kwa kweli leo ndo mtakubaliana nami kuwa Supershine Modern Taarabu si kama ile ya Zamani, tumejipanga vyema kutoa burudani kwa mashabiki zetu, karibuni sana".

Monday, August 26, 2013

HAMMER Q NA SALHA ABDALLAH: TUMEWAKOSEA NINI? SEMENI TUWALIPE...!

Hammer Q na Mkewe Salha.
 Wasaani wawili ambao ni wanandoa Hammer Q wa 5 Stars na Salha Abdallah wa Kings Modern Taarabu hivi karibu walitoa wimbo wenye mahadhi ya mduara na waliuimba pamoja wimbo huo uitwao TUNAPENDANA ni wimbo ambao umekuwa ukifanya vizuri sana katika vituo mbalimbali vya redio, juzi umezua balaa baada ya mtu asie julikana kuanza kusambaza sms kwa watangazaji wa redio kwamba wasiupige wimbo huo, Sms yenyewe hii hapa:- "Asalaam aleykum ulickia Hammer Q na Salha walivyo wakashifu watangazaji? Ucjaribu wala kupiga nyimbo zao ili wakione maana wanajua dunia wanaitawala wao".

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Hammer Q alisema Unajua ndugu mwandishi, ndoa yangu na mke wangu Salha imekuwa na maadui wengi haijapata tokea! na sijui ni nini tumewakosea!, kama kuna kitu wanatudai waseme tuwalipe!.


Juzi nilikuwa nahojiwa mimi na mke wangu Salha katika kipindi cha ng'aring'ari na Sakina Lyoka Clouds TV. Sasa inasemekana mimi niliwaponda watangazaji wa redio na kuwakashifu kitu ambacho sio kweli kabisa, hata kama kipindi kitarudiwa wataona sikusema jambo lolote baya la kuwatusi wala kuwakashifu, Mungu shahidi! Sasa from no where! mtu anatuma sms kwa watangazaji kwamba mimi na mke wangu tunajidai, tunajiona kama dunia tumeibeba, ni jambo ambalo sio kweli, hii ni katika kuchafuliana majina kwa chuki binafsi tu!.

Yaani ndugu mwandishi hatujui kosa letu, tunafuatiliwa sana kwa kila tunalofanya! naomba nichukue nafasi hii kuwaomba radhi watangazaji wote kama waliumizwa na hayo maneno ya uzushi watusamehe mimi na mke wangu kwani wao tunawategemea sana kucheza kazi zetu na mke wangu!.

Ila waelewe wazi kamwe hatuwezi kuwasema vibaya abadani, tunawapenda sana kwani wao ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya sanaa yetu. alimalizia.

Sisi pia tunawaomba watu hao kuacha kuchafu wenzao, kwani mtu anapokosea huambiwa ili ajirekebishe sio kumzunguka na kuanza kumsema au kumzushia kitu ambacho hajakifanya kwa lengo la kumvuruga na kumchonganisha na watu.


Hii hapa ni Msg ya Hammer Q kwa niaba ya Salha pia aliyoitoa katika ukurasa wake wa Facebook:-

Sunday, August 25, 2013

HASSAN VOCHA NA HASNA MASAUTI WA G5 KUTIMKIA BENDI NYINGINE...

Hasna Juma (Masauti) na Hassan Vocha.
 Hassan Vocha na msanii mwenzake wa G5 Modern Taarabu Hasna Masauti kutimkia katika bendi ya King's Modern Taarabu.

Wasanii chipukizi Hassan Vocha na Hasna Masauti wa bendi ya G5 Modern Taarabu wanawindwa kwa udi na uvumba na bendi inayokuja kwa kasi ya Kings Modern Taarabu ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Rais wa Kings Mrisho Rajabu alisema wamegundua uwezo mkubwa walionao vijana hao na wao kama Kings wanahisi itakuwa vyema zaidi kama watawanunua ili kuja kuipa nguvu bendi ya Kings. 

Alipopigiwa simu Hassan Vocha alisema ni kweli amepigiwa simu na kiongozi huyo ila hawajafikia muafaka bado, mazungumzo yanaendelea!.

BANDARI MODERN TAARABU, YAMNYEMELEA MSANII WA KING'S...

Mape Kibwana wa Bandari Modern.

Bendi iliyoanzishwa hivi karibuni ya Bandari Modern Taarabu iliyo chini ya ukurugenzi wa "Mzee wa Bandari" imeamua kuvunja Benki yake na kuimarisha kikosi ili kukabiliana na upinzani ulipo katika soko la Taarabu nchini. 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Kiongozi mwandamizi wa bendi hiyo ambae hakupenda kutajwa jina lake alisema kwamba baada ya kufanikiwa kumchukua msaani nguli Mape Kibwana kwa sasa wapo mbioni kumnasa mpiga kinanda wa King's Modern Taarabu MZAKA NUNDU kwa gharama yoyote ile, "Sisi kwetu pesa sio tatizo kabisa" Alimaliza kwa kusema Mzee wa Bandari.

AHMED MGENI UPO WAPI?.TUMEMISS BURUDANI ZAKO!

Muimbaji wa Zanzibar njema Modern Taarab Ahmed Mgeni amepotea kwa kipindi kirefu haonekani kwenye maukumbi wala mazoezini. 

Mtandao huu umekuwa ukipigiwa simu na wadau mashabiki na wapenzi wanaompenda Ahmed Mgeni kutaka kujua huyu mtu yupo wapi kwa sasa.

Mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com ulifanya uchunguzi wake na kugundua kwamba Ahmed Mgeni alikwenda Uarabuni lakini hakukaa sana akaanza kuugua ndipo aliporudishwa Tanzania na kwenda moja kwa moja Visiwani Zanzibar kwa matibabu zaidi. 

Hata hivyo alipopigiwa simu mkurugenzi wake hakupatikana kwenye simu lakini tutaendelea kumtafuta ili aweze kutueleza mambo mengine hasa kuhusu Ahmed Mgeni..

ZANZIBAR STARS KURUDI TENA KWA NGUVU MPYA...!!

Baadhi ya wasanii wa Zanzibar Stars.
Nipo mbioni tena kuirudisha Zanzibar Stars...
Hayo ni maneno ya muanzilishi wa bendi ya Zanzibar Star's, Bakary Shomari wa visiwani Zanzibar.

Akizungumza kwa njia ya simu toka visiwani humo Bakari Shomari alisema kwa sasa yupo tiyari kabisa kuirudisha kwenye game bendi yake hiyo kongwe ya Zanzibar Stars, kinachompa moyo zaidi wa kuanzisha tena kundi hilo ni kuona baadhi ya waanzilishi wenzake kama Bi Sihaba Juma na Rukia Ramadhan wakisema kwamba wapo tayari kuungana nae pindi bendi itakapokuwa tayari. 

Kipindi cha hivi karibuni kuna wajanja flani flani wamekuwa wakijikusanya na kufanya show kwa jina la Zanzibar Star's feki na kupiga hela nzuri tu kutokana na umaalufu wa bendi hiyo!

Bwana  Bakari Shomari alisema pindi atakapokuwa amekamilisha mambo yake, ataizindua rasmi ili wapenzi wote wajue kuwa Zanzibar Star ipo hewani na wala si ile feki tena.

Saturday, August 24, 2013

MAPENZI YA FACEBOOK...!!!

Hemedi Omary
 Mapenzi ya Facebook kutambulishwa rasmi Jumatatu...!! 

Wimbo mpya wa Muimbaji Hemedi Omary "Mapenzi ya Facebook" ambao umerekodiwa jana katika Studio ya BMD RECORD Mbagala jijini Dar umekamilika na utatambulishwa rasmi siku ya Jumatatu katika radio mbalimbali, pia utaipata katika mtandao huu wa taarabuzetu.

Hemed Omary alisema kwamba anamshukuru mungu kwa kumuwezesha kurekodi wimbo huo na wadau wasubiri kusikia kazi nzuri toka kwake. 

Katika wimbo huo kinanda kimepigwa na Mzaka Nundu, 
Gitaa la Solo limepigwa Jongo na gitaa la besi limechalazwa nae Hamadi besi. 

Hemdi Omary ni msaani wa bendi ya TOT TAARABU pia ni mtunzi mzuri wa nyimbo za Taarabu. 

Nyimbo alizowahi kutunga Hemed ni "Tugawane ustaarabu" ya Isha, "Top in Town" ya Khadija kopa na zingine nyingi.

WASANII WA G5 MODERN TAARABU WASEMA, MTUACHEEE...

Baadhi ya wasanii wa G5 Modern Taarabu.
 Wasanii wa Bendi mpya ya G5 Modern Taarabu wamesema kwamba wamekuwa wakionewa kijicho na baadhi ya wasanii wa bendi zingine kutokana na jinsi mkurugenzi wao Hamisi Slim anavyo wajali na kuwathamini sana. 

Yaani inafikia wakati wenzetu wanatuambia tunalelewa kama kuku wa amadoli!. 

Ndugu mwandishi tunaomba uwafikishie ujumbe huu kwamba tunaomba watuache na mambo yetu, mbona wao wakimaliza show wanatembea na miguu kurudi makwao sisi hatuwatangazi? tunajua mambo yao mengi... watuache kabisa waambie, alimalizia kusema msaani mmoja wa G5 ambae hakupenda kutajwa jina lake.

VIDEO YA "NIMECHOKA NA KASHFA ZENU" KUFANYWA LEO KIBAHA..

Aisha Vuvuzela.
 Watu waliisubiri kwa hamu na bashasha kubwa Audio ya wimbo "Nimechoka na kashfa zenu" toka kwa Aisha Vuvuzela, na walipoisikia wenyewe walikubali. Sasa pia wanaisubiri kwa hamu Video ya wimbo huo ambayo inatarajia kufanyika leo huko Kibaha mkoani Pwani. Kundi zima la wanamziki wa King's Modern Taarabu watakuwepo huko katika shindano la mamiss wa wilaya hiyo. 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Video shouter wa wimbo huo Saidi Abdallah alisema kwamba wameamua kubadilisha mandhari ili kuleta ushindani na radha nzuri zaidi katika kazi. 

Aisha Vuvuzela ni muimbaji ambae ametokea katika bendi ya Mashauzi Classic.

Friday, August 23, 2013

JOKHA KASIM, KAPOTELEA WAPI...??

Jokha Kassim
 Unapolizungumzia Jina la Jokha Kasim katika muziki huu wa taarabu hapa nchini, basi kila mmoja anajua kwamba huyo ni mtu wa aina gani katika tasnia hii. 

Jokha Kasimu amekuwa kimya sana tokea atoe wimbo wa "Domo la udaku" mapema mwaka jana akiwa na kundi zima la T MOTTO mpaka sasa hajulikani yupo wapi na anafanya nini katika tasnia hii. 

Wadau wa taarabu wamekuwa wakipiga simu ofisi kwetu kutaka kujua mpendwa wao yupo bendi gani kwa sasa? kwani hata T MOTTO ambayo alikuwepo haifanyi show yoyote jambo linalotafsriwa na wadau kwamba inawezekana imekufa. 

Jokha kasimu ni msanii anaependwa sana na wapenzi wengi wa Taarabu, mwandishi wa mtandao huu alijaribu kumtafuta katika simu yake ili aweze kuwaeleza mashabiki wake aliko, lakini bila mafanikio simu yake ilikuwa haipatikani, hata hivyo tutamtafuta ili aweze kuelezea ukimya wake ni nini hasa...!!?

Thursday, August 22, 2013

HASHIM SAIDI:- SIJAMLENGA YEYOTE...

Hashim Said Igwee (Mzee wa Majanga).
 Sijamuimba mtu yeyote katika wimbo wangu nilioutoa hivi karibuni wa Bonge la Bwana naomba nisieleweke vibaya.

Kiongozi wa wasanii katika bendi ya Mashauzi Classic na muimbaji wakutumainiwa Hashim Saidi au mzee wa Majanga amekuwa akilalamikiwa kwamba wimbo wake wa Bonge la Bwana amemuimba mke wake wa zamani, jambo ambalo mwenyewe amekanusha. 

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Hashim Saidi alisema kwamba kumuimba mtu ulieachana nae inaonyesha kama bado unamuhitaji jambo ambalo kwangu halipo na wala sithubutu, nilichokitapika kamwe siwezi kukila tena ni sawa na kutia ulimi puani jambo lisilo wezekana!. 

Huo ni wimbo tu, sikumlenga yeyote

HASSAN ZUMO AAMUA KUTOKA KIVYAKE...

Hassan Zumo.
 Muimbaji wa kutegemewa wa bendi ya Supershine Modern Taarabu Hassan Zumo, anakuja na wimbo uitwao "Niacheni Nipagawe" nje ya bendi yake. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Zumo alisema wimbo huo anategemea utamnyanyua na kumuweka juu zaidi kulingana na mashairi, muziki na ujumbe husika uliopo katika wimbo huo, katika wimbo huo kinanda kimepigwa nae Omary Kisila solo gitaa limepigwa na Ramadhan Kisolo na Besi gitaa kapiga Side James. 

Zumo amewaomba wapenzi kumpa sapoti ili aweze kufikia malengo aliyojiwekea katika suala zima la sanaa.

Wednesday, August 21, 2013

MAPE KIBWANA ATIMKIA BANDARI MODERN TAARABU...

Mape Kibwana, Msanii wa Bandari Modern Taarabu.
 Zile tetesi zilizozagaa jijini kwamba Mape kibwana ana mpango wa kujiunga na bendi ya Supershine Modern Taarabu wiki hii zimefikia kikomo baada ya yeye mwenyewe kuweka wazi kwamba kwa sasa yupo Bandari Modern Taarabu. 

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Mape alisema kuwa "wakati viongozi wa Supershine waliponifuata kwa ajiri ya kujiunga na bendi yao, tayari nilikuwa na mazungumzo na viongozi wa Bandari Modern Taarabu japo hatukuwa tumeelewana vizuri. Sasa juzi ndio nimemalizana na Bandari modern taarabu na kwa sasa ni msanii wao rasmi". alimaliza.

VIDEO: Uzinduzi 5Stars Album UKURASA MPYA SEHEMU YA 2 - 4

Ilikuwa ni uzinduzi wa Album ya kundi la 5Stars "UKURASA MPYA" iliyofanyika DAR LIVE, ni kubwa sana ndo maana tumeiweka katika sehemu 4, ile sehemu ya kwanza tuliyaitoa hapa, sasa ni sehemu ya 2 mpaka ya 4. ITIZAME KWA RAHA ZAKO...!!!


  

NDAGE NDAGE AITOSA MASHAUZI CLASSIC....!!

Ndage Ndage, mpiga kinanda mpya wa Supershine Modern Taarabu.
 Mpiga kinanda wa Bendi ya Mashauzi Classic Ndage Ndage ameiacha bendi yake hiyo na kujiunga na Supershine Modern Taarabu. 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Ndage alisema kwamba kikubwa kilicho mfanya aihame Mashauzi ni masirahi tu wala hakuna kingine "sijagombana na yeyote katika bendi na hata mkurugenzi wangu Isha nimemuaga, Huku nilipo sasa namshukuru mkurugenzi wangu DR NOH! kwani tokea nimeingia Supershine amekuwa akinijali na kunithamini sana. 

Dr NOH alisema pia kuwa, Supershine kwa sasa ipo katika mipango ya kupanga upya kikosi chake ili kwenda na wakati ndo maana imekuwa ikiongeza wasanii wazuri zaidi na kuimarisha Bendi.

Tuesday, August 20, 2013

CHAMA CHA TAARABU TANZANIA, MBONA MPO KIMYA JUU YA MGOGORO WA BI MWANAHAWA NA MMILIKI WA 5 STAR'S...!!?


 Mgogoro wa mwanamuziki mkongwe wa taarabu nchini Bi Mwanahawa Ally na mmiliki wa 5 Star's Modern Taarabu Mr Shark's umeingia sura mpya ya malumbano juu ya mkataba waliowekeana wakati wa kusaini. 


Mtandao huu ulikuwa wa kwanza kabisa kuandika juu ya malalamiko ya Bi Mwanahawa akilalamika kukiukwa baadhi ya vipengele katika mkataba huo, na kuongeza kwamba yeye si msanii tena wa bendi hiyo sababu mmiliki huyo ameshindwa kutimiza masharti ya mkataba. 

Jumapili ya wiki iliyopita nae mr Shark's alisikika katika kituo kimoja cha redio hapa jijini akilalamika kwamba Bi Mwanahawa amekuwa haheshimu mkataba wa miaka miwili aliosaini mwenyewe huku akiwa na akili timamu kabisa, amekuwa akimtia hasara mbalimbali ikiwemo kumlaza hotel kwa siku zote alizokuwa akiishi hapa Dar! na hasara nyingine nyingi sana. 

Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com kama mdau mkubwa wa muziki huu tumekuwa tukijiuliza maswali kadhaa, hivi chama cha taarabu nchini hakiyasikii malumbano haya?, na kama inasikia ni hatua gani wamechukua katika kutatua tatizo hili kati ya mmiliki wa bendi na msanii?. au hakuna kabisa chama hicho hapa nchini?, haki za msanii wa Taarabu hapa atazipata wapi kama hakuna chama?. 

Kila muziki una chama chake hapa Tanzania lakini katika Taarabu kama chama kipo basi hakina makali na wala hakiwezi kutoa kalipio la aina yoyote wanachama wake ambao ni bendi wakaelewa!, ndio maana hata katika mashindano ya Kilimanjaro Music Awards Taarabu imekuwa haitendewi haki katika kupanga makundi ya wagombea, mfano hakuna wagombea chipukizi, pili kipengele cha mburudishaji bora wamekiondoa na watu wapo kimya tu! 

Wakati umefika kwa viongozi wa mabendi ya Taarabu kuitisha mkutano na kuwaomba Basata kuitisha mkutano wa kuchagua viongozi wakuongoza Chama hicho. 

Na kama kweli chama kipo hai basi waamke sasa katika kutetea haki za wasanii wa taarabu nchini na sio kukaa kimya tu kama ilivyo sasa. 

Hili tatizo la Bi Mwanahawa Ally liwe mfano kwa utendaji bora wa chama hicho, tutoke giza na kuangaza macho!, ndio maana watu binafsi wamekuwa wakifaidika zaidi kwa muziki huu na kuacha msaani ambae ni mvuja jasho akibaki na labda!.

Kalamu naweka chini...kamwe siwezi kuwa adui kwa kusema kweli. TAARABU DAIMA MBELE KURUDI NYUMA MWIKO!!.

WAIMBAJI WENGI WAKIUME WA TAARABU WANABANA PUA...!!

Hassan Kumbi (Hassan Vocha).
 Jina lake halisi ni Hassan Kumbi, ila kwa sasa amekuwa akitambulika zaidi kwa jina la Hassan Vocha. 

Huyu ni muimbaji wa bendi ya G5 Modern Taarabu kwa sasa, hapo kabla alikuwa anaimba Bongo fleva na alitamba na kibao chake cha mahadhi ya mduara kiitwacho VOCHA. 

Msaani huyu siku ya Jumapili katika Bonanza la G5 Ikweta grill, alimwambia mwandishi wa Habari hizi kwamba "najiamini na sitishwi na msaani yeyote wakiume kwa uwezo wa kuimba kwani walio wengi wanabana pua tu kama bongofleva! ila mimi naimbia sauti yangu halisi na nitawasumbua daima milele!"

SALHA ALIKUWA MPENZI WANGU TOKEA MWAKA 2005...!!

 Muimbaji wa kutumainiwa wa bendi ya 5 Star's Modern Taarabu Hammer Q amesema kwamba walianza uhusiano wao yeye na Salha tokea mwaka 2005. 

Hammer aliyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na Sakina Lyoka ambae ni mtangazaji wa Clouds TV katika kipindi cha ng'aring'ari. 

Katika mahojiano hayo ambayo pia alikuwepo na Salha mkewe, Hammer alitumia nafasi hiyo kuwaonya wale wote "vizavizabina" wanaopenda kuingilia mapenzi yao kwamba wafanye yao sasa kwani wamesha wagundua. 

Walichukua nafasi hiyo pia kutambulisha video yao mpya kabisa iitwayo TUNAPENDANA. ambayo pia ipo katika mtandao huu tuliwawekea wapenzi wetu wa taarabuzetu.blogspot.com.

Monday, August 19, 2013

UTENDAJI MBOVU NA USIO MAKINI NDIO CHANZO CHA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YA BENDI CHANGA ZA TAARABU NCHINI...


Huu ni uchunguzi uliofanywa na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com ya kuwa, hapa Tanzania kwa sasa unapoamua kuzungumzia bendi ya taarabu zinazofanya vizuri basi utataja tatu au nne tu, wakati kuna bendi za Taarabu takribani kumi na tano au kumi na sita hapa Dar es Salaam peke yake. 

Bendi zinazofanya vizuri ni:- 
Jahazi modern Taarabu, 
Mashauzi Modern Taarabu, 
5Star Modern Taarabu na wakongwe 
East African Melody tu basi!. 

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu makini kabisa umegundua kwamba takribani viongozi wote na wasanii wao wamekuwa ni watu wasiojiamini katika hii fani na ndio maana wanafikia hata kupiga nyimbo za kopi ambazo zinatamba katika bendi hizo ambazo wenyewe wanaziita kubwa!.

Kingine ni umakini wakati wakutengeneza nyimbo, madirector karibia wote waliopo katika hizi bendi ndogo ndogo wamekosa ubunifu, jinsi ya kubuni muziki wenyewe na mpangilio wa sauti kwa ujumla!, mbona mnaweza tu! hebu muwe mnajikubali na kamwe msitazame Jahazi au Mashauzi wamefanya nini. 

Hebu fanyeni kazi kwa uangalifu na umakini muone kama watu hawatowakubali!, kifurugobe alimdondokea kobe akaingiwa na hofu ya milele! acheni kukimbia kivuli chenu!. 

Wao waweze wana nini na ninyi mushindwe muna nini? 
PIGENI KAZI

DOWNLOAD:- Nyimbo mpya ya Supershine Modern Taarabu - Nimempata wa ukweli...

Supershine Modern Taarabu 
Mwimbaji: Ally Mikidadi (High Light) 
Nyimbo: Nimempata wa ukweli

DOWNLOAD:- Nyimbo mpya ya Supershine Modern Taarabu - Professionally Love...

Supershine Modern Taarabu 
Mwimbaji: Hassan Zumo 
Nyimbo: Professionally Love

DOWNLOAD:- Nyimbo mpya ya Supershine Modern Taarabu - Huna Style...


Supershine Modern Taarabu 
Mwimbaji:Queen Salma
Nyimbo: Huna Style

Sunday, August 18, 2013

UZINDUZI WA MASHAUZI PUB KATIKA PICHA, WASANII NA WADAU KIBAO WA TAARABU...!!

Kaptaini-Temba-&-Mkurugenzi wa Mashauzi Pub, Mama-Shija wakiweka pouse kwenye kamera ya Taarabu Zetu katika uzinduzi wa Mashauzi Pub jana 17 August maeneo ya Vingunguti Dar es Salaam.
Kaptaini-Temba akitoa Burudani...
Mdau mkubwa-Mama-Zeka.. alikuwepo kushuhudia uzinduzi.

ANGALIA VIDEO YA UZINDUZI WA 5STARS, ALBUM YA UKURASA MPYA (1)

IFIKE WAKATI WASANII WA TAARABU WASAINI MIKATABA YAO MBELE YA WANASHERIA...

 Muziki wa taarabu umekuwa ukipata mafanikio kila kukicha na kufanya hata makampuni makubwa hapa Tanzania kuanza kutangaza bidhaa zao kupitia vipindi vya muziki huo katika Redio na televisheni mbalimbali, Lakini asilimia kubwa ya wasanii wa muziki huu wamekuwa hawajui haki zao au wao pia kukiuka mikataba ambayo wamekuwa wakiwekeana kiholela na wamiliki mbalimbali wa mabendi husika. 

Mfano Msaani kama Bi mwanahawa ally! amekuwa akizitumikia bendi zaidi ya mbili ama tatu kwa kurekodi nyimbo mpya au kufanya Show katika bendi zote hizo.

Sasa balaa ni pale bendi hizo zote zinapoingiza albamu zake sokoni, utakuta katika kila albamu moja kuna nyimbo mpya kaimba Bi Mwanahawa Ally, sasa hapa kwanza mashabiki wanashindwa kujua huyu mama yupo bendi ipi moja wapo kati ya hizo?.

Ukirudi upande wa pili wakulaumiwa ni viongozi wa bendi hizo, ni kwanini wanamuimbisha Bi mkubwa huyo wakati hawana mkataba nae?. 

Imefika wakati sasa kwa viongozi wa Taarabu na wasanii kwa ujumla kuzijua haki zao kisheria ili kila mmoja afanye kazi kulingana na mkataba unavyosema. 

Hii tabia ya kuandikishiana mkataba kama mnapeana maji ya kunywa imepitwa na wakati sasa. TUBADILIKE

AISHA VUVUZELA:- SIJAMLENGA MTU KATIKA WIMBO WANGU, ATAKAE JISHUKU SHAURI YAKE..

Aisha Vuvuzela.
 Muimbaji machachari wa bendi ya King's Morden Taarabu, Aisha Vuvuzela amesema kwamba wimbo wake mpya wa "Nimechoka na kashifa zenu", ni tungo isiyomhusu mtu yeyote na hajamkusudia mtu kama inavyodaiwa. 

Ameyasema hayo jana wakati akihojiwa na mtangazaji Nyawana Kais wa kipindi cha Ambaa na mwambao kinachorushwa na Passion FM ya jijini Dar. 

Kiukweli nimekuwa nikipata maswali mengi sana toka kwa watu mbalimbali tokea wimbo wangu ulivyotoka. kiukweli huo ni utunzi wa kawaida kama tungo zingine na niliyoyazungumza humo yanatokea sana kwenye jamii, naomba wadau wanielewe hivyo!!.

TETESI:- MAPE KIBWANA AJIUNGA NA SUPERSHINE MODERN TAARABU...

Mape Kibwana.
 Muimbaji aliewahi kutamba kwa kipindi kirefu katika bendi ya Dar Modern Taarabu kipindi hicho Mape Kibwana inasemekana yupo katika hatua za mwisho katika mazungumzo ya kujiunga na kundi la Supershine Modern Taarabu. 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Mape alisema ni kweli mipango hiyo ipo sababu kuna kiongozi mmoja wa bendi hiyo alinipigia simu kunijulisha hivyo na Jumatatu panapo majaaliwa basi nitakwenda kumalizana nao kabisa. 

Mape Kibwana kwa sasa ni msanii huru baada ya yeye mwenyewe kuamua kuiacha bendi yake ya zamani ya Dar Modern Taarabu.

Saturday, August 17, 2013

TETESI:- SALEHE MUSSA WA SUPERSHINE ATIMKIA GUSAGUSA MIN BEND...!!

Salehe Mussa
 Kuna tetesi zimevuma kuwa, mpiga kinanda wa kutumainiwa wa bendi ya Supershine Modern Taarabu "Chuo cha mafunzo" ametimkia kwa wana Gusagusa Min Bend ya hapahapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi wa Supershine Dr Noh! alisema kwamba yeye hana uhakika kama msanii wake Salehe Mussa amehama bendi, kwani hajamwambia lolote isipokuwa ameshangaa tu kuona Salehe Mussa hajatokea katika show ya pale Max Bar Ilala jumatano na pia hajatokea siku ya alhamisi katika show ya pale Lango la Jiji Magomeni. 

Mwandishi wa taarabuzetu.blogspot aliamua kumtafuta Salehe Mussa kwa namba yake ya simu ya mkononi lakini hakupatikana na mpaka habari hizi zinachapishwa simu yake haipatikani.

Hata hivyo Salehe Mussa ameonekana katika show ya Gusagusa Min Bend akipapasa kinanda kwa raha zake.

Friday, August 16, 2013

ALLY STAR AMPONDA THABIT ABDUL...!!

Ally Hemed Star wa T.O.T.
 Muimbaji mkongwe wa T.O.T. Taarabu Ally Star amemponda Thabit Abdul kwa kujiita yeye ndo muanzilishi wa mtindo wa TARADANCE.

Ameshangazwa na habari iliyoandikwa na mtandao huu kwamba Thabit Abdul yeye ndio muanzilishi wa taradance hapa nchini kitu ambacho sio kweli kabisa. na kusema kwamba muanzilishi wa Taradance hapa nchini ni yeye. 

Aliyasema hayo wakati alipopiga simu ofisini kwetu na kusema kwamba huyo Thabit asijisifie kwa kitu ambacho hajakiunda yeye wala hana uzoefu nacho zaidi ya kukopi tu!, mimi nimetoa wimbo wenye miondoko ya Taradance uitwao MVUVI KINDA kabla yake yeye!, hivyo yeye kakopi toka kwangu na kujitangazia kuwa muanzilishi, tafuta hiyo nyimbo usikiliza kaka kisha uniambie!.

THABIT ABDUL ANAKUJA NA "WHY ME"...!!

Thabit Abdul
 Mpiga kinanda wa 5 Stars Modern Taarab Thabit Abdul yupo katika maandalizi ya ku-record wimbo wake binafsi nje ya bendi yake ya 5 Stars. 

Thabit Abdul ni msanii wa siku nyingi akiwa kama Mpiga Kinanda, Director, Mtunzi wa Mashairi nk. amesema wimbo huo ameupa jina la WHY ME? utarekodiwa katika studio ya Soundcrafters Temeke 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Thabit alisema kwamba wimbo wake huo ambao anategemea utakuja kufanya vizuri zaidi, Solo gitaa atampigia Kisolo au J4 na gitaa la Besi atapiga Mussa Mipango. 

Katika wimbo huo kama ilivyo kawaida yangu kinanda nitapiga mwenyewe na sauti pia nimeweka mwenyewe. Mashabiki wasubirie kitu cha ukweli!.

Thursday, August 15, 2013

G5 MODERN TAARABU, KUANZA "BONANZA" KILA JUMAPILI...

Baadhi ya wasanii wa G5 Modern Taarabu.
 Bendi ya G5 Modern Taarabu itakuwa ikifanya onyesho la Bonanza kila Jumapili, na itaanza jumapili hii tarehe 18/8/2013.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mkurugenzi wa bendi hiyo Hamisi Slim alisema kwamba katika bonanza hilo kutakuwa na vikundi mbalimbali vya burudani vitakavyokuwa vikishirikiana nao, Hamis alivitaja vikundi hivyowakiwemo kundi la Kanga moja na Mavampaya watoto wa TMK, Vile vile Dogo Asley ataongoza kundi la Mkubwa na wanawe, kama hiyo haitoshi wanafikilia kuwaongeza kundi la Baikoko na Msagasumu ili kunogesha zaidi Bonanza hilo.

Mkurugenzi Hamisi Slim alisema Bonanza hilo litakuwa likifanyika kila Jumapili katika ukumbi wa IKWETA GRILL Mtoni kwa Azizi Ally.

Wapenzi wa G5 wameombwa kuhudhulia ili kupata burudani kila Jumapili kabla ya kuingia makazini Jumatatu, Pata burudani kibao na G5 Modern Taarabu!

Wednesday, August 14, 2013

VIDEO MPYA: Surprise = Omary Tego - "Coast Modern Taarabu".

VIDEO MPYA: Wapendanao = Hammer Q & Salha (Mr & Mrs)

DAR MODERN TAARABU, KUFANYA KWELI LEO JUMATANO...!

Baadhi ya wasanii wa Dar Modern Taarabu.
 Bendi ya Dar Modern Taarabu yenye makazi yake magomeni jijini Dar-es-salaam inatarajia kukonga nyoyo za wakazi wa Magomeni na vitongoji vyake pale watakaposhusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa Lango la jiji Magomeni jijini Dar. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Muimbaji wa bendi hiyo Twaha Nassoro alisema kwamba bendi yao imepania kuwadhihirishia mashabiki wake ni kwanini wao ni bora kila idara!. "unajua sisi Dar modern sio watu wakusema sana, sisi ni vitendo tu siku zote"!. 

Ikumbukwe Dar modern walikuwa jikoni kupika vibao vyao vipya.

FUNGA KAZI MODERN TAARABU KUACHIA NYIMBO MBILI KALI...

Funga Kazi Modern Taarabu.
 Bendi ya Funga kazi Modern Taarabu ya jijini Dar inatarajia kuachia nyimbo zao mbili mpya kali katikati ya wiki ijayo. 

Akizungumza na mwandishi wa mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Mkurugenzi wa bendi hiyo Kapteni Temba alisema kwamba Bendi yake itaachia nyimbo mbili ambazo ni:- 
1. "Una nini Nzi wa kijani" iliyoimbwa na Ashura Machupa na ya pili ni 
2. "Muungwana haumbuki hata avuliwe nguo" Iliyoimbwa na Wahida Daddy. 

Hizo nyimbo ni hatari ndugu mwandishi nawaomba wapenzi wa muziki wa Taarabu kujiandaa kupata kitu kizuri, mara nyingi huwa hatubahatishi.

SUPERSHINE MODERN TAARABU KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA MAX BAR ILALA.

Baadhi ya wasanii wa Supershine
 Bendi ya Supershine Modern Taarabu baada ya kutoka katika Shangwe za sikukuu ya IDD, leo siku ya Jumatano wanatarajia kuporomosha burudani ya nguvu katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala. 

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Msanii wa bendi hiyo ambae pia ni MC Hassan Zumo aliwaomba wapenzi wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia mambo mazuri ambayo wameyaandaa kwa muda wote wa kipindi cha Ramadhani. 

Supershine Modern Taarabu huwa wanatoa burudani zao katika kumbi za Max Bar Ilala kila Jumatano na Lango la jiji kila Alhamisi, wapenzi wote mnakaribishwa.

MWANAHAWA CHIPOLOPOLO AITAMBULISHA "WAJA MSINIHUKUMU"...

 Muimbaji wa zamani katika bendi ya King's Modern Taarabu, Mwanahawa Chipolopolo, jana tarehe 13/08/2013 jumanne! alitambulisha kibao chake kipya kiitwacho "Waja msinihukumu" katika vituo mbalimbali vya redio hapa Dar. 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Mwanahawa Chipolopolo alisema kuwa wimbo wake huo utamrudisha katika game kama ule wa "Dunia duara" ambao aliuimbia akiwa Kings Modern Taarabu. 

Chipolopolo kwa sasa ni msaani wa bendi ya Delas Modern Taarabu ya Keko jijini Dar es Salaam.

ALLY STAR, A.K.A. "SHARO BABU" AKAMILISHA ALBAM.



Muimbaji wa siku nyingi na muajiliwa wa bendi ya T.O.T. Taarabu Ally Star au "Sharo Babu" amekamilisha albamu yake binafsi iitwayo "Bahati ya paka si bahati ya mbwa". 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Ally star alizitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo kuwa ni:- 
1. Bahati ya paka si bahati ya mbwa 
2. Mvuvi kinda, 
3. Hauvumi lakini umo remix, 
4. Muwa remix 
5. Fikira Ulioimbwa na Bi Ridhik.

Ameendelea kusema kuwa albamu yake hiyo ni nzuri sana kwani studio aliyorekodia ya Kazi Record ina ubora mkubwa sana. watu wasubiri kusikia kazi nzuri.

Tuesday, August 13, 2013

TETESI:- RAMADHAN KISOLO ATAKIWA NA BENDI ZAIDI YA TATU...

Ramadhan Kisolo "Mwana Malui", Mpiga Solo wa Mashauzi Classic.
 Katika kile kinachooneka ni kutaka kuidhoofisha bendi ya Mashauzi Classic, Zaidi ya Bendi tatu za taarabu nchini zimeanza kumuwania kwa udi na uvumba Mpiga solo maarufu wa bendi hiyo aitwae Ramadhan Kisolo "Mwana Malui", 

Akizungumza na msanii huyo mwandishi wa habari hizi alitaka kujua je tetesi hizi zinaukweli wowote?, Kisolo alisema "mimi ni msanii wa Mashauzi Classic na sina mpango wa kuhama bendi hii kwani mkurugenzi wangu Isha amekuwa akinitimizia kila kitu hivyo nawaambia hao wanaozusha habari hizi kuacha kuniharibia kwa Bosi wangu".

IDDI TATU... TAARABU YAADIMIKA DAR...

Wasanii wa Jahazi
 Imegundulika kwamba kwa sasa muziki wa taarabu umekuwa una soko zaidi mikoani ukilinganisha na Dar kama ilivyokuwa zamani. 

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini hilo haswa baada ya kuona katika shamrashamra za sikukuu ya IDD bendi nyingi zikitokomea mikoani na kuacha wapenzi wa Dar wakihaha kusaka burudani hiyo. 

Siku ya IDD tatu bendi ya Jahazi ilikuwa Morogoro, 
Bendi ya Kings ilikuwa Morogoro, 
Bendi ya 5 Stars ilikuwa Kibiti, 
Mashauzi walikuwa Songea. 
T Motto waliku Chanika.

Na Bendi zingine zilipumzika kabisa:-


East African Melody hawakuwa na show 
Supeshine hawakuwa na show 
Dar modern hawakuwa na show pia.
Coast Modern Taarab nao hawakuwa na show. 

Bendi ambayo ilikuwa na show siku ya IDDI tatu Dar nzima kwa upande wa Taarabu ni G5 Modern Taarabu pekee ambao walikuwa wanapiga pale Kalembo Bar maeneo ya Buguruni. 

Mpenzi mmoja wa Taarabu aitwae Jumanne Shabban aliuambia mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kwamba hawa viongozi wa hizi bendi hawakufanya vizuri kutuondolea burudani ya taarabu jijini. 

Bendi za Jahazi na Mashauzi bado zinaendelea na burudani za IDDI.