TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, September 25, 2013

BARUA YA WAZI:- KWA MAKAMPUNI YANAYODHAMINI VIPINDI VYA TAARABU REDIONI NA KATIKA TELEVISION MBALIMBALI NCHINI TANZANIA...

Taarabu ni muziki wenye asili ya mwambao na ukanda wa pwani kwa ujumla, muziki huu hapo zamani ulikuwa ni kiburudisho haswa mida ya jioni ambapo watu wanakuwa wametoka pwani au baharini kutafuta kitoweo kwa ajiri ya familia zao na wengine kuuza!, muziki huu umekuwa ukijizolea sifa na mashabiki lukuki kila kukicha jambo linalopelekea kupata udhamini wa makampuni makubwa wakiwekeza mamilioni ya pesa katika redio na television mbalimbali hapa nchini, hii yote ni kuonyesha ni kwa kiasi gani muziki huu unavyokubarika katika jamii. 

Lakini jambo la kushangaza na kustaajabisha ni kuona khali duni ya kimaisha anayoishi msaani husika ambae amesababisha hata hayo makampuni makubwa kuwekeza na kujinafasi kwa upana zaidi katika kujitangaza!, "waswahili wanasema, baniani mbaya kiatu chake dawa" wakati umefika sasa kwa haya makampuni kusaidia vikundi mbalimbali vya taarabu nchini bila ubaguzi wowote ili kuweza kujikimu na kumpa hamasa msanii kutengeneza nyimbo nzuri zaidi, nchi yetu bado haijafikia msanii au bendi kulipwa na vituo vya redio au television kulingana na kazi yao, basi ninyi makampuni mnawajibu wakudhamini pia bendi husika ili kujikimu na gharama za uendeshaji na sio kukimbilia katika vituo vya redio na television tu kudhamini. 

Khali inapoendea ipo siku viongozi wa bendi za taarabu watagoma kupigwa kwa nyimbo zao katika vipindi ambavyo ninyi makampuni mnadhamini humo mpaka mkae meza moja na kuona mnawajari kwa kiasi gani, "waungwana wanasema ukila na kipofu usimshike mkono", Taarabu inawatangazia bidhaa zenu, nanyi ni lazima muoneshe kuwajari, na sio kuwajari wamiliki wa vituo vya redio na television tu siku zote chanda chema huvikwa pete. 

KUWENI MAKINI NA MAKALA HII SIKU MOJA MTAKUMBUKA HAYA...

0 comments:

Post a Comment