![]() |
Baadhi ya wasanii wa G5 Modern Taarabu. |
Mr Slim amesema katika Video ya Albam hii anataka avunje rekodi ya taarabu hapa nchini kwa kufanya video nzuri na iwe mfano kwa makundi mengine, video itafanyika kwa wiki mbili mfululizo ili kuhakikisha wanatoa kitu mashabiki wanataka.
Albam itakuwa na Nyimbo Nne (4):
1. DONT BREAK MY HEART - HASSAN VOCHA,
2. NYUMBA IMEPATA MWENYEWE - MWANAHAWA ALLY,
3. EPUKA MIFARAKANO - HADIJA KIMOBITEL NA
4. FAHARI YA MWANAMKE yake Malkia wa mipasho HADIJA KOPA.
Unaweza kushangaa ni kwanini katika Albam hii wapo Hadija Kopa na Kimobitel!? Mr Slim alisema: “Sisi kama G5 tumeamua kuwashirikisha kama wasanii wenzetu, hii tumejaribu kuwaonyesha njia wasanii wenzetu kuwa miziki ni kushirikiana na wala sio kubaguana na kuwekeana chuki kwasababu msanii kazi yake ni Kuburudisha na Kuelimisha jamii”.
Mkurugenzi Mr. Slim alimalizia kwa kusema:-
“WAKAZI WA KIGAMBONI KAEENI MKAO WA KULA JUMATANO YA 11/9/2013 (Wiki ijayo) NA KILA SIKU YA JUMATANO TUTAKUWA TUNATOA BURUDANI CLUB KAKALA KATIKA AFRICAN NIGHT, KARIBUNI SANA MJE KUPATA BURUDANI YA G5 MODERN TAARABU”.
0 comments:
Post a Comment