TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, September 5, 2013

"NDONDO" NI TATIZO KUBWA KWA WASANII WA TAARABU NCHINI TANZANIA!...

 "NDONDO" ni msemo uliozoeleka hususani kwa wasanii wengi wa Taarabu waliopo katika mabendi mbalimbali hapa nchini. 

Hii ni khali ya msanii wa bendi moja kwenda kufanya kazi katika bendi nyingine kwa kificho pasipo viongozi wa bendi yake kujua. 

Tathimini iliyofanywa na mtandao wa taarabuzetu.blogspo.com umegundua kwamba karibia wasanii wa bendi zote wanafanya ndondo hata wale wanaojiita wapo katika bendi kubwa na zinazokubalika kama Jahazi, Mashauzi na hata Melody!, zipo bendi ambazo wameweka sheria ya kutomruhusu msanii wao yeyote kupanda katika jukwaa la bendi yoyote pasipo ruhusa ya uongozi. Mfano wa bendi hizo ni Gusagusa Min Bendi na Jahazi Modern Taarabu, msaani wa bendi hizi mbili akikutwa katika jukwaa la bendi nyingine anafanya kazi adhabu yake ni kusimamishwa bendi au kufukuzwa kabisa. 

Akilizungumzia tatizo hili meneja wa Bendi ya Supershine Modern Taarabu Mr Kais Mussa alisema kweli ni tatizo kubwa sababu wapenzi wamekuwa wakiyumbishwa wasijue msanii husika yupo katika bendi ipi, kwa upande wa pili wasanii wengi wa taarabu hawana mishahara wanategemea Gate correction tu! sasa inakuwa ngumu kumbana msanii wa hivi wakati ukijua wazi ana familia inamtegemea. ila ni tatizo.

Pia alisisitiza kwa upande wa bendi yake haruhusiwi msanii yoyote kwenda Kufanya Show, Kuimba au Kurekodi nyimbo katika bendi nyingine au binafsi, yote hayo lazima yapitie kwa uongozi na kuangalia kama inafaa kufanya hivyo, vinginevyo msanii hana ruksa hiyo na kila msanii analitambua hilo katika bendi yake.

Hapohapo na sisi mtandao wa Taarabu Tanzania hatuna budi kupitia hapahapa katika mada hii kuwaeleza viongozi wote wa Bendi kuwa, Wasanii wapewe MIKATABA ya kufanya kazi na walipwe vizuri ili waendeshe maisha yao vizuri kwa kutegemea Muziki, vinginevyo waachwe wajitafutie na pembeni kama wafanyavyo sasa.
Naamini mikataba itakuwa minono tuu...

0 comments:

Post a Comment