TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 17, 2013

ISHA MASHAUZI SIKIA HII... WAKATI UKIJIANDAA KUGONGA KOPI KWA MUHINDI, VIDEO YA VIWAVI JESHI YAZAGAA KAMA NJUGU MITAANI....

Isha Mashauzi
Tatizo la wizi wa kazi za wasanii limekuwa likiota mizizi na kushamili kila kukicha, inakuwa inaumiza sana unapotumia gharama kubwa kuandaa albam yako halafu anatokea mtu na kujinufaisha tena bila kutoa jasho lolote!.

Video mpya kabisa ya wimbo wa "VIWAVI JESHI" ulioimbwa na mkurugenzi wa mashauzi classic Isha mashauzi imekuwa ikiuzwa kama njugu mitaani na kwenye makompyuta mbalimbali tena kwa wizi na kwa bei ndogo kabisa.

Jambo la kushangaza hata huyo Isha Mashauzi mwenyewe hajapata senti hata tano toka kwa muhindi msambazaji, kweli hii ni haki?.

Cover kwa Juu mbele.
Mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com ulipo mtafuta Isha kuthibitisha hilo akajibu kwamba
yeye hana taarifa zozote kuhusu issue hiyo, ila msanii mmoja wa Mashauzi amekili kuwa jambo hilo limefikishwa kwenye uongozi na taratibu za kisheria kwa wahusika zinaendelea kufuatwa. Tunaumia sana sisi wasanii kiukweli... Tunaomba serikali itunge sheria kali kwa wezi wa kazi za wasanii kama hawa alimalizia.

Mtandao huu baada ya kupata taarifa na data zote hizi uliingia mitaani kuisaka hiyo Video inayodaiwa kusambaa mtaani, tulipita maeneo ya Ubungo hatukuiona lakini maeneo ya Buguruni tulizikuta nyingi tu, tena kwa gharama ya Tshs. 1,000/= VCD ambayo ina collection ya Video za wasanii wenye Majina makubwa katika muziki wa Taarabu.

VCD hiyo imeandika:
WAKALI WA MIONDOKO YA PWANI - VIDEO.

Ndani ya CD hiyo kuna wasanii na Nyimbo zao kama ifuatavyo:-
1. Viwavi Jeshi - Isha Ramadhan
2. Wasiwasi wako - Mzee Yusuph
3. Aliyeniumba ajanikosea - Mwanahawa Ally
4. Hata bado ujanuna - Fatma Ally (Jahazi)

Mtaandao wa Taarabuzetu.blogspot.com inayo kopi iliyonunua kwa Tshs. 1,000/= tu.
CD ni mbaya sana kwa (Quality), inakatisha tamaa sana kwa wasanii, sisi kama wadau wakubwa wa muziki wa taarabu na wasanii wote hapa Bongo kwa ujumla, tunaiomba Serikali iangalie na itunge sheria kali kwa wezi hawa wa kazi za wasanii na kuwe na ufuatiliaji wasikae tu kukusanya kodi wakati kazi haziuziki katika matarajio ya wenyewe.

Tunatoa pole sana kwa wote...