Leo hii inakuja sehemu ya pili ya taarifa hiyo ambayo inatolewa ufafanuzi wa kina na ndugu "BAKARY SHOMARI" toka visiwani Znz ambae yeye anasema kwamba ndio mmiliki halali kabisa wa Zanzibar Stars na wala sio Hakim Shafii kama anavyosema. "Unajua niliposoma katika blog yenu nilishangazwa sana! Ukweli ni kwamba kuna bendi mbili tofauti kaka! Kuna Zanzibar Stars ambayo imesajiliwa hapa Znz, na kuna New Zanzibar Modern Taarabu ambayo usajili wake umefanyika huko Dar.
Wamiliki wa Zanzibar Stars ni Bakary Shomary, Adam Mlamali, Sihaba Juma, Mzee Yusuph na Zuhura Shabban. Lakini baadae wenzangu walijitoa nikabakia peke yangu.
Na mmiliki wa New Zanzibar Modern Taarab ni SAHIM ambae anaishi nchi za kiarabu kwa sasa na wala sio Hakim Shafii. Labda huyo Hakim Shafii awe amekabidhiwa kuiendesha tu lakini si mmiliki kama inavyosemwa. Kwahiyo anapoamua kujiita yeye mmiliki inabidi aeleze ni mmiliki wa New Zanzibar Modern Taarabu na sio Zanzibar Stars alimaliza kwa kusema".
Sisi mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com tunafunga mjadala huu rasmi leo natumai wasomaji wetu wamefaidika sana na ufafanuzi huu.