TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, July 25, 2013

MAKUNDI YA KANGA MOJA, KITU TIGO NA BAIKOKO YANAHARIBU MAUDHUI YA TAARABU NCHINI!!...

Kanga Moja
 Wadau na wapenzi wa tasnia hii ya burudani hasa Taarabu hapa nchini Tanzania, wanayalalamikia makundi yaliyojitokeza ya kucheza nusu uchi na kudai kuwa yanapotosha jamii na kuyashutumu kujihusisha na kuchukua waume wa watu kwa michezo yao michafu. 

Wadau pia wameshangazwa na ukimya unaoonyeshwa na viongozi wa Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) juu ya hawa wasichana wanaojiita "Kanga moja, Kitu tigo na Baikoko" kwani wamekuwa ni chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa jamii inayotuzunguka, wamekuwa wakizungu sehemu mbalimbali hapa nchini wakifanya matamasha tena katika kumbi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitambulika na afisa utamaduni pia anatoa kibali cha show husika! 

Kiukweli inashangaza sana, hawa madada ukiwakuta wanacheza unaweza kuangalia pembeni kwa aibu! hawana stara hata kidogo wanacheza uchi kabisa na pengine show zao zikiwa zimepewa ulinzi na Serikali.

"Kwakweli ni aibu tupu kwa Taifa letu tukiendelea kufuga na kuwalea watu kama hawa wanaofanya uchafu huu maana wanaonekana hadi nchi jirani na pengine hatuna habari wanapata vibari kwenda kufanya show nchi za nje, wanatutia aibu kwakweli, kwanini wasipigwe marufuku wakayafungia kabisa!?"  Mdau mmoja alilalamika.

Sisi mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kama wananchi wengine na wadau wakubwa wa miondoko ya Taarabu nchini, tunaiomba Serikali ijaribu kulitizama kwa makini suala hili na kulipatia ufumbuzi.
Kitu Tigo
BAADHI YA PICHA ZA LAANA KATIKA MAONYESHO YA MAKUNDI HAYA... 

<<<BOFYA HAPA>>>

BAIKOKO INAYOSADIKIWA KUTOKA TANGA.
HAPO MZEE MZIMA NA FAMILIA YAKO INAKUTIZAMA...
MAJANGA...!!
???

HAWA NAO NI KITU TIGO...
SIJUI NDO MIELEKA...!!!
KANGA MOJA...
CHUPA HUTUMIKA...!!!
ULINZI UKIIMARISHWA ILI SHOW IFANYIKE KWA USALAMA...!!!!!
POVU LINAHUSIKA...
WANAITA "MILIMA PACHA"...
WANAITA "NDEMBENDEMBE"...!!!

0 comments:

Post a Comment