Kinanda ni chombo muhimu sana katika muziki
wa Taarabu, Kumekuwa na wapigaji wengi sana wa vinanda karibu kila
bendi. lakini ifuatayo ni orodha ya wapigaji watano bora wa vinanda.
ikumbukwe hii ni kwa mujibu wa mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com na
wala si-vinginevyo!!.
1.= Thabit Abdul:- Inawezekana ni sababu amepiga
miziki aina tofauti, kwani amekuwa akifanya vizuri sana katika nyimbo
tofauti. Thabit kwa sasa ndio mtu anae ongoza kwa kufanya kazi na
waimbaji tofauti wa Taarabu na kuwatengenezea nyimbo zao.
Thabit Abdul kwa sasa ni Director wa 5 Stars na albam
ya sasa ya 5 Stars katunga yeye nyimbo zote na kupiga kinanda pia.
2.= Ally J:- Yeye anakamata nafasi ya pili kwa upigaji wa kinanda, ni
Director anaekubalika sana katika tasnia hii hususani Modern Taarabu. Ally
J ambae pia hivi karibuni amejiingiza kwenye uimbaji na wimbo wake wa
"Ukurasa mpya" unafanya vizuri sana katika vituo mbalimbali vya redio. Ni miongoni mwa
wasaani waanzilishi wa 5 Stars pia.
3.= Chidy Boy:- Tegemeo
kubwa la Mzee Yusuph kwa sasa pale Jahazi. wakati anaingia Jahazi wengi
walimbeza na kumuona hafai lakini kadri siku zilivyokuwa zinakwenda alionyesha ushupavu mpaka
kufikia Mzee Yusuph kumuamini na kumpa nyimbo muhimu kabisa za bendi
kupiga yeye. kwa sasa ndio mpiga kinanda namba moja pale Jahazi Modern
Taarabu.
4.= Omary Kisila:- Wasiomjua huwa wanafikiri Omary Kisila kaibuka tu katika wimbo wa Domo la udaku!, lah! hasha! Kisila ni
mkongwe katika muziki wa Taarabu kwani ameshawahi kufanya kazi na mzee
yusuph, Bi Sihaba Juma, Zuhura Shabban na wengineo pale Zanzibar Stars,
kwa sasa ni mpiga kinanda namba moja wa T MOTTO chini ya mkurugenzi Amin
Salmin "komandoo".
5.= Ndage Ndage:- Alianza kupiga kinanda akiwa na umri mdogo kabisa, tena anatoroka
shule na kwenda kwa kaka yake Ally J kufundishwa kinanda. hivi sasa Ndage Ndage amekuwa mwalimu na yeye anawafundisha wengine. Kwa sasa yupo
katika bendi ya Mashauzi, ila kuna muda alienda Kings modern taarabu kwa
muda mchache lakini akarejea Mashauzi Classic ambapo ameendelea kuwepo
mpaka sasa. Huyo ndio Ndage Ndage midole ya tembo a.k.a. mtoto wa Thabit
abdul.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Mmmmmh.... mbona mfalme mzee yusuph hayupo humu ndani????????
Kwel kabisa me mwnyw nljua mzee atakuepo lakin cvyo.penye cfa achen pasifiwe ata km unasema kwa mujibu wa blog hii.me naona mfalme alistahli kabisa tena namba1.cjasema km hao hawastahl ila mzee anaweza kiukwel.lilian masika mdau no1
yaa mzee amgekuwepo lkn hamfikii Thabit wala ally j!labda angakaa namba tatu,moja na mbili no!hao watu wakali sn!
Ushaambiwa mfalme ye kawaachia wadogo zake
Post a Comment